111 Mungu Ndiye Mkuu wa Mpango wa Usimamizi wa Miaka Elfu Sita
1 Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho; ni Yeye Mwenyewe ndiye Anayeanzisha kazi Yake na hivyo lazima iwe ni Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani na huishinda dunia. Kila wakati Yeye Mwenyewe Anapofanya kazi miongoni mwa mwanadamu, ni mwanzo wa mapigano mapya. Bila mwanzo wa kazi mpya, kwa kawaida hakutakuwa na kikomo kwa enzi ya kale. Na bila kikomo kwa enzi ya kale ina maana kuwa vita na Shetani havijafika mwisho. Ni kama tu Mungu Mwenyewe Anakuja miongoni mwa mwanadamu na kutenda kazi mpya ndipo mwanadamu atakapoweza kujitoa kutoka katika umiliki wa Shetani na kupata maisha na mwanzo mpya. Vinginevyo, mwanadamu ataishi milele katika wakati wa kale na milele kuishi katika ushawishi wa kale wa Shetani.
2 Kazi ya Mungu hufanywa na Mungu Mwenyewe. Ni Yeye ndiye Anayeweka kazi katika mwendo, na pia Yeye ndiye Anayemaliza. Ni Yeye ndiye hupanga kazi, na pia Yeye ndiye Anayesimamia, na zaidi ya hayo, ni Yeye ndiye Anayeleta kazi kuzaa matunda. Ni ilivyoandikwa katika Biblia, “Mimi ndiye Mwanzo na Mwisho: Mimi ndiye Mpanzi na Mvunaji.” Yote yanayohusiana na usimamizi wa kazi Yake yanafanywa na mkono Wake. Yeye ndiye Mtawala wa mpango wa miaka elfu sita; hakuna anayeweza kufanya kazi Yake kwa niaba Yake ama kuleta kazi Yake hadi mwisho, kwani Yeye ndiye Aliye katika uongozi wa yote. Kwa kuwa Aliumba dunia, Ataongoza ulimwengu mzima kuishi katika nuru Yake, na Atamaliza enzi yote na kuleta mpango Wake wote kwa mafanikio!
Umetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili