779 Mungu Anatumaini Mwanadamu Anaweza Kumjua na Kumwelewa

1 Tangu Mungu alipojihusisha kwanza na wanadamu, Alianza kuweka wazi kwa mwanadamu, bila kusita, kiini Chake halisi na kile Anacho na alicho. Licha ya kama watu wa awali au watu wa leo wanaweza kuona au kuelewa kiini hicho, kwa ufupi Mungu anamzungumzia mwanadamu na kufanya kazi miongoni mwa binadamu, Akifichua tabia Yake na Akionyesha kiini Chake—jambo ambalo ni ukweli, na lisilopingika na mtu yeyote.

2 Hii inamaanisha pia kwamba tabia ya Mungu, kiini cha Mungu, na kile Anacho na alicho vyote vinatolewa daima na kufichuliwa huku naye Akifanya kazi na kujihusisha na binadamu. Hajawahi kusetiri au kumfichia binadamu chochote, lakini badala yake anatangaza kwa umma na kuachilia tabia Yake binafsi bila ya kuficha chochote.

3 Mungu anatumai kwamba binadamu anaweza kumjua Yeye na kuielewa tabia Yake na kiini chake. Hapendi binadamu kuchukulia tabia Yake na kiini Chake kuwa mafumbo ya milele, wala Hataki wanadamu kumchukulia Mungu kama fumbo lisiloweza kutatuliwa. Mpaka tu pale ambapo wanadamu watakapomjua Mungu ndipo binadamu atakapojua njia ya kufuata na kuweza kuukubali mwongozo wa Mungu, na wanadamu tu kama hawa ndio wanaoweza kuishi kwa kweli katika utawala wa Mungu, na kuishi katika mwangaza, na kuishi katikati ya baraka za Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 778 Watu Wanapaswa Kutafuta Kuishi kwa Kudhihirisha Maisha ya Maana

Inayofuata: 780 Mungu Anataka Kuwapata Wale Walio na Maarifa ya Kweli Kumhusu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp