B. Kuhusu Tabia ya Haki ya Mungu
554. Katika kazi Yake ya mwisho ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ya kuadibu na hukumu, ambapo Anafichua yote yasiyo ya haki, ili kuhukumu hadharani watu wote, na kuwakamilisha wale wanaompenda kwa moyo wa kweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Vitu vyote katika uumbaji vitatenganishwa kulingana na aina yao, na kugawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yao. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Ikiwa watu hawatapitia kuadibu na hukumu, basi hakutakuwa na njia ya kufichua uasi wao na udhalimu wao. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe thawabu, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote lazima itimizwe kupitia kuadibu kwa haki na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefikia kilele chake na kutotii kwake kuwa kubaya kupita kiasi, ni tabia ya Mungu tu ya haki, ambayo kimsingi imechangiwa na kuadibu na hukumu na kufichuliwa wakati wa siku za mwisho, inayoweza kumbadilisha na kukamilisha mwanadamu kikamilifu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa enzi, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kwa kudhania kwamba, katika kufichua matokeo ya mwanadamu katika siku za mwisho, Mungu bado angempa mwanadamu huruma na upendo usio na kikomo na kuendelea kuwa na upendo kwake, bila kumweka mwanadamu chini ya hukumu ya haki lakini badala yake kumwonyesha uvumilivu, subira, na msamaha; na kumsamehe mwanadamu haijalishi dhambi zake ni kubwa kiasi gani, bila hukumu yoyote ya haki: ni lini basi usimamizi wote wa Mungu ungefikishwa mwisho? Je, ni wakati gani tabia kama hii ingeweza kuwaongoza watu kwenye hatima inayofaa ya wanadamu? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kumtenganisha mwanadamu kulingana na aina yake na kumleta mwanadamu katika ufalme mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
555. Jina Langu litaenea nyumba hadi nyumba katika mataifa yote na katika pande zote na litatangazwa kutoka kwenye vinywa vya watu wazima na watoto vilevile katika ulimwengu dunia mzima; huu ni ukweli mtupu. Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee, hata zaidi Mimi pekee ndimi nafsi ya Mungu, na Mimi, ukamilifu wa mwili, ni hata zaidi dhihirisho kamili la Mungu. Yeyote asiyethubutu kuniheshimu Mimi, yeyote anayethubutu kuonyesha dharau machoni pake, yeyote anayethubutu kusema maneno ya chuki dhidi Yangu hakika atakufa kutokana na laana na ghadhabu Yangu (kutakuwa na kulaani kwa sababu ya ghadhabu Yangu). Na yeyote ambaye hatathubutu kuwa mwaminifu au na upendo Kwangu, yeyote anayethubutu kujaribu kunihadaa hakika atakufa katika chuki Yangu. Haki yangu, uadhama na hukumu yangu vitadumu milele na milele. Mwanzoni, Nilikuwa mwenye upendo na rehema, lakini hii si tabia ya uungu Wangu kamili; haki, uadhama na hukumu ni tabia Yangu tu—Mungu Mwenyewe mkamilifu. Wakati wa Enzi ya Neema Nilikuwa mwenye upendo na rehema. Kwa sababu ya kazi Niliyopaswa kumaliza Nilikuwa na fadhila na rehema, lakini baadaye hakukuwa na haja ya fadhila yoyote au rehema (hakujakuwepo na yoyote tangu wakati huo). Yote ni haki, uadhama na hukumu na hii ni tabia kamili ya ubinadamu Wangu wa kawaida pamoja na uungu Wangu kamili.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 79
556. Kuielewa tabia ya haki ya Mungu, kwanza mtu anapaswa kuelewa hisia za Mungu: kile Anachokichukia, kile Anachokikataa kabisa, kile Anachokipenda, ni mvumilivu na mwenye huruma kwa nani, na ni aina gani ya mtu anayepokea rehema hiyo. Hii ni hoja ya msingi kufahamu. Aidha, mtu anapaswa kuelewa kwamba haijalishi Mungu ni mwenye upendo kiasi gani, haijalishi ni Mwenye rehema na upendo kiasi gani kwa watu, Mungu hamvumilii mtu yeyote anayekosea hadhi na nafasi Yake, wala Hamvumilii mtu yeyote anayekosea heshima Yake. Ingawa Mungu anawapenda watu, Hawadekezi. Anawapatia watu upendo Wake, rehema Yake, na uvumilivu Wake, lakini hajawahi kuwadekeza; Ana kanuni Zake na mipaka Yake. Bila kujali ni kwa kiwango gani umeuhisi upendo wa Mungu ndani yako, bila kujali upendo huo ni wa kina kiasi gani, hupaswi kamwe kumtendea Mungu kama ambavyo ungemtendea mtu mwingine. Ingawa ni kweli kwamba Mungu anawachukulia watu kama wako karibu Naye, ikiwa mtu anamwangalia Mungu kama mtu mwingine, kana kwamba ni kiumbe mwingine wa uumbaji, kama rafiki au kama kitu cha kuabudu, Mungu atawaficha uso Wake na kuwatelekeza. Hii ndiyo tabia Yake, na watu hawapaswi kulichukulia jambo hili kwa mzaha. Hivyo, mara nyingi sisi huona maneno kama haya yakinenwa na Mungu kuhusu tabia Yake: Haijalishi umesafiri njia nyingi kiasi gani, umefanya kazi kubwa kiasi gani au umevumilia kiasi gani, mara tu unapoikosea tabia ya Mungu, Atamlipa kila mmoja wenu kulingana na kile ulichokifanya. Hii ina maana kwamba Mungu huwaona watu kama wapo karibu na Yeye, lakini watu hawapaswi kumchukulia Mungu kama rafiki au ndugu. Usimchukulie Mungu kama rafiki yako. Haijalishi ni upendo kiasi gani umepokea kutoka Kwake, haijalishi Amekuvumilia kwa kiasi gani, hupaswi kabisa kumchukulia Mungu kama rafiki tu. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII
557. Mungu kutoweza kuvumilia kosa ndicho kiini Chake cha kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; ukuu wa Mungu ndiyo kiini Chake cha kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Ni dhahiri kwamba pia ni ishara ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ni asili Yake Mwenyewe, ambayo haibadiliki hata kidogo na kupita kwa wakati, na wala haibadilishwi na mabadiliko ya eneo la kijiografia. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Bila kujali ni nani Anayemfanyia kazi Yake juu yake, kiini Chake hakibadiliki, na wala tabia Yake ya haki haibadiliki. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika kiini Chake au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini ni kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake huikosea tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anaijaribu ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapoijaribu mara kwa mara ghadhabu ya Mungu—na pia wakati ambapo dhambi inaenea—ghadhabu ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitakoma kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote za adui zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu unapopingwa, wakati nguvu za haki zinapozuiliwa na kutoonekana na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya kiini cha Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na zinapozuiliwa na kutoonekana na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu Asiye na dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
558. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za uovu hudhibitiwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Lengo la hasira ya Mungu si kulinda hadhi na utambulisho Wake mwenyewe, bali ni kulinda uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, ili kulinda sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni ufunuo sahihi sana wa asili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna nia potovu katika ghadhabu Yake, na wala hakuna udanganyifu au njama zozote, achilia mbali tamaa, hila, udhalimu, vurugu, uovu au tabia zingine zozote ambazo binadamu wote waliopotoka huwa nazo. Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua kiini cha kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila kitu Anachofanya ni wazi kabisa, kama vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu aliyechanganyikiwa; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hiki ndicho kipengele cha kivitendo cha ghadhabu ya Mungu, na ni kwa sababu ya kipengele hiki cha kivitendo cha ghadhabu ya Mungu kwamba ubinadamu umefikia uwepo wake wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, binadamu wangeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, vyema na vizuri vingeangamizwa na kukoma kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na amri za kuwepo kwa viumbe vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa. Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki ili kulinda na kudumisha maisha ya kawaida ya binadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na uadhama, watu wote waovu, mambo, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa binadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Katika kipindi cha milenia kadhaa zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na ambao wanachukua nafasi ya wasaidizi na watumishi wa Shetani katika kazi ya Mungu ya kuwasimamia binadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu za haki zaidi miongoni mwa wanadamu hazijawahi kuharibiwa.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
559. Mungu huwashughulikia wanadamu wajinga na wapumbavu kwa huruma na uvumilivu. Lakini, kwa upande mwingine ghadhabu ya Mungu imefichwa mara nyingi na katika matukio mengi, na haijulikani kwa watu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati mwanadamu anapokabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya mwisho ya uvumilivu na msamaha kwa mwanadamu—yaani, wakati tukio la mwisho la Mungu la rehema na onyo Lake la mwisho linapowajia wanadamu—ikiwa watu bado wanatumia mbinu zilezile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali rehema Zake, basi Mungu hataweka tena uvumilivu na subira Yake juu yao. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu atabatilisha rehema Zake wakati huu. Kufuatia haya, Ataituma tu ghadhabu Yake. Anaweza kudhihirisha ghadhabu Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.
Matumizi ya Mungu ya moto kuuangamiza mji wa Sodoma ndio mbinu Yake ya haraka zaidi ya kuondoa kabisa binadamu au kitu. Kuwachoma watu wa Sodoma kuliangamiza zaidi ya miili yao ya nyama; kuliangamiza uzima wa roho zao, nafsi zao na miili yao, na kuhakikisha kwamba watu waliokuwa ndani ya mji wangekoma kuwepo kwenye ulimwengu wa anasa na hata ulimwengu usioonekana na mwanadamu. Hii ni njia mojawapo ambayo Mungu hufichua na kuonyesha hasira Yake. Mfano huu wa ufunuo na maonyesho ni kipengele kimoja cha dutu ya ghadhabu ya Mungu, kama vile ilivyo kwa kawaida pia ufunuo wa kiini cha tabia ya haki ya Mungu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, Anaacha kufichua rehema au wema wowote, na wala haonyeshi tena uvumilivu au subira Yake; hakuna mtu, kitu au sababu inayoweza kumshawishi kuendelea kuwa na subira, kutoa rehema Zake tena, na kumpa binadamu uvumilivu wake kwa mara nyingine. Badala ya mambo haya, bila kusita hata kidogo, Mungu atashusha hasira Yake na adhama, kufanya kile Anachotamani, na Atafanya mambo haya kwa haraka na kwa njia safi kulingana na matamanio Yake binafsi. Hii ndiyo njia ambayo Mungu hushusha hasira na adhama Yake, ambavyo binadamu hatakiwi kuvikosea, na pia ni maonyesho ya kipengele kimoja cha tabia Yake ya haki. Wakati watu wanamshuhudia Mungu akionyesha wasiwasi na upendo kwa binadamu, hawawezi kugundua hasira Yake, kuona ukuu Wake au kuhisi kutovumilia Kwake kosa. Mambo haya siku zote yamewaongoza watu kusadiki kwamba tabia ya haki ya Mungu ni ile ya huruma, uvumilivu na upendo tu. Hata hivyo, wakati mtu anapoona Mungu akiuangamiza mji au akichukia binadamu, hasira Yake katika kuangamiza binadamu na adhama Yake huruhusu watu kuona kidogo upande ule mwingine wa tabia Yake ya haki. Huku ni kutovumilia kosa kwa Mungu. Tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa lolote inapita fikira za kiumbe chochote kilichoumbwa, na miongoni mwa viumbe visivyoumbwa, hakuna chenye uwezo wa kuiingilia au kuiathiri; hata zaidi, haiwezi kughushiwa au kuigwa. Kwa hivyo, kipengele hiki cha tabia ya Mungu ndicho ambacho cha tabia ya Mungu ndicho ambacho binadamu anafaa kukijua zaidi. Ni Mungu Mwenyewe Pekee ndiye aliye na aina hii ya tabia, na Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki aina hii ya tabia. Mungu anamiliki aina hii ya tabia kwa sababu Anachukia maovu, giza, maasi na vitendo viovu vya Shetani—vya kuwapotosha na kuwaangamiza wanadamu—kwa sababu Anachukia vitendo vyote vya dhambi vinavyompinga Yeye na kwa sababu ya kiini Chake kitakatifu na kiisicho na doa. Ni kwa sababu ya hali ndiyoHataacha viumbe vyovyote kati ya vile vilivyoumbwa au ambavyo havikuumbwa vimpinge waziwazi au kushindana na Yeye. Hata mtu ambaye Aliwahi kumwonea huruma, au wale ambao Aliwachagua, endapo tu wataikasirisha tabia Yake na kukiuka kanuni Zake za subira na uvumilivu, Yeye bila huruma na bila kusita Ataachilia na kufichua tabia Yake ya haki ambayo haiwezi kuvumilia kosa lolote.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
560. Ingawa kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni kipengele kimojawapo cha onyesho la tabia Yake ya haki, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au isiyo na kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa hasira hata kidogo, na wala Yeye hakimbilii kufichua ghadhabu Yake na ukuu Wake kirahisi. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Mazungumzo mengi kati ya binadamu na Mungu yamerekodiwa kwenye Biblia. Maneno ya baadhi ya watu hawa binafsi yalikuwa ya juujuu, yasiyo na ujuzi na yasiyofaa, lakini Mungu hakuwaangusha chini, wala Hakuwashutumu. Hususan, wakati wa majaribio ya Ayubu, je, Yehova Mungu aliwachukuliaje marafiki watatu wa Ayubu na wale wengine baada ya Yeye kusikia maneno waliyomwambia Ayubu? Je, Aliwashutumu? Je, Aligeuka na kushikwa na hasira kali kwao? Hakufanya kitu kama hicho! Badala yake Alimwambia Ayubu aweze kusihi kwa niaba yao na kuwaombea, na Mungu Mwenyewe hakuyachukua makosa yao moyoni Mwake. Matukio haya yote yanawakilisha mtazamo wa kimsingi ambao Mungu huwachukulia binadamu waliopotoka, na wasiojua. Kwa hivyo, kuachiliwa kwa ghadhabu ya Mungu si onyesho la hali Yake, wala si njia Yake ya kuonyesha hisia Zake. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu haachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho na udhihirisho kamili wa tabia Yake ya haki, na ni ishara ya ufunuo wa kiini Chake kitakatifu. Mungu ni mwenye hasira, Asiyevumilia kukosewa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni binadamu waliopotoka ambao wana umiliki wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii kati ya sababu mbalimbali. Mara tu binadamu anapokuwa na hadhi, mara nyingi atapata ugumu wa kudhibiti hali ya moyo wake, na kwa hivyo atafurahia kutumia nafasi mbalimbali kueleza kutotosheka kwake na kutoa nje hisia zake; mara nyingi atawaka kwa hasira kali bila sababu yoyote, ili kuonyesha uwezo wake na kuwafanya wengine kujua kwamba hadhi yake na utambulisho wake ni tofauti na ule wa watu wa kawaida. Bila shaka, watu waliopotoka wasiokuwa na hadhi yoyote mara kwa mara pia watapoteza udhibiti wao. Ghadhabu yao mara nyingi husababishwa na uharibifu wa manufaa yao ya kibinafsi. Ili kulinda hadhi yake binafsi na heshima, mara kwa mara atatoa nje hisia zake na kufichua asili yake yenye kiburi. Mwanadamu atawaka kwa hasira na kutoa hisia zake ili kutetea na kudumisha uwepo wa dhambi, na vitendo hivi ni njia ambazo mwanadamu huonyesha kutoridhika kwake; wamejawa na uchafu, njama na fitina, upotovu na uovu wa wanadamu, na zaidi ya kitu kingine chochote, wamejawa na malengo na tamaa mbaya za wanadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, hasira ya mwanadamu haitawaka ili kutetea uwepo wa haki; kinyume chake ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateswa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kuliondoa. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, mwanadamu anapolipukwa na hasira ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiozuilika kwa mwandamu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote zinazomdhuru mwanadamu zitasitishwa; nguvu zote za uadui zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; na watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kupotshwa naye; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ruzuku ya Mungu katika mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni ulinzi unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kuenezwa kwa nguvu, na pia ni ulinzi unaolinda kuwepo na kuenezwa kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
561. Wakati unaposhughulikia kila mojawapo ya vitendo vya Mungu, lazima uwe na uhakika kwamba tabia ya haki ya Mungu iko huru dhidi ya vipengele vingine vyovyote, kwamba ni takatifu na haina dosari; vitendo hivi vinajumuisha binadamu kuweza kuangushwa chini, kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu. Bila kuacha, kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu kinatekelezwa kulingana na tabia yake ya asili na mpango Wake—hii haijumuishi maarifa ya binadamu, mila na falsafa—na kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake na kiini Chake, kisichohusiana na chochote kinachomilikiwa na binadamu aliyepotoka. Mwanadamu ana dhana kwamba upendo, huruma na uvumilivu wa Mungu pekee kwa binadamu ndivyo visivyokuwa na dosari, visivyoghoshiwa na vilivyo vitakatifu. Hata hivyo, hakuna anayejua kwamba ghadhabu ya Mungu na hasira Yake vilevile vyote havijatiwa unajisi; aidha, hakuna yule aliyefikiria maswali kama vile: kwa nini Mungu havumilii kosa lolote au kwa nini ghadhabu Yake ni kubwa mno. Kinyume ni kwamba, baadhi ya watu hukosa kuelewa hasira ya Mungu na kudhania kuwa ni hasira kali sawa na ile ya binadamu waliopotoka: wanaelewa ghadhabu ya Mungu kuwa ni sawa na hasira za binadamu waliopotoka; wao hata hudhania kimakosa kwamba ghadhabu ya Mungu ni sawa tu na ufunuo wa kiasili wa tabia potovu ya binadamu. Wanasadiki kimakosa kwamba ghadhabu ya Mungu inapoachiliwa ni sawa tu na ghadhabu ya binadamu waliopotoka, jambo linalotokana na kutoridhika; wanasadiki hata kwamba Mungu anapoachilia ghadhabu Yake ni maonyesho ya hali Yake ya moyo. Baada ya ushirika huu, Ninatumai kwamba kila mmoja wenu hatakuwa tena na shaka, fikira au kukisia kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na Natumai baada ya kusikiliza maneno Yangu mnaweza kuwa na utambuzi wa kweli wa ghadhabu ya tabia ya haki ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba mnaweza kuweka kando ufahamu wowote potofu wa hapo awali kuhusiana na ghadhabu ya Mungu, na kwamba mnaweza kubadilisha imani zenu zilizopotoka na maoni yenu potovu kuhusiana na kiini cha ghadhabu ya Mungu. Vilevile, Natumai kwamba mnaweza kuwa na ufafanuzi sahihi wa tabia ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba hamtakuwa tena na mashaka yoyote kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na kwamba hamtaweka mawazo ama fikira zozote za kibinadamu kuhusiana na tabia ya kweli ya Mungu. Tabia ya haki ya Mungu ni kiini cha kweli cha Mungu mwenyewe. Si kitu kilichotungwa au kuundwa na binadamu. Tabia Yake ya haki ni tabia Yake na haina uhusiano au muunganiko wowote na kiumbe chochote kilichoumbwa. Mungu Mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Hatawahi kuwa sehemu ya uumbaji, na hata kama Atakuwa mwanachama miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, tabia Yake ya asili na kiini Chake havitabadilika. Hivyo basi, kumjua Mungu si sawa na kujua kitu; kumjua Mungu si kuchunguza kitu, na wala si sawa na kumwelewa mtu. Kama mwanadamu atatumia dhana au mbinu yake ya kujua kifaa au kumwelewa mtu ili kumjua Mungu, basi hutawahi kuweza kutimiza maarifa ya Mungu. Kumjua Mungu hakutegemei uzoefu au kufikiria kwako, na hivyo basi hufai kulazimisha uzoefu wako au kufikiria kwako kwa Mungu. Haijalishi uzoefu au kufikiria kwako ni kwa kipekee namna gani, huko kote bado ni finyu; na hata zaidi, kufikiria kwako hakulingani na hoja, isitoshe hakulingani na ukweli, na pia hakulingani na tabia na kiini cha kweli cha Mungu. Hutawahi kamwe kufanikiwa kama utategemea mawazo yako ili kuelewa kiini cha Mungu. Njia ya pekee ni hii: kukubali yote yanayotoka kwa Mungu, kisha kwa utaratibu uweze kuyapitia na kuyaelewa. Kutakuwa na siku ambayo Mungu atakupa nuru ili uweze kuelewa kwa kweli na kumjua Yeye kwa sababu ya ushirikiano wako na kwa sababu ya njaa na kiu yako ya kupenda ukweli.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
562. Mungu kamwe si wa kusitasita au asiye na uamuzi katika vitendo Vyake; kanuni na makusudio yaliyo katika matendo Yake yote ni wazi na dhahiri, yasiyo na dosari wala doa, yasiyo kabisa na hila ama njama zozote zilizochanganywa ndani. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu hakina giza wala maovu. Mungu aliwakasirikia Waninawi kwa sababu vitendo vyao viovu vilikuwa vimefikia macho Yake; wakati ule hasira Yake ilitokana na kiini Chake. Hata hivyo, wakati hasira ya Mungu ilitoweka na akatoa uvumilivu Wake kwa watu wa Ninawi kwa mara nyingine tena, kila kitu Alichofichua kilikuwa bado ni kiini Chake. Mabadiliko haya yote yalitokana na mabadiliko katika mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu. Katika kipindi hiki chote cha muda, tabia ya Mungu isiyokosewa haikubadilika; kiini cha Mungu cha uvumilivu hakikubadilika; kiini cha Mungu cha upendo na huruma hakikubadilika. Wakati watu wanapotekeleza vitendo viovu na kumkosea Mungu atawashushia ghadhabu Yake. Wakati watu wanatubu kwa kweli, moyo wa Mungu utabadilika, na hasira Yake itakoma. Wakati watu wanapoendelea kumpinga Mungu kwa ukaidi, hasira Yake kali haitakoma; hasira Yake itawalemea hatua kwa hatua mpaka watakapoangamizwa. Hiki ndicho kiini cha tabia ya Mungu. Haijalishi kama Mungu anaonyesha hasira au huruma na wema, mwenendo wa binadamu, tabia na mtazamo wake kwa Mungu ndani ya kina cha moyo wake vinaamrisha kile ambacho kinaonyeshwa kupitia kwa ufunuo wa tabia ya Mungu. Kama Mungu anaendelea kumfanya mtu apitie hasira Yake, moyo wa mtu huyu bila shaka humpinga Mungu. Ni kwa sababu mtu huyu hajawahi kutubu kwa kweli, kuinamisha kichwa chake mbele ya Mungu au kumiliki imani ya kweli kwa Mungu, hajawahi kupata huruma na uvumilivu wa Mungu. Kama mtu hupokea utunzaji wa Mungu mara nyingi na hupokea huruma na uvumilivu Wake mara nyingi, basi mtu huyo bila shaka ana imani ya kweli kwa Mungu ndani ya moyo wake, na moyo wake haumpingi Mungu. Mtu huyu mara nyingi anatubu kwa kweli mbele ya Mungu; kwa hivyo, hata kama nidhamu ya Mungu mara nyingi humshukia mtu huyu, hasira Yake haitamshukia.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
563. Licha ya vile ambavyo Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Waninawi, mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo za magunia pamoja na kuketi kwenye majivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwao kwa dhambi zao—Mungu alikuwa bado ana ghadhabu juu yao. Baada ya wao kupitia mfululizo wa vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ilibadilika polepole kuwa huruma na uvumilivu kwao. Hakuna kitu kinachohitilafiana kuhusu ufunuo wenye ulinganifu wa vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika tukio moja. Kwa hivyo, ni kwa jinsi gani mtu anapaswa kuelewa na kujua kwamba hazihitilafiani? Mungu alionyesha na kufichua viini hivi viwili tofauti kabisa kwa mfululizo wakati watu wa Ninawi walipokuwa wakitubu na Akawaruhusu watu kuona uhalisi na kutokosewa kwa kiini cha Mungu. Mungu alitumia mtazamo Wake kuambia watu yafuatayo: Si kwamba Mungu hawavumilii watu, au hataki kuwaonyesha huruma; ni kwamba wao hutubu kwa kweli kwa nadra sana mbele za Mungu, na ni nadra kwa watu kugeuka kwa kweli kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, wakati Mungu ameghadhabishwa na binadamu, Anatumaini kwamba binadamu ataweza kutubu kwa kweli na Anatumaini kumwona binadamu akitubu kwa kweli, ambapo Ataendelea kumpa binadamu huruma na uvumilivu Wake kwa ukarimu. Hivi ni kusema kwamba mwenendo mbovu wa mwanadamu ndio husababisha hasira ya Mungu, huku nazo rehema na uvumilivu wa Mungu zikipewa wale wanaomsikiliza Mungu na kutubu kwa kweli mbele Yake, kwa wale wanaoweza kugeuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Mtazamo wa Mungu ulifichuliwa waziwazi sana katika jinsi Alivyowatendea Waninawi: Huruma na uvumilivu wa Mungu si vigumu kuvipokea hata kidogo; Anahitaji toba ya kweli ya mtu. Mradi tu watu wageuka kutoka kwa njia zao ovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao, Mungu atabadilisha moyo Wake na kubadilisha mtazamo Wake kwao.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
564. Wakati Mungu alibadilisha moyo Wake kwa minajili ya watu wa Ninawi, je, huruma na uvumilivu Wake ulikuwa wa bandia? Bila shaka la! Basi mabadiliko kati ya vipengele hivi viwili vya tabia ya Mungu katika hili suala moja yanakuruhusu kuona nini? Tabia ya Mungu ni kamili kabisa; haijagawanywa hata kidogo. Haijalishi kama Anaonyesha ghadhabu au huruma na uvumilivu kwa watu, haya yote ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Tabia ya Mungu ni ya kweli na wazi. Yeye hubadilisha fikira na mitazamo Yake kulingana na maendeleo ya mambo. Mabadiliko ya mtazamo Wake kwa Waninawi yanawaambia binadamu kwamba Anazo fikira na mawazo Yake mwenyewe; Yeye si roboti au sanamu ya udongo, bali Yeye ni Mungu Mwenyewe aliye hai. Angeweza kuwa na ghadhabu kwa watu wa Ninawi, sawa tu na vile ambavyo Angeweza kusamehe dhambi zao za kale kulingana na mitazamo yao; Angeweza kuamua kuwaletea Waninawi msiba na Angeweza kubadilisha uamuzi Wake kwa sababu ya kutubu kwao. Watu hupenda kutumia sheria bila kupinda na kutumia sheria kama hizo ili kumwekea mipaka na kumfafanua Mungu, sawa tu na vile watu wanavyopendelea kutumia kanuni kujaribu kuelewa tabia ya Mungu. Kwa hivyo, katika uwanja wa fikira za binadamu, Mungu hafikirii wala Yeye hana mawazo yoyote halisi. Kwa uhalisi, fikira za Mungu zinabadilika siku zote kulingana na mabadiliko katika mambo, na mazingira; huku fikira hizi zikiwa zinabadilika, vipengele tofauti vya kiini cha Mungu vitafichuliwa. Katika kipindi hiki cha mabadiliko, wakati ule Mungu hubadilisha moyo Wake, Yeye humfichulia mwanadamu ukweli wa uwepo wa maisha Yake na kufichua kwamba tabia Yake ya haki ni halisi na wazi. Aidha, Mungu hutumia ufunuo Wake mwenyewe wa kweli kuthibitisha kwa mwanadamu ukweli wa uwepo wa hasira Yake, huruma Yake, wema Wake na uvumilivu Wake. Kiini Chake kitafichuliwa wakati wowote na mahali popote kulingana na maendeleo ya mambo. Anamiliki hasira ya simba na huruma na uvumilivu wa mama. Tabia Yake ya haki hairuhusiwi kutiliwa shaka, kukiukwa, kubadilishwa au kupotoshwa na mtu yeyote. Miongoni mwa masuala yote na mambo yote, tabia ya haki ya Mungu, yaani, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, vyote vinaweza kufichuliwa wakati wowote na mahali popote. Anaonyesha waziwazi vipengele hivi kwa kila sehemu ya viumbe vyote, na Anavitekeleza kila wakati kwa uwazi. Tabia ya haki ya Mungu haiwekewi mipaka na muda au eneo, au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Mungu haionyeshwi bila kufikiri au kufichuliwa kulingana na mipaka ya muda au eneo. Badala yake, tabia ya haki ya Mungu inaonyeshwa kwa njia huru na kufichuliwa mahali popote na wakati wowote. Unapoona Mungu akibadilisha moyo Wake na kukoma kuonyesha hasira Yake na kujizuia dhidi ya kuuangamiza mji wa Ninawi, je, unaweza kusema kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo tu? Je, unaweza kusema kwamba hasira ya Mungu inajumuisha maneno matupu? Wakati Mungu anapoonyesha hasira kali na kuiondoa huruma Yake, je, unaweza kusema kwamba Hana hisia zozote za upendo wa kweli kwa binadamu? Mungu huonyesha hasira kali kutokana na vitendo viovu vya watu, hasira Yake haina dosari. Moyo wa Mungu unavutiwa na toba ya watu, na ni toba hii ambayo hubadilisha moyo Wake. Anapohisi kuguswa, Anapokuwa na mabadiliko katika moyo Wake pamoja na huruma na uvumilivu Wake kwa binadamu, vyote havina kosa kabisa; ni safi, havina kasoro, havina doa na havijachafuliwa. Uvumilivu wa Mungu ni uvumilivu mtupu; Huruma Yake ni huruma tupu. Tabia Yake itafichua hasira, pamoja na huruma na uvumilivu, kulingana na kutubu kwa binadamu na mwenendo wake tofauti. Haijalishi kile ambacho Anafichua na kuonyesha, yote hayo hayana kasoro; yote ni ya moja kwa moja; kiini Chake ni tofauti na ile ya kiumbe chochote kilichoumbwa. Wakati Mungu anapoeleza kanuni zinazohusu matendo Yake, mawazo Yake, fikira Zake, na kila uamuzi Anaoufanya, pamoja na kila hatua Anazozichukua, huwa hazina doa au dosari zozote. Kama jinsi ambavyo Mungu huamua na jinsi Atendavyo, ndivyo Anavyokamilisha shughuli Zake. Aina hizi za matokeo ni sahihi na hazina dosari kwa sababu chanzo chake hakina dosari na doa lolote. Hasira ya Mungu haina dosari. Vilevile, huruma na uvumilivu wa Mungu, ambazo hazimilikiwi na kiumbe yeyote ni takatifu na hazina kosa, na zinaweza kustahimili fikira na uzoefu.
Baada ya kuelewa hadithi ya Ninawi, je, sasa mnauona upande ule mwingine wa kiini cha tabia ya haki ya Mungu? Je, mnauona upande ule mwingine wa tabia ya haki na ya kipekee ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote miongoni mwa binadamu anayemiliki aina hii ya tabia? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki aina hii ya hasira kama ile ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki huruma na uvumilivu kama ule wa Mungu? Ni nani miongoni mwa viumbe anayeweza kuitisha ghadhabu kuu namna hii na kuamua kuangamiza au kuleta maafa juu yawanadamu? Na ni nani anazo sifa zinazostahili kutoa huruma kuvumilia na kumsamehe binadamu na hivyo basi kubadilisha uamuzi wake wa kuangamiza binadamu? Muumba huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni Zake za kipekee; na Hayuko chini ya udhibiti au vizuizi vilivyowekwa na watu, matukio au vitu vyovyote. Akiwa na tabia Yake ya kipekee, hakuna mtu anayeweza kubadilisha fikira na mawazo Yake, wala hakuna yule anayeweza kumshawishi Yeye na kubadilisha maamuzi Yake yoyote. Tabia zote na mawazo yote yaliyopo katika viumbe vyote vilivyoumbwa vipo chini ya hukumu ya tabia Yake ya haki. Hakuna anayeweza kudhibiti kama atatumia hasira au huruma; ni kiini cha Muumba tu—au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Muumba—inaweza kuamua hili. Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Baada ya kuchambua na kuelewa mabadiliko katika mtazamo wa Mungu kwa watu wa Ninawi, je, unaweza kutumia neno “upekee” kufafanua huruma inayopatikana katika tabia ya haki ya Mungu? Hapo awali tulisema kwamba hasira ya Mungu ni kipengele kimoja cha kiini cha tabia Yake ya haki na ya kipekee. Sasa Nitafafanua vipengele viwili, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, kama tabia Yake ya haki. Tabia ya haki ya Mungu ni takatifu; ni isiyokosewa na isiyoweza kutiliwa shaka; ni kitu kisichomilikiwa na yeyote miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Ni ya kipekee na maalum kwa Mungu pekee. Hivi ni kusema kwamba hasira ya Mungu ni takatifu na isiyoweza kukosewa Vivyo hivyo, kipengele kile kingine cha tabia ya haki ya Mungu—huruma ya Mungu—ni takatifu na haiwezi kukosewa. Hakuna yeyote kati ya viumbe vile vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa, anayeweza kuchukua nafasi Yake au kumwakilisha Mungu katika matendo Yake, wala hakuna yeyote ambaye angeweza kuchukua nafasi Yake au kumwakilisha Yeye katika kuangamiza Sodoma au wokovu wa Ninawi. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya tabia ya haki ya kipekee ya Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
565. Ingawa mji wa Ninawi ulikuwa umejaa watu waliopotoka, walio waovu, na wenye udhalimu kama wale wa Sodoma, kutubu kwao kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake na kuamua kutowaangamiza. Kwa sababu mwitikio wao kwa maneno na maagizo ya Mungu ulionyesha mtazamo ambao ulitofautiana kabisa na ule wa wananchi wa Sodoma, na kwa sababu ya utiifu wao wa dhati kwa Mungu na kutubu kwa uaminifu dhambi zao, pamoja na tabia yao ya kweli na ya dhati katika mambo yote, Mungu kwa mara nyingine tena alionyesha huruma Yake ya moyoni naye akaweza kuwapa. Kile ambacho Mungu huwapa binadamu na huruma Yake kwa binadamu haiwezekani kwa yeyote yule kuiga, na haiwezekani kwa mtu yeyote kumiliki huruma au uvumilivu wa Mungu, wala hisia Zake za dhati kwa binadamu. Je, yupo yeyote unayemwona kuwa mwanamume au mwanamke mkuu, au hata mwanadamu mkuu zaidi, ambaye angeweza, kutoka katika mtazamo mkuu, kuongea kama mwanamume au mwanamke mkuu au kwenye sehemu ya mamlaka ya juu, kutoa aina hii ya kauli kwa mwanadamu au viumbe? Ni nani miongoni mwa wanadamu anayeweza kujua hali za maisha ya binadamu kama viganja vya mikono yao? Ni nani anayeweza kubeba mzigo na jukumu la uwepo wa mwanadamu? Nani aliye na sifa ya kutangaza kuangamizwa kwa mji? Na ni nani aliye na sifa ya kuusamehe mji? Ni nani anayeweza kusema kwamba anauthamini uumbaji Wake wote? Ni Muumba pekee! Muumba pekee ndiye Anayethamini jamii hii ya wanadamu. Muumba pekee ndiye Anaewaonyesha wanadamu hawa huruma na upendo. Ni Muumba pekee ndiye aliye na upendo wa kweli, usioweza kutenganishwa kwa wanadamu hawa. Vivyo hivyo, ni Muumba pekee ndiye Anayeweza kuwahurumia wanadamu hawa, na kuvithamini viumbe Vyake vyote. Moyo Wake unavutwa na kuumizwa kwa kila kitendo cha mwanadamu: Anagadhibishwa, Anahuzunishwa na kuumizwa kwa uovu na upotovu wa mwanadamu; Anakuwa radhi, Anafurahishwa, Anasamehe na kushangilia kutokana na toba na imani ya mwanadamu; kila moja ya mawazo Yake na fikira Zake vipo kwa ajili ya wanadamu na yanawazunguka wanadamu; kile Alicho na Anacho kinaonyeshwa kikamilifu kwa ajili ya wanadamu; hisia Zake zote zinahusiana sana na uwepo wa wanadamu. Kwa ajili ya wanadamu, Anasafiri na kukimbia huku na kule; Anatoa kwa ukimya kila sehemu ya maisha Yake; na Anajitolea kila dakika na sekunde ya maisha Yake…. Hajawahi kujua jinsi ya kuyathamini maisha Yake Mwenyewe, lakini daima Amewatunza wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe…. Anatoa kila Alichonacho kwa wanadamu hawa…. Anatoa rehema na uvumilivu Wake bila masharti na bila kutarajia malipo. Anafanya hivi tu ili kwamba wanadamu waweze kuendelea kuishi mbele ya macho Yake, wakipokea utoaji Wake wa maisha. Anafanya hivi tu ili kwamba wanadamu waweze siku moja kujisalimisha mbele Zake na kutambua kwamba Yeye ndiye Anayetosheleza maisha ya wanadamu na kutoa uhai wa viumbe vyote.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
566. Rehema na uvumilivu wa Mungu kwa kweli vipo, lakini utakatifu na haki ya Mungu Anapoachilia hasira Yake pia inamwonyesha mwanadamu upande wa Mungu usiovumilia kosa lolote. Wakati binadamu anaweza kabisa kutii amri za Mungu na kutenda kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu ni mwingi wa huruma Zake kwa mwanadamu; wakati mwanadamu amejawa na upotovu, chuki na uadui kwake Yeye, Mungu anakuwa mwenye ghadhabu nyingi. Je, ni kwa kiwango gani Anakuwa amekasirika sana? Hasira yake itaendelea kuwepo mpaka pale ambapo Mungu hataona tena upinzani wa binadamu na matendo maovu, mpaka pale yatakapokuwa hayapo tena mbele ya macho Yake. Hapo tu ndipo ghadhabu ya Mungu itakapotoweka. Kwa maneno mengine, haijalishi mtu huyo ni nani, kama moyo wake umekuwa mbali na Mungu, na yeye amemkataa Mungu, asirudi tena, basi haijalishi ni vipi, kwa mwonekano wote au kuhusiana na matamanio yao binafsi, wanataka kumwabudu na kumfuata na kujinyenyekeza kwa Mungu katika miili yao au katika fikira zao, mara tu mioyo yao inapomwacha Mungu, ghadhabu ya Mungu itaachiliwa bila kikomo. Itakuwa kwamba wakati Mungu anapoiachilia kabisa ghadhabu Yake, akiwa amempa binadamu fursa za kutosha, mara tu inapoachiliwa hakutakuwepo na njia yoyote ya kuirudisha, na hatawahi tena kuwa mwenye huruma na mvumilivu kwa mtu kama huyo. Huu ni upande mmoja wa tabia ya Mungu isiyovumilia kosa. … Yeye ni mvumilivu na mwenye huruma kwa vitu vilivyo vyema, na vizuri na vya kupendeza; kwa vitu viovu, na vyenye dhambi, na vilivyojaa maovu, Yeye anayo hasira kali, kiasi cha kwamba Haachi kuendeleza hasira Yake. Hivi ndivyo vipengele viwili vikuu na vinavyojitokeza zaidi kuhusu tabia ya Mungu, na, zaidi, vimefichuliwa na Mungu kutoka mwanzo hadi mwisho: huruma nyingi na ghadhabu kuu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
567. Watu husema Mungu ni Mungu wa haki, na kwamba mradi tu mwanadamu atamfuata mpaka mwisho, basi Hatakuwa na upendeleo kwa mwanadamu, kwani Yeye ni mwenye haki. Je, mwanadamu akimfuata mpaka mwisho kabisa, Mungu anaweza kumtupa mwanadamu nje? Sina upendeleo kwa mwanadamu yeyote, na Huwahukumu wanadamu wote kwa tabia Yangu ya haki, ilhali kuna mahitaji yanayofaa Ninayohitaji kutoka kwa mwanadamu, na Ninahitaji yakamilishwe na wanadamu wote, bila kujali ni nani. Sijali jinsi sifa zako zilivyo nyingi au za kuheshimiwa; najali tu kama utatembea kwa njia Yangu, na kama unapenda na una kiu ya ukweli. Kama huna ukweli, na unaleta aibu katika jina Langu, na matendo yako ni kinyume cha njia Yangu, kufuata tu bila kujali, basi wakati huo nitakupiga na kukuadhibu kwa uovu wako, na utakuwa na nini la kusema? Utaweza kusema Mungu si mwenye haki? Leo kama umezingatia maneno ambayo nimenena, basi wewe ni mtu ambaye Namkubali. Unasema umeteseka kila wakati ukimfuata Mungu, kwamba umemfuata Yeye katika hali ngumu na mbaya, na umeshiriki Naye nyakati nzuri na mbaya, lakini hujaishi kulingana na maneno yaliyosemwa na Mungu; unataka tu kukimbia huku na kule kwa ajili ya Mungu na kujitumia kwa ajili ya Mungu kila siku, na hujafikiria kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Unasema pia, “Kwa vyovyote, naamini Mungu ni mwenye haki. Nimeteseka kwa ajili Yake, nikashughulika kwa ajili Yake, kujitoa kikamilifu Kwake, na nimefanya bidii ingawa sijapata kutambuliwa; Yeye hakika atanikumbuka.” Ni ukweli kwamba Mungu ni mwenye haki, na haki hii haijatiwa doa na uchafu wowote: Haina mapenzi ya binadamu, na haijatiwa doa na mwili, ama kitendo chochote cha binadamu. Wale wote ambao ni waasi na wako kwa upinzani, na hawazingatii njia Zake wataadhibiwa; hakuna atakayesamehewa, na hakuna atakayeepuka! Watu wengine husema, “Leo ninakimbia kwa ajili Yako; mwisho ukifika, utaweza kunipa baraka kidogo?” Sasa Nakuuliza, “Umezingatia maneno Yangu?” Haki unayoongelea inategemea matendo. Unafikiria kwamba Mimi ni mwenye haki, na asiye na mapendeleo kwa binadamu wote, na kwamba wale wanifuatao hadi mwisho wataokolewa na kupata baraka Yangu. Kuna maana ya ndani kwa maneno Yangu kwamba “wale wote wanifuatao hadi mwisho wataokolewa”: Wale wanifuatao mpaka mwisho ndio Nitakaowapata, ni wale, baada ya kushindwa Nami, watautafuta ukweli na kufanywa wakamilifu. Ni hali gani umepata? Umepata kunifuata hadi mwisho, lakini nini kingine? Je, umezingatia maneno Yangu? Umekamilisha moja kati ya tano ya mahitaji Yangu, ilhali huna mpango wa kumaliza manne yaliyobaki. Umepata ile njia rahisi, na ukaifuatilia ukiwa na mtazamo wa kutumaini kuwa utabahatika. Kwa mtu kama wewe, haki Yangu ni kuadibu na hukumu, ni adhabu ya haki, na ni adhabu ya haki kwa watenda maovu wote; wale wote wasiotembea kwa njia Yangu wataadhibiwa, hata kama watafuata mpaka mwisho. Hii ndio haki ya Mungu. Wakati tabia hii ya haki inapodhihirishwa katika adhabu ya mwanadamu, mwanadamu atakosa la kusema, na kujuta kwamba, alipokuwa akimfuata Mungu hakutembea katika njia Yake. “Wakati huo niliteseka kidogo tu nikimfuata Mungu, lakini sikutembea katika njia ya Mungu. Kuna udhuru gani? Hakuna namna ila kuadibiwa!” Ila kwa akili yake anafikiria, “Nimefuata hadi mwisho, hata Ukiniadibu haitakuwa adabu kali, na baada ya kuadibu kwa kuchosha, bado Utanihitaji. Najua Wewe ni mwenye haki, na Hutanifanyia hivyo milele. Mimi si kama wale watakaofagiliwa nje; wale watakaofagiliwa watapokea adabu kuu, na adabu Yangu itakuwa kidogo.” Adabu ya Mungu ya tabia ya haki si unavyosema. Sio kwamba wale ambao wanatubu dhambi zao kila wakati wataadibiwa kwa huruma. Haki ni utakatifu, na ni tabia ambayo haivumilii makosa ya mwanadamu, na yale yote ambayo ni machafu na hayajabadilika ndiyo shabaha ya chukizo kwa Mungu. Haki ya Mungu si sheria, lakini amri ya utawala: Ni amri ya utawala katika ufalme, na hii amri ya utawala ni adhabu ya haki kwa yeyote asiye na ukweli na hajabadilika, na hakuna kiwango cha wokovu. Mwanadamu akiwekwa kulingana na aina, wazuri watazawadiwa na wabaya kuadhibiwa. Ndio wakati hatima ya mwanadamu itawekwa wazi, na ndio ni wakati ambao kazi ya wokovu itafika mwisho, baada ya hapo, kazi ya kuokoa binadamu haitafanyika tena, na adabu italetwa kwa wale waliotenda maovu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu
568. Huruma Yangu inaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima. Kwa sasa, adhabu itakayowapata waovu, ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, hata zaidi, ushuhuda wa ghadhabu Yangu. Maafa yatakapokuj, njaa na tauni zitawapata wale wote wanaonipinga na watalia. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima. Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia matendo yake maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa nikitamani kwa hamu kupata kundi la watu wenye nia moja na Mimi. Wale ambao hawana nia moja na Mimi, wakati huo huo, Siwasahau kamwe; Ninawachukia kabisa moyoni Mwangu daima, Nikisubiri nafasi ya kutoa adhabu kwao, jambo ambalo Nitafurahia kuona. Sasa siku Yangu imefika hatimaye, na Sihitaji kusubiri zaidi!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako