116 Upendo wa Mungu Huuamsha Moyo Wangu

Shetani ameipotosha roho yangu, mimi ni mwenye majivuno na bure sana.

Shetani ameyatia sumu mawazo yangu,

Natamani kumpenda Mungu lakini napungukiwa, eh, lakini napungukiwa.

Hukumu ya maneno ya Mungu hunifanya nijijue.

Nimepotoka sana kiasi kwamba hakuna sehemu yangu iliyo nzuri.

Hakuna dhamiri, hakuna akili, hakuna heshima iliyobaki.

Bila wokovu, ningeweza kuishi kama mtu aliyekufa.

Mungu anakabili hatari kufanya kazi na kutuokoa.

Anatuhukumu kwa maneno,

huzifanya upya roho zetu potovu, basi maisha yetu yana thamani.

Nitavumilia yote yanayopaswa kuvumiliwa, nitoe ibada yangu ya mwisho.

Nitakuwa mtu mwaminifu, na sitatoa madai yoyote.

Nimebarikiwa, Mungu ananiinua, ili niweze kutekeleza wajibu wangu.

Lakini namkaidi na kuumaliza kwa kubahatisha,

eh, kuumaliza kwa kubahatisha.

Maneno ya Mungu yanifunua, na naona asili yangu ya kishetani.

Najichukia zaidi kwa sababu ya upotovu wangu wa kina.

Sina dhamiri wala akili, siwezi kuufariji moyo wa Mungu.

Lakini Ananionea huruma na kuniokoa mara kwa mara.

Mungu anakabili hatari kufanya kazi na kutuokoa.

Anatuhukumu kwa maneno,

huzifanya upya roho zetu potovu, basi maisha yetu yana thamani.

Nitavumilia yote yanayopaswa kuvumiliwa, nitoe ibada yangu ya mwisho.

Nitakuwa mtu mwaminifu, na sitatoa madai yoyote.

Kupitia hukumu ya Mungu na usafishaji Wake, hatimaye nimetakaswa;

Nimeona jinsi wokovu wa Mungu ulivyo wa kweli na halisi!

Kwa sababu ya uvumilivu mkubwa wa Mungu, naweza kuurejesha upendo Wake.

Lakini nafahamu nikiwa nimechelewa, deni langu ni kubwa sana.

Mungu anakabili hatari kufanya kazi na kutuokoa.

Anatuhukumu kwa maneno,

huzifanya upya roho zetu potovu, basi maisha yetu yana thamani.

Nitavumilia yote yanayopaswa kuvumiliwa, nitoe ibada yangu ya mwisho.

Nitakuwa mtu mwaminifu, na sitatoa madai yoyote.

Iliyotangulia: 115 Nimeuona Upendo wa Mungu

Inayofuata: 117 Nitalipa Upendo wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki