520 Mungu Atawabariki Wale Wanaofuatilia Ukweli kwa Dhati
1 Ni nini kufundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu, ni nini lawama inayotokana na nia ya mwanadamu, ni nini mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini mpango wa mazingira, ni nini maneno ya Mungu yanatolea nuru ndani, kama huna uhakika juu ya mambo haya, hutakuwa na utambuzi. Unapaswa kujua kile ambacho huja kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini tabia ya uasi, jinsi ya kulitii neno la Mungu, na jinsi ya kuacha uasi wako mwenyewe; ikiwa una ufahamu wa vitendo wa mambo haya, utakuwa na msingi; kitu kinapotendeka, utakuwa na ukweli unaofaa wa kutumia kukipima na maono yanayofaa kama msingi. Utakuwa na kanuni katika kila kitu unachofanya, na utaweza kutenda kulingana na ukweli. Halafu maisha yako yatajazwa na nuru ya Mungu, yatajazwa na baraka za Mungu.
2 Ikiwa, unapokula na kunywa maneno ya Mungu, unaweza kuzingatia hali yako mwenyewe ya kweli, kuzingatia vitendo vyako mwenyewe, na kuzingatia ufahamu wako mwenyewe, basi, unapokabiliwa na tatizo, utapokea nuru na utapata ufahamu wa utendaji. Kisha utakuwa na njia ya kutenda na utakuwa na utambuzi kwa kila kitu. Mtu aliye na ukweli si rahisi kudanganywa, na rahisi kutenda kwa vurugu au kutenda kwa kupita kiasi. Kwa sababu ya ukweli amelindwa, na pia kwa sababu ya ukweli yeye hupata ufahamu zaidi. Kwa sababu ya ukweli ana njia zaidi za kutenda, hupata fursa zaidi za Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yake, na hupata fursa zaidi za kukamilishwa.
Mungu hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye humtafuta kwa kweli. Hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye huishi kwa kumdhihirisha na ambaye hushuhudia kwa ajili Yake, na hatamlaani mtu yeyote ambaye kwa kweli anaweza kuona kiu ya ukweli.
Umetoholewa kutoka katika “Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili