678 Ni Kupitia Taabu na Usafishaji tu Ndiyo Unaweza Kukamilishwa na Mungu

1 Upendo wa kweli wa Mungu ni tabia Yake kamili. Tabia ya haki ya Mungu inapoonyeshwa kwa watu, bila shaka miili yao iapata uchungu mkubwa zaidi. Iwapo hutapata haya maumivu, basi huwezi kufanywa mkamilifu na Mungu, wala huwezi kumpa Mungu mapenzi ya kweli. Mungu akikufanya mkamilifu kwa hakika atakuonyesha tabia Yake kamili. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu hajawahi kumwonyesha mwanadamu tabia Yake kamili—ila katika siku za mwisho Anaifichua kwa hili kundi la watu ambao Aliwateua awali na kuwachagua, na kwa kuwafanya watu wakamilifu, Anaiweka wazi tabia Yake, na kupitia kwayo Analifanya kamili kundi la watu. Huo ndio upendo wa kweli wa Mungu kwa watu.

2 Kuyapitia mapenzi ya kweli ya Mungu kunawapasa watu wastahimili uchungu mkali, na kulipa gharama kubwa. Ni baada tu ya hili ndipo watapatikana na Mungu na waweze kutoa tena mapenzi ya kweli kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo Moyo wa Mungu utaridhishwa. Ikiwa watu wanataka wafanywe wakamilifu na Mungu, na kama wanataka kufanya na mapenzi Yake, na kumpa Mungu mapenzi yao ya dhati kikamilifu, ni sharti wapitie mateso mengi na maumivu makali kutokana na hali hizo, kupata uchungu mkali kuliko mauti, hatimaye watashurutishwa kuirejesha mioyo yao ya kweli kwa Mungu. Ikiwa mtu anampenda Mungu kwa dhati au la, itafichuliwa wakati wa shida na usafishaji. Mungu hutakasa mapenzi ya watu, na hili vilevile hupatikana tu ndani ya shida na usafishaji.

Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 677 Jinsi ya Kumpenda Mungu Katika Usafishaji

Inayofuata: 679 Usafishaji Ndiyo Mbinu Bora ya Mungu Kumkamilisha Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp