326. Matamanio ya Pekee ya Mungu ni Kwa Mwanadamu Kusikiliza na Kutii
I
Kwa kuwa Mungu aliiumba dunia miaka mingi iliyopita,
Amefanya kazi kubwa sana duniani humu,
Yeye amepitia kukataliwa kubaya mno kwa binadamu
na kupitia kashfa nyingi.
Hakuna aliyekaribisha kufika kwa Mungu duniani.
Wote walimpuuza kwa dharau sana.
Yeye alipitia maelfu ya miaka ya shida.
Mwenendo wa mtu kwa muda mrefu uliuvunja moyo Wake.
Yeye hajali tena uasi wa mwanadamu,
lakini Anapanga kuwabadilisha na kuwatakasa badala yake.
Nia ya pekee ya Mungu ni kwa mwanadamu kusikiliza na kutii,
kuhisi kuaibika mbele ya mwili Wake na sio kupinga.
Yote Anayotaka kwa kila mtu, kwa watu wote leo, ni kuamini tu kuwa Yeye anaishi.
II
Mungu katika mwili amepatwa na dhihaka ya kutosha
na kupitia kutengwa na kusulubiwa;
Pia amevumilia maovu ya mwanadamu.
Baba mbinguni hakuweza kuvumilia kuona hili.
Alirejeza kichwa Chake na kufunga macho Yake
kusubiri kurudi kwa Mwanawe mpendwa.
Nia ya pekee ya Mungu ni kwa mwanadamu kusikiliza na kutii,
kuhisi kuaibika mbele ya mwili Wake na sio kupinga.
Yote Anayotaka kwa kila mtu, kwa watu wote leo, ni kuamini tu kuwa Yeye anaishi.
III
Mungu aliacha kutaka zaidi kwa mwanadamu zamani sana.
Thamani Aliyolipa tayari ni ya juu sana,
na bado mwanadamu anaendelea kupumzika bila wasiwasi;
kwa kazi ya Mungu, yeye hupuuza tu.
Nia ya pekee ya Mungu ni kwa mwanadamu kusikiliza na kutii,
kuhisi kuaibika mbele ya mwili Wake na sio kupinga.
Yote Anayotaka kwa kila mtu, kwa watu wote leo, ni kuamini tu kuwa Yeye anaishi.
kutoka katika "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili