39. Nimekaribisha Kurudi Kwa Bwana
Majira ya baridi kali ya mwaka wa 2010 huko Amerika yaliniacha nikihisi baridi sana. Kando na baridi kali yenye upepo na theluji, kilichokuwa kibaya zaidi ni kwamba moyo wangu ulihisi kana kwamba ulikuwa umevamiwa na aina fulani ya “wimbi baridi.” Kwa wale kati yetu wanaofanya biashara ya mapambo ya nyumba, majira ya baridi kali ni wakati mgumu zaidi wa mwaka, kawa kuwa pindi majira ya baridi kali yanapoanza kuna kazi chache sana. Hata sisi hukabiliwa na kupoteza kazi zetu. Mwaka huu ulikuwa mwaka wangu wa kwanza nchini Amerika, nilikuwa nimeshuka tu kutoka kwenye mashua, na kila kitu kilionekana kuwa kigeni kwangu. Wala kupangisha nyumba au kupata kazi haikuwa rahisi—na siku zangu zilikuwa na shida chungu nzima. Hali ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba ilinibidi kukopa pesa ili nilipe kodi ya nyumba yangu. Nikiwa nimekabiliwa na shida hii, nilikuwa na huzuni, nami nilihisi kana kwamba ilikuwa vigumu sana kwangu kuvumilia maisha yangu. Usiku nilikabiliwa na ukuta uliokuwa baridi kama barafu, nikiwa na huzuni kiasi kwamba nilitaka kulia tu. Siku moja, nilipokuwa nikitembea huku na kule kwa utepetevu nikiwa katika hali yangu ya huzuni na wasiwasi, mtu fulani aliyekuwa akieneza injili ya Bwana Yesu alinipa kadi, na kusema, “Bwana Yesu anakupenda. Ndugu, njoo kanisani kwetu na uisikilize injili ya Bwana!” Niliwaza: “Nadhani hakuna kitu ambacho ninahitaji kufanya hivi sasa, kwa hivyo hakuna madhara yoyote kwangu kwenda kuisikiliza. Afadhali niende, ni jambo la kufanya.” Kwa hiyo hivyo tu, niliingia kanisani. Nilimsikiliza mchungaji akisoma kwa sauti jambo ambalo Bwana Yesu alikuwa Amesema: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu sana, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asiangamie, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Niliposikia haya, nilihisi kusisimuliwa sana na upendo wa Bwana. Siwezi kufafanua wazi jinsi nilivyohisi, lakini nilihisi kuwa upendo wa Bwana ulikuwa halisi, na kwamba ulizidi upendo wowote ambao ungeweza kupatikana ulimwenguni. Moyo wangu wenye huzuni ulihisi kufarijika sana. Kwa hiyo, niliamua kuweka tumaini langu katika Bwana Yesu kwa bidii. Baadaye, nilianza kushiriki katika mikutano kila Jumapili kwa shauku, na kwa sababu ya kufuatilia kwangu kwa shauku nilikuwa mfanyakazi-mwenza kanisani kwa haraka.
Baada ya kuhudumu kanisani kwa miaka miwili, nilikuwa nikihisi kidogo zaidi na zaidi kwamba Bwana alikuwa nami. Sikuhisi kupata nuru nilipokuwa nikiisoma Biblia, sikuhisi kuchochewa niliposali, na sikuhisi kama nilikuwa nikipata chochote kwa kuhudhuria mikutano. Zaidi ya hayo, niliona jinsi kila mtu kanisani alivyokuwa akiishi maisha ambapo alitenda dhambi mchana na kukiri tu usiku, na jinsi kila mtu, iwe wachungaji, wazee au waumini wa kawaida, alikuwa amefungwa na dhambi, akishiriki katika mizozo ya wivu, akishirikiana mmoja kwa mwingine katika kuunda vikundi, akipigania umaarufu na faida, na kutamani mambo ya kidunia. Vitendo visivyo halali vya kila aina vilikuwa vikifanywa zaidi na zaidi. Niliona pia kuwa watu katika jamii kwa ujumla walikuwa wanazidi kupotoshwa kila siku, kuwa waovu na wachoyo zaidi na zaidi, na kwamba majanga yalikuwa yakitokea ulimwenguni kote—matetemeko ya ardhi, njaa na magonjwa ya mlipuko yalikuwa yakiibuka kila wakati. Ishara za kila aina zilifanya iwe wazi kuwa siku za mwisho zilikuwa zimeshafika, na kwamba Bwana Yesu atarudi hivi karibuni. Mara nyingi wachungaji na wazee walihubiri kuhusu aya hizi za Biblia: “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:23–24). Katika mahubiri yao, walidai bila kujali kwamba Makristo wa uongo watatokea katika siku za mwisho, na walituambia kwamba hatupaswi hata kidogo kuwasikiliza wageni wakihubiri. Hata walisema kwamba, mbali na wale walio kanisani kwetu, waumini katika madhehebu mengine yote walikuwa wamekosea, na kwamba lazima tujihadhari na kuwa wenye utambuzi kuhusu watu wengine ili tuepuke kudanganywa na kuishia kufuata njia mbaya. Kwa kuwa nilisikia mara kwa mara wachungaji wakihubiri kwa njia hii, nilijiambia: “Sipaswi kuiacha njia katika wakati huu muhimu wa kurejea kwa Bwana ambako kuko karibu, na lazima nihakikishe nimeiweka imani yangu katika Bwana.”
Siku moja katikati ya mwezi wa Septemba mwaka wa 2016, nilipokea simu isiyotarajiwa kutoka kwa Dada Zhu. Dada Zhu alikuwa muumini wa muda mrefu na mtafutaji mwenye shauku katika kanisa letu, na mara zote tulikuwa na uhusioano mzuri, kwa hiyo nilifurahi sana kupokea simu kutoka kwake. Nilimsikiliza Dada Zhu akizungumza nami kwa furaha, “Ndugu, nina habari njema za kukueleza: Bwana Yesu amerudi kama Mwenyezi Mungu! Wakati huu Mungu amakuwa mwili ili Atekeleze kazi ya kumhukumu, kumtakasa na kumwokoa mwanadamu!” Nilishangaa kwa kiasi fulani kusikia habari hizi, nami niliwaza: “Je, Dada Zhu hajaifuata njia ya Bwana? Je, amejiunga na dhehebu lingine? Anawezaje kuwa mpumbavu namna hii? Wachungaji na wazee wamesisitiza mara kwa mara kwamba Makristo wa uongo watatokea katika siku za mwisho, kwa hiyo kwa nini hakuwasikiliza? Tukiiacha imani yetu wakati huu muhimu ambapo Bwana yuko karibu kuja, basi hatutakuwa tumeifuata imani yetu bure miaka hii yote?” Nilipokuwa nikiwaza kuhusu jambo hili, nilimwuliza Dada Zhu kwa hofu, “Dada, katika Biblia inasema kwamba katika siku za mwisho kutakuwa na uwongo—” lakini bila angoje nimalize kuongea, Dada Zhu aliingilia kati. “Ndugu, Bwana Yesu alituonya ‘Msitoe hukumu,’ na hatupaswi kutoa hukumu tunavyotaka, ili tusishutumiwe na Mungu.” Onyo la dada huyo lilinifanya nifikirie maneno haya ya Bwana: “Msitoe hukumu, nanyi hamtahukumiwa: msishutumu, nanyi hamtashutumiwa” (Luka 6:37). Sikuthubutu kusema chochote zaidi. Hata hivyo, kuhusu tukio muhimu kama kurudi kwa Bwana, Mimi na Dada Zhu tulikuwa na maoni yetu wenyewe, na sisi sote tulitaka kushawishiana. Kwa hiyo tulibadilishana kujaribu kuonyesha misimamo yetu, lakini mwishowe hakuna yeyote aliyeweza kumshawishi mwenzake.
Kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya tukio hili, Dada Zhu alinipigia simu mara kwa mara ili kuhubiri injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu kwangu, lakini siku zote nilikataa kuikubali, na kuendelea kumhimiza arudi kanisani kwetu na kuendelea kumwamini Bwana. Kadri muda ulivyoendelea, niliona kwamba alikuwa thabiti sana katika imani yake katika Mwenyezi Mungu na kwamba hakuyumbayumba katika imani yake, kwa hivyo ilibidi niache jambo hilo, na kuacha kujaribu kumshawishi. Nilisema, “Kuanzia sasa na kuendelea, bado nitamwamini Bwana wangu Yesu na unaweza kumwamini Mwenyezi Mungu wako, na hatutaingilia imani ya kila mmoja wetu!” Baada ya hapo, kila wakati Dada Zhu aliponipigia simu ili kutoa ushahidi kuhusu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, ningetafuta kisingizio cha kumwepa. Niliendelea kukataa kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, lakini hakuacha kujaribu kuieneza injili kwangu.
Asubuhi moja mnamo Novemba muda mfupi baada ya saa 11 asubuhi, kabla hata ya jua kuchomoza, mtu fulani akapiga kengele ya mlango nyumbani kwangu. Nilifungua mlango na kumwona Dada Zhu, naye alikuwa ameandamana na ndugu na dada fulani. Nilipomwona Dada Zhu, nilihisi kuwa mwenye mwelekeo wa kujitetea kabisa. Niliwaza: “Sijawa wazi na wewe? Kwa nini bado usafiri mwendo mrefu sana kuja nyumbani kwangu? Haijalishi unachosema sitamwamini Mwenyezi Mungu.” Bila kujali miaka yote ambayo tulikuwa tumejuana kama washiriki wa kanisa moja, niliwaambia maneno yasiyofurahisha na kukataa kuwaruhusu kuingia. Dada Zhu alipoona jinsi nilivyokuwa nimedhamiria, alionyesha uso wenye huzuni naye aliniambia kwa sauti iliyojawa hisia, “Ndugu, sababu nimekuja kueneza injili ya ufalme kwako ni kuwa nimechochewa na Roho Mtakatifu. Isingekuwa kwa upendo wa Mungu, nisingeweza kujinyenyekeza na kuendelea kujaribu kueneza injili kwako mara kwa mara. Ndugu, Bwana Yesu amerudi kweli. Hivi sasa, Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa wale ambao wameikubali kazi mpya ya Mungu. Isingekuwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu, mtu yeyote angewezaje kuwa na imani nyingi na nguvu ya kuja kukuhubiria injili namna hii? Wewe pia umeona hali ya sasa ya kanisa letu. Ndugu zetu wote wanaishi wakiwa wamefungwa kwa dhambi na wanakosa nguvu ya kujinasua. Mungu amekuja wakati huu kuonyesha maneno Yake ili kumhukumu mwanadamu na kutekeleza kazi ya kutuondolea dhambi na kututakasa. Tukiikosa kazi ya Mungu ya siku za mwisho, hatutakuwa na fursa nyingine ya kupata wokovu wa Mungu.” Maneno ya dhati ya yule dada yalinichochea nami nilitulia kidogo. Hasa, alipokuwa akizungumza kuhusu hali katika kanisa letu, mambo yote niliyokuwa nimeona yakitokea katika makanisa yalianza kung'aa akilini mwangu ghafla: Katika kanisa la kwanza nililohudumu, wachungaji walisema jambo moja na kutenda jambo lingine, na yeyote aliyechanga pesa nyingi alikaribishwa na wachungaji kwa nyuso zenye tabasamu na kuzingatiwa kwa makini. Mtu yeyote ambaye hakuchanga pesa nyingi sana, hata hivyo, alipuuzwa na kudharauliwa na wachungaji. Sikuweza kuvumilia hata kidogo kuona jambo hili likitendeka, kwa hiyo nilijiunga na kanisa lingine. Katika kanisa hili nilishuhudia wafanyikazi-wenzi wakitengana, wakishiriki katika mabishano yenye wivu, na kushirikiana mmoja kwa mwingine ili kuunda vikundi tofauti, na hawakuwa tofauti na watu katika ulimwengu wa kidunia. Jambo hili liliniudhi sana. Mwanzoni, nilitaka kuhamia kanisa lingine tena, lakini ndugu mmoja aliniambia kuwa alikuwa amekwishakwenda katika makanisa mengi, na kwamba bila kujali alikokwenda alikuta ukiwa na giza lilo hilo kila wakati…. Mimi pia nilifikiria kuhusu tabia mbali mbali ambazo mimi mwenyewe nilizionyesha nilipokuwa nikiishi katika dhambi, jambo ambalo lilinisababisha nianze kuyumbayunba moyoni mwangu. Niliwaza: “Je, inawezekana kuwa Bwana Yesu amerudi katika mwili ili kutekeleza kazi ya kukomesha dhambi?” Wakati uo huo, Dada Zhu aliendelea, akisema, “Ikiwa ni Mwenyezi Mungu ndiye Bwana aliyerejea au la, unachohitaji kufanya tu ni kusoma neno la Mwenyezi Mungu, na kisha utajua. Wakati Bwana Yesu alipokuja kutekeleza kazi Yake, wanafunzi Wake walimfuata kwa sababu walitambua kupitia maneno Yake na kazi Yake kwamba Yeye ndiye Masihi aliyetabiriwa. Leo, ili kuamua ikiwa Mwenyezi Mungu ni kuonekana kwa Bwana Yesu ambaye amekuja kutekeleza kazi Yake au la, lazima pia tufanye hivyo kwa kuangalia kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu. Ikiwa, baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, bado unaamini kuwa Yeye si Bwana aliyerejea, basi sitajaribu kukulazimisha kuamini, nami nitaacha kukuhubiria injili, kwa kuwa Mungu hajawahi kumlazimisha mtu yeyote kuikubali injili Yake.”
Baada ya Dada Zhu kusema maneno haya, nilitasita kwa muda na kutafakari: “Afadhali niyasome na kuona ni ukweli gani hasa unazungumziwa katika maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo yamempa Dada Zhu imani thabiti kama hiyo katika Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo, niliufungua mlango na kuwaruhusu Dada Zhu na wengine wote nyumbani mwangu. Dada Zhu aliwajulisha wenzake, nao walikuwa Dada Zhang Qing na ndugu Liu Kaiming kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu. Dada Zhu alisema, “Ndugu Chuanyang, imekuwa miezi kadhaa tangu niikubali kazi ya Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho. Nilikwenda katika Kanisa la Mwenyezi Mungu ili kujithibitishia, nami nimeshiriki katika maisha yao ya kanisa. Kupitia uzoefu wa kibinafsi na kupitia uchunguzi wa dhati, nimeona kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa kweli ni kanisa ambalo lina kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kanisa la kweli, na bila shaka limetoka kwa Mungu. Wewe na mimi tumekuwa washiriki wa kanisa pamoja kwa miaka, na kama mfanyakazi-mwenza kanisani, unapaswa kujua bora kuniliko kuhusu kile kinachoendelea ndani huko kanisani sasa. Roho Mtakatifu aliacha kufanya kazi kanisani kwetu zamani, na hili ni jambo ambalo kila mtu anajua. Wachungaji hawawezi kuhubiri mahubiri ambayo yanatupatia uzima. Wanahubiri tu kuhusu jinsi ya kushambulia au kuwa macho dhidi ya madhehebu mengine, wakituambia kwamba lazima tuhifadhi jina la Bwana na kwamba tutaokolewa mradi hatuliachi kanisa letu. Lakini kwa kweli hakuna msingi katika neno la Bwana kwao kutenda namna hii. Wao hufanya hivyo tu ili kulinda nafasi zao na riziki zao, na hawayafikirii maisha yetu. Ikiwa kweli wangehisi kuwajibika kwa ajili ya maisha yetu basi wanapaswa kuchukua hatua na kutuongoza ili kutafuta kanisa ambalo Roho Mtakatifu anafanya kazi, badala ya kututaka tuendelee kubaki kwa ukaidi katika dini ambalo Roho Mtakatifu aliacha kufanya kazi zamani, tukingojea vifo vyetu kwa kufa kwa njaa au kutokana na kunaswa katika kanisa lisilo na kazi ya Roho Mtakatifu.” Baada ya kusikia maneno haya niliwaza: “Kwa kweli Dada Zhu anaelezea kinachoendelea. Hakika kanisa leo halina kazi ya Roho Mtakatifu, kila kitu ambacho wachungaji na wazee hufanya kweli hakifanywi kwa kuzingatia maisha yetu sisi waumini, na jinsi nimelishikilia kanisa hili kwa miaka mingi nimehisi zaidi na zaidi kana kwamba Bwana hayuko nasi. Roho yangu ilihisi kuwa imekauka na kuwa mbali na nuru kwa muda mrefu, kana kwamba imefikia kikomo.” Nilipomsikia akiongea kwa njia hii yenye busara na yenye msingi imara, sikuhisi tena kuipinga ziara yao.
Wakati uo huo, ndugu ambaye alikuwa amekuja naye—Ndugu Liu—alisema, “Ndugu, sababu ambayo ulimwengu wa kidini ni ukiwa jinsi hii ni kwa sababu Mungu amekuja kutekeleza kazi mpya na kazi ya Roho Mtakatifu imeendelea, lakini watu hawajaendelea sawa na kazi mpya ambayo Mungu anafanya. Sababu kubwa hata zaidi ni kwamba wachungaji na wazee hawajatii amri za Bwana au kuyatia maneno ya Bwana katika vitendo, lakini badala yake wamewaongoza waumini kufuata mienendo mibaya ya ulimwengu, na hata wameikataa na kuishutumu kazi mpya ya Mungu. Ni kama tu wakati Bwana Yesu alipokuja kutekeleza kazi Yake, hekalu lilikuwa limegeuzwa na kuwa mahali ambapo ng’ombe, kondoo na njiwa waliuzwa na pesa kubadilishwa. Makuhani walivunja sheria na kutoa na kafara wanyama waliokuwa na mawaa kama sadaka ili kumlaghai Mungu, Mafarisayo walitamani utajiri na walifurahia nyara za vyeo vyao, na dhambi zingine kama hizo zilitendwa. Hata wale ambao walimtumikia Mungu waliishi katika dhambi, bila kumcha Mungu mioyoni mwao hata kidogo. Hii ilitosha kuonyesha kuwa Roho Mtakatifu hakufanya kazi tena hekaluni, kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ilikuwa imeenda mbele, na kwamba kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria ilikuwa imekamilika. Bwana Yesu alikuwa Amekuja kutekeleza kazi ya ukombozi juu ya msingi wa kazi ya Enzi ya Sheria, na Roho Mtakatifu hakufanya kazi tena kwa wale walioliamini jina la Yehova Mungu na kuzishikilia sheria kikaidi. Badala yake, kazi ya Roho Mtakatifu ilihamia kwa wale walioikubali kazi mpya ya Bwana Yesu. Kwa kuwa uwepo wa Mungu haukuwa kwenye hekalu tena, hekalu lilizidi kuwa lenye ukiwa zaidi na zaidi, hadi mwishowe likawa pango la wezi. Wanafunzi wa Bwana Yesu, kwa upande mwingine, waliupokea wokovu wa Bwana, waliyatia mafundisho ya Bwana katika vitendo, walimfuata Bwana kwa imani na nguvu, waliyaacha makao yao na kuzitelekeza kazi zao ili kushuhudia na kuieneza injili ya Bwana, wasiogope kuteswa au shida. Je, haya yote hayakuwa matokeo yaliyopatikana ndani yao na kazi ya Roho Mtakatifu? Vivyo hivyo, leo kurudi kwa Bwana kunaashiria kuwa enzi ya kale imekamilika na enzi mpya imeanza. Roho Mtakatifu aliacha kufanya kazi katika makanisa ya Enzi ya Neema kitambo sana; badala yake, Ameanza kufanya kazi kwa wale ambao wameikubali kazi mpya ya Mungu, jambo ambalo linatimiza unabii huu katika Biblia: ‘Na pia nimeizuia mvua isije kwenu, ilipokuwa miezi mitatu kabla ya wakati wa mavuno: Na nimefanya kunyeshe katika mji mmoja, na kufanya kusinyeshe katika mji mwingine: kulinyesha katika sehemu moja, na sehemu ambayo haikunyesha ikanyauka’ (Amosi 4:7). ‘Tazama, siku zinafika … ambapo nitaileta njaa ardhini, sio njaa ya ukosefu wa chakula, au kiu ya maji, ila ya kutoyasikia maneno ya Yehova’ (Amosi 8:11). Mwenyezi Mungu asema pia: ‘Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini itapitia njaa kubwa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea’ (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili). ‘Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndio mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu’ (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?). ‘Kwani walio katika dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu’ (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu). Kutoka kwa maneno haya ya Mungu, tunaweza kuona kwamba Roho Mtakatifu hafanyi kazi tena katika makanisa ya Enzi ya Neema, kwa hiyo haijalishi ni kwa namna gani watu wanavyojaribu au ni mbinu za aina gani ambazo wanadamu wanatumia kuyafufua makanisa, haina maana. Kanisa la Katoliki na madhehebu ya Kiprotestanti yote ni sawa; roho za waumini wao zina ukiwa na zinakufa kwa njaa, imani yao na upendo wao unapungua pole pole, hawawezi kutimiza mafundisho ya Bwana, na wengi wao wanafuata mienendo mibaya ya ulimwengu, wakifuatilia utajiri na kutamani vitu vya ulimwengu. Makanisa yamekuwa maeneo ya ukiwa. Kwa upande mwingine, ndugu katika Kanisa la Mwenyezi Mungu ni wale ambao wameyaacha madhehebu tofauti na wale wanaotoka katika taaluma tofauti ili kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Wao ni mabikira wenye busara ambao, baada ya kusikia sauti ya Mungu, wamerudi mbele ya kiti Chake cha enzi. Wanapokea ruzuku ya maji ya uhai ya uzima yanayotiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu, wanachungwa na kuongozwa na Mungu Mwenyewe, nao wanaieneza na kuishuhudia injili ya ufalme wa Mungu kwa uwiano. Wanavumilia kudharauliwa na kukashifiwa na ulimwengu, wanavumilia dhuluma na lawama kutoka kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali, na hata kupigwa, na wanavumilia kukamatwa, nyumba zao kupekuliwa, mali zao kunyang’anywa, na kuteswa kikatili na kufungwa jela na mengine zaidi na serikali ya CCP. Bado, wana imani, wana nguvu, wana upendo, na wao ni washupavu na wasiokubali kushindwa wanapomfuata Mwenyezi Mungu na kuishuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Si kwa nguvu zao wenyewe kwamba wanaweza kufanya hivyo. Haya yote ni matokeo yanayopatikana kupitia kwa kazi ya Roho Mtakatifu! Zaidi ya hayo, mapenzi ya Mungu yanapatikana katika kusababisha njaa katika ulimwengu wa kidini. Kusudi Lake kwa kufanya hivyo ni ili kuwalazimisha wale ambao wanamwamini Mungu kwa kweli na walio na kiu ya ukweli kuachana na dini, kujiondolea udanganyifu na udhibiti wa wapinga-Kristo wa kidini, na kuachana na dini. Kwa kufanya hivyo, wanaweza kutafuta nyayo za Mungu na muonekano wa Mungu, kuikubali kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, na kutakaswa na kukamilishwa na Mungu. Wakati huo huo, wale wasioamini wanaobaki katika dini, wanaotafuta kula na kushiba na ambao hawamwamini Mungu kwa moyo wa kweli, lakini badala yake wanaowaabudu watu kama mungu na kuwafuata, watafunuliwa na kuondolewa. Kwa njia hii, watu wote watatengwa kulingana na aina zao. Je, hii sio hekima na uweza wa Mungu?”
Baada ya kusikiliza maneno ya Mungu na ushirika wa ndugu huyu, nilihisi kuwa yote yalikuwa ya manufaa sana, na kwamba yalikubaliana kabisa na jinsi mambo yalivyokuwa kweli. Nilihisi kana kwamba nilikuwa nimeamshwa kutoka katika ndoto, nami nilielewa chanzo cha ukiwa wa makanisa mbalimbali. Katika wakati huu, mwishowe niliona jinsi nilivyokuwa mtu asiyejali. Ingawa nilikuwa nimeona kwamba, kutoka kwa wachungaji na wazee hadi kwa waumini wa kawaida, wote walikuwa wamefungwa kwa dhambi, na kwamba kanisa lilikuwa limejawa uhalifu na uovu, bado sikuwa nimetafuta mapenzi ya Mungu, wala sikuwa nimeitafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Pia sikuwa nimekuwa makini katika kuisikiliza sauti ya Mungu na, kwa hiyo, nilikuwa nimeondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu bila hata kufahamu. Niligundua kuwa nilihitaji kusoma neno la Mwenyezi Mungu kwa uangalifu. Siku hiyo, Dada Zhu na wenzake walipokuwa wakitoka, walipanga wakati ambapo wangerudi na kushiriki nami tena, na pia waliniacha na nakala ya Kitabu Chafunguliwa na Mwanakondoo, ambayo niliipokea kwa furaha.
Baadaye, niliposoma Kitabu Chafunguliwa na Mwanakondoo, kitabu cha neno la Mwenyezi Mungu, niliona kwamba neno la Mwenyezi Mungu linafichua siri nyingi, kama vile hatua tatu za kazi zilizotekelezwa na Mungu ili kuwaokoa wanadamu, kazi ya hukumu Yake katika siku za mwisho, uzuri wa ufalme Wake, na kadhalika, ambavyo vilinipa ufahamu zaidi wa kazi ya Mungu. Roho yangu iliyokauka ilihisi kuridhishwa, na kadri nilivyozidi kusoma kitabu hiki ndivyo nilivyozidi kukipenda. Nilikuwa nimezoea kuamka saa 11:30 asubuhi, lakini baada ya kupokea nakala yangu ya Kitabu Chafunguliwa na Mwanakondoo, nilianza kuamka saa 10:30 asubuhi ili kusoma neno la Mwenyezi Mungu na kutafakari kuhusu maneno Yake, na yangu roho ilihisi kutosheka kabisa. Asubuhi moja, nilipokuwa nikisoma kifungu “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” nilihisi msukumo mkubwa moyoni mwangu. Mwenyezi Mungu ni Mungu ambaye huichunguza mioyo ya ndani kabisa ya watu, na Ameifunua asili yetu potovu ambayo hatungeweza kuijua sisi wenyewe, kwa hivyo niliweza kuona ukweli wa upotovu wangu uliosababishwa na Shetani. Hii ilikuwa kweli hasa wakati niliposoma maneno haya ya Mwenyezi Mungu: “Kwa vyovyote vile, Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni wasioamini na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo. … Unafaa kufahamu kuwa Mungu si wa ulimwengu huu au wa mtu yeyote, bali ni wa wale wote wanaoamini katika Mungu kwa kweli, wote wale wanaomwabudu, na wote wale waliojitolea na wanaoamini katika Mungu.” Nilipokuwa nikitafakari maneno haya, niliendelea kujiuliza: Je, mimi ni mtu ambaye anamwamini Mungu kweli? Ninauthamini ukweli? Nimethamini nini kwa miaka hii iliyopita ya imani yangu katika Bwana? Nilifikiri kuhusu jinsi nilivyokuwa sawa na ndugu wengi: Kwa nje, nilisoma Biblia na kuhudhuria mikutano, lakini sikutilia maanani kupata uzoefu au kutekeleza neno la Bwana; badala yake, nilithamini mahubiri yaliyohubiriwa na wachungaji na maana halisi ya nyaraka katika Biblia. Niliweka imani isiyo na shaka katika ufahamu wa kibiblia na mafundisho ya kitheolojia yaliyohubiriwa na wachungaji. Sikuwahi kufikiri kuhusu ikiwa kile walichohubiri kilikuwa na ukweli wowote ndani yake hasa au la, au ikiwa kililingana na mapenzi ya Bwana au la, na kwa kweli sikuwahi kuyatumia maneno ya Bwana kuchunguza na kupima kile walichokuwa wakisema. Sisi waumini tuliamini tu chochote walichohubiri. Nikifikiria kuhusu jambo hilo sasa, niligundua jinsi nilivyokuwa mpumbavu na mjinga kwa kuwaabudu watu kama mungu bila kufikiri! Nilifikiria kuhusu mahubiri yaliyotolewa na wachungaji na wazee. Ama walitoa mahubiri kuhusu kutoa sadaka au kuhusu kujilinda dhidi ya madhehebu mengine na kulizingia kanisa, au wangehubiri tu kuhusu mambo yaleyale ya zamani ambayo walikuwa wakihubiri kwa miaka mingi. Hakukuwa na mwangaza mpya, hakukuwa na nuru mpya, hawakuwa na kitu chochote kabisa cha kutupatia, hawangeweza kutatua shida ya ukavu katika roho zetu, na kwa kweli hawangeweza kutatua ukiwa kanisani. Hii ilisababisha ndugu wafanye tu mambo kwa namna isiyo ya dhati waliposhiriki katika mikutano. Wakati wa mikutano wengine wangepiga gumzo, wengine wangesinzia, na wengine wangecheza michezo kwenye simu zao. Nilikuwa nimeishi katika kanisa hili lenye giza na ukiwa, lakini sikuwa nimejua jinsi ya kutafuta mapenzi ya Mungu, lakini sikuwa nimejua jinsi ya kuitafuta kazi ya Roho Mtakatifu. Inavyoonekana, sikuwa mtu aliyeutafuta ukweli au aliyemwamini Mungu kwa kweli hata kidogo. Mwenyezi Mungu anasema: “Wote wale wasioenzi ukweli ni wasioamini.” “Mungu si wa ulimwengu huu au wa mtu yeyote, bali ni wa wale wote wanaoamini katika Mungu kwa kweli, wote wale wanaomwabudu.” Maneno haya yalikuwa halisi, na yalinifanya nifikirie ghafla kuhusu maneno ya Bwana Yesu: “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai” (Yohana 14:6). Nilielewa wakati huo kwamba Mungu ndiye ukweli, kwamba Mungu hutekeleza kazi Yake ili kumpa mwanadamu ukweli, njia na uzima, na kwamba watu wanaomwamini Mungu kwa kweli huwa makini kuutafuta ukweli na kuupata ukweli. Kama muumini katika Mungu, sikuwa nikizingatia kuutafuta ukweli, kwa hiyo si nilikuwa nimevurugika kabisa katika imani yangu? Ikiwa hii ndiyo namna ambayo nilimwamini Mungu, basi ningewezaje kupata kibali cha Mungu? Maneno ya Mwenyezi Mungu yalinifaidi sana! Kadri nilivyozidi kusoma neno la Mwenyezi Mungu, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba nilikuwa nimepungukiwa kwa njia nyingi sana. Na kwa hiyo, isipokuwa wakati nilipopaswa kufanya kazi, nilitumia wakati wangu wote wa ziada kusoma neno la Mwenyezi Mungu. Nilihisi hakika kwamba hii ndiyo njia ya kweli kwa dhati. Lakini bado nilihisi kufadhaishwa na maneno haya yaliyosemwa na Bwana Yesu: “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:23–24). Sikujua maana ya ndani ya maneno haya ilikuwa nini, kwa hiyo niliamua kutafuta maana yake wakati Dada Zhu na wengine watakapokuja tena.
Dada Zhu na yule ndugu na dada mwingine walipita nyumbani kwangu wakati tuliopanga, nami nilimwambia Dada Zhang, “Siku hizi chache zilizopita nimekuwa nikisoma mengi kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu, nami ninahisi kuwa kila Neno lililosemwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, na kwamba ni kile ninachohitaji kwa kweli. Awali, Dada Zhu alijaribu kunialika niangalie kazi ya Mwenyezi Mungu tena na tena, lakini kwa sababu wachungaji wangu walikuwa wamehubiri kuhusu jinsi Makristo wa uongo watakavyotokea katika siku za mwisho ili kuwahadaa watu, nilikataa kuichunguza njia ya kweli, na sasa najuta kweli. Hata hivyo, bado ninahisi kuchanganyikiwa kuhusu jambo hili, kwa hivyo ningependa kujua kutoka kwenu. Bwana Yesu alisema: ‘Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi’ (Mathayo 24:23–24). Je, ninyi mnaelewaje maneno haya?”
Dada Zhang alisema, “Shukrani ziwe kwa Mungu, na hebu Atuongoze katika ushirika huu. Kuhusu swali ambalo umeuliza, kwanza lazima tuelewe kusudi la Bwana Yesu kusema maneno haya ni nini, na Alimaanisha nini Alipoyasema. Bwana Yesu alituambia kwamba, wakati Atakaporudi, Atakuwa mwili tena kama Kristo, kama Mwana wa Adamu, na katika kifungu hiki Bwana alisema kwamba Makristo wa uongo pia watatokea, wakionyesha ishara na maajabu ili kuwahadaa watu. Hiyo ni kusema, wakati ujao Mungu atakapotokea katika mwili, hawa Makristo wa uongo pia wataonekana. Kutoka kwa hili, tunaweza kuona kwamba Bwana alisema maneno haya ili kutuambia kwamba lazima tukuze utambuzi ili kutuzuia kudanganywa na Makristo hawa wa uongo. Hakusema maneno haya ili kwamba tukatae kumsikiliza mtu yeyote anayeeneza habari njema ya kuwasili kwa Bwana na kukataa kuwasikiliza kila wakati. Itakuwa kosa kutenda kwa namna hii, na itakuwa ni kutoelewa kabisa kusudi la Bwana. Bwana Yesu alitabiri: ‘Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha’ (Mathayo 25:6). ‘Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi’ (Ufunuo 3:20). ‘Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata’ (Yohana 10:27). Maneno ya Bwana yanaonyesha wazi kabisa kuwa wakati Bwana atakaporudi, Atatumia sauti Yake kuwaita kondoo wa Mungu, na kupitia sauti Yake kondoo wa Mungu watamtambua na kurudi kwake. Hiyo ni kusema, ikiwa tunaweza kukaribisha kurudi kwa Bwana au la kunategemea hasa ikiwa tunaweza kuitambua sauti ya Mungu au la. Ikiwa hatujitahidi kuisikiliza sauti ya Mungu, na kuwakataa kila wakati wale wanaoieneza injili ya kurudi kwa Bwana, basi hatutakuwa na uelekeo wa kumfungia Bwana mlango na kumfungia nje? Kutoka kwa maneno ya Bwana tunaona kuwa sifa za kuwatofautisha Makristo wa uongo ni uwezo wa kufanya ishara na kufanya miujiza, kuiga kazi ambayo Bwana Yesu alifanya hapo zamani na kufanya baadhi ya ishara na maajabu, kama kuwaponya wagonjwa na kutoa pepo, ili kumdanganya mwanadamu. Hata hivyo, Makristo wa uongo ni mfano wa pepo wabaya, kwa hivyo bila kujali ni aina gani ya ishara ambazo wanafanya, hawawezi kuonyesha ukweli wowote. Hili ni jambo lisilopingika. Maneno ya Mwenyezi Mungu huonyesha wazi kabisa maonyesho na kiini cha Makristo wa uongo. Hebu tuangalie vifungu kadhaa kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu nawe utaelewa. Mwenyezi Mungu anasema: ‘Ikiwa katika siku za mwisho “Mungu” sawa na Yesu Angeonekana, Ambaye Anaponya wagonjwa, Anafukuza mapepo na Anayesulubiwa kwa ajili ya wanadamu, “Mungu” huyo, japo Analingana na maelezo ya Mungu katika Biblia, na rahisi kwa mwanadamu kukubali, Hangeweza, katika kiini chake, kuwa mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu, bali na roho mwovu. Kwani ni kanuni ya kazi ya Mungu kutorudia Alichokikamilisha. Hivyo basi kazi ya kupata mwili wa Mungu kwa mara ya pili ni tofauti na kule kwa kwanza’ (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu). ‘Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. … Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili’ (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo). Maneno ya Mwenyezi Mungu yanaonyesha wazi kabisa kuwa Makristo wa uongo ni pepo wabaya wanaojifanya kuwa Kristo. Hata ingawa wanajiita Mungu, hawana ukweli hata kidogo na hakika hawawezi kutekeleza kazi ya Mungu, kwa kuwa hawana kiini cha Kristo. Wanaweza tu kumfuata Mungu kwa karibu sana ili waige kazi ambayo Bwana Yesu amekwishaifanya ili kuwahadaa watu. Makristo wa uongo hawatawahi kuweza kuleta ukweli au njia mpya ya utendaji kwa watu. Kila mtu anajua kuwa bidhaa zote bandia katika ulimwengu huu zimetengenezwa kwa kuiga bidhaa halisi. Makristo wa uongo wako vivyo hivyo. Wanawaponya wagonjwa na kutoa pepo na kufanya miujiza kadhaa rahisi ili kuwahadaa watu kwa kuiga kazi iliyotekelezwa na Bwana Yesu, lakini Makristo wa uongo hawawezi kufanya miujiza kama vile kuwafufua wafu na kuwalisha watu 5,000 kwa mikate mitano na samaki wawili. Kwa hivyo, mtu yeyote anayejiita Kristo, anayesema yeye ni Bwana Yesu aliyerejea na anayeonyesha ishara na maajabu na huwaponya wagonjwa na kutoa pepo, watu hawa bila shaka ni Makristo wa uongo wanaowahadaa watu. Hata hivyo, Kristo ndiye kupata mwili kwa Mungu mwenyewe, Yeye ni Roho wa Mungu aliyefanyika katika mwili, Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili, na bila shaka Yeye ni Mungu Mwenyewe. Mwenyezi Mungu anasema: ‘Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe’ (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Kwa hiyo, ni Kristo pekee ndiye Anayeweza kutekeleza kazi ya Mungu mwenyewe, ni Kristo pekee ndiye Anayeweza kuonyesha ukweli, na Kristo pekee ndiye Anayeweza kuonyesha tabia ya Mungu na kumkimu mwanadamu na kumchunga mwanadamu. Ni Kristo pekee ndiye Anayeweza kutekeleza kazi ya kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu, ni Yeye pekee ndiye Anayeweza kuikonesha enzi ya kale na kuikaribisha enzi mpya. Zaidi ya hayo, kazi ya Mungu ni mpya kila wakati na sio ya kale kamwe, na Mungu harudii kazi iyo hiyo kamwe. Kwa hiyo, kila wakati Kristo atakapokuja kufanya kazi Ataleta kazi mpya daima, Akionyesha tabia ya Mungu na kile Anacho na Alicho. Wakati Bwana Yesu alipokuja kutekeleza kazi, kwa mfano, Aliikamilisha Enzi ya Sheria na kuikaribisha Enzi ya Neema, Alitoa mahubiri ambayo yaliwawezesha watu kukiri dhambi zao na kutubu, na Aliwafunza watu kuwapenda adui zao, kuwa wanyenyekevu, kuwa na subira na kuwasamehe wengine. Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo Bwana Yesu alifanya. Bwana Yesu alimfichulia mwanadamu tabia ya Mungu yenye upendo na huruma. Vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho, na Ameikomesha Enzi ya Neema na kuikaribisha Enzi ya Ufalme. Anatekeleza kazi ya kumhukumu mwanadamu na kumtakasa mwanadamu kwa maneno Yake kwa msingi wa kazi ya ukombozi wa Bwana Yesu, Akitupatia ukweli wote ambao tunahitaji ili tutakaswe na kupata wokovu, Akituonyesha njia ya kuepuka dhambi na kupata wokovu, na kuonyesha tabia ya Mungu yenye haki, yenye uadhama na yenye hasira. Kupitia kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu, tunaweza kabisa kutambua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mungu mwenye mwili na kwamba Yeye ndiye Mungu Mwenyewe anayeonekana kati ya wanadamu katika siku za mwisho.”
Baada ya kusikiliza maneno ya Mungu na ushirika alionipa dada huyu, nilihisi kana kwamba nilikuwa nimeamshwa kutoka ndotoni, na mwishowe nilielewa jinsi ya kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo. Jambo hili lilinifanya nifurahi na kuona aibu vilevile, kwani niliona jinsi ninavyokuwa wa kusikitisha na bila ukweli. Nilifikiri kuhusu jinsi nilivyoikataa kazi ya Mungu ya siku za mwisho mara kwa mara, na nikagundua kwamba ilikuwa ni kwa sababu nilikuwa nimeogopa kudanganywa na Makristo wa uongo, na hivyo nilimkataa Kristo wa kweli kama mtu asiyekula kwa kuhofia kunyongwa na chakula. Bwana aliporudi na kubisha mlangoni kwangu, nilikuwa nimekataa kuisikiliza sauti ya Mungu, nikimfungia Bwana mlango mara kwa mara. Lakini Mungu hakukata tamaa kuniokoa, badala yake Aliwachochea ndugu hawa kuja nyumbani kwangu ili kuieneza injili. Mungu hakuwahi kuniacha—upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Kwa sababu nilikuwa nimeamini kile wachungaji wangu walikuwa wamesema, nilikuwa nimeamua kwamba kila mtu aliyeshuhudia kwa Bwana aliyerejea alikuwa akihubiri Kristo wa uongo. Nilikuwa nimeelewa visivyo neno la Bwana, na nilikuwa nimemkataa, kumhukumu na kumpinga Mwenyezi Mungu, na pia nilikuwa nimeamini kuwa mawazo niliyoshikilia yalikuwa sawa—nilikuwa mpumbavu sana! Nisingesoma neno la Mwenyezi Mungu na kusikiliza ushirika wa ndugu hawa kuhusu tofauti kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo, basi nisingewahi kuweza kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo, nami ningekuwa nimedanganywa tu na yale wachungaji na wazee waliyosema. Ningekuwa nimewafuata wachungaji na wazee katika kupinga kwao na kukataa kuwasili kwa Mungu, na kwa hiyo ningepoteza fursa hii nadra sana ya kupata wokovu wa Mungu. Nilipokuwa nikifikiri kuhusu jambo hili, nilimwambia Dada Zhu na wengine, “Kupitia kusoma neno la Mwenyezi Mungu na kusikiliza ushirika wenu, sasa najua jinsi ya kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo. Sasa ninasadiki kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, nami niko tayari kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho.”
Baada ya kuanza kushiriki katika maisha ya kanisa, niliona kuwa ndugu hao walielewa ukweli mwingi, na kwamba nilikuwa nimepungukiwa sana ikilinganishwa na wao. Niliwaza: “Lazima niwaambie Dada Zhu na ndugu wengine wote washiriki nami zaidi kuhusu neno la Mungu na kunisaidia ili niuelewe ukweli haraka.” Nilijadili jambo hili na Dada Zhu, nikimwuliza ikiwa tungeweza kugeuza nyumba yangu iwe mahali pa mkutano, naye akakubali mara moja. Baada ya hapo, tulikusanyika pamoja kila juma ili kusoma neno la Mungu na kushiriki kuhusu ukweli. Hatua kwa hatua nilikuja kuwa na ufahamu zaidi na zaidi kuhusu maneno ya Mungu na kuelewa ukweli zaidi na zaidi. Niliweza kuhisi kwa dhati kwamba maneno haya yalikuwa maonyesho ya ukweli. Katika wakati huo, nilifikiri kuhusu maneno ambayo Bwana Yesu alikuwa Amesema: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajay” (Yohana 16:12–13). Nilihisi kuchochewa zaidi, nami nikaona kwamba maneno haya yote ya Bwana yalikuwa yametimia. Neno la Mwenyezi Mungu ni “neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7). Mwenyezi Mungu yuko katika mchakato wa kumwongoza mwanadamu ili aelewe na kupata kuingia katika ukweli wote. Ni kwa kuibali kazi ya Mungu katika siku za mwisho tu na kwa kuukubali ukweli ulioonyeshwa na Mungu tu ndipo mtu anaweza kutakaswa, kupata wokovu na kuwa mtu anayeupendeza moyo wa Mungu. Ni neno la Mwenyezi Mungu ndilo lililonirudisha katika nyumba ya Mungu na ndilo lililonileta mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Sasa, kila siku ninayo maneno ya Mungu yanayonikimu na kuniongoza, nami ninahisi kuwa mwenye amani na furaha, mwenye raha na kujazwa na mwanga. Nanitamani kufanya yote niwezayo ili kuufuata ukweli na kumfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho!