163 Pamoja Kupitia Katika Upepo na Mvua Uaminifu Mpaka Kifo

1

Ulikuja kutoka mbinguni hadi duniani, Ukijificha katika mwili.

Unafanya kazi kati ya mwanadamu, na Umestahimili miaka mingi ya dhoruba.

Kutembea katika njia yenye mabonde, Umeikaribisha enzi mpya.

Ulionyesha ukweli ili kuhukumu, Ukiwaokoa kabisa wanadamu wote.

Kwa miaka mingi umevumilia shida, na kustahimili uchungu wa kukataliwa na mwanadamu.

Mnyenyekevu na Uliyejificha, Umevumilia mpaka leo.

2

Napitia uchungu wa hukumu, na mateso moyoni mwangu ni mengi.

Nikiadibiwa na kufundishwa nidhamu, naelea kati ya uzima na kifo.

Nikikumbuka utunzaji Wako, nakupenda zaidi.

Nikitazama zamani, moyo wangu umejaa majuto.

Baada ya majaribu na usafishaji mwingi, upendo wangu Kwako ni safi zaidi.

Nitakuwa nawe kupitia katika upepo na mvua, nitakuwa mwaminifu hadi kifo.

3

Unaonyesha huruma Yako, ukiuhurumia udhaifu wangu.

Unaonyesha ghadhabu Yako, Ukilaani kutotii kwangu.

Huruma Yako inaenea kote, ghadhabu Yako ni ya kina.

Ninaona uadhama Wako na kuthamini hekima Yako.

Baada ya kupogoa na kushughulika kwingi, upendo wangu Kwako ni safi zaidi.

Nitakuwa nawe kupitia katika upepo na mvua, nitakuwa mwaminifu hadi kifo.

4

Unanena na kunafanya kazi, Ukifanyiza kundi la washindi.

Usafishaji mchungu ulipangwa na Wewe.

Nimeionja kazi Yako, na kuhisi fadhila Zako.

Nikikumbuka uchungu na utamu, nabadilika kati ya huzuni na furaha.

Baada ya hukumu na kuadibu kwingi, upendo wangu Kwako ni safi zaidi.

Nitakuwa nawe kupitia katika upepo na mvua, nitakuwa mwaminifu hadi kifo.

5

Kujitolea kwa ajili Yako ni tamanio langu.

Katika majaribu, azimio langu linasimama imara.

Upendo wangu Kwako unakuwa wa kina, napata utamu katika uchungu.

Nikiwa na maneno Yako kama mwenzi, maisha yangu yamejaa nuru.

Baada ya kupigwa na kuvunjwa mara nyingi, upendo wangu Kwako ni safi zaidi.

Nitakuwa nawe kupitia katika upepo na mvua, nitakuwa mwaminifu hadi kifo.

6

Nabeba mzigo mkubwa, siko radhi kuchelewa zaidi.

Kimo changu ni kidogo sana, lakini napokea upendo Wako.

Nitakamilisha agizo Lako na maisha yangu yakamilishwe.

Nitatimiza mapenzi Yako na kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi ya binadamu.

Miaka ya upepo na mvua, njia ya maisha imejaa msukosuko.

Iwe uchungu, furaha, au kifo, sina malalamiko.

Kupitia miaka ya upepo na mvua, upendo Wako umekuwa nami niendeleapo mbele.

Nitakuwa mwaminifu Kwako, na kufa bila majuto.

Iliyotangulia: 162 Wakati wa Kuachana

Inayofuata: 164 Sisi ni Mashahidi wa Kristo wa Siku za Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki