C. Kuhusu Enzi ya Ufalme–Enzi ya Mwisho
33. Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji
34. Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi ya Shetani ilikuwa imepandwa ndani yake tayari. Baada ya miaka mingi ya upotovu wa Shetani, mwanadamu tayari ana asili ndani yake inayompinga Mungu. Hivyo, mwanadamu atakapokombolewa, hakitakuwa kitu kingine ila ni ukombozi, ambapo mwanadamu ananunuliwa kwa gharama kuu, lakini asili ya sumu ndani yake haijaondolewa. Mwanadamu ambaye amechafuliwa lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa wa kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. Kwa mfano, wakati ambapo watu walijua kwamba walitoka kwa Moabu, walitoa maneno ya malalamiko, hawakutafuta tena uzima, na wakawa hasi kabisa. Je, hili halionyeshi kwamba bado hawawezi kutii kwa ukamilifu kutawaliwa na Mungu? Je, hii siyo tabia ya kishetani ya upotovu kabisa? Ulipokuwa hupitii kuadibu, mikono yako iliinuliwa juu zaidi ya wengine wote, hata ile ya Yesu. Na ulilia kwa sauti kubwa: “Kuwa mwana mpendwa wa Mungu! Kuwa mwandani wa Mungu! Ni heri tufe kuliko kumtii Shetani! Muasi Shetani wa zamani! Liasi joka kuu jekundu! Acha joka kuu jekundu lianguke kabisa kutoka mamlakani! Acha Mungu atufanye kamili!” Vilio vyako vilikuwa vikubwa zaidi ya wengine. Lakini kisha ukaja wakati wa kuadibu na, mara tena, tabia ya upotovu ya watu ilifichuliwa. Kisha, vilio vyao vikakoma, na hawakuwa tena na azimio. Huu ni upotovu wa mwanadamu; unaingia ndani zaidi kuliko dhambi, ulipandwa na Shetani na umekita mizizi ndani zaidi ya mwanadamu. Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)
35. Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini hili halikumaanisha kuwa mwanadamu hakuwa na dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)
36. Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli
37. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli
38. Wanadamu kwa ajili ya kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumcha kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. Wanadamu watashindwa vipi hasa? Watapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kwa dhati; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma dhibiti kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimu wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu. Kwa kiwango kikubwa, ni matumizi ya maneno haya yatakayomshinda mwanadamu na kumshawishi kabisa. Maneno ndiyo njia ya kuwashinda wanadamu na wote wanaokubali ushindi lazima wakubali mapigo na hukumu ya maneno.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)
39. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno "maneno" linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno
40. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, “Neno kuonekana katika mwili”; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapumziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaufanyikia Misri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu
41. Leo Mungu Amekuwa mwili kimsingi ili kukamilisha kazi ya “Neno kuonekana katika mwili,” kutumia neno kumfanya mwanadamu kamili, na kumfanya mwanadamu kukubali ushughulikiaji wa neno na usafishaji wa neno. Katika maneno Yake, anakufanya kupata kupewa na kupata uzima; katika maneno Yake, unaona kazi Yake na matendo. Mungu Anatumia neno kukuadibu na kukutakasa, na hivyo ukipata ugumu wa maisha, ni pia kwa sababu ya neno la Mungu. Leo, Mungu hafanyi kazi kwa kutumia mambo ya hakika, ila ni kwa maneno. Baada tu ya neno Lake kuja juu yako ndipo Roho Mtakatifu Atafanya kazi ndani yako na kukufanya upate uchungu ama uhisi utamu. Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukuleta katika hali halisi, na ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukufanya mkamilifu. Kwa hivyo, angalau lazima uelewe hili: Kazi inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho kimsingi ni kutumia neno Lake kumfanya kila mwanadamu kamili na kumwongoza mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ni kupitia kwa neno; Hatumii ukweli kuadibu. Kuna wakati ambapo watu wengine humpinga Mungu. Mungu hasababishi ukosefu mkubwa wa starehe kwako, mwili wako hauadibiwi wala wewe kupitia ugumu—lakini pindi tu neno Lake linapokuja juu yako, na kukutakasa, hutaweza kuvumilia. Je si hivyo ndivyo ilivyo? Wakati wa “watendaji huduma” Mungu Alisema mwanadamu atupwe katika shimo lisilo na mwisho. Mwanadamu aliweza kufika kwenye shimo lisilo na mwisho? Kupitia kwa maneno tu kumtakasa mwanadamu, mwanadamu aliingia kwenye shimo lisilo na mwisho. Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha. Hii ni kwa sababu Amekuja kimsingi kufanya kazi hii, kumruhusu mwanadamu aone nguvu Zake na ukuu ulio kwenye neno Lake, kumruhusu mwanadamu kuona kupitia kwa maneno Yake jinsi Alivyojificha kwa unyenyekevu, na kumruhusu mwanadamu kujua ukamilifu Wake kupitia kwa maneno Yake. Kila kitu Alicho nacho na kile Alicho kiko katika maneno Yake, hekima Yake na ajabu yako katika maneno Yake. Katika hii ndipo unapofanywa kuona mbinu nyingi ambazo Mungu anatumia kuongea maneno Yake. Kazi ya Mungu nyingi katika wakati huu wote imekuwa kutoa, ufunuo, na kushughulika mwanadamu. Hatoi laana kwa mwanadamu kijuu juu, na hata Akifanya hivyo, ni kupitia kwa neno. Na hivyo, katika enzi hii ya Mungu kuwa mwili, usijaribu kuona Mungu akiponya wagonjwa na kufukuza mapepo tena, usijaribu kila mara kuona ishara—hakuna haja! Ishara hizo haziwezi kumfanya mwanadamu kamili! Kuongea wazi: Leo Mungu wa kweli Mwenyewe wa mwili Anaongea tu, na hatendi. Huu ni ukweli! Anatumia maneno kukufanya mkamilifu, na Anatumia maneno kukulisha na kukunyunyizia. Pia Anatumia maneno kufanya kazi, na Anatumia maneno badala ya uhakika kukufanya ujue ukweli Wake. Kama una uwezo wa kutazama aina hii ya kazi ya Mungu, basi itakuwa vigumu kuwa wa kutoonyesha hisia. Badala ya kulenga vitu vilivyo vibaya, mnapaswa tu kulenga yale yaliyo mazuri—hivyo ni kusema, bila kujali kama maneno ya Mungu yamekamilika au la, ama iwapo kuna majilio ya ukweli ama haupo, Mungu anamfanya mwanadamu kupata uzima kutoka kwa maneno Yake, na hii ndiyo ishara kuu kushinda zote, na hata zaidi, ni ukweli usiopingika. Huu ndio ushahidi bora wa kupata ufahamu kumhusu Mungu, na ni ishara hata kuu kushinda ishara. Maneno haya pekee yanaweza kumfanya mwanadamu kamili.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu
42. Katika siku za mwisho, Mungu hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kumfanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu. Hili ndilo lengo la kazi Anayofanya na maneno Anenayo. Mungu hatumii mbinu ya kuonyesha ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kamili—Anatumia maneno, na Anatumia mbinu nyingi za kazi kumfanya mwanadamu kamili. Iwe ni usafishaji, kushughulikia, upogoaji, ama kupewa maneno, Mungu hunena kutoka taswira nyingi tofauti kumfanya mwanadamu kamili, na kumpa mwanadamu maarifa kuu ya kazi, hekima na ajabu ya Mungu. … Nimesema hapo awali kuwa kikundi cha washindi wanapatwa kutoka Mashariki, washindi ambao wanatoka katika mashaka makubwa. Je maneno haya yana maana gani? Yanamaanisha kuwa watu hao ambao wamepatwa waliamini kwa kweli tu baada ya kupitia hukumu na kuadibu, na kushughulikiwa na kupogolewa, na aina yote ya usafishaji. Imani ya watu kama hao si isiyo dhahiri na dhahania, bali ni ya kweli. Hawajaona ishara na maajabu yoyote, ama miujiza yoyote; hawazungumzi kuhusu barua ngumu kueleweka na kanuni, ama mitazamo ya muhimu sana; badala yake, wana ukweli, na maneno ya Mungu, na maarifa ya kweli kuhusu ukweli wa Mungu. Je kikundi hiki hakina uwezo wa kuweka wazi nguvu za Mungu?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu
43. Wakati wa siku za mwisho, Mungu katika mwili Amekuja duniani hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno. Yesu Alipokuja, Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni, na Akatimiza kazi ya wokovu wa msalaba. Alihitimisha Enzi ya Sheria, na Akakomesha mambo yote ya kale. Ujio wa Yesu ulihitimisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema. Ujio wa Mungu katika mwili wa siku za mwisho umehitimisha Enzi ya Neema. Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake, kutumia maneno ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, kumwangazia na kumpa nuru mwanadamu, na kumwondoa Mungu asiye yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii sio hatua ya kazi ambayo Yesu Aliifanya Alipokuja. Yesu Alipokuja, Alifanya miujiza mingi, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alifanya kazi ya wokovu ya msalaba. Na matokeo yake ni kwamba, katika dhana za mwanadamu, mwanadamu anaamini kwamba hivi ndivyo Mungu Anapaswa kuwa. Maana Yesu Alipokuja, hakufanya kazi ya kuondoa taswira ya Mungu asiye yakini moyoni mwa mwanadamu; Alipokuja, Alisulubishwa, Aliponya wagonjwa na kutoa mapepo, na Alieneza injili ya ufalme wa mbinguni. Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo
44. Wakati wa siku za mwisho, Mungu Amekuja mahususi kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake. Anazungumza kutokana na mtazamo wa Roho, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, na kutokana na mtazamo wa nafsi ya tatu; Anazungumza kwa namna tofauti, Akitumia njia moja kwa kipindi fulani, na Anatumia njia za kuzungumza ili kubadilisha dhana za mwanadamu na kuondoa taswira ya Mungu yakini katika moyo wa mwanadamu. Hii ndiyo kazi kuu iliyofanywa na Mungu. Kwa sababu mwanadamu anaamini kwamba Mungu Amekuja kuponya wagonjwa, kutoa mapepo, kufanya miujiza, na kumpatia mwanadamu baraka za vitu, Mungu Anatekeleza hatua hii ya kazi—kazi ya kuadibu na hukumu—ili kuweza kuondoa mambo hayo kutoka katika dhana za mwanadamu, ili mwanadamu aweze kuuelewa uhalisia na ukawaida wa Mungu, na ili kwamba taswira ya Yesu iweze kuondolewa moyoni mwake na kuwekwa taswira mpya ya Mungu. Mara tu taswira ya Mungu ndani ya mwanadamu inapozeeka, basi inakuwa sanamu. Yesu alipokuja na kutekeleza hatua hii ya kazi, Hakuwakilisha Mungu kikamilifu. Alifanya baadhi ya ishara na maajabu, Alizungumza maneno kadhaa, na hatimaye Akasulubishwa, na Aliwakilisha upande mmoja wa Mungu. Hakuweza kuwakilisha yale yote ambayo ni ya Mungu, bali Alimwakilisha Mungu katika kufanya upande mmoja wa kazi ya Mungu. Hiyo ni kwa sababu Mungu ni mkuu, na ni wa ajabu sana, na Haeleweki, na kwa sababu Mungu Anafanya upande mmoja tu wa kazi Yake katika kila enzi. Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu; kufunuliwa kwa tabia potovu ya mwanadamu na kiini cha asili ya mwanadamu; na uondoaji wa fikira za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Alimwongoza Musa kutoka Misri kwa maneno Yake, na Akazungumza maneno fulani kwa Wanaisraeli; wakati huo, sehemu ya matendo ya Mungu yaliwekwa wazi, lakini kwa sababu ubora wa tabia ya mwanadamu ulikuwa finyu na hakuna kitu chochote ambacho kingeweza kufanya maarifa yake kukamilika, Mungu Aliendelea kuzungumza na kufanya kazi. Wakati wa Enzi ya Neema, mwanadamu aliweza kuona tena sehemu ya matendo ya Mungu. Yesu Aliweza kuonyesha ishara na maajabu, kuponya wagonjwa na kutoa mapepo, na kusulubishwa, siku tatu baadaye. Akafufuka na Akawatokea watu Akiwa katika mwili. Kumhusu Mungu, mwanadamu hakujua chochote zaidi ya hiki. Mwanadamu anajua tu kile ambacho Mungu Amemwonyesha, na kama Mungu Asingeonyesha chochote zaidi kwa mwanadamu, basi hicho kingekuwa kiwango cha mwanadamu kumwekea mipaka Mungu. Hivyo, Mungu Anaendelea kufanya kazi, ili maarifa ya mwanadamu juu Yake yaweze kuwa ya kina zaidi, na ili taratibu aweze kuijua hulka ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anatumia maneno yake kumkamilisha mwanadamu. Tabia yako iliyoharibika imewekwa wazi kwa maneno ya Mungu, na dhana zako za kidini zinaondolewa na uhalisia wa Mungu. Mungu katika mwili wa siku za mwisho Amekuja hasa kwa ajili ya kutimiza maneno haya kwamba “Neno Lafanyika kuwa mwili, Neno Lakuwa mwili, na Neno Laonekana katika mwili,” na kama huna maarifa ya kina kuhusu hili, basi hutaweza kusimama imara. Wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili, na hii ni sehemu moja ya mpango wa usimamizi wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo
45. Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kuokolewa kikamilifu kutoka kwa dhambi zake kwa kuponya magonjwa na kukemea mapepo na hawezi kufanywa mkamilifu kabisa kwa udhihirisho wa ishara na maajabu. Mamlaka ya kuponya na kukemea mapepo yanapatia mwanadamu neema tu, lakini mwili wa mwanadamu bado ni wa Shetani na tabia potovu za kishetani zitabaki ndani ya mwanadamu. Kwa maneno mengine, yale ambayo hayajatakaswa bado inahusu dhambi na uchafu. Ni baada tu ya mwanadamu kufanywa safi kupitia kwa maneno ndipo mwanadamu atakapopatwa na Mungu na kutakaswa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)
46. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa umuhimu na kiini cha mpango huu wa usimamizi wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kuelewa kabisa. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kufanya kazi ya ukamilishaji? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kukamilisha. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimyakimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)
47. Watu wakibaki katika Enzi ya Neema, basi hawatawahi kujiweka huru kutokana na tabia zao za upotovu, sembuse kujua tabia ya asili ya Mungu. Wanadamu wakiishi daima katika wingi wa neema ila hawana njia ya maisha inayowaruhusu kumjua Mungu na kumridhisha Mungu, basi kamwe hawataweza kumpata Mungu kwa kweli hata ingawa wanaamini Kwake. Hiyo ni aina ya imani ya kutia huruma. Wakati umemaliza kusoma kitabu hiki, wakati umepitia matukio yote ya kazi ya Mungu mwenye mwili katika Enzi ya Ufalme, utahisi kwamba matumaini ya miaka mingi hatimaye yametimika. Utahisi kwamba ni sasa tu ndipo umemwona Mungu uso kwa uso; ni sasa tu ndipo umeutazama uso wa Mungu, umesikia matamshi ya Mungu Mwenyewe, umeifahamu hekima ya kazi ya Mungu, na kuhisi kwa kweli jinsi Mungu ni wa kweli na mwenye nguvu. Utafahamu kuwa umepata vitu vingi ambavyo watu wa nyakati zilizopita hawajawahi kuviona wala kuwa navyo. Wakati huu, utajua kwa uhakika ni nini hasa kuamini katika Mungu, na ni nini kupendeza nafsi ya Mungu. Bila shaka, ukikwamilia maoni ya kitambo, na ukatae au ukane ukweli wa kupata mwili kwa Mungu mara ya pili, basi utabaki mkono mtupu na hutapata chochote, na mwishowe utakuwa na hatia ya kumpinga Mungu. Wale wanaotii ukweli na kunyenyekea kwa kazi ya Mungu watakuja chini ya jina la Mungu mwenye mwili wa pili—Mwenyezi. Wataweza kukubali uelekezi binafsi wa Mungu, na watapata ukweli zaidi na wa juu zaidi na watapokea maisha ya kweli ya mwanadamu. Wataona maono ambayo watu wa zamani hawajawahi kuona kamwe: “Na nikapinduka ili kuiona sauti hiyo iliyonizungumzia. Na baada ya kupinduka, nikatazama vinara saba vya taa vilivyokuwa vya dhahabu; Na hapo katikati ya hivyo vinara saba vya taa nilimwona mtu aliyefanana na Mwana wa Adamu, aliyekuwa amevalia nguo iliyofika katika miguu yake, na kifuani alikuwa amefungwa kanda ya dhahabu. Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye” (Ufunuo 1:12-16). Maono haya ni maonyesho ya tabia kamilifu ya Mungu, na maonyesho ya aina hii ya tabia Yake nzima pia ndiyo maonyesho ya kazi ya Mungu Anapopata mwili mara hii. Katika mibubujiko ya kuadibu na hukumu, Mwana wa Adamu Anaonyesha tabia Yake ya asili kupitia kuzungumza kwa maneno, Akiwaruhusu wale wote wanaokubali kuadibu Kwake na hukumu kuuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, uso ulio mfano wa kuaminika wa Mwana wa Adamu Alivyooneka na Yohana. (Bila shaka, yote haya hayatawaonekania wote wasioikubali kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.) Uso wa kweli wa Mungu hauwezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu, na hivyo Mungu Hutumia maonyesho ya tabia Yake asili kuuonyesha uso Wake wa kweli kwa mwanadamu. Ambayo ni kusema wote ambao wamepitia tabia asili ya Mwana wa Adamu wameuona uso wa kweli wa Mwana wa Adamu, kwa kuwa Mungu ni mkuu zaidi na Hawezi kuelezwa kikamilifu na maneno ya mwanadamu. Mara tu mwanadamu amepitia kila hatua ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme, basi atapata kujua maana kamili ya maneno ya Yohana alipozungumza kuhusu Mwana wa Adamu kati ya vinara vya taa: “Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye.”
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji
48. Ni kwa nini kazi ya kushinda ni hatua ya mwisho? Je, si kudhihirisha kwa usahihi hatima ya kila tabaka la wanadamu? Si kumruhusu kila mtu, katika harakati ya kazi ya kushinda ya kuadibu na hukumu, kuonyesha tabia zake halisi na kisha kuwekwa katika aina yake baadaye? Badala ya kusema kuwa huku ni kuwashinda wanadamu, inaweza bora kusema kuwa huku ni kuonyesha hatima ya kila aina ya mwanadamu. Yaani, huku ni kuhukumu dhambi zao halafu kuonyesha matabaka mbalimbali ya wanadamu, na kwa njia hiyo kubaini kama ni waovu au ni wenye haki. Baada ya kazi ya kushinda, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Hivyo, mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiwe na mwanga wa jua tena kamwe, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza. Mwisho wa vitu vyote uko karibu; mwisho wa mwanadamu umebainishwa wazi machoni mwake, na vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina yake. Ni vipi basi wanadamu wataepuka kuathiriwa na kuanisha huku? Kufichua mwisho kwa kila jamii ya mwanadamu kutafanywa hatima ya kila kitu ikikaribia, na kutafanywa wakati wa kazi ya kushinda ulimwengu mzima (ikiwemo kazi yote ya kushinda kuanzia kazi ya sasa). Huku kufichua mwisho wa wanadamu kunafanywa mbele ya kiti cha hukumu, katika harakati ya kuadibu, na harakati ya kazi ya kushinda ya siku za mwisho. …
Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, wale wa kila nchi na watu wote watapitia kazi ya ushindi. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)
49. Hatua ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni hatua ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na hatua ya mwisho katika kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na wanadamu kamwe hawangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilishwa kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu ya usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha usimamizi wote wa Mungu, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, yaani mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kutekwa nyara na Shetani. Hivyo, Shetani lazima ashindwe kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani, mabadiliko ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye ametekwa nyara, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu
50. Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaoruhusiwa kubaki wote watatakaswa na kuingia katika hali ya juu zaidi ya ubinadamu ambapo watafurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. Walikuwa wamekombolewa wakati mmoja, na pia walikuwa wamehukumiwa na kuadibiwa; walikuwa pia wamemhudumia Mungu wakati mmoja, lakini siku ya mwisho itakapofika, bado wataondolewa na kuangamizwa kwa sababu ya uovu wao na kwa sababu ya kutotii na kutokombolewa kwao. Hawatakuwa tena katika ulimwengu wa baadaye, na hawatakuweko tena miongoni mwa jamii ya binadamu ya baadaye. Watenda maovu wote na yeyote na wote ambao hawajaokolewa wataangamizwa wakati watakatifu miongoni mwa binadamu wataingia rahani, bila kujali kama wao ni roho za wafu ama wale wanaoishi bado katika mwili. Bila kujali enzi ya hizi roho zitendazo maovu na watu watenda maovu, ama roho za watu wenye haki na watu wanaofanya haki wako, mtenda maovu yeyote ataangamizwa, na yeyote mwenye haki ataishi. Iwapo mtu ama roho inapokea wokovu haiamuliwi kabisa kulingana na kazi ya enzi ya mwisho, lakini inaamuliwa kulingana na iwapo wamempinga ama kutomtii Mungu. Kama watu wa enzi ya awali walifanya maovu na hawangeweza kuokolewa, bila shaka wangekuwa walengwa wa adhabu. Kama watu wa enzi hii wanafanya maovu na hawawezi kuokolewa, hakika wao pia ni walengwa wa adhabu. Watu wanatengwa kwa msingi wa mema na mabaya, sio kwa msingi wa enzi. Baada ya kutengwa kwa msingi wa mema na mabaya, watu hawaadhibiwi ama kutuzwa mara moja; badala yake, Mungu atafanya tu kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wema baada ya Yeye kumaliza kutekeleza kazi Yake ya ushindi katika siku za mwisho. Kwa kweli, Amekuwa akitumia mema na mabaya kutenga binadamu tangu Afanye kazi Yake miongoni mwa binadamu. Atawatuza tu wenye haki na kuwaadhibu waovu baada ya kukamilika kwa kazi Yake, badala ya kuwatenga waovu na wenye haki baada ya kukamilika kwa kazi Yake mwishowe na kisha kufanya kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wazuri mara moja. Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja