141 Tabia ya Mungu Inaonekana Katika Kila Hatua ya Kazi Yake

1 Kwa hivyo, kazi iliyofanywa na Mungu mwenyewe kwa kila enzi ina dhihirisho la tabia Yake ya ukweli, na jina Lake na kazi anaofanya hubadilika na enzi—zote ni mpya. Wakati wa Enzi ya Sheria, kazi ya kumwelekeza mwanadamu ilifanyika katika Jina la Yehova, na awamu ya kwanza ya kazi ilifanyika duniani. Kazi ya awamu hii ilikuwa ni kujenga hekalu na madhabahu, na kutumia sheria kuwaongoza watu wa Israeli na kufanya kazi miongoni mwao. Kwa msingi huu, Yeye Alipanua kazi yake nje ya Israeli, ambayo ni kusema kwamba, kuanzia Israeli, Aliendeleza kazi yake nje, ili vizazi vya baadaye walikuja kujua polepole kwamba Yehova Alikuwa Mungu, na kuwa Yehova Alikuwa Ameumba mbingu na nchi na vitu vyote, Alitengeneza viumbe vyote. Yeye Alieneza kazi yake kupitia kwa watu wa Israeli. Hiyo ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria.

2 Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu, ambalo lina maana kuwa Mungu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu, na ya kwamba Alikuwa Mungu wa rehema na wa upendo. Mungu Alikuwa na mwanadamu. Upendo wake, huruma yake, na wokovu wake uliandamana na kila mtu. Mwanadamu angeweza tu kupata amani na furaha, kupokea baraka zake, kupokea neema yake kubwa na nyingi, na kupokea wokovu wake iwapo mwanadamu angekubali jina lake na akubali uwepo wake. Kupitia kusulubiwa kwa Yesu, wale wote ambao walimfuata Yeye walipokea wokovu na walisamehewa dhambi zao. Katika siku za mwisho, jina lake ni Mwenyezi Mungu—mwenye uweza, na yeye hutumia nguvu zake kumwongoza mwanadamu, kumshinda mwanadamu, kumtwaa mwanadamu, na mwishowe, kuhitimisha enzi hiyo. Katika kila enzi, katika awamu yote ya kazi yake, tabia ya Mungu ni dhahiri.

Umetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 140 Mungu Huchukua Majina Tofauti Kuwakilisha Enzi Tofauti

Inayofuata: 142 Unathubutu Kudai Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika Kamwe?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp