33 Hukumu ya Mungu Inafichuliwa Kabisa

1 Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami. Wale wasiosikiza kile Ninachosema na hawatendi maneno Yangu wanahukumiwa vikali na kupokea laana ya ghadhabu Yangu. Sauti Yangu ni hukumu na ghadhabu, nami si mpole kwa yeyote na simwonei mtu yeyote huruma, kwa kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki Mwenyewe, na Mimi ni mwenye ghadhabu, Nina kuchoma, utakaso, na maangamizo.

2 Ndani Yangu, hakuna kitu kilichofichika, au chenye mhemuko, lakini badala yake, kila kitu kiko wazi, chenye haki, na kisicho na upendeleo. Kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza tayari wako nami katika kiti cha enzi, wakitawala mataifa yote na watu wote, yale mambo na watu walio dhalimu na waovu wanaanza kuhukumiwa. Nitawafanyia uchunguzi mmoja baada ya mwingine, bila kukosa kitu chochote, Nikiwafichua kabisa. Kwa kuwa hukumu Yangu imefichuliwa kikamilifu na imefunguliwa kikamilifu, na hakuna chochote ambacho kimebakizwa; Nitatupa chochote kisichokubaliana na mapenzi Yangu na kukisababisha kiangamie kuzimu milele; Nitakisababisha kiungue kuzimu milele. Hii ni haki Yangu; huu ni uaminifu Wangu. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha hili, na lazima kinitii.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 103” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 32 Mungu Anashuka Na Hukum

Inayofuata: 34 Hukumu ya Mungu Yenye Haki Inakaribia Ulimwengu Mzima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp