84 Mungu Amhukumu na Kumkamilisha Mwanadamu kwa Maneno Yake Katika Siku za Mwisho

1 Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika maisha ya mwanadamu, kuonyesha yale ambayo mwanadamu anapaswa kuingia kwayo, kumwonesha mwanadamu matendo ya Mungu, na kumwonesha mwanadamu hekima, uweza na uajabu wa Mungu. Kupitia njia nyingi ambazo Mungu Anazungumza, mwanadamu anatazama ukuu wa Mungu, aidha, unyenyekevu na usiri wa Mungu. Mwanadamu anatazama kwamba Mungu ni mkuu, lakini ni mnyenyekevu na msiri, na Anaweza kuwa mdogo kuliko vitu vyote. Baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa Roho, baadhi ya hayo moja kwa moja kutoka katika mtazamo wa mwanadamu, na baadhi kutoka katika mtazamo wa nafsi ya tatu. Katika hili, inaweza kuonekana kwamba namna ya kazi ya Mungu inatofautiana kwa kiasi kikubwa na ni kwa njia ya maneno ndipo Anamruhusu mwanadamu kuiona.

2 Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu; kufunuliwa kwa tabia potovu ya mwanadamu na kiini cha asili ya mwanadamu; na uondoaji wa fikira za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa usimamizi wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 83 Maelezo ya Ndani ya Maneno ya Mungu Katika Siku za Mwisho

Inayofuata: 85 Hukumu kwa Neno Inawakilisha Mamlaka ya Mungu Bora Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp