116 Mungu Amekuwa Akifanya Kazi Kumwongoza Mwanadamu Daima

1 Tangu kuwepo kwa usimamizi wa Mungu, siku zote amejitolea kabisa katika kutekeleza kazi Yake. Licha ya kuficha nafsi Yake kutoka kwao, siku zote Amekuwa katika upande wa binadamu, akiwafanyia kazi, akionyesha tabia Yake, akiongoza binadamu wote na kiini Chake, na kufanya kazi Yake kwa kila mmoja kupitia nguvu Zake, hekima Yake, na mamlaka Yake, hivyo akiileta Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na sasa Enzi ya Ufalme katika uwepo. Ingawaje Mungu huificha nafsi Yake kutoka kwa binadamu, tabia Yake, uwepo Wake na miliki Yake, na mapenzi Yake kwa binadamu yanafichuliwa bila wasiwasi wowote kwa binadamu kwa minajili ya kuona na kupitia hali hiyo. Kwa maneno mengine, ingawaje binadamu hawawezi kumwona au kumgusa Mungu, tabia na kiini cha Mungu ambacho binadamu wamekuwa wakigusana nacho ni maonyesho kabisa ya Mungu Mwenyewe.

2 Licha ya ni mbinu gani au ni kutoka katika mtazamo gani Mungu hufanya kazi Yake, siku zote Anawatendeakaribisha watu kulingana na utambulisho Wake wa kweli, akifanya kile ambacho Anafaa kufanya na kusema kile Anachofaa kusema. Haijalishi ni nafasi gani Mungu anazungumzia kutoka—Anaweza kuwa amesimama kwenye mbingu ya tatu, au amesimama akiwa mwili Wake, au hata kama mtu wa kawaida—siku zote Anaongea kwa binadamu kwa moyo Wake wote na kwa akili Zake zote, bila uongo na bila ufichaji wowote. Wakati Anapotekeleza kazi Yake, Mungu huonyesha neno Lake na tabia Yake, na huonyesha kile Anacho na alicho, bila kuficha chochote. Anamwongoza mwanadamu na maisha Yake na uwepo Wake na miliki yake.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 115 Usimamizi wa Mungu Unasonga Mbele Daima

Inayofuata: 117 Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho ni ya Kina Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp