947 Onyo la Maangamizi ya Mungu ya Sodoma kwa Wanadamu

Kuhusiana na matendo yote ya uovu yaliyotendwa na watu hawa wa Sodoma, kuwadhuru watumishi wa Mungu kulikuwa mfano tu wa tone baharini ya kile walichokuwa wakifanya, na asili yao ya uovu uliofichuliwa kwa kweli ulionekana tu kuwa mdogo zaidi kuliko hata tone moja ndani ya bahari kubwa. Kwa hivyo, Mungu alichagua kuwaangamiza kwa moto.

1 Mungu hakutumia gharika, wala Hakutumia zilizala, mtetemeko wa ardhi, sunami au mbinu yoyote nyingine ya kuuangamiza mji huu. Kule kutumia moto na Mungu kuangamiza mji huu kulimaanisha nini? Kulimaanisha uangamizaji kamili wa mji huo; kulimaanisha kwamba mji huu ulitoweka kabisa kutoka ulimwenguni na kutoka katika kuwepo kwake. Hapa, “kuangamiza” hakurejelei tu kule kutoweka kwa umbo na muundo au sura ya nje ya mji huo; kunamaanisha pia kwamba nafsi za watu ndani ya mji huo zilisita kuwepo, baada ya kufutwa kabisa. Kwa ufupi, watu wote, matukio na mambo yote yaliyohusiana na mji huu yaliangamizwa. Kusingekuwa na maisha ya baadaye au roho kuwa mwilini mwao tena; Mungu alikuwa amewafuta kabisa kutoka katika binadamu, uumbaji Wake, mara moja na tena milele.

2 Yale “matumizi ya moto” yalimaanisha kusitisha dhambi, na yalimaanisha mwisho wa dhambi; dhambi hii ingesita kuwepo na kuenea. Yalimaanisha kwamba uovu wa Shetani ulikuwa umepoteza mahali pake pa kunawiri pamoja na eneo la kaburi ambalo liliupatia mji huo mahali pa kukaa na kuishi. Kwenye vita kati ya Mungu na Shetani, matumizi ya moto na Mungu ni alama ya ushindi Wake ambayo Shetani anatajiwa. Kuangamizwa kwa Sodoma ni hatua kubwa ya kuzuia maono ya Shetani ya kupinga Mungu kwa kupotosha na kudanganya binadamu, na vilevile ni ishara ya kudhalilishwa kwa muda kwenye maendeleo ya binadamu ambapo binadamu alikataa mwongozo wa Mungu na akajiachilia kutenda maovu. Aidha, ni rekodi ya ufunuo wa kweli wa tabia ya haki ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 946 Hasira ya Mungu ni Onyesho la Tabia Yake ya Haki

Inayofuata: 948 Watu wa Siku za Mwisho Hawajawahi Kuona Hasira ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp