271 Upendo wa Mwenyezi Mungu Ndio Safi Zaidi

1

Ee Mungu! Umekuwa mwili na kuacha kila kitu ili kuwaokoa wanadamu.

Hujawahi kupata upendo kati ya wanadamu au kupata moyo wa mwanadamu.

Umeonja uchungu wote wa ulimwengu,

Ukifanya kazi kimya kimya kwa miongo kadhaa.

Maneno Uliyoonyesha yote ni ukweli wa kumletea mwanadamu njia ya uzima wa milele.

Lakini watu hawajui, wanakushutumu na kukukashifu,

wakikataa kukubali wokovu Wako.

Umevumilia dhihaka lakini bado unawagusa watu kupitia upendo,

ukiwaokoa wanadamu kwa kiwango kikubwa zaidi.

Ee Mungu! Umempa mwanadamu mapenzi Yako yote bila ubinafsi.

Mbinguni na duniani ni Wewe tu ndiwe upendo,

upendo wa Mwenyezi Mungu ndio safi zaidi.

2

Ee Mungu! Ukweli Unaoonyesha kuhukumu na kuadibu vyote ni ili kuwaokoa wanadamu.

Maneno Yako yanafichua asili ya mwanadamu,

ugumu na majaribio hutakasa upotovu wa mwanadamu.

Unapanga watu, matukio, na vitu ili kutusaidia kuelewa ukweli.

Lakini hatuelewi mapenzi Yako, tunashikilia fikira na hatuwezi kutii mipango Yako.

Tunaepuka hukumu Yako, sisi ni wakaidi na waasi,

tunakosa mantiki yote na tumeuumiza moyo Wako sana.

Umekuwa mvumilivu na mstahimilivu daima, ukitulisha na kutunyunyizia,

mioyo yetu isiyo na hisia sasa inajua.

Ee Mungu! Umefanya kazi kwa moyo Wako wote ili kutuokoa,

Ukilipa gharama ya maisha.

Mbinguni na duniani ni Wewe tu ndiwe upendo,

upendo wa Mwenyezi Mungu ndio safi zaidi.

Mwenyezi Mungu! Unastahili upendo wa mwanadamu,

tutakupenda daima na kukushuhudia.

Iliyotangulia: 270 Upendo wa Mungu Ni Halisi Kweli

Inayofuata: 272 Kujitolea Kwa Upendo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki