257 Moyo wa Mungu Haujaliwazwa Bado

1

Baada ya kuonja uchungu kamili wa kupotoshwa kwa mwili, ninamchukia na kumkirihi Shetani hata zaidi.

Maneno ya Mungu yananifunua na kunihukumu vikali, sasa ninaona wazi ukweli wa upotovu wangu mwenyewe.

Kwa kukubali hukumu na usafishaji wa Mungu napata utakaso, na ni hapo tu ndipo najua kwamba wanadamu lazima afuatilie ukweli katika maisha yao.

Ninaona kwamba kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu si rahisi. Kwa dhamiri na mantiki, ninapaswa kumtii Mungu.

Mungu huumia sana kwa ajili ya mwanadamu, hata leo bado Hajapata upendo wake.

Nahisi hatia na kujikaripia moyoni mwangu; nisipoulipa upendo wa Mungu, basi mimi sistahili kuitwa mwanadamu.

Mungu anasubiri mwanadamu atubu. Siwezi tena kushusha hali na kuishi maisha matupu.

Sijapata ukweli au kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu, hivyo nawezaje kukata tamaa kwa urahisi?

2

Kazi ya Mungu itafika mwisho, sijakuwa bado na mabadiliko mengi katika tabia yangu.

Bila uhalisi wa ukweli, niwezaje kusimama imara? Ninawezaje kuyatuliza mawazo ya Mungu na kupata uaminifu Wake?

Sijakaribia kile ambacho Mungu anahitaji, nawezaje kumridhisha Mungu ikiwa sitendi kweli?

Moyo wa Mungu haujaliwazwa, ninapaswa kumuishia Mungu ili kulipa fadhila Yake.

Ili kuuridhisha moyo wa Mungu, niko radhi kuteseka machungu yoyote.

Na nikimwangusha Mungu, nitajuta maisha yangu yote na nitakuwa na aibu sana kukutana na Yeye.

Kama mwanadamu, ni lazima nichukue msimamo na nisimfadhaishe Mungu tena.

Natamani kila mara kuigeukia haki, kumpenda na kujitolea milele kwa Mungu, na nikiwa na ukweli tu ndiyo nastahili kuitwa mwanadamu.

Iliyotangulia: 256 Jinsi ya Kurudisha Wokovu Uliopotea

Inayofuata: 258 Nimeamua Kumpenda Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp