274 Tambua Kuwa Kristo Ni Ukweli Milele

1

Hapo zamani, nilipomwamini Bwana, sikujua uhalisi wa ukweli.

Sikuweza kutofautisha kati ya viongozi wa kweli, na viongozi wa uwongo na wapinga Kristo.

Ningestahi, kuabudu, kufuata yoyote ambaye aliweza kueleza nadharia za Biblia.

Nilidhani kwamba yeyote aliyefanya kazi na kuteseka sana kwa ajili ya kanisa alikuwa kiongozi mzuri.

Nilifikiria kwa ujinga kuwa kwa kuwafuata, ningeingia katika ufalme wa mbinguni.

2

Ni baada tu ya kupata hukumu ndipo niligundua jinsi kufikiria kwangu kulivyokuwa kwa ujinga na kwa kuchekesha,

Sikuwahi kuwatambua watu kwa ukweli, lakini kwa dhana na mawazo.

Nilifanya chochote ambacho kiongozi alisema na nilidhani kwamba nilikuwa nikimtii Mungu.

Niliabudu hadhi na mamlaka, Mungu hakuwa na nafasi hata kidogo moyoni mwangu.

Ni leo tu ndipo natambua jinsi imani yangu katika Mungu ilivyokuwa potovu.

3

Leo, natambua vyema jinsi ilivyo vigumu kupata ukweli na uzima katika kumwamini Mungu.

Ni kwa kupitia tu hukumu ya Mungu na kutenda ukweli ndipo ninaweza kumjua Mungu kwa kweli.

Wakati ambapo watu hawamjui Mungu, hata kama mwenendo wao ni mzuri, bado ni unafiki.

Bila kujali dhana na mawazo ya watu ni mazuri kiasi gani, ni uwongo, na hayalingani na ukweli.

Maneno ya Mungu tu ndiyo ukweli, maneno Yake tu ndiyo yanayoweza kuwatakasa na kuwaokoa watu.

4

Tunapomwamini Mungu, ni lazima tuamini kuwa Kristo ndiye ukweli, na hatupaswi kuwafuata watu.

Tunapoelewa ukweli na kumjua Mungu, tutaweza kutambua aina tofauti za watu kwa urahisi.

Tunapomwamini Mungu, lazima tu tutende utiifu kwa ukweli wa maneno ya Mungu, na lazima tujihadhari na watu.

Bila ukweli, bila uwezo wa kutofautisha, hatuna budi kudanganywa, na kujiletea maangamizo.

Ni tunapotambua tu kuwa Kristo ni ukweli milele ndipo tunaweza kufuata kwa uaminifu hadi mwisho.

Iliyotangulia: 273 Sitapumzika Mpaka Nipate Ukweli

Inayofuata: 275 Wimbo wa Onyo Jema

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp