92 Katika Siku za Mwisho, Mungu Anatimiza Yote Kupitia Maneno Yake

1 Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa umuhimu na kiini cha mpango huu wa usimamizi wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kuelewa kabisa. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia.

2 Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kufanya kazi ya ukamilishaji? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kukamilisha. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno.

3 Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.

Umetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 91 Kazi ya Siku za Mwisho ni Hasa ili Kumpa Mwanadamu Uzima

Inayofuata: 93 Katika Enzi ya Ufalme, Neno Linatimiza Kila Kitu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp