Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

7 Ufalme Mtakatifu Umeonekana

1

Mungu mwenye mwili amewasili kati ya wanadamu,

na hukumu imeanza na nyumba ya Mungu.

Tunainuliwa mbele ya kiti Chake kuhudhuria

karamu ya harusi ya Kristo, Mwenyezi Mungu.

Hukumu inatutakasa, hubadilisha tabia yetu.

Tumezaliwa upya na kuwa watu wapya.

Kwa kumcha Mungu, tunasujudu mbele Yake,

tukisifu utakatifu na haki Yake.

Tukiwa tayari kutii na kutoa uaminifu wetu,

tunatimiza wajibu wetu kwa uaminifu.

Mungu, tunakupenda kwa mioyo yetu yote,

na milele tunakuimbia sifa zetu.

Ufalme mtakatifu umeonekana

Ufalme mtakatifu umeonekana.

2

Mungu anaonyesha ukweli kuuhukumu ulimwengu

na kufichua kikamilifu haki Yake.

Nguvu mbaya zinazompinga Mungu,

zitaangamizwa na majanga makubwa.

Sasa Mungu amefanya kila kitu kipya

kwa matumizi na starehe Yake.

Hii siyo tena nchi chafu, ya uasherati,

bali ni ufalme mtakatifu milele.

Neno la Mungu limekamilisha kila kitu,

Mungu anatawala kama Mfalme ulimwenguni.

Mungu amepata utukufu Wake kikamilifu

Ufalme wa Kristo umeonekana duniani.

Ufalme mtakatifu umeonekana.

Ufalme mtakatifu umeonekana.

3

Jua la haki linang'aa juu ya nchi nzima,

na vitu vyote vinafufuliwa.

Watu wa Mungu wakusanyika kwa furaha,

wakiimba na kucheza katika ushindi Wake.

Wote wasifu mafanikio Yake makubwa.

Ulimwengu wote umejawa shangwe na kicheko.

Kila kitu chenye pumzi kinaimba sifa za Mungu,

kwa kuwa Amerudi kwa ushindi kamili.

Ulimwengu mzima umefanywa upya,

na tunasherehekea siku ya utukufu wa Mungu.

Sauti za sifa zinaipasua anga,

tunamwimbia Mungu sifa bila kukoma.

Ufalme mtakatifu umeonekana.

Ufalme mtakatifu umeonekana.

Iliyotangulia:Kristo wa Siku za Mwisho, Wokovu wa Mwanadamu

Inayofuata:Ufalme Wenye Haki wa Kristo Umetimia

Maudhui Yanayohusiana

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…

 • Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

  1 Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza; kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa; kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfiki…

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  1 Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…