269 Mungu Anautafuta Moyo Wako na Roho Yako

1 Wanadamu, baada ya kuuwacha utoaji wa uzima kutoka kwa Mwenye uweza, hawajui azma ya kuishi, lakini hata hivyo wanaogopa kifo. Hawana usaidizi wala msaada, lakini bado wanasita kufumba macho yao, na wanajitayarisha kuendeleza uwepo wa aibu ulimwenguni humu, magunia ya miili wasio na hisia za roho zao wenyewe. Unaishi hivi, bila matumaini, kama vile wafanyavyo wengine, bila lengo. Kuna aliye Mtakatifu tu katika hekaya atakayekuja kuwaokoa watu ambao, wakiwa wanapiga kite katika mateso yao, wanatamani sana kufika Kwake. Hadi sasa, imani hii haijafikiwa kwa wale ambao hawana fahamu. Hata hivyo, watu bado wanaitaka sana.

2 Mwenye uweza ana rehema kwa watu hawa ambao wameteseka sana. Wakati uo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na fahamu, maana imembidi Asubiri sana kupata jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kutafuta, kuutafuta moyo wako na roho yako, kukuletea chakula na maji na kukuzindua, ili usione kiu na kuhisi njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote.

3 Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo utarudisha ghafla kumbukumbu yako: ukitambua ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, lakini wakati fulani usiojulikana ukapoteza mwelekeo wako, wakati fulani usiojulikana ukaanguka barabarani ukiwa hujitambui na tena wakati fulani usiojulikana ukampata “baba.” Isitoshe, unagundua kuwa Mwenye uweza amekuwa hapo muda huo wote, akiangalia, akisubiri kurejea kwako, kwa muda mrefu sana.

4 Amekuwa akitazama na tamanio kubwa, Akingoja itiko pasipo jibu. Kusubiri Kwake kunazidi thamani, na ni kwa ajili ya moyo na roho ya wanadamu. Pengine kusubiri huku hakuna mwisho, na pengine kumefikia mwisho. Lakini unapaswa kujua moyo wako na roho yako hasa viko wapi sasa hivi.

Umetoholewa kutoka katika “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 268 Jinsi Shetani Atumiavyo Mitindo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu

Inayofuata: 270 Mungu Anatafuta Wale Walio na Kiu ya Kuonekana Kwake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp