28 Kondoo wa Mungu Waisikia Sauti Yake

1 Siku zitafika mwisho; mambo yote katika dunia yatakuwa bure, na mambo yote yatazaliwa upya. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Hapawezi kuwa na utata! Mbingu na nchi zitapita lakini maneno Yangu hayatapita! Acha Niwasihi kwa mara nyingine tena: Msikimbie bure! Amkeni! Tubuni na wokovu umekaribia! Tayari Nimeonekana miongoni mwenu na sauti Yangu imetokea.

2 Sauti yangu imetokea mbele yenu, uso kwa uso na nyinyi kila siku, safi na mpya kila siku. Unaniona Mimi na Ninakuona wewe, Ninasema na wewe mara kwa mara, uso kwa uso na wewe. Na, bado unanikataa Mimi, hunijui Mimi; Kondoo Wangu wasikia sauti Yangu na bado mnasita! Mnasita! Mioyo yenu imepumbaa, macho yenu yamepofushwa na Shetani na hamuwezi kuuona uso Wangu mtukufu—ni kusikitisha kulikoje! Kusikitisha kulikoje!

3 Roho saba mbele ya kiti Changu cha enzi watumwa kwa kila pembe ya dunia na Mimi Nitamtuma Mjumbe Wangu kuzungumza kwa makanisa. Mimi ni mwenye haki na mwaminifu, Mimi ni Mungu achunguzaye sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mtu. Roho anaongea na makanisa na ni maneno Yangu yanayotiririka kutoka ndani ya Mwanangu; wale wote ambao wana masikio wanapaswa kusikiliza! Wale wote ambao wanaishi wanapaswa kukubali! Yaleni tu na kuyanywa, na msitilie shaka. Wale wote ambao huyatii na kuyasikiza maneno Yangu watapokea baraka kuu!

4 Wale wote wautafutao uso Wangu kwa kweli watapata mwanga mpya kwa hakika, nuru mpya na ufahamu mpya; wote watakuwa wasafi na wapya. Maneno Yangu yataonekana kwako wakati wowote na yatafungua macho ya roho yako ili uweze kuona siri zote za ulimwengu wa kiroho na kwamba ufalme uko miongoni mwa binadamu. Ingia katika hifadhi na neema yote na baraka zitakuwa juu yako, njaa na baa hazitaweza kukugusa, mbwa mwitu, nyoka, chui wakubwa na chui hawataweza kukudhuru. Utaenda na Mimi, utembee na Mimi, na uingie katika utukufu pamoja na Mimi!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 15” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 27 Umeme Uwakapo Kutoka Mashariki

Inayofuata: 29 Neno la Mwenyezi Mungu Latimiza Kila Kitu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp