993 Unapaswa Kuthamini Siku ya Utukufu wa Mungu

1 Watu hawathamini kuja Kwangu, wala hawaiwekei thamani siku ya utukufu Wangu. Wao hawasherehekei kupokea adabu Yangu, sembuse kuwa tayari kuurejesha utukufu Wangu Kwangu. Wala hawako tayari kutupa mbali sumu ya yule mwovu. Wanadamu bado siku zote wananidanganya kwa njia ile ile ya zamani, bado wakivaa tabasamu za kung’aa na nyuso zenye furaha kwa njia ile ile ya zamani. Wao hawajui kina cha huzuni ambayo wanadamu watakabiliwa nao baada ya utukufu Wangu kuwaondoka, na hasa hawajui kwamba siku Yangu itakapokuja kwa wanadamu wote, watakuwa na wakati hata mgumu zaidi kuliko watu katika nyakati za Nuhu. Kwa maana wao hawajui giza iliyokuwepo Israeli wakati utukufu Wangu ulitoweka kwa kuwa mwanadamu husahau kunapokucha jinsi ilivyokuwa vigumu kupita katika giza la usiku wa manane. Jua linaporejea mafichoni tena na giza kumshukia mwanadamu, ataanza tena kuomboleza na kusaga meno yake gizani.

2 Je, mmesahau, wakati utukufu Wangu ulipotoweka kutoka Israeli, ilivyokuwa vigumu kwa watu wake kuishi siku zao za mateso? Huu ndio wakati ambapo mnaona utukufu Wangu, na pia ndio wakati ambapo mnashiriki siku ya utukufu Wangu. Mwanadamu ataomboleza katikati ya giza wakati utukufu Wangu unapoondoka kutoka katika nchi chafu. Sasa ndio siku ya utukufu Ninapofanya kazi Yangu, na pia ndio siku ambapo Namwondoa mwanadamu kutoka kwa mateso, kwa kuwa sitapitia nyakati za uchungu na ugumu nao. Mimi Nataka tu ushindi kamili juu ya wanadamu na kumshinda kikamilifu yule mwovu wa wanadamu. Kwa maana wao hawajui giza iliyokuwepo Israeli wakati utukufu Wangu ulitoweka kwa kuwa mwanadamu husahau kunapokucha jinsi ilivyokuwa vigumu kupita katika giza la usiku wa manane. Jua linaporejea mafichoni tena na giza kumshukia mwanadamu, ataanza tena kuomboleza na kusaga meno yake gizani.

Umetoholewa kutoka katika “Maana ya Kuwa Mtu Halisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 992 Maonyo Matatu ya Mungu kwa Mwanadamu

Inayofuata: 994 Mungu Anawaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi ya Maisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp