C. Kuhusu Utakatifu wa Mungu
569. Mungu alifanyika mwili katika mahali pa nyuma kimaendeleo na pachafu zaidi, na ni kwa njia hii tu ambapo Mungu anaweza kuonyesha kwa uwazi ukamilifu wa tabia Yake takatifu na ya haki. Na tabia Yake yenye haki inaonyeshwa kupitia nini? Inaonyeshwa Anapozihukumu dhambi za mwanadamu, Anapomhukumu Shetani, Anapochukia dhambi sana, na Anapowadharau maadui wanaompinga na kuasi dhidi Yake. Maneno Ninayonena leo ni kwa ajili ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, kuhukumu udhalimu wa mwanadamu, kulaani uasi wa mwanadamu. Upotovu na udanganyifu wa mwanadamu, maneno na vitendo vya mwanadamu—yote ambayo hayapatani na mapenzi ya Mungu lazima yatapitia hukumu, na uasi wote wa mwanadamu kushutumiwa kama dhambi. Maneno Yake yanahusu kanuni za hukumu; Yeye hutumia hukumu ya udhalimu wa mwanadamu, laana ya uasi wa mwanadamu, na mfichuo wa asili mbaya za mwanadamu ili kudhihirisha tabia Yake mwenyewe yenye haki. Utakatifu ni kielelezo cha tabia Yake yenye haki, na kwa kweli utakatifu wa Mungu ni tabia Yake yenye haki. Tabia zenu potovu ni muktadha wa maneno ya leo—Ninazitumia kunena na kuhukumu, na kutekeleza kazi ya ushindi. Hii pekee ndiyo kazi halisi, na hii pekee inadhihirisha kabisa utakatifu wa Mungu. Ikiwa hakuna dalili ya tabia potovu ndani yako, basi Mungu hatakuhukumu, wala hatakuonyesha tabia Yake yenye haki. Kwa kuwa unayo tabia potovu, Mungu hatakusamehe, na ni kwa njia hii ndiyo utakatifu Wake unaonyeshwa. Mungu angaliona kuwa uchafu na uasi wa mwanadamu vilikuwa vikubwa sana lakini Asinene au kukuhukumu, wala kukuadibu kwa ajili ya udhalimu wako, basi hii ingethibitisha kwamba Yeye si Mungu, kwa maana Asingeichukia dhambi; Angelikuwa mchafu sawasawa na mwanadamu. Leo, ni kwa sababu ya uchafu wako ndiyo Ninakuhukumu, na ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako ndiyo Ninakuadibu. Mimi sijivunii nguvu Zangu kwenu au kuwadhulumu kwa makusudi; Ninafanya mambo haya kwa sababu ninyi, ambao mmezaliwa katika nchi hii ya uchafu, mmenajisiwa vikali kwa uchafu. Mmepoteza uadilifu na ubinadamu wenu kabisa na mmekuwa kama nguruwe waliozaliwa katika pembe chafu zaidi za ulimwengu, na kwa hiyo ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mnahukumiwa na kwamba Ninaaachilia ghadhabu Yangu juu yenu. Ni kwa sababu hasa ya hukumu hii ndiyo mmeweza kuona kuwa Mungu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba Mungu ndiye Mungu mtakatifu; ni kwa sababu hasa ya utakatifu Wake na haki Yake ndiyo Anawahukumu na kuachia huru hasira Yake juu yenu. Kwa sababu Anaweza kufichua tabia Yake yenye haki Aonapo uasi wa mwanadamu, na kwa sababu Anaweza kufichua utakatifu Wake anapoona uchafu wa mwanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na wa asili, na bado Anaishi katika nchi ya uchafu. Mungu angelikuwa mtu na kufuata mfano wa mwanadamu na kugaagaa na wanadamu katika matope machafu, basi kusingelikuwa na chochote kitakatifu kumhusu, na Asingelikuwa na tabia yenye haki, na kwa hiyo Asingelikuwa na haki ya kuhukumu uovu wa mwanadamu, wala Asingelikuwa na haki ya kutekeleza hukumu ya mwanadamu. Mtu angelimhukumu mtu mwingine, haingekuwa kana kwamba anajipiga kofi usoni? Watu ambao wote ni wachafu kwa kiwango sawa wanastahili vipi kuwahukumu wale ambao ni sawa na wao? Ni Mungu mtakatifu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu. Mwanadamu angewezaje kuhukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na mwanadamu angewezaje kuwa na sifa za kulaani dhambi hizi? Mungu Asingelikuwa na sifa ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki Mwenyewe? Tabia potovu za watu zinapofichuliwa, Mungu hunena ili Awahukumu watu, na ni hapo tu ndipo watu wanapoona kuwa Yeye ni mtakatifu. Anapomhukumu na kumwadibu mwanadamu kwa ajili ya dhambi zake, wakati huo wote Akizifichua dhambi za mwanadamu, hakuna mtu au kitu kinachoweza kuepuka hukumu hii; mambo yote ambayo ni machafu yanahukumiwa na Yeye, na ni kwa sababu hiyo tu ndiyo tabia Yake inaweza kusemwa kuwa yenye haki. Kama ingekuwa vinginevyo, ingewezaje kusemwa kwamba ninyi ni foili kwa jina na kwa kweli?
… Ni kupitia watu ambao wanatoka katika nchi ya uchafu ndipo utakatifu wa Mungu unaonyeshwa; leo, Yeye hutumia uchafu ulioonyeshwa katika watu hawa wa nchi ya uchafu, naye Anahukumu, na kwa kufanya hivyo, kile Alicho kinafichuliwa katika hukumu Yake. Kwa nini Anahukumu? Anaweza kunena maneno ya hukumu kwa sababu Anadharau dhambi; Je, Angewezaje kukasirika sana hivyo ikiwa hakuchukia uasi wa wanadamu? Kusingekuwa na karaha ndani Yake, kusingekuwa na machukio, Asingejali uasi wa watu, basi hiyo ingethibitisha Yeye kuwa mchafu kama mwanadamu. Kwamba Yeye anaweza kumhukumu na kumwadibu mwanadamu ni kwa sababu Yeye huchukia uchafu, na Anachokichukia hakimo ndani Yake. Kama pia kungekuwa na upinzani na uasi ndani Yake, Asingewadharau wale ambao ni wapinzani na waasi. Kazi ya siku za mwisho ingekuwa ikifanywa Israeli, hakungekuwa na maana yoyote kwayo. Mbona kazi ya siku za mwisho inafanywa nchini China, mahali paovu na palipo nyuma kabisa kimaendeleo kuliko sehemu zote? Ni ili kuonyesha utakatifu na haki Yake. Kwa kifupi, kadri mahali palivyo paovu, ndivyo utakatifu wa Mungu unavyoweza kuonyeshwa wazi zaidi. Kwa kweli, yote haya ni kwa ajili ya kazi ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa
570. Kwa muda mrefu Nimeona waziwazi matendo mbalimbali ya pepo wabaya. Na watu wanaotumiwa na pepo wabaya (wale wenye nia mbaya, wale wanaotamani mwili au utajiri, wale wanaojikuza, wale wanaolivuruga kanisa, nk.) kila mmoja wao pia amebainika na Mimi. Usifikiri kwamba kila kitu kimemalizika punde pepo wabaya watatupwa nje. Hebu Nikwambie! Kuanzia sasa na kuendelea, Nitawaondoa watu hawa mmoja baada ya mwingine, nisiwatumie kamwe! Yaani, mtu yeyote aliyepotoshwa na pepo wabaya hatatumiwa na Mimi, na atafukuzwa! Usifikiri kuwa Sina hisia! Fahamu jambo hili! Mimi ndimi Mungu mtakatifu, na Sitakaa katika hekalu chafu! Mimi huwatumia tu watu waaminifu na wenye hekima ambao ni waaminifu kabisa Kwangu na wanaoweza kuudhukuru mzigo Wangu. Hii ni kwa sababu watu kama hao walijaaliwa na Mimi, na bila shaka hakuna pepo wabaya wanaowafanyia kazi hata kidogo. Hebu Nieleze wazi jambo moja: Kuanzia sasa na kuendelea, wale wote ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wana kazi ya pepo wabaya. Hebu Nirudie: Simtaki hata mtu mmoja ambaye pepo wabaya humfanyia kazi. Wote watatupwa kuzimuni pamoja na miili yao!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 76
571. Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe. Roho wa Mungu ni mwenye mamlaka; Yeye ni mwenye uweza, mtakatifu, na mwenye haki. Vivyo hivyo, mwili Wake pia ni wenye mamlaka, wenye uweza, mtakatifu, na wenye haki. Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile ambacho ni cha haki na chenye faida kwa wanadamu, kile ambacho ni kitakatifu, kitukufu na chenye nguvu; Yeye hawezi kutenda jambo lolote ambalo linakiuka ukweli, ambalo linakiuka maadili na haki, sembuse kufanya jambo lolote linaloweza kumsaliti Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni mtakatifu, na kwa hivyo mwili Wake hauwezi kupotoshwa na Shetani; mwili Wake ni wenye kiini tofauti na mwili wa mwanadamu. Kwa maana ni mwanadamu na si Mungu, ambaye anapotoshwa na Shetani; Shetani hawezi kamwe kuupotosha mwili wa Mungu. Kwa hiyo, licha ya ukweli kwamba mwanadamu na Kristo wanaishi katika sehemu sawa, ni mwanadamu tu ndiye anayemilikiwa, anayetumiwa, na anayenaswa na Shetani. Kinyume na hilo, Kristo hawezi kuathiriwa kabisa na upotovu wa Shetani, kwa sababu Shetani hatawahi kuweza kupanda hadi mahali pa juu zaidi, na hatawahi kuweza kumkaribia Mungu. Leo, nyote mnapaswa kuelewa kuwa ni wanadamu tu, waliopotoshwa na Shetani, ndio wanaonisaliti. Usaliti hautawahi kuwa suala linalomhusisha Kristo hata kidogo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)
572. Mungu Mwenyewe hana mambo ya kuasi; dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote. Hata katika mwili, Mungu hafanyi lolote linalomuasi Mungu Baba. Hata kwa gharama ya kutoa sadaka maisha Yake, Angekuwa kwa ukamilifu tayari na kutofanya uchaguzi mwingine. Mungu hana vipengele vya kujihesabia haki na kujiona kuwa muhimu, au vile vya majivuno na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na zile za Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelaghaiwa na kushughulikiwa na Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni
573. Utakatifu wa Mungu” unamaanisha kuwa kiini cha Mungu hakina dosari, kwamba upendo wa Mungu hauna ubinafsi, yote ambayo Mungu humpa mwanadamu hayana ubinafsi; na utakatifu wa Mungu hauna dosari wala haushutumiki. Hivi viini vya Mungu si maneno tu ambayo Yeye hutumia kuonyesha utambulisho Wake, bali Mungu hutumia kiini Chake kwa kimya na kwa dhati kushughulika na kila mtu. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu si tupu, wala si cha nadharia au mafundisho ya dini na hakika si aina ya maarifa. Si aina ya elimu kwa mwanadamu, lakini badala yake ni ufunuo wa kweli wa matendo ya Mungu mwenyewe na ni kiini ambacho kimefichuliwa cha kile Mungu anacho na alicho.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
574. Utakatifu wa Mungu ninaozungumzia unarejelea nini? Lifikirie kidogo. Je, ukweli wa Mungu ni utakatifu Wake? Je, uaminifu wa Mungu ni utakatifu Wake? Je, kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu ni utakatifu Wake? Je, unyenyekevu wa Mungu ni utakatifu Wake? Je, upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni utakatifu Wake? Mungu humpa mwanadamu ukweli na uhai bure—huu ni utakatifu Wake? Naam, yote ni sahihi. Yote haya ambayo Mungu anafichua ni ya kipekee; hayapo ndani ya ubinadamu mpotovu, wala hayawezi kuonekana hapo. Hakuna hata chembe ya hayo yanaweza kuonekana katika mchakato wa upotovu wa Shetani kwa mwanadamu, wala katika tabia potovu ya Shetani wala katika kiini ama asili ya Shetani. Chote ambacho Mungu Anacho na Alicho ni ya kipekee na Mungu tu Mwenyewe anacho kiini cha aina hii, ni Mungu Mwenyewe tu anamiliki kiini cha aina hii. … Kiini cha utakatifu ni upendo wa kweli, lakini hata zaidi ya hili ni kiini cha ukweli, cha haki na mwanga. Neno “takatifu” linafaa tu linapotumika kwa Mungu; hakuna chochote katika uumbaji kinachostahiki kuitwa kitakatifu. Mwanadamu lazima aelewe hilo.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
575. Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utuu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Hata ingawa Alizaliwa katika nchi yenye uchafu, na ingawa Anaishi na watu hao ambao wamejawa uchafu, kama vile Yesu alivyoishi na wenye dhambi katika Enzi ya Neema, si kazi Yake yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote? Je, si yote ni ili mwanadamu aweze kuupata wokovu mkuu? Miaka elfu mbili iliyopita Aliishi na wenye dhambi kwa miaka kadhaa. Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya ukombozi. Leo, Anaishi na kikundi cha watu wachafu, wa hali ya chini. Hii ni kwa ajili ya wokovu. Je, si kazi Yake yote ni kwa ajili yenu, wanadamu hawa? Kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeishi na kuteswa pamoja na wenye dhambi kwa miaka mingi sana baada ya kuzaliwa horini? Na kama si kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angerudi katika mwili mara ya pili, kuzaliwa katika nchi hii ambako mapepo hukusanyika, na kuishi na watu hawa ambao wamepotoshwa kwa kina na Shetani? Je, si Mungu ni mwaminifu? Ni aina gani ya kazi Yake ambayo haijakuwa kwa ajili ya wanadamu? Ni aina gani ambayo haijakuwa kwa ajili ya kudura yako? Mungu ni mtakatifu. Hili haliwezi kubadilika! Yeye hanajisiwi na uchafu, ingawa Amekuja katika nchi yenye uchafu; yote haya yanamaanisha tu kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wenye kuwajali wengine sana, mateso na aibu Anayoyavumilia ni makubwa sana!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu
576. Fikira zako, mawazo yako, tabia yako, maneno na matendo yako—si kila kitu unachoonyesha katika namna unavyoishi ni foili kwa haki na utakatifu wa Mungu? Si kile kinachofunuliwa katika maneno ya leo ni tabia potovu ya mwanadamu? Fikira zako, motisha zako—yote ambayo yamefunuliwa ndani yako yanaonyesha tabia ya Mungu yenye haki na utakatifu Wake. Mungu pia Alizaliwa katika nchi ya uchafu, lakini Anabaki kutopakwa matope na uchafu. Anaishi katika ulimwengu huo huo mchafu kama wewe, lakini Anayo mantiki na utambuzi, naye huchukia uchafu. Huenda usiweze hata kugundua kitu chochote kilicho kichafu katika maneno na vitendo vyako, lakini Yeye anaweza, na Yeye hukuonyesha kitu hicho. Mambo hayo yako ya zamani—ukosefu wako wa ukuzaji, utambuzi, na akili, na njia zako za kuishi za kuelekea nyuma—sasa vimedhihirishwa na ufunuo wa leo; ni kwa Mungu kuja duniani kufanya kazi tu ndipo watu wanaona utakatifu Wake na tabia Yake yenye haki. Yeye hukuhukumu na kukuadibu, Akikusababisha upate ufahamu; wakati mwingine, asili yako ya kishetani inadhihirishwa, na Yeye hukuonyesha asili hiyo. Anajua kiini cha mwanadamu vyema sana. Anaishi miongoni mwenu, Anakula chakula sawa na nyinyi, na Anaishi katika mazingira yale yale—lakini hata hivyo, Anajua zaidi; Anaweza kukufichua na kuona kupitia kiini potovu cha ubinadamu. Hakuna kitu Anachodharau zaidi ya falsafa za mwanadamu za kuishi na upotovu na udanganyifu. Yeye anadharau mambo haya na hataki kuyatilia maanani hata kidogo. Anachukia hasa maingiliano ya kimwili ya mwanadamu. Huenda Asijue baadhi ya mazoea ya maingiliano ya binadamu, lakini Anajua kabisa watu wanapofichua tabia potovu. Yeye hufanya kazi ili kuongea na kumfundisha mwanadamu kupitia mambo haya, Yeye hutumia mambo haya ili Awahukumu watu, na kuonyesha tabia Yake mwenyewe yenye haki na takatifu. Hivyo, watu wanakuwa foili kwa kazi Yake. Ni Mungu mwenye mwili tu ndiye Anayeweza kuweka wazi tabia potovu za mwanadamu na sura zote mbaya za Shetani. Kwa kufanya hivi, Yeye hakuadhibu, lakini badala yake Anakutumia tu kama foili kwa ajili ya utakatifu Wake, na huwezi kusimama imara, kwa sababu wewe ni mchafu sana. Yeye huzungumza Akitumia mambo hayo ambayo yamefunuliwa ndani ya mwanadamu, na ni wakati ambapo mambo haya yanawekwa wazi tu ndipo watu wanajua jinsi Mungu alivyo mtakatifu. Yeye hapuuzi uchafu hata kidogo ndani ya watu, hata mawazo machafu yaliyo mioyoni mwao; ikiwa maneno na matendo ya watu hayapatani na mapenzi Yake, basi Yeye hawasamehi. Katika maneno Yake, hakuna nafasi ya uchafu wa wanadamu au kitu kingine chochote—lazima yote yafunuliwe.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa
577. Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno Alilolisema na kila hatua Aliyoichukua inahusiana na ukweli. Ukweli huu sio tu ndoto isiyo na msingi; ukweli huu na maneno haya yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu ambacho Mungu amefanya ni ukweli, tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vizuri na uhalisi wa vitu hivyo vizuri, na inaelekeza njia kwa ajili ya wanadamu ili waweze kutembea katika njia sahihi. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
578. Unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kumwamini Mungu; unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kutambua maana halisi ya maneno haya “Mungu Mwenyewe, wa Kipekee.” Hutafikiria tena kwamba unaweza kuchagua kutembea njia zingine, na hutakuwa tena radhi kusaliti kila kitu ambacho Mungu amekupangia. Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka katika ukweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwenye madhara na udhibiti wa Shetani. Kando na Mungu, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuokoa kutoka kwa bahari ya mateso, ili usiteseke tena: Hili linaamuliwa na kiini cha Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu hukuokoa bila ubinafsi wowote, ni Mungu pekee anayehusika na maisha yako ya baadaye, na hatima yako na maisha yako, na Yeye anapanga mambo yote kwa ajili yako. Hili ni jambo ambalo hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kinaweza kutimiza. Kwa sababu hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kina kiini cha Mungu kama hiki, hakuna mtu au kitu chenye uwezo wa kukuokoa au kukuongoza wewe. Huu ndio umuhimu wa kiini cha Mungu kwa mwanadamu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
579. Kwa muda huu wote, Nimemweka mwanadamu katika nidhamu ya hali ya juu. Iwapo uaminifu wako unakuja na nia na masharti, basi ni heri Nisijihusishe na huo mnaoita uaminifu wenu hata kidogo, kwa maana Ninachukia wale hunidanganya kupitia kwa nia zao na kunanihadaa kwa masharti. Natamani tu mwanadamu awe mwaminifu kabisa Kwangu, na afanye mambo yote kwa ajili ya, na kudhibitisha neno hilo moja: imani. Ninachukizwa na matumizi yenu ya maneno matamu ili Unifurahishe Mimi. Kwa maana daima Mimi napenda mtende pia kwa ukweli mtupu na uwazi na hivyo Natamani pia mnitendee Mimi kwa imani ya kweli.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?
580. Ni lazima ujue ni watu wa aina gani ambao Ninataka; wale walio wachafu hawaruhusiwi kuingia katika ufalme, wale walio wachafu hawaruhusiwi kuchafua nchi takatifu. Ingawa unaweza kuwa umefanya kazi nyingi, na kufanya kazi kwa miaka mingi, mwishowe kama bado wewe ni mchafu kupindukia, kisha itakuwa haivumiliki kwa sheria ya Mbinguni kwamba unataka kuingia katika ufalme Wangu! Tangu mwanzo wa dunia hadi leo, kamwe Sijawahi kutoa njia rahisi ya kuingia katika ufalme Wangu kwa wale wanaojipendekeza Kwangu. Hii ni sheria ya Mbinguni, na hakuna awezaye kuivunja. Ni lazima utafute uzima. Leo, wale watakaofanywa wakamilifu ni wa aina sawa na Petro: ni wale ambao wanatafuta mabadiliko katika tabia zao wenyewe, na wako tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutekeleza wajibu wao kama kiumbe wa Mungu. Ni watu kama hawa pekee ndio watakaofanywa wakamilifu. Kama wewe unatazamia tu tuzo, na hutafuti kubadilisha tabia ya maisha yako mwenyewe, basi juhudi zako zote zitakuwa za bure—na huu ni ukweli usiobadilika!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
581. Mungu Mwenyewe ana milki na nafsi Yake. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukifichua ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Kila Alicho na anacho, pamoja na dutu na utambulisho Wake vyote ni vitu ambavyo haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, faraja kwa binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa binadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini chanya, changamfu, au isiyo na hisia. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai, na Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukuu, na zaidi ya yote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Zaidi ya hayo, tabia Yake ni ishara ya Yeye kutoweza kushindwa au kushambuliwa na giza au na nguvu yoyote ya adui, pamoja na ishara ya Yeye kutoweza kukosewa (wala Hatavumilia kukosewa) na kiumbe chochote kilichoumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wenye uwezo au wanaoweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini sifa bainifu za mwanadamu ishara tu ya mamlaka madogo ya mwanadamu juu ya mnyama. Mwanadamu ndani yake na kwake hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuenda zaidi ya nafsi, lakini katika kiini chake ni mtu ambaye anajinyenyekeza chini ya kila aina ya watu, matukio, na vitu. Furaha ya Mungu inatokana na kuwepo na kuzuka kwa haki na nuru; kwa sababu ya uharibifu wa giza na uovu. Anafurahi kwa sababu Ameleta nuru na maisha mazuri kwa wanadamu; Furaha Yake ni furaha ya haki, ishara ya kuwepo kwa yote ambayo ni chanya na, hata zaidi, ishara ya fanaka. Ghadhabu ya Mungu ni n kwa sababu ya madhara ambayo kuwepo na kuingiliwa kwa dhulma kunaleta juu ya binadamu Wake, kwa sababu ya kuwepo kwa uovu na giza, kwa sababu ya kuwepo kwa vitu vinavyofukuza ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya kuwepo kwa vitu vinavyopinga vitu vilivyo vyema na vizuri. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote hasi havitakuwepo tena, na hata zaidi ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya wanadamu, ambao Amekuwa na matumaini nao lakini ambao wameanguka katika giza, ni kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya wanadamu wasio na hatia, kwa sababu ya yule ambaye ni mwaminifu lakini ni mjinga, na kwa sababu yule mwanadamu mzuri lakini ana upungufu katika maoni yake mwenyewe. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya uzuri na ukarimu. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda maadui Zake na kupata imani nzuri ya mwanadamu. Zaidi ya hayo, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na kwa sababu wanadamu wamepokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na raha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko raha. Furaha Yake ni ishara ya wanadamu kuwa huru dhidi ya mateso kuanzia wakati huu na kuendelea, na ni ishara ya wanadamu kuingia katika ulimwengu wenye mwanga. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote huibuka kwa ajili ya masilahi yake mwenyewe, na wala si kwa ajili ya haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, sembuse neema inayotolewa na Mbingu. Hisia za wanadamu zina ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo hazipo kwa ajili ya mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo mwanadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa kwa njia sawa. Mungu ni mkuu milele na Anaheshimiwa milele, ilhali mwanadamu siku zote ni wa chini, siku zote hana thamani. Hii ni kwa sababu daima Mungu anajitoa na kugharimika kwa ajili ya wanadamu, ilhali mwanadamu daima anatafuta na kujitahidi kwa ajili yake mwenyewe. Mungu daima anajitaabisha kwa ajili ya kuwepo kwa wanadamu, ilhali mwanadamu hachangii chochote kamwe kwa ajili ya haki au nuru, na hata kama mwanadamu atafanya jitihada ya muda, yeye ni dhaifu sana hawezi kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake mwenyewe na wala si kwa ajili ya wengine. Mwanadamu siku zote ni mbinafsi, wakati Mungu hana ubinafsi milele. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo vya haki, vyema, na vizuri, huku naye mwanadamu ni yule anayerithi na kudhihirisha vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na uzuri, ilhali mwanadamu anaweza kabisa, wakati wowote, kuisaliti haki na kujiweka mbali na Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu
582. Mungu kutoweza kuvumilia kosa ndicho kiini Chake cha kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; ukuu wa Mungu ndiyo kiini Chake cha kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Ni dhahiri kwamba pia ni ishara ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ni asili Yake Mwenyewe, ambayo haibadiliki hata kidogo na kupita kwa wakati, na wala haibadilishwi na mabadiliko ya eneo la kijiografia. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Bila kujali ni nani Anayemfanyia kazi Yake juu yake, kiini Chake hakibadiliki, na wala tabia Yake ya haki haibadiliki. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika kiini Chake au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini ni kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake huikosea tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anaijaribu ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapoijaribu mara kwa mara ghadhabu ya Mungu—na pia wakati ambapo dhambi inaenea—ghadhabu ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitakoma kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote za adui zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu unapopingwa, wakati nguvu za haki zinapozuiliwa na kutoonekana na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya kiini cha Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na zinapozuiliwa na kutoonekana na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu Asiye na dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II