248 Upendo wa Kweli wa Mungu

1

Mara nyingi sana, nimekuwa hasi na nimeomboleza kwa sababu nilipoteza sifa na hadhi.

Mara nyingi sana, majaribio yalifunua kwamba nilijali tu matarajio yangu ya baadaye na nilizidiwa na huzuni.

Mara nyingi sana, nilikuwa mkaidi na mwasi, nikijaribu kujiondolea hukumu ya Mungu na dhamiri yangu haikunisuta.

Mara nyingi sana, niliazimia kutubu na bado nilitenda maovu kwa makusudi, na niliruhusu dhambi ienee pote ndani yangu.

Ee Mungu, hukumu ya maneno Yako inaifunua roho yangu mbaya,

na ninaona waziwazi ukweli wa upotovu wangu na hakuna mahali ambapo naweza kujificha kwa aibu.

2

Nilikuwa nimeamua kuwa singeweza kuokolewa, lakini maneno Yako yaliondoa kuelewa kwangu visivyo.

Mara nyingi sana, nilianguka katika majaribu ya Shetani, lakini kwa siri Ulinilinda na kunihifadhi.

Mara nyingi sana, nilikuwa na dhana mbaya na nikakupinga, lakini Ulinionyesha huruma na uvumilivu kila wakati.

Hukukumbuka nyakati zote nilizotenda dhambi, na Ulinipa nafasi ya kutubu.

Ee Mungu, mimi ni wa thamani ndogo sana na duni, lakini Unanijali wakati wote.

Ninawezaje kustahili kuitwa binadamu ikiwa bado siwezi kulipa upendo Wako?

3

Kwa kupitia Hukumu, majaribio, kukaripiwa na kufundishwa nidhamu Kwako, mwishowe najua upendo Wako.

Ingawa ninapatwa na maumivu makali ya usafishaji, lakini tabia yangu potovu inatakaswa.

Kutenda ukweli, kukutii Wewe na kuishi mbele Yako, ninahisi utulivu na amani.

Kwa kuwa mtu mwaminifu anayemwogopa Mungu na kuepukana na uovu, ninahisi furaha sana.

Ee Mungu, hukumu Yako ni upendo na imeniwezesha kupata wokovu Wako mkuu.

Nimepitia upendo Wako wa kweli, na ninatamani kukupenda na kukutii milele.

Iliyotangulia: 247 Ee Mungu, Moyo Wangu Tayari ni Wako

Inayofuata: 249 Mungu Amenipa Upendo Mwingi Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp