74 Hukumu na Kuadibu kwa Mungu ni ili Kumwokoa Mwanadamu

1 Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Wokovu uliopewa leo unatokea wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa.

2 Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo?

3 Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? Nyote mmeona Mungu mwenye mwili na kutambua kudura na hekima Yake; zaidi ya hayo, umepitia hali ya kupigwa na kufundishwa nidhamu mara kwa mara. Lakini je, hujapokea pia neema kubwa?

4 Je, baraka zako si kubwa zaidi kuliko za mtu yeyote mwingine? Neema zako ni nyingi zaidi kuliko utukufu na utajiri uliofurahiwa na Sulemani! Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, kuwaadhibu ninyi wanadamu wa kufa hakuwezi kufanywa kwa kutamka neon moja tu? Ningekuwa bado na haja ya kuwaangamiza baada ya kuwashutumu kwa makusudi? Je, bado hamwamini haya maneno Yangu?

Umetoholewa kutoka katika “Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 73 Hukumu na Kuadibu Vinafichua Wokovu wa Mungu

Inayofuata: 75 Hukumu ya Neno la Mungu ni Kumwokoa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp