62 Nitaukaribisha Uso Wako Unaotabasamu Utakapoonekana Mbele Yangu

1

Sauti ya kawaida inaniita mara kwa mara,

ikiiamsha roho yangu, ikiniamsha kutoka usiku mrefu.

Kupitia katika ukungu naona uso Wako unaotabasamu.

Kamwe sikuota kuwa ningeuona uso wa Mungu.

Mimi ni binadamu mpotovu, asiye na heshima,

lakini Mfalme mtukufu na mwenye heshima zaidi Anakuja kwangu.

Maneno Yako yanivutia, moyo wangu umejawa na furaha.

Kuishi mbele Yako kila siku ni utamu na furaha kamili.

2

Kimya mbele Yako, nasikiliza maneno Yako.

Maneno Yako ni yenye joto na nguvu.

Upendo katika hukumu na kuadibu Kwako vimeuamsha moyo wangu.

Naona kuwa maneno Yako ni ukweli, ya thamani sana!

Upendo Wako, wa dhati na mzuri,

huujaza moyo wangu na kuusisimua upendo wangu.

Kuna mengi sana ya kupenda ndani Yako na yamechongwa moyoni mwangu.

Kukupa moyo wangu na mapenzi yangu ni tamanio langu.

3

Uko wapi sasa, Mpendwa wangu?

Ninavyotamani sana upendo Wako, usiku usio na usingizi ni mrefu.

Unanipenda, kwa nini Ujifiche?

Moyo Wangu hauna amani wakati siwezi kuuona uso Wako.

Katika dhiki na majaribu, nakuita na kukutegemea.

Maneno Yako yakiniongoza, ni kama kuuona uso Wako.

Nikikupenda kwa moyo wangu wote, nikifuata nyayo Zako, nakua thabiti katika imani.

Kuishi kwa kufuata neno Lako kwanifanya nihisi mwenye amani na raha.

Kiitiko

Neno Lako ndilo ukweli na limeumiliki moyo wangu.

Kuishi kwa kufuata neno Lako ndicho kilele cha furaha.

Natamani kukupenda na kukushuhudia na kukufuata maisha yangu yote.

Kisha, ushuhuda wangu ukikamilika, nitaukaribisha uso Wako unaotabasamu Utakapoonekana mbele yangu.

Iliyotangulia: 61 Ni Mwenyezi Mungu Anayetuokoa

Inayofuata: 63 Nashukuru kwa Upendo wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki