A. Kuhusu Mamlaka ya Mungu

529. Katika upana wa ulimwengu na anga, viumbe wasiohesabika wanaishi na kuzaliana, hufuata sheria ya mzunguko wa maisha na kufuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani aliyemuumba mwanadamu huyu? Je, kweli wanadamu waliumbwa na mazingira asilia? Je, kweli wanadamu wana uamuzi juu ya hatima yao? … Kwa maelfu ya miaka wanadamu wameyauliza haya maswali, tena na tena. Kwa bahati mbaya, jinsi wanadamu wanavyopagawa na haya maswali, ndivyo kiu yao ya sayansi huendelea kukua. Sayansi hupatiana kutosheleza kwa muda na raha ya muda ya mwili, ila haitoshi kumpa mwanadamu uhuru kutokana na upweke, ukiwa, na hofu isiyodhihirika na kutosaidika ndani ya moyo wake. Wanadamu hutumia ujuzi wa kisayansi ambao wanaweza kuona kwa macho na kuelewa kwa akili yao ili kuutuliza moyo wao. Ilhali maarifa kama hayo ya kisayansi hayatoshi kuwazuia wanadamu kutafiti siri. Wanadamu hawajui kabisa Mkuu wa ulimwengu na vitu vyote ni nani, sembuse kujua mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yako kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyopo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha. Wanadamu huishi na hufa chini ya macho yake Mungu. Wanadamu anaishi kwa ajili ya usimamizi wa Mungu, na macho Yake yanapofumba kwa mara ya mwisho, hiyo pia ni kwa ajili ya usimamizi huo huo. Tena na tena, mwanadamu huja na kwenda, nyuma na mbele. Bila mapendeleo, yote ni sehemu ya mamlaka ya Mungu na muundo Wake. Usimamizi wa Mungu unaendelea mbele kwa kudumu; haujawahi kusimama. Atawafanya wanadamu wafahamu uwepo Wake, waamini katika mamlaka Yake, watazame matendo Yake, na warudi katika ufalme Wake. Huu ndio mpango Wake, na kazi ambayo Amekuwa akiitekeleza kwa maelfu ya miaka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

530. Tangu Alipoanza uumbaji wa vitu vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni kwa njia gani Aliviumba, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, vitu vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwa wakati ambao bado mwanadamu hajaonekana ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba vitu vyote kwa ajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu Zake za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Yake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwa viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, mwanga, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, vikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila kimoja kilipewa uhai kwa matamshi ya Muumba, na kila kila kimoja kiliongezeka kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimoja kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawa hawakupokea pumzi ya Muumba, bado walionyesha uhai na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa maumbo na miundo yao tofauti; Ingawa hawakupokea uwezo wa kuongea waliopewa wanadamu na Muumba, kila kimoja kilipokea namna ya kuelezea uhai wao ambao wamepewa na Muumba, na ambao ulitofautiana na ile lugha ya wanadamu. Mamlaka ya Muumba sio tu kwamba yanatoa nguvu za uhai katika vitu vinavyoonekana kuwa tulivu, ili visiwahi kutoweka, bali pia, Anatoa silika ya kuzaliana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, viweze kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatumia mamlaka Yake haifuati kwa uthabiti mtazamo wa mambo makubwa makubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka na taratibu zozote; Anaweza kuamuru utendakazi wa ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya uhai na kifo kwa vitu vyote, na, vilevile, Anaweza kuendesha vituvyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala vitu vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya kipekee ya Muumba miongoni mwa vitu vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu katika maisha haya tunayoishi; kamwe hayatakoma, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kuchukua nafasi ya utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki kiini cha Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, Ingawa vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kumwakilisha Mungu. Ingawa wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba vitu vyote, kuamuru vitu vyote, na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haziwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Katika Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba vitu vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kumtuma yeyote kati ya wajumbe Wake au malaika kuumba vitu vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote vilivyoumbwa, vyote viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni bora au duni, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kuchukua nafasi ya utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

531. Mungu alitazama vitu vyote Alivyokuwa ameviumba vikitokea na kusimama imara kwa sababu ya matamshi Yake, na polepole vilianza kubadilika. Je, kwa wakati huu, Mungu alikuwa Ameridhika na vitu mbalimbali Ambavyo alikuwa Amevifanya kwa matamshi Yake, na vitendo mbalimbali Alivyokuwa ametimiza? Jibu ni kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Je unaona nini hapa? Kunawakilisha nini kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri”? Kusema hivi kunaashiria nini? Kunamaanisha kwamba Mungu alikuwa na nguvu na hekima ya kukamilisha kile Alichokuwa amepanga na kuamua, ili kutimiza malengo ambayo Alikuwa amekusudia kuyatimiza. Baada ya Mungu kukamilisha kila kazi, je, Alijutia chochote? Jibu lingali kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Kwa maneno mengine, sio tu kwamba Hakujutia chochote, bali pia Aliridhika. Inamaanisha nini kwamba Hakujutia chochote? Inamaanisha kwamba mpango wa Mungu ni sahihi, kwamba nguvu na hekima Zake ni kamili, na kwamba ni kwa mamlaka Yake tu ndipo ukamilifu huo unaweza kutimizwa. Wakati binadamu anapotekeleza kazi, je, anaweza, kama Mungu, kuona kwamba kazi hiyo ni nzuri? Je, kila kitu anachofanya binadamu kinaweza kufikia ukamilifu? Je, binadamu anaweza kukamilisha kitu mara moja na kikawa hivyo daima dawamu? Kama vile tu binadamu anavyosema, “hakuna kitu kilicho kamili, kinaweza tu kuwa bora zaidi,” hakuna kitu ambacho binadamu hufanya kinaweza kufikia ukamilifu. Wakati Mungu alipoona kwamba kile Alichokuwa amefanya na kutimiza kilikuwa chema, kila kitu kilichoumbwa na Mungu kiliwekwa kwa matamshi Yake, hivi ni kusema kwamba, wakati “Mungu alipoona ya kuwa ni vyema,” kila kitu Alichokiumba kilichukua umbo la kudumu, kikaainishwa kulingana na aina, na kikapewa nafasi maalum, kusudio, na kazi, kwa mara ya kwanza na milele yote. Zaidi ya hayo, jukumu lao miongoni mwa vitu vyote, na safari ambayo ni lazima waichukue wakati wa usimamizi wa Mungu wa vitu vyote, ilikuwa tayari imeamriwa na Mungu, na isingebadilishwa. Hii ilikuwa ni sheria ya mbinguni iliyotolewa na Muumba kwa vitu vyote.

“Mungu akaona kwamba ni vizuri,” maneno haya mepesi, yasiyothaminiwa, yanayopuuzwa mara nyingi, ni maneno ya sheria ya mbinguni na amri ya mbinguni iliyotolewa na Mungu kwa viumbe vyote. Ni udhihirisho mwingine wa mamlaka ya Muumba, ambao ni wa kivitendo zaidi, na wa kina zaidi. Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kupata yale yote Aliyokusudia kuyapata, na kutimiza yale yote Aliyokusudia kuyatimiza, lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa amekiumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa amekiumba chini ya mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa na utaratibu na cha kawaida. Viumbe vyote pia viliongezeka, vikawepo, na kupotea kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kinachoweza kukiuka! Sheria hii ilianza punde tu “Mungu alipoona ya kuwa ni vyema,” na itakuwepo, itaendelea, na kufanya kazi kwa minajili ya mpango wa Mungu wa usimamizi mpaka siku ile itakapobatilishwa na Muumba! Mamlaka ya kipekee ya Muumba hayakuonyeshwa tu katika uwezo Wake wa kuumba vitu vyote na kuamuru vitu vyote vije kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya vitu vyote, na kuweka uhai na nguvu juu ya vitu vyote, na, zaidi ya hayo, katika uwezo Wake wa kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa milele yote, vitu vyote ambavyo Angeviumba katika mpango Wake vionekane na kuwepo katika ulimwengu vilivyofanywa na Yeye katika umbo kamili, na muundo kamili wa uhai, na jukumu kamili. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo mawazo ya Muumba hayakuwa chini ya vizuizi vyovyote, hayakuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia bila kubadilika milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

532. Mungu aliumba vitu vyote, na hivyo Yeye huvifanya viumbe vyote vije chini ya utawala Wake, na kunyenyekea chini ya utawala Wake; Ataamuru vitu vyote, ili kwamba kila kitu kiwe mikononi Mwake. Vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, pamoja na wanyama, mimea, wanadamu, milima na mito, na maziwa—vyote ni lazima vije chini ya utawala Wake. Vitu vyote vilivyo mbinguni na ardhini lazima viwe chini ya utawala Wake. Haviwezi kuwa na uchaguzi wowote na vyote ni lazima vitii mipango Yake. Hii iliamuliwa na Mungu, na ni mamlaka ya Mungu. Mungu huamuru kila kitu, na Anaagiza na kupangilia kila kitu, ambapo kila kimoja kinapangwa kulingana na aina, na kutengewa nafasi zao zenyewe, kulingana na mapenzi ya Mungu. Bila kujali kitu ni kikubwa namna gani, hakuna kitu kinachoweza kumpita Mungu, na vitu vyote vinawatumikia wanadamu walioumbwa na Mungu, na hakuna kitu kinachothubutu kumwasi Mungu au kutoa madai yoyote kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

533. Kabla ya binadamu hawa kuwepo, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa kuwepo kwao kote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata mifumo maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data sahihi; njia ambazo zinasafiria, kasi na mifumo ya mizunguko yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa usahihi na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kukosea hata kidogo. Hakuna nguvu inayoweza kubadilisha au kuharibu njia zao au mifumo ambayo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum ambazo zinaongoza mizunguko yao na data maalum inayozifafanua ziliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu mifumo fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na mifumo inayoamuru mizunguko yao, vyote vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Ukweli huu unamlazimisha mwanadamu kukabiliana na kukiri kwamba kuna Mwenye Nguvu katikati ya mifumo hii ya mizunguko, Anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei kiasili lakini zinaamrishwa na Mtawala. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.

Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi. Kwa nini hali iko hivi? Jibu la pekee tu ni, kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Au, nikijibu kwa njia nyingine, kwa sababu ya fikira za Mungu na matamshi ya Mungu; kwa sababu Mungu Mwenyewe hufanya haya yote. Hivi ni kusema, ni mamlaka ya Mungu na ni akili ya Mungu ambayo iliunda sheria hizi; zitasonga na kubadilika kulingana na fikira Zake, na kusonga huku na mabadiliko haya yote yanafanyika au kutoweka kwa minajili ya mpango Wake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

534. Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua amri ya kazi hii, na ukweli ulioahidiwa kwa kinywa cha Mungu polepole unaanza kuwa halisi. Kama matokeo, mabadiliko yanaanza kuonekana kati ya vitu vyote, kama vile, wakati wa majira ya kuchipua, nyasi hubadilika kuwa kijani kibichi, maua huchanua, chipukizi huchipuka kutoka kwenye miti, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Majira ya kuchipua yanapowadia vitu yote vinahuishwa, na hili ndilo tendo la kimiujiza la Muumba. Mungu anapotimiza ahadi zake, vitu vyote mbinguni na duniani vinafanywa upya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati patano au ahadi inapotamkwa kutoka katika kinywa cha Mungu, vitu vyote vinatimiza wajibu wao, na vinaongozwa kwa minajili ya kutimizwa kwao, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kutumikia jukumu lao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Je, kuna kiwango cha mamlaka ya Mungu? Je, kuna ukomo wa wakati? Je, yanaweza kusemwa kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, yanaweza kusemwa kuwa na ukubwa fulani au nguvu fulani? Je, yanaweza kupimwa kwa vipimo vya kibinadamu? Mamlaka ya Mungu sio kitu kinachopepesa, hayaonekani na kutoweka ghafla, na hakuna mtu anayeweza kupima jinsi mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, Mungu anapombariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutamruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za uhai zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho kamili la maneno kutoka kinywani Mwake, ambayo yanaonyeshwa katika vitu vyote, na kwa wanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa kwa mamlaka Yake ni chenye ubora usio na kifani, na hakina dosari kabisa. Inaweza kusemwa kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyo na kifani, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, kila kitu kinachomhusu kinafahamika kwa Mungu kama tu sehemu ya nyuma ya mkono Wake mwenyewe, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanapoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au jinsi ambavyo mageuzi yamekuwa makubwa katika mazingira yao ya kuishi. Haijalishi ni muda gani umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kana kwamba ndio yametoka tu kutamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutimiza kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutimizwa, na, zaidi ya hayo, kukamilishwa kwake na kutimizwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba ukubwa wa mamlaka na nguvu za Mungu unatosha kuudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

535. Katika maendeleo ya mwanadamu leo, sayansi ya mwanadamu inaweza kusemwa kwamba imeongezeka, na mafanikio ya uchunguzi wa kisayansi wa binadamu unaweza kufafanuliwa kama wa kuvutia. Uwezo wa kibinadamu, lazima isemwe, unazidi kuwa mkubwa zaidi, lakini kuna utafiti mmoja wa kisayansi ambao mwanadamu hajaweza kuufanya: Mwanadamu ameunda ndege, vifaa vya angani, na hata bomu la atomiki, mwanadamu ameenda angani, ametembea mwezini, amevumbua Intaneti, na ameishi maisha ya kiwango cha juu cha teknolojia, ilhali mwanadamu hawezi kuumba kiumbe hai kinachopumua. Silika za kila kiumbe kilicho hai na sheria ambazo zinatawala kuishi kwao na mzunguko wa maisha na kifo cha kila kiumbe kilicho hai—vyote hivi haviwezekani na havidhibitiki na sayansi ya mwanadamu. Wakati huu, lazima isemwe kwamba haijalishi ni viwango gani vya juu zaidi vitakavyofikiwa na sayansi ya binadamu, haviwezi kulinganishwa na fikira zozote za Muumba na haiwezekani kutambua miujiza ya uumbaji wa Muumba na uwezo wa mamlaka Yake. Kuna bahari nyingi sana juu ya nchi, ilhali hazijawahi kukiuka mipaka yao na kuja kwenye ardhi kwa nguvu, na hiyo ni kwa sababu Mungu aliweka mipaka kwa kila moja ya bahari hizo; zilikaa popote pale Alipoziamuru kukaa; na bila ya ruhusa ya Mungu haziwezi kuzunguka kwa uhuru. Bila ruhusa ya Mungu, haziwezi kuingiliana, na zinaweza kusonga tu pale ambapo Mungu anasema hivyo, na pale ambapo zinaenda na kubakia inaamuliwa na mamlaka ya Mungu.

Ili kuiweka kwa uwazi zaidi, “mamlaka ya Mungu” ina maana kwamba ni wajibu wa Mungu. Mungu anayo haki ya kuamua namna ya kufanya kitu na kinafanywa kwa vyovyote vile Anavyopenda. Sheria ya vitu vyote ni juu ya Mungu, na sio juu ya mwanadamu; wala haiwezi kubadilishwa na mwanadamu. Haiwezi kubadilishwa kwa mapenzi ya mwanadamu, lakini inaweza badala yake kubadilishwa kwa fikira za Mungu, na hekima ya Mungu, na amri za Mungu, na huu ni ukweli usiopingika kwa binadamu yeyote. Mbingu na nchi na viumbe vyote, ulimwengu, mbingu yenye nyota, misimu minne ya mwaka, kile kinachoonekana na kisichoonekana kwa mwanadamu-vyote vipo, vinafanya kazi, na vinabadilika bila ya kosa hata dogo, chini ya mamlaka ya Mungu, kulingana na maagizo ya awali ya Mungu, kulingana na amri za Mungu, na kulingana na sheria za mwanzo wa uumbaji. Hakuna mtu au kitu hata kimoja kinachoweza kubadilisha sheria zao, au kubadilisha mkondo wa asili ambao sheria hizi zinafanya kazi; zilianza kutumika kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na zitaangamia kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

536. Mamlaka yenyewe yanaweza kufafanuliwa kama nguvu za Mungu. Kwanza, inaweza kusemwa kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni chanya. Hazina uhusiano na kitu chochote kilicho kibaya, na hazina uhusiano na viumbe vyovyote vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Nguvu za Mungu zinaweza kuumba kusemwa kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni chanya. Hazina uhusiano na kitu chochote kilicho kibaya, na hazina uhusiano na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe vyote vyenye uhai. Zaidi ya hayo, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuongezeka kwa amri ya Mungu, kisha, Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote vyenye uhai, na hakutakuwa na kupotoka, milele na milele. Hakuna mtu au kitu chenye vitu hivi; ni Muumba pekee ndiye Anayemiliki na kubeba nguvu kama hizo, na hivyo yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Kwa hivyo, haijalishi kama ni neno lenyewe “mamlaka” au kiini cha mamlaka hayo, kila moja inaweza tu kuhusishwa na Muumba, kwa sababu ni ishara ya utambulisho wa kipekee na kiini cha Muumba, na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba; mbali na Muumba, hakuna mtu au kitu kinachoweza kuhusishwa na neno “mamlaka.” Hii ni tafsiri ya mamlaka ya kipekee ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

537. “Mimi nauweka upinde Wangu mawinguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati Yangu na nchi.” Haya ni matamshi halisi yaliyotamkwa na Muumba kwa mwanadamu. Aliposema matamshi haya, upinde wa mvua ulionekana mbele ya macho ya binadamu, ambapo ulibakia mpaka leo. Kila mmoja ameuona upinde wa mvua kama huo, na unapouona, je, unajua namna unavyojitokeza? Sayansi haiwezi kuthibitisha haya, au kutafuta chanzo chake, au kutambua mambo yanayosababisha upinde huu wa mvua. Hiyo ni kwa sababu, upinde wa mvua ni ishara ya agano lilioanzishwa kati ya Muumba na binadamu; hauhitaji msingi wowote wa kisayansi, haukuumbwa na binadamu, wala binadamu hawezi kuubadilisha. Ni maendelezo ya mamlaka ya Muumba baada ya Yeye kuongea matamshi Yake. Muumba alitumia mbinu Yake mahususi kutii agano lake na binadamu na ahadi Yake, na hivyo basi matumizi Yake ya upinde wa mvua kama ishara ya agano ambalo Alianzisha ni maelekezo na sheria ya mbinguni yatakayobakia milele bila kubadilika, haijalishi kama ni kuhusiana na Muumba au mwanadamu aliyeumbwa. Ilhali sheria hii isiyobadilika ni, inaweza kusemwa, maonyesho mengine ya kweli ya mamlaka ya Muumba kufuatia uumbaji Wake wa vitu vyote, na lazima isemwe kwamba mamlaka na nguvu za Muumba hayana mipaka; matumizi Yake ya upinde wa mvua ni ishara ya maendelezo na upanuzi wa mamlaka ya Muumba. Hiki kilikuwa kitendo kingine kilichotekelezwa na Mungu kwa kutumia matamshi Yake, na ilikuwa ni ishara ya agano ambalo Mungu alikuwa ameanzisha na mwanadamu kwa kutumia matamshi. Alimwambia binadamu kuhusu kile ambacho Aliamua kuleta, na kwa njia gani kingekamilishwa na kutimizwa, na kwa njia hii suala liliweza kutimizwa kulingana na matamshi kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na leo, miaka elfu kadhaa baada ya Yeye kuongea matamshi haya, binadamu angali bado anaweza kuangalia upinde wa mvua uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kwa sababu ya matamshi hayo yaliyotamkwa na Mungu, kitu hiki kimebakia bila ya kusongezwa na kubadilishwa mpaka kufikia leo. Hakuna anayeweza kuuondoa upinde huu wa mvua, hakuna anayeweza kubadilisha sheria zake, na upo kimsingi kutokana na matamshi ya Mungu. Haya kwa hakika ni mamlaka ya Mungu. “Mungu humaanisha kile Anachokisema, na kile Anachokisema kinatimizwa, na kile Anachokitimiza kitadumu milele.” Matamshi kama haya kwa kweli yanaonyeshwa waziwazi hapa, na ni ishara na sifa wazi kuhusu mamlaka na nguvu za Mungu. Ishara au sifa kama hiyo haimilikiwi na au kuonekana katika viumbe vyovyote vile vilivyoumbwa, wala kuonekana kwenye viumbe vyovyote vile ambavyo havikuumbwa. Inamilikiwa tu na Mungu wa kipekee, na inatofautisha utambulisho na kiini kinachomilikiwa na Muumba pekee na kile cha viumbe vilivyoumbwa. Wakati uo huo, ni ishara na sifa pia ambayo mbali na Mungu Mwenyewe, haitawahi kuzidiwa kiwango na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa.

Uanzishaji wa agano Lake na binadamu ilikuwa ni kitendo chenye umuhimu mkubwa, na ambao Alinuia kutumia ili kuwasilisha hoja kwa binadamu na kumwambia binadamu mapenzi Yake, na mpaka kufikia hapa, Alitumia mbinu ya kipekee, kwa kutumia ishara maalum ya kuanzisha agano na binadamu, ishara ambayo ilikuwa ahadi ya agano ambalo Alikuwa ameanzisha na binadamu. Kwa hivyo, je, uanzishaji wa agano hili ulikuwa ni tukio kubwa? Na tukio hili lilikuwa kubwa kiasi gani? Hii haswa ndiyo inayoonyesha namna ambavyo agano hili lilivyo maalum: si agano lililoanzishwa kati ya binadamu mmoja na mwingine, au kundi moja na jingine, au nchi moja na nyingine, lakini agano lililoanzishwa kati ya Muumba na wanadamu kwa ujumla, na litabakia halali mpaka siku ambayo Muumba atakomesha mambo yote. Mtekelezaji wa agano hili ni Muumba, na mwendelezaji pia ni Muumba. Kwa ufupi, ukamilifu wa agano la upinde wa mvua ulioanzishwa pamoja na mwanadamu ulikamilishwa na kutimizwa kulingana na mazungumzo kati ya Muumba na mwanadamu, na umebakia vivyo hivyo mpaka leo. Ni nini kingine ambacho viumbe vinaweza kufanya mbali na kujinyenyekeza, na kutii, na kusadiki, na kufahamu, na kutolea ushuhuda, na kusifu mamlaka ya Muumba? Kwa kuwa hakuna yeyote yule isipokuwa Mungu wa pekee anayemiliki nguvu za kuanzisha agano kama hilo. Kujitokeza kwa upinde wa mvua mara kwa mara, kunatangaza kwa mwanadamu na kumtaka azingatie agano lile kati ya Muumba na mwanadamu. Katika muendelezo wa kuonekana kwa agano kati ya Muumba na binadamu, kile kinachoonyeshwa kwa mwanadamu si upinde wa mvua au agano lenyewe, bali ni mamlaka ya Muumba yasiyobadilika. Kujitokeza kwa upinde wa mvua, mara kwa mara, kunaonyesha yale matendo ya ajabu na ya kimiujiza ya Muumba katika mahali pa siri, na, kwa wakati huo huo ni onyesho muhimu la mamlaka ya Muumba ambayo hayatawahi kupungua, na wala kubadilika. Je, hili si onyesho la kipengele kingine cha mamlaka ya kipekee ya Muumba?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

538. Baada ya kusoma “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye” kwenye Mwanzo 18:18, je, unaweza kuhisi mamlaka ya Mungu hapo? Je, unaweza kuhisi ubora wa ajabu wa Muumba? Je, unaweza kuhisi ukuu wa Muumba? Maneno ya Mungu yana uhakika. Mungu hasemi maneno kama hayo kwa sababu ya, au katika uwakilishi wa, ujasiri Wake katika ufanisi; badala yake, hayo ni, uthibitisho wa mamlaka ya matamshi, na ni amri inayotimiza maneno ya Mungu. Kuna maneno mawili ambayo unapaswa kuzingatia hapa. Wakati Mungu anaposema “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye,” je, kuna dalili ya kutoeleweka katika maneno haya? Je, kuna dalili yoyote ya wasiwasi? Je, kuna dalili yoyote ya hofu? Kwa sababu ya maneno “hakika utakuwa” na “watakuja” katika matamshi ya Mungu, dalili hizi, ambazo zinapatikana tu kwa binadamu na mara nyingi zinajionyesha ndani yake, hazijawahi kupata uhusiano wowote na Muumba. Hakuna mtu angethubutu kutumia maneno kama haya wakati akiwatakia wengine mema, hakuna ambaye angethubutu kumbariki mwingine apate taifa kubwa na lenye nguvu kwa uhakika kama huo, au kutoa ahadi kwamba mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia kwake. Kadiri maneno ya Mungu yanavyokuwa ya hakika zaidi, ndivyo yanavyothibitisha zaidi kitu fulani—na kitu hicho ni nini? Yanathibitisha kuwa Mungu anayo mamlaka kama hayo, kuwa mamlaka Yake yanaweza kutimiza mambo haya, na kwamba utimizaji wake hauzuiliki. Mungu alikuwa na uhakika katika moyo Wake, bila kusita kokote, kwa kila kitu Alichombariki Ibrahimu. Aidha, ukamilifu wa haya utakamilishwa kulingana na maneno Yake, na hakuna nguvu ingeweza kubadilisha, kuzuia, kuharibu, au kutatiza kukamilika kwake. Haijalishi kile ambacho kingetokea, hakuna kitu ambacho kingebatilisha au kuathiri kutimia na kukamilika kwa matamshi ya Mungu. Huu ndio uwezo mkubwa wa maneno yaliyotamkwa kutoka kinywa cha Muumba, na mamlaka ya Muumba ambayo hayavumilii kanusho la binadamu! Baada ya kuyasoma maneno haya, ungali unahisi shaka? Maneno haya yalitamkwa kutoka kinywani mwa Mungu, na kuna nguvu, ukuu na mamlaka katika maneno ya Mungu. Uwezo na mamlaka kama haya, na kutozuilika kwa kukamilika kwa hoja, haviwezi kufikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa na haviwezi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa. Muumba pekee ndiye anaweza kuongea na binadamu kwa sauti na mkazo kama huo, na ukweli umethibitisha kwamba ahadi Zake si maneno matupu, au majigambo yasiyo na maana, bali ni maonyesho ya mamlaka ya kipekee yasiyoweza kupitwa na mtu, kitu, au kifaa chochote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

539. Wakati Mungu alisema “uzao wako nitazidisha,” hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hata milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Ni Mungu pekee ndiye mwenye sifa na uwezo wa kufanya ahadi hii itimie. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yatatimizwa kwa uhakika, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Vitu vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hata milele. Kwa hakika, siku ambayo vitu vyote vitatoweka ndiyo siku hasa ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kufanya kitu kiwe si kitu, na Anadhibiti mabadiliko ya vitu vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi zaidi kama kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kulifikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kulifikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni uhalisia ambao Mungu tayari aliuona, na ambao kwa hakika utaweza kutimizwa. Je, unaelewa hili? Je, ukweli wa mambo unathibitisha kwamba wazao wa Abrahamu walikuwa wengi? Na je, walikuwa ni wengi kiasi gani? Je, walikuwa ni wengi kama “nyota za mbinguni, na kama mchanga uliokopwani” kama ilivyosemwa na Mungu? Je, waliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza ukweli huu? Je, iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa mamia au maelfu kadhaa ya miaka baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na siku zote yaliendelea kuwa halisi; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na uthibitisho wa mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba vitu vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Alimruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa kiini cha mamlaka ya Mungu, na Akamruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyopimika, na zaidi ya hayo, Alimruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

540. Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Hakuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, mara tu Mungu alipotamka maneno Yake, chini ya uongozi wa mamlaka ya Mungu, vitu vyote vilianza kuendana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutekelezwa katika nchi nzima, na Aliweka njia ya kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, Mungu hakuwadhibiti tu wajumbe Wake, bali pia vitu vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivi ni kusema kwamba, upeo ambao mamlaka ya Mungu yalitekelezwa haukujumuisha wajumbe tu, bali, vitu vyote katika uumbaji, ambavyo viliongozwa ili kuendana na kazi Aliyokusudia kuikamilisha; hizi ndizo tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitekelezwa. Katika mawazo yenu, wengine wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao wa mamlaka ya Mungu: Mungu ana mamlaka, na Mungu ana nguvu, na hivyo Mungu anahitaji tu kubaki katika mbingu ya tatu, au sehemu moja tu, na hahitaji kufanya kazi yoyote mahususi, na ukamilifu wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, Ingawa Mungu alimbariki Ibrahimu, Mungu hakuhitaji kufanya lolote, na ilitosha Kwake tu kutamka maneno Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka, sivyo! Ingawa Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisi, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka na nguvu za Mungu hufichuliwa na kuonyeshwa hatua kwa hatua katika uumbaji Wake wa vitu vyote, katika udhibiti Wake juu ya vitu vyote, na katika mchakato ambao Yeye anawaongoza na kuwasimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyote—yote yanathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo halisi wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angewapa Ibrahimu na Ayubu—ilikuwa ni uamuzi wa Mungu kuufanya. Ingawa wajumbe wa Mungu waliwatembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, matendo yao yalikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawa binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hamshuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote katika rekodi za Biblia, kwa hakika, Yule pekee ambaye kwa kweli anatumia nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kutiliwa shaka na binadamu yeyote! Ingawa umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kitu kimoja kilicho, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kitu chochote kinachoweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

541. Je, Mungu angeweza kufanya jambo fulani ili kuthibitisha utambulisho Wake Mwenyewe? Kwa Mungu, huu ulikuwa upepo mwanana—lilikuwa jambo rahisi sana. Angefanya kitu popote, wakati wowote ili kuthibitisha utambulisho na kiini Chake, lakini Mungu alikuwa na njia Yake ya kufanya mambo—kwa mpango, na kwa hatua. Hakufanya vitu bila mpangilio; Alitafuta muda unaofaa, na fursa inayofaa kufanya kitu chenye maana zaidi kwa wanadamu kuweza kuona. Hili lilithibitisha mamlaka Yake na utambulisho Wake. Kwa hivyo, je, kufufuka kwa Lazaro kungeweza kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu? Hebu tuangalie kifungu hiki cha maandiko: “Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekuwa amekufa ….” Wakati Bwana Yesu alipofanya haya, Alisema tu jambo moja: “Lazaro, kuja nje.” Kisha Lazaro akatoka nje ya kaburi—hii ilitimizwa kwa sababu ya maneno machache tu yaliyotamkwa na Bwana. Kwa wakati huu, Bwana Yesu Hakuanzisha madhabahu, na Hakufanya vitendo vingine vyovyote. Alisema tu hili jambo moja. Je, hii inapaswa kuitwa muujiza au amri? Au ilikuwa ni aina fulani ya uchawi? Kwa juujuu, inaonekana inaweza kuitwa muujiza, na ukiangalia kutoka kwa mtazamo wa kisasa, bila shaka bado mnaweza kuuita muujiza. Hata hivyo, kwa hakika haikuweza kuchukuliwa kuwa ni uchawi wakuiita nafsi kurudi kutoka kwa wafu, na bila shaka si uchawi. Ni sahihi kusema kwamba muujiza huu ulikuwa ni udhihirisho wa kawaida, mdogo sana wa mamlaka ya Muumba. Haya ndiyo mamlaka, na uwezo wa Mungu. Mungu ana mamlaka ya kumfanya mtu afe, kuruhusu nafsi yake iondoke mwilini mwake na kurudi kuzimu au popote pale itakapoenda. Wakati wa kifo cha mtu, na mahali atakapokwenda baada ya kifo—haya yanaamuliwa na Mungu. Yeye anaweza kufanya haya wakati wowote na mahali popote. Yeye hazuiliwi na binadamu, matukio, vitu, nafasi, au jiografia. Akitaka kufanya hivyo, Anaweza kufanya hivyo, kwa sababu vitu vyote na viumbe hai viko chini ya utawala Wake, na vitu vyote vinaongezeka, vinaishi, na kupotea kwa neno Lake na mamlaka Yake. Anaweza kumfufua binadamu aliyekufa, na pia hiki ni kitu Anachoweza kufanya wakati wowote mahali popote. Haya ndiyo mamlaka ambayo Muumba pekee humiliki.

Wakati Bwana Yesu alipofanya jambo kama vile kumfufua Lazaro kutoka kwa wafu, lengo Lake lilikuwa ni kutoa uthibitisho kwa wanadamu na kwa Shetani ili waweze kuona, na kuwafanya wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu, maisha na kifo cha wanadamu vyote vinaamuliwa na Mungu, na kwamba ingawa Alikuwa amefanyika mwili, daima, Alibakia katika kuuamuru ulimwengu wa kimwili unaoweza kuonekana pamoja na ulimwengu wa kiroho ambao wanadamu hawawezi kuuona. Huku kulikuwa kuwaruhusu wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu hakiko katika amri ya Shetani. Huu ulikuwa ni ufunuo na onyesho la mamlaka ya Mungu, na ilikuwa pia njia ya Mungu kuutuma ujumbe wake kwa viumbe vyote kwamba maisha na kifo cha wanadamu viko mikononi mwa Mungu. Bwana Yesu kumfufua Lazaro—kutenda kwa aina hii ni mojawapo ya njia za Muumba za kuwafunza na kuwaelekeza wanadamu. Ilikuwa ni hatua madhubuti ambayo kwayo Aliutumia uwezo Wake na mamlaka Yake kuwaelekeza wanadamu, na kutoa kwa ajili ya wanadamu. Ilikuwa ni njia, isiyo na matumizi ya maneno kwa ajili ya Muumba kuwaruhusu wanadamu kuweza kuuona ukweli wa Yeye kuwa na mamlaka juu ya vitu vyote. Ilikuwa ni mbinu Yake ya kuwaambia wanadamu kupitia hatua za kivitendo kwamba hakuna wokovu isipokuwa kupitia Kwake. Mbinu hii ya kimyakimya ambayo Aliitumia kuwaelekeza wanadamu inadumu milele, haitafutika, na iliweza kuleta mshtuko na nuru katika mioyo ya wanadamu ambayo kamwe haiwezi kufifia. Kufufuliwa kwa Lazaro kulimtukuza Mungu—hii ina athari kubwa kwa kila mmoja wa wafuasi wa Mungu. Inaweka kwa uthabiti ndani ya kila mmoja anayeelewa kwa kina tukio hili, ufahamu, maono kwamba ni Mungu tu anayeweza kuamuru maisha na kifo cha wanadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

542. Kuanzia wakati unapokuja ulimwenguni humu ukilia, unaanza kutimiza majukumu yako. Kwa ajili ya mpango wa Mungu na kutawaza Kwake, unafanya wajibu wako na kuanza safari yako ya maisha. Haijalishi ulikokulia kulivyo, na haijalishi safari iliyo mbele yako ilivyo, kwa vyovyote vile, hakuna anayeweza kuepuka mipango na mipangilio ya Mbinguni, na hakuna anayeweza kudhibiti hatima yake mwenyewe, kwani ni Yeye tu aliye na mamlaka juu ya vitu vyote ndiye Anayeweza kufanya kazi hiyo. Tangu kuwepo kwa mwanadamu hapo mwanzo, Mungu daima amekuwa Akifanya kazi Yake kwa namna hii, Akiusimamia ulimwengu, na kuelekeza sheria za mabadiliko kwa vitu vyote na mweleke wa kusonga kwao. Kama vitu vyote, mwanadamu kwa ukimya na bila kujua anastawishwa kwa utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu; kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua, anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimo katika mshiko wa Mungu, na kila kitu cha maisha yake kinatazamwa machoni pa Mungu. Bila kujali kama unaamini haya yote au la, chochote na vitu vyote, viwe vilivyohai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilishwa, kufanywa vipya, na kupotea kulingana na fikira za Mungu. Hivi ndivyo ambavyo Mungu anashikilia mamlaka juu ya vitu vyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uzima wa Mwanadamu

543. Kama kuzaliwa kwa mtu kulipangiwa kutokana na maisha yake ya awali, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa hatima hiyo. Kama kuzaliwa kwa mtu ndiyo mwanzo wa kazi maalum ya mtu katika maisha haya, basi kifo cha mtu kinaashiria mwisho wa kazi hiyo maalum. Kwa sababu Muumba ameweka mpangilio maalum wa hali kwa ajili ya kuzaliwa kwa mtu, ni wazi kwamba Yeye pia Amepanga mpangilio maalum wa hali za kifo cha mtu. Kwa maneno mengine, hakuna anayezaliwa kwa bahati na hakuna kifo cha mtu kinachotokea kwa ghafla, na kuzaliwa kwa mtu na kifo chake vyote vina uhusiano na maisha ya mtu ya awali na ya sasa. Hali za kuzaliwa na kifo cha mtu, vyote viliamuliwa kabla na Muumba; hii ni kudura ya mtu, hatima ya mtu. Kwa kuwa kuna maelezo mengi ya kuzaliwa kwa mtu, ni kweli pia kwamba kifo cha kila mtu kitatokea chini ya hali maalum zinazotofautiana. Hii ndiyo sababu ya kutofautiana kwa urefu wa maisha ya watu, njia na nyakati tofauti za vifo vyao. Baadhi ya watu wana nguvu na afya na ilhali wanakufa mapema; wengine ni wanyonge na wanauguaugua ilhali wanaishi hadi umri wa uzee, na wanaaga dunia kwa amani. Baadhi ya watu hupoteza maisha kwenye matukio yasiyotarajiwa, na wengine hufariki kutokana na sababu za kawaida. Baadhi wanakata roho wakiwa mbali na nyumbani, wengine wanayafumba macho yao kwa mara ya mwisho wakiwa na wapendwa wao kando yao. Baadhi ya watu hufia angani, na wengine hufia chini ya ardhi. Wengine huzama chini ya maji, wengine nao kwenye majanga. Baadhi hufa asubuhi, wengine hufa usiku. … Kila mtu anataka kuzaliwa kwa heshima, kuwa na maisha mazuri, na kifo kitukufu, lakini hakuna mtu anayeweza kufika zaidi ya hatima yake mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kukwepa ukuu wa Muumba. Hii ni hatima ya binadamu. Mwanadamu anaweza kupanga kila aina ya mipango kwa ajili ya maisha yake ya baadaye, lakini hakuna mtu anayeweza kupanga njia na muda wa kuzaliwa kwake na kuondoka kwake ulimwenguni. Ingawa watu wanajitahidi kadiri wawezavyo kuepuka na kuzuia ujio wa kifo chao, lakini bado, bila wao kujua, kifo huwa kinawakaribia kimyakimya. Hakuna ajuaye ni lini ataaga dunia na kwa njia ipi, sembuse kujua ni wapi ambapo hilo litatokea. Bila shaka, si binadamu wanaoshikilia nguvu za maisha na kifo, wala si kiumbe fulani kwenye ulimwengu wa asili, bali ni Muumba, ambaye mamlaka yake ni ya kipekee. Maisha na kifo cha binadamu si zao la sheria fulani ya ulimwengu wa asili, bali ni matokeo ya ukuu wa mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

544. Chini ya mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi potovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye njia ya hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali ya kutoweza kushindwa kwa mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanadhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoweza kushindwa, aina hii ya udhibiti na utawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya kila kitu, ambayo inawaruhusu wanadamu kuzaliwa upya tena na tena bila kuingiliwa, ambayo inaufanya ulimwengu kuzunguka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Mmezishuhudia kweli hizi zote na mmezielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Jinsi unavyojua vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, jinsi unavyojua vyema kiini cha Mungu na tabia Yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, kuwepo kwa ukuu na mipangilio ya Mungu kunategemea ikiwa wanadamu wanaitii? Je, ukweli kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na iwapo wanadamu wanayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, na mapenzi Yake. Hili halitabadilika kutokana na mabadiliko ya mwanadamu; haitegemei mapenzi ya mwanadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya wakati, anga, na jiografia, kwa kuwa mamlaka ya Mungu ni kiini Chake hasa. Iwapo mwanadamu anaweza kujua na kukubali ukuu wa Mungu, na kama mwanadamu anaweza kuunyenyekea—hakuna lolote kati ya haya linalobadilisha hata kidogo ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu. Hiyo ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, haiwezi tu kubadilisha ukweli kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu na juu ya vitu vyote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, bado Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kuujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na ukweli wa ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, na hayabadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila mara. Mbingu na nchi zitapita, lakini mamlaka Yake hayatapita kamwe, kwa kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala vitu vyote, Anatosheleza vitu vyote, Anapangilia vitu vyote—kama tu Anavyofanya daima. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Huu ni ukweli; umekuwa ukweli usiobadilika tangu zamani!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

545. Ukweli kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni ukweli ambao kila mmoja lazima atilie maanani kwa umakinifu, lazima apitie na aelewe katika moyo wake; kwani ukweli huu unao uhusiano katika maisha ya kila mmoja, kwenye maisha ya kale, ya sasa, na ya siku za usoni za kila mmoja, kwenye awamu muhimu ambazo kila mtu lazima apitie maishani, katika maarifa ya binadamu kuhusu ukuu wa Mungu na mtazamo ambao anafaa kuwa nao katika mamlaka ya Mungu, na kwa kawaida, kwenye hatima ya mwisho ya kila mmoja. Kwa hivyo inachukua nguvu za maisha yako yote kujua na kuyaelewa. Unapochukulia mamlaka ya Mungu kwa umakinifu, unapoukubali ukuu wa Mungu, kwa utaratibu utaanza kutambua na kuelewa kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo. Lakini kama hutawahi kutambua mamlaka ya Mungu, hutawahi kuukubali ukuu Wake, basi haijalishi ni miaka mingapi utakayoishi, hutapata maarifa hata kidogo ya ukuu wa Mungu. Kama hutajua na kuelewa kwa kweli mamlaka ya Mungu, basi utakapofika mwisho wa barabara, hata kama utakuwa umesadiki katika Mungu kwa miongo kadhaa, hutakuwa na chochote cha kuonyesha katika maisha yako, na kwa kawaida hautakuwa na maarifa hata kidogo ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya mwanadamu. Je, hili si jambo la kusikitisha sana? Kwa hivyo haijalishi umetembea kwa umbali gani maishani, haijalishi unao umri wa miaka mingapi sasa, haijalishi safari yako iliyosalia itakuwa ya umbali gani, kwanza lazima utambue mamlaka ya Mungu na uyachukulie kwa uzito, na ukubali ukweli kwamba Mungu ni Bwana wako wa kipekee. Kutimiza maarifa yaliyo wazi, sahihi na kuelewa ukweli huu kuhusiana na ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni funzo la lazima kwa kila mmoja, ndio msingi wa kuyajua maisha ya binadamu na kupata ukweli, ndiyo maisha na funzo la msingi la kumjua Mungu ambalo kila mtu anakabiliana nalo kila siku, na ambayo hakuna yeyote anayeweza kuyakwepa. Kama mmoja wenu angependa kuchukua njia za mkato ili kufikia lengo hili, basi Ninakuambia, hilo haliwezekani! Kama mmoja wenu anataka kukwepa ukuu wa Mungu, basi hilo nalo ndilo haliwezekani zaidi! Mungu ndiye Bwana wa pekee wa binadamu, Mungu ndiye Bwana wa pekee wa hatima ya binadamu, na kwa hivyo haiwezekani kwa binadamu kuamuru hatima yake mwenyewe, haiwezekani kwake kuizidi hatima yake. Haijalishi uwezo wa mtu ni mkubwa kiasi gani, mtu hawezi kuathiri, sembuse kuunda, kupangilia, kudhibiti, au kubadilisha hatima za wengine. Ni Mungu Mwenyewe wa kipekee tu ndiye Anayeweza kuamuru mambo yote kwa binadamu, kwani Yeye tu ndiye anayemiliki mamlaka ya kipekee yanayoshikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu; na kwa hivyo Muumba pekee ndiye Bwana wa kipekee wa binadamu. Mamlaka ya Mungu yanashikilia ukuu sio tu juu ya binadamu walioumbwa, lakini hata juu ya viumbe ambavyo havikuumbwa visivyoweza kuonekana na binadamu, juu ya nyota, juu ya ulimwengu mzima. Huu ni ukweli usiopingika, ukweli ambao upo kiuhalisia, ambao hakuna mtu au kitu kinachoweza kuubadilisha. Kama mmoja wenu angali hajatosheka na mambo kama yalivyo, akiamini kwamba kwa kiasi fulani ana ujuzi au uwezo maalum, na bado anafikiria kwamba anaweza kubahatika na kubadilisha hali yake ya sasa au hata kuiepuka; kama utajaribu kubadilisha hatima yako mwenyewe kupitia kwa juhudi za kibinadamu, na hivyo basi kujitokeza kati ya wengine na kupata umaarufu na utajiri; basi Ninakwambia, unayafanya mambo kuwa magumu kwako, unajitakia taabu tu, unajichimbia kaburi lako mwenyewe! Siku moja, hivi karibuni au baadaye, utagundua kwamba ulifanya chaguo baya, kwamba jitihada zako ziliambulia patupu. Malengo yako, tamanio lako la kupambana dhidi ya hatima, na mwenendo wako mwenyewe ulio mbaya, utakuongoza kwenye barabara isiyoweza kukurudisha kule ulikotoka, na kwa hili utaweza kujutia baadaye. Ingawa sasa huoni ubaya wa athari hiyo, unapopitia na kuelewa zaidi na zaidi ukweli kwamba Mungu ndiye Mtawala wa hatima ya mwanadamu, utaanza kwa utaratibu kutambua kile Ninachozungumzia leo na athari zake za kweli. Ikiwa kweli una moyo na roho, na ikiwa wewe ni mtu anayependa ukweli, inategemea ni mtazamo wa aina gani ambao utachukua kuhusiana na ukuu wa Mungu na kuhusiana na ukweli. Na kwa kawaida, hili linaamua kama kweli unaweza kujua na kuelewa mamlaka ya Mungu. Kama hujawahi katika maisha yako kuhisi ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hujawahi kutambua na kukubali mamlaka ya Mungu, basi utakuwa huna thamani kabisa, na bila shaka utakuwa ni mlengwa wa kuchukiwa na kukataliwa na Mungu, hayo yote ni kutokana na njia uliyochukua na chaguo ulilofanya. Lakini wale ambao, katika kazi ya Mungu, wanaweza kukubali jaribio Lake, kukubali ukuu Wake, kujinyenyekeza katika mamlaka Yake, na kupata kwa utaratibu uzoefu halisi wa matamshi Yake, watakuwa wametimiza maarifa halisi ya mamlaka ya Mungu, ufahamu halisi wa ukuu Wake, na watakuwa kwa kweli wamejisalimisha kwa Muumba. Watu kama hao tu ndio watakaokuwa wameokolewa kwa kweli.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

546. Mungu aliumba ulimwengu huu, Alimuumba mwanadamu huyu na, zaidi ya hayo, Alikuwa muasisi wa utamaduni wa kale wa Kigiriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu pekee Anayewafariji wanadamu hawa, na ni Mungu pekee Anayewajali wanadamu hawa usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatenganishwi na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu hauwezi kuepuka mipango inayofanywa na mikono ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi kwa hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote kunafanyika chini ya mipango ya Mungu. Mungu pekee ndiye Anayejua hatima ya nchi ama taifa lolote, na ni Mungu pekee ndiye Anayedhibiti mwenendo wa wanadamu hawa. Ikiwa wanadamu wanataka kuwa na hatima nzuri, ikiwa nchi inataka kuwa na hatima nzuri, basi mwanadamu lazima amsujudie Mungu katika ibada, na aje mbele za Mungu akitubu na kuungama, kama sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Ana Mamlaka Juu ya Hatima ya Wanadamu Wote

547. Hatima za binadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa undani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na katika mizunguko ya maisha ya wanadamu na vitu vyote, mwanadamu kwa kweli huja kupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zingine zote. Kwa mujibu wa haya, binadamu wanashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzaliana, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

548. Ingawa Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, Ana msimamo sana na Anafuata kanuni katika vitendo Vyake, na Anashikilia maneno Yake. Msimamo Wake na kanuni za vitendo Vyake, vinaonyesha namna Muumba asivyoweza kukosewa na kutoweza kushindwa kwa mamlaka ya Muumba. Ingawa Anamiliki mamlaka ya juu, na kila kitu kinatawaliwa na Yeye, na japokuwa Anazo nguvu za kutawala vitu vyote, Mungu hajawahi kuharibu mpango Wake au kutatiza mpangilio Wake mwenyewe, na kila wakati Anapotumia mamlaka Yake, ni kulingana na umakinifu unaohitajika kwenye kanuni Zake mwenyewe na hasa kwa kufuata kile kilichotamkwa kutoka kwenye kinywa Chake, na kufuata hatua na majukumu ya mpango Wake. Bilas haka, kila kitu kinachotawaliwa na Mungu pia kinatii kanuni ambazo mamlaka ya Mungu yanatumika, na hakuna mwanadamu au kitu kisichojumuishwa kwenye mipangilio ya mamlaka Yake, wala hakuna anayeweza kubadilisha kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumika. Machoni pa Mungu, wale wanaobarikiwa hupokea utajiri mzuri unaoletwa na mamlaka Yake, na wale wanaolaaniwa hupokea adhabu yao kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, hakuna binadamu au kitu ambacho hakijumuishwi katika utumiaji wa mamlaka Yake, wala hakuna kinachoweza kubadilisha kanuni hizi ambazo mamlaka Yake yanatekelezwa. Mamlaka ya Muumba hayabadilishwi kwa mabadiliko ya aina yoyote ile, na, vilevile, kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumiwa hazibadiliki kwa sababu yoyote ile. Mbingu na ardhi vyote vinaweza kupitia misukosuko mingi, lakini mamlaka ya Muumba hayatabadilika; vitu vyote vitatoweka, lakini mamlaka ya Muumba hayatawahi kutoweka. Hiki ndicho kiini cha mamlaka ya Muumba ambayo hayabadiliki na yasiyokosewa kukosewa, na huu ndio upekee wenyewe wa Muumba!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

549. Shetani hajawahi kuthubutu kukiuka mamlaka ya Mungu, na, vilevile, amesikiliza kwa umakinifu siku zote na kutii shurutisho na amri mahususi za Mungu, asiwahi thubutu kuzivunja, na, bila shaka asithubutu kubadilisha kwa hiari shurutisho zozote za Mungu. Hiyo ndiyo mipaka ambayo Mungu amemwekea Shetani, na hivyo Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka hiyo. Je, huu si uwezo wa mamlaka ya Mungu? Je, huu si ushuhuda wa mamlaka ya Mungu? Shetani ana ufahamu wa wazi zaidi kuliko wanadamu kuhusu jinsi ya kuenenda mbele za Mungu, na jinsi ya kumtazama Mungu, hivyo, katika ulimwengu wa kiroho, Shetani anaona hadhi na mamlaka ya Mungu vizuri sana, na anatambua sana ule uwezo wa mamlaka ya Mungu na kanuni zinazoongoza utekelezaji wa mamlaka Yake. Hathubutu, kamwe, kutozitilia maanani kanuni hizo, wala hathubutu kukiuka kanuni hizo kwa vyovyote vile, au kufanya chochote ambacho kinakiuka mamlaka ya Mungu, na hathubutu kukabiliana na hasira ya Mungu kwa njia yoyote ile. Ingawa ni mwovu na mwenye kiburi kiasili, Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka na viwango alivyowekewa na Mungu. Kwa mamilioni ya miaka, ametii kwa umakinifu mipaka hii, ametii kila amri na shurutisho lililotolewa na Mungu na hajawahi kuthubutu kuvuka alama hiyo. Ingawa ni mwovu, Shetani ni “mwerevu” zaidi kuliko mwanadamu aliyepotoka; anajua utambulisho wa Muumba, na anajua mipaka yake. Kutokana na vitendo vya Shetani vya kunyenyekea tunaweza kuona kwamba mamlaka na nguvu za Mungu ni maagizo ya mbinguni ambayo hayawezi kukiukwa na Shetani, na kwamba ni kwa sababu hasa ya upekee na mamlaka ya Mungu ndio maana vitu vyote vinabadilika na kuzaliana katika njia ya mpangilio, kwamba wanadamu wanaweza kuishi na kuongezeka ndani ya mkondo uliowekwa na Mungu, hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kuvuruga mpangilio huu, na hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kubadilisha sheria hii—kwani vyote vinatoka kwenye mikono ya Muumba na kwenye mpangilio na mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

550. Ule utambulisho maalum wa Shetani umewafanya watu wengi waonyeshe kupendezwa sana na udhihirisho wake wa vipengele mbalimbali. Kuna hata watu wengi wapumbavu wanaoamini kwamba, kama vile Mungu, Shetani anamiliki mamlaka, kwani Shetani anaweza kuonyesha miujiza, na anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya. Kwa hivyo, mbali na kumwabudu Mungu, mwanadamu pia anahifadhi nafasi kwa Shetani moyoni mwake, na hata anamwabudu Shetani kama Mungu. Watu wote hawa ni wa kusikitikiwa na kuchukiwa. Ni wa kusikitikiwa kwa sababu ya ujinga wao, na ni wa kuchukiwa kwa sababu ya uzushi wao na asili yao ovu. Kwa wakati huu, Ninahisi kwamba ni muhimu niwafahamishe kuhusu maana ya mamlaka, yanaashiria nini, na yanawakilisha nini. Kwa mazungumzo ya jumla, Mungu Mwenyewe ni mamlaka, mamlaka Yake yanaashiria ukuu na kiini cha Mungu, na mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanawakilisha hadhi na utambulisho wa Mungu. Kwa hiyo, je, Shetani atathubutu kusema kwamba yeye ni Mungu? Je, Shetani atathubutu kusema kwamba aliumba vitu vyote, na anashikilia ukuu juu ya vitu vyote? Bila shaka hawezi! Kwa sababu hawezi kuumba vitu vyote; mpaka leo, hajawahi kuumba chochote kilichoumbwa na Mungu, na hajawahi kuumba chochote chenye uhai. Kwa sababu hana mamlaka ya Mungu, hawezi kamwe kumiliki hadhi na utambulisho wa Mungu, na hii inaamuliwa na kiini chake. Je, anazo nguvu sawa na za Mungu? Bila shaka hana! Je, tunaitaje matendo ya Shetani, na miujiza inayoonyeshwa na Shetani? Je, ni nguvu? Je, inaweza kuitwa mamlaka? Bila shaka sivyo! Shetani anaongoza wimbi la uovu, na kuvuruga, kuharibu, na kuingilia kila kipengele cha kazi ya Mungu. Kwa miaka elfu kadhaa iliyopita, mbali na kuwapotosha na kuwanyanyasa wanadamu, na kumrubuni na kumdanganya mwanadamu hadi kufikia kiwango cha uovu, na kumkataa Mungu, ili mwanadamu atembee kwenye bonde la uvuli wa mauti, je, Shetani amefanya jambo lolote linalostahili hata kuadhimishwa, kupongezwa, au kuthaminiwa na mwanadamu? Kama Shetani angekuwa na mamlaka na nguvu, je, wanadamu wangepotoshwa naye? Kama Shetani angekuwa na mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angepata madhara kutokana nayo? Kama Shetani anamiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angemwacha Mungu na kugeukia mauti? Kwa sababu Shetani hana mamlaka au nguvu, ni nini ambacho tunafaa kuhitimisha kuhusu kiini cha kila kitu anachofanya? Kunao wale wanaofafanua kila kitu ambacho Shetani anafanya kama hila tu, ilhali Ninaamini kwamba ufafanuzi kama huo haufai sana. Je, matendo maovu ya upotoshaji wake wa mwanadamu ni hila tu? Nguvu za maovu ambazo Shetani alimnyanyasia Ayubu, na tamanio lake la kikatili la kumnyanyasa na kumwangamiza, lisingeweza kutimizwa kwa hila tu. Tukiangalia nyuma, tunaona kwamba, mara moja, kondoo na ng’ombe wa Ayubu walitawanyishwa kila pahali katika milima na vilima, walitoweka; kwa muda mfupi tu, utajiri mwingi wa Ayubu ulitoweka. Je, inawezekana kwamba haya yote yalitimizwa kwa hila tu? Asili ya yale yote ambayo Shetani anafanya yanalingana na kuingiliana na mambo mabaya kama vile kudhoofisha, kuvuruga, kuharibu, kudhuru, uovu, nia mbaya, na giza, na kwa hivyo matukio haya yote ambayo si ya haki na ni maovu yanaunganishwa bila kutenganishwa na matendo ya Shetani, na hayawezi kutenganishwa na kiini kiovu cha Shetani. Haijalishi jinsi Shetani “alivyo na nguvu”, haijalishi jinsi Shetani alivyo jasiri na mwenye tamaa ya makuu, haijalishi jinsi uwezo wake ulivyo mkubwa katika kusababisha uharibifu, haijalishi jinsi zilivyo nyingi mbinu anazotumia kumpotosha na kumshawishi mwanadamu, haijalishi jinsi zilivyo mahiri hila na njama zake anazotumia kumtishia mwanadamu, haijalishi jinsi mfumo wa kuwepo kwake unavyoweza kubadilika, hajawahi kuweza kuumba hata kiumbe kimoja kilicho hai, hajawahi kuweza kuweka sheria au kanuni za kuwepo kwa vitu vyote, na hajawahi kutawala na kudhibiti kitu chochote, kiwe ni chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Katika ulimwengu na anga, hakuna hata mtu au kitu kimoja kilichotokana na Shetani, au kilichopo kwa sababu ya Shetani; hakuna hata mtu au kitu kimoja ambacho kinatawaliwa na Shetani, au kudhibitiwa na Shetani. Kinyume chake ni kwamba, sio tu kuwa hana budi kuishi chini ya utawala wa Mungu, lakini, vilevile, lazima atii masharti na amri zote za Mungu. Bila ruhusa ya Mungu, ni vigumu sana kwa Shetani kugusa hata tone la maji au chembe ya mchanga juu ya nchi; bila ruhusa ya Mungu, Shetani hana hata uhuru wa kusogeza mchwa wanaotembea juu ya nchi, licha ya wanadamu, ambao waliumbwa na Mungu. Machoni pa Mungu, Shetani ni duni kuliko yungiyungi mlimani, kuliko ndege warukao angani, kuliko samaki wa baharini, na kuliko funza juu ya nchi. Jukumu lake miongoni mwa vitu vyote ni kutumikia vitu vyote, kuwatumikia wanadamu, na kuhudumia kazi ya Mungu na mpango Wake wa usimamizi. Haijalishi jinsi asili yake ilivyo na nia mbaya, na jinsi kiini chake kilivyo kiovu, kitu pekee anachoweza kufanya ni kutii jukumu lake: kuwa mtoa huduma kwa Mungu, na kutoa kipingamizi kwa Mungu. Hicho ndicho kiini na nafasi ya Shetani. Asili yake haijaunganishwa na maisha, haijaunganishwa na nguvu, haijaunganishwa na mamlaka; ni kitu tu cha kuchezea mikononi mwa Mungu, ni mashine tu ya kutoa huduma kwa Mungu!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

551. Ingawa Shetani alimtazama Ayubu kwa macho ya tamaa, bila ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja kwenye mwili wa Ayubu. Ingawa Shetani kwa asili ni mwovu na mkatili, baada ya Mungu kutoa agizo lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo ila kutii amri yaMungu. Na kwa hivyo, hata Ingawa Shetani alionekana kana kwamba ameshikwa na kichaa sawa na mbwa-mwitu miongoni mwa kondoo alipomjia Ayubu, hakuthubutu kusahau mipaka aliyowekewa wazi na Mungu, hakuthubutu kukiuka maagizo ya Mungu, na kwa hayo yote, Shetani hakuthubutu kutoka kwenye kanuni ya maneno ya Mungu—je, hii si kweli? Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba Shetani hathubutu kukiuka matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwa Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni amri, na sheria ya mbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu kunadokezwa adhabu ya Mungu kwa wale wanaokiuka maagizo ya Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za mbinguni. Shetani anajua wazi kwamba kama atakiuka maagizo ya Mungu, basi lazima akubali athari za kukiuka mamlaka ya Mungu na kupinga sheria za mbinguni. Na sasa athari hizi ni zipi? Sina haja ya kusema kwamba, athari hizi bila shaka, ni adhabu kutoka kwa Mungu. Vitendo vya Shetani kwa Ayubu vilikuwa ni mfano mdogo tu wa upotoshaji wake kwa mwanadamu, na Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, mipaka ambayo Mungu aliweka na maagizo ambayo Alitoa kwa Shetani ilikuwa ni mfano mdogo tu wa kanuni zilizo nyuma ya kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa Shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu. Ni onyo gani ambalo mifano hii midogo inakupa? Miongoni mwa vitu vyote, ikiwa ni pamoja na Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kitu kinachoweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za mbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa vitu vyote, na hivyo, haiwezekani kusema kwamba “Mungu ndiye mkuu na Shetani ni namba mbili.” Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwingine.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

552. Shetani amekuwa akiwapotosha wanadamu kwa maelfu ya miaka. Ametenda maovu mengi sana, amepotosha kizazi baada ya kizazi, na amefanya uhalifu wa kutisha duniani. Amemdhulumu mwanadamu, kumpotosha mwanadamu, kumshawishi mwanadamu kumpinga Mungu, na amefanya matendo maovu ambayo yamesumbua na kuharibu mpango wa usimamizi wa Mungu mara kwa mara. Hata hivyo, chini ya mamlaka ya Mungu, vitu vyote na viumbe vyenye uhai vinaendelea kutii kanuni na sheria zilizowekwa wazi na Mungu. Ikilinganishwa na mamlaka ya Mungu, asili ovu ya Shetani na kuenea kwake ni vitu vibaya mno, vinakera mno na ni vya kuleta aibu na ni vidogo mno na vinyonge. Hata Ingawa Shetani anatembea kati ya vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, hawezi kutekeleza mabadiliko madogo zaidi kwa watu, vitu, na vifaa vilivyoamriwa na Mungu. Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia vitu vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku bado zinabadilishana bila kukoma; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje juu ya nchi wanaimba kwa mioyo yao kwenye siku za kiangazi; chenene kwenye nyasi wanaimba kwa sauti za polepole huku wakikaribisha msimu wa vuli, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia peke yao; makundi ya simba yanajitosheleza yenyewe kwa kuwinda; nao kulungu hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni moja yanatokea kwa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kuishi. Wanaishi chini ya riziki na usitawishaji wa Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawa mwanadamu, anayeishi miongoni mwa vitu vyote, amepotoshwa na kudanganywa na Shetani, mwanadamu bado hawezi kuacha maji yaliyoumbwa na Mungu, na, na, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu bado anaishi na kuzaliana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu bado hazijabadilika. Binadamu bado anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na nyayo zake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali utoaji wa Mungu umebaki bila kubadilishwa, uwezo ambao kupitia huo mwanadamu anashirikiana na Mungu haujabadilika, uwezo wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili yake haijabadilika, shauku ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi chini ya mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawa mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena ambao waliumbwa hapo mwanzo, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira, dhana na kadhalika, na amejaa tabia potovu za kishetani, machoni pa Mungu, mwanadamu bado ni mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu bado yuko chini ya ukuu na mipangilio ya Mungu, na bado anaishi ndani ya mkondo uliowekwa na Mungu, na hivyo machoni pa Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya polepole kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na ni ya zamani kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Hawa ndio wanadamu ambao Mungu anakusudia kuwaokoa. Wanadamu hawa wanahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona sura ya Muumba na atapuuzia mengine yote, na kuacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wanadamu wanapofahamu kutoka mioyoni mwao sauti ya moyo wa Muumba, watamkataa Shetani na kuja upande wa Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine tena utolewaji na utunzaji wa Muumba, kumbukumbu ya mwanadamu itarejeshwa na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

553. Mamlaka ya Mungu hayawezi kuigwa na binadamu, na utambulisho na hadhi ya Mungu haiwezi kuigizwa na binadamu. Ingawa unaweza kuiga sauti ambayo Mungu huongea nayo, huwezi kuiga kiini cha Mungu. Ingawa unaweza kusimama katika nafasi ya Mungu na kujifanya kuwa Mungu, hutawahi kuweza kufanya kile ambacho Mungu ananuia kukifanya, na hutawahi kutawala na kuamuru vitu vyote. Katika macho ya Mungu, utabakia kuwa kiumbe kidogo, na haijalishi ni vipi ambavyo mbinu na uwezo wako ulivyo mkubwa, haijalishi ni vipaji vingapi unavyo, vitu vyote kuhusu wewe vipo chini ya utawala wa Muumba. Ingawa unaweza kusema baadhi ya maneno yenye ukali, hilo haliwezi kuonyesha kwamba una kiini cha Muumba, wala kuwakilisha ya kwamba unamiliki mamlaka ya Muumba. Mamlaka na nguvu za Mungu ni kiini cha Mungu Mwenyewe. Hayakufunzwa wala kusomwa, au kuongezewa kutoka nje, lakini ni kiini cha Mungu Mwenyewe. Na kwa hivyo uhusiano kati ya Muumba na viumbe vilivyoumbwa hauwezi kamwe kubadilishwa. Kama mmoja wa wanadamu walioumbwa, lazima ushikilie nafasi yako inayofaa, na ujiendeshe kwa adabu. Shikilia kwa uwajibikaji kile ulichokabidhiwa na Muumba. Usivuke mipaka, au kufanya mambo yaliyo nje ya upeo wa uwezo wako au ambayo yanamchukiza Mungu. Usifuatilie kuwa mtu mkuu, mtu mwenye uwezo upitao wa kibinadamu, au mtu adhimu sana, na usifuatilie kuwa Mungu. Yote haya ni matamanio ambayo watu hawapaswi kuwa nayo. Kufuatilia kuwa mtu mkuu au mtu mwenye uwezo upitao wa kibinadamu ni upuuzi. Kufuatilia kuwa Mungu ni jambo la aibu zaidi; ni jambo la kuchukiza, na la kudharauliwa. Kilicho cha thamani kweli, na kile ambacho viumbe walioumbwa wanapaswa kushikilia kuliko kitu kingine chochote, ni kuwa kiumbe aliyeumbwa wa kweli; hili ndilo lengo pekee ambalo watu wote wanapaswa kufuatilia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Iliyotangulia: XI. Maneno Juu ya Kumjua Mungu

Inayofuata: B. Kuhusu Tabia ya Haki ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp