385 Kusudi la Mipangilio ya Mungu kwa Mwanadamu

1 Kama unaamini katika utawala wa Mungu, basi lazima uamini kuwa mambo ambayo hutokea kila siku, yawe mema au mabaya, si matukio ya kubahatisha. Sio kwamba mtu fulani ni mkali kwako au anakulenga kwa makusudi; yote kwa kweli husafidiwa na kupangwa na Mungu. Kwa nini Mungu hupanga mambo haya? Sio ili kuzifichua kasoro zako au kukukashifu; kukukashifu si lengo la mwisho. Lengo la mwisho ni kukukamilisha na kukuokoa. Mungu anafanyaje hilo? Kwanza, Anakufanya ufahamu tabia yako potovu, kufahamu asili na hali yako, kasoro zako, na kile unachokosa. Ni kwa kuelewa mambo haya yaliyomo katika moyo wako tu ndiyo utaweza kufuatilia ukweli na kuacha tabia yako potovu hatua kwa hatua. Huku ni Mungu kukupa fursa.

2 Kama unaamini katika utawala wa Mungu, basi lazima uamini kuwa mambo ambayo hutokea kila siku, yawe mema au mabaya, si matukio ya kubahatisha. Sio kwamba mtu fulani ni mkali kwako au anakulenga kwa makusudi; yote kwa kweli husafidiwa na kupangwa na Mungu. Lazima ujue jinsi ya kuitumia fursa hii na usiwe mkaidi kwa Mungu. Hasa unapokabiliwa na watu, matukio, na mambo ambayo Mungu anapanga kando yako, usifikiri kila mara kwamba mambo hayako kama unavyotaka yawe, kila mara ukitaka kutoroka, kila mara ukimlaumu na kumwelewa Mungu visivyo. Huko si kuipitia kazi ya Mungu, na hiyo itafanya iwe vigumu sana kwako kuingia katika uhalisi wa ukweli. Lolote lile ambalo huwezi kulielewa kikamilifu, wakati ambapo una matatizo, lazima ujifunze kutii. Unapaswa kwanza kuja mbele ya Mungu na kuomba zaidi. Kwa njia hiyo, kabla ya wewe kujua kutakuwa na mabadiliko katika hali yako ya ndani na utaweza kutafuta ukweli ili kutatua tatizo lako utaweza kuipitia kazi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 384 Maana ya Kweli ya Imani kwa Mungu

Inayofuata: 386 Kusudi Ambalo Mwanadamu Anapaswa Kuwa Nalo Katika Imani Yake kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp