199 Ninapoamka Katika Ukungu

1

Naona Neno laonekana katika mwili na Mungu ameifanya upya mbingu na nchi,

Akitamatisha milenia sita ya ugumu na kutokuwa na utulivu.

Mungu mwenye mwili huonyesha ukweli, akiletea wanadamu nuru.

Mungu kufanya kazi kumkamilisha mwanadamu ni fursa nadra sana, nina bahati sana.

Neno Lake linafichua, kuhukumu, kuadibu na kufunua tabia potovu ya mwanadamu.

Hatimaye najua kuwa binadamu wamepoteza dhamiri yao kwa sababu ya kupotoshwa na Shetani.

Wanafiki, wanaonena kwa wepesi kuhusu maadili, wakati kwa kweli walishapoteza ubinadamu kitambo.

Kula njama na kupigania umaarufu na faida, wanaishi dhambini.

2

Moyo mbaya wa mwanadamu ni mwovu sana kuuona.

Kujinajisi na kujipotosha makusudi, hajipendi kabisa.

Anaweza kupata wapi chembe yake ya mwisho ya uadilifu na heshima?

Moyo wa mwanadamu sio mwaminifu na ni mdanganyifu sana, na mwanadamu hastahili kuja mbele za Mungu.

Nikiwa mwenye moyo usumbukao, na mwenye woga na huzuni, natoa nafsi yangu yote mbele Zake.

Natanafusi kwa kuwa ni sasa tu ndipo najua jinsi ilivyo vigumu kuwa mwanadamu.

Nimepotoka sana na siwezi kuokolewa bila kupitia hukumu na utakaso.

Naamka katika ukungu, mwenye aibu sana kuutazama uso wa Mungu.

Nikitiwa nuru na hukumu, mara moja najua jinsi ya kuwa mtu.

Ukweli na uzima havikuja kwa urahisi, yote ni fadhila ya Mungu.

Kujua kupendeza kwa Mungu kumesisimua upendo wangu Kwake hata zaidi.

Acha nipitie usafishaji na nitakaswe ili niweze kumpenda Mungu na kumridhisha.

Iliyotangulia: 198 Kukubali Ukweli ni Kuwa Mwanamwali Mwenye Busara

Inayofuata: 201 Kuzinduka kwa Barakala

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki