Ujana Usio na Majuto Yoyote

10/03/2018

Xiaowen Jijini Chongqing

‘Upendo,’ kama unavyoitwa, unaashiria hisia safi isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi, na kuwa na mawazo. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi na hakuna kutenga. Katika upendo hakuna shaka, hakuna uongo na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna mabadilishano na hakuna kitu kisicho safi(“Upendo Safi Bila Dosari” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo huu wa neno la Mungu siku moja ulinisaidia kupitia maumivu ya maisha ya muda mrefu yaliorefuka bure gerezani ambao ulidumu miaka 7 na miezi 4. Ingawa serikali ya CCP ilininyang’anya miaka mizuri zaidi ya ujana wangu, nimepata ukweli halisi na wa thamani zaidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa hiyo sina malalamiko au majuto.

Mnamo mwaka wa 1996 nilikubali wokovu wa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kupitia kusoma maneno ya Mungu na kukusanyika katika ushirika, nilidhihirisha kwamba yote ambayo Mungu amesema ni ukweli, ambayo ni tofauti kabisa na maarifa na nadharia zote za dunia hii mbovu. Neno la Mwenyezi Mungu ni methali ya juu zaidi kwa maisha. Kilichofanya nisisimke zaidi kilikuwa kwamba ningeweza kuwa wa kawaida na wazi na kuzungumza kwa uhuru juu ya chochote na ndugu wa kiume na wa kike. Sikuwa na haja hata kidogo ya kujilinda dhidi ya lawama au kushindwa kwa akili na watu wakati wa kuingiliana nao. Nilihisi faraja na furaha ambayo sikuwahi kuhisi awali; kwa kweli niliipenda familia hii. Hata hivyo, si muda mrefu ulipita kabla sijasikia kwamba nchi hii haikuwaruhusu watu kumwamini Mwenyezi Mungu. Jambo hili lilinifanya kuchanganyikiwa kabisa, kwa sababu neno Lake liliwaruhusu watu kumwabudu Mungu na kuitembea njia sahihi ya maisha; liliwaruhusu watu kuwa waaminifu. Kama kila mtu angemwamini Mwenyezi Mungu, basi ulimwengu wote ungekuwa na amani. Kwa kweli sifahamu: Kumwamini Mungu kulikuwa ndiko shughuli ya haki zaidi; kwa nini serikali ya CCP ilitaka kutesa na kupinga kumwamini Mwenyezi Mungu kiasi kwamba ingewakamata waumini Wake? Niliwaza: Bila kujali ni vipi serikali ya CCP inatutesa au ni jinsi gani maoni ya umma ya kijamii ni makubwa, nimeamua kuwa hii ndiyo njia sahihi ya maisha na mimi kwa hakika nitaitembelea hadi mwisho!

Baada ya haya, nilianza kutekeleza wajibu wangu katika kanisa wa kusambaza vitabu vya neno la Mungu. Nilijua kwamba kutimiza wajibu huu katika nchi hii ambayo ilimpinga Mungu ilikuwa hatari sana na ningeweza kukamatwa wakati wowote. Lakini nilijua pia kuwa kama sehemu ya uumbaji wote, ulikuwa ni misheni yangu katika maisha wa kutumia kila kitu kwa ajili ya Mungu na kutimiza wajibu wangu; lilikuwa ni jukumu ambalo sikuweza kulikwepa. Nilipokuwa tu nikianza kushirikiana na Mungu kwa imani, siku moja mnamo Septemba mwaka wa 2003, nilikuwa njiani kuwapelekea ndugu fulani wa kiume na wa kike vitabu vya neno la Mungu na nilikamatwa na watu kutoka kwa Ofisi ya Usalama wa Taifa ya mjini.

Katika Ofisi ya Usalama wa Taifa, nilihojiwa tena na tena na sikujua jinsi ya kujibu; nilimlilia Mungu kwa haraka: “Ee Mwenyezi Mungu, nakuuliza Wewe unipe hekima Yako, na unipe maneno ambayo napaswa kuzungumza ili nisikusaliti Wewe na niweze kuwa shahidi kwa ajili Yako.” Wakati huo, nilimlilia Mungu kila siku; Sikuthubutu kumwacha Mungu, nilimwomba tu Mungu anipe akili na hekima ili niweze shughulikia polisi hao waovu. Shukrani kwa Mungu kwa kunichunga na kunilinda; kila wakati nilipohojiwa, ama nilikuwa nikitema mate, au nilikuwa na kwikwi mfululizo na sikuweza kuzungumza. Katika kuona kazi ya ajabu ya Mungu, nikaamua kwa dhati: Kuwa waziwazi! Wanaweza kuchukua kichwa changu, wanaweza kuchukua maisha yangu, lakini kabisa hawatanifanya kumsaliti Mungu leo kamwe! Ninapoweka azimio langu kwamba ningependa kuhatarisha maisha yangu kuliko kumsaliti Mungu kama Yuda, Mungu alinipa “endelea” kwa kila namna: Kila wakati nilipohojiwa, Mungu angenilinda na kuniruhusu nipitie majaribu. Ingawa sikusema chochote, serikali ya CCP ilinishtaki kwa “kutumia shirika la Xie Jiao kuangamiza utekelezaji wa sheria” na kunihukumu kifungo cha miaka 9 katika jela! Niliposikia hukumu ya mahakama, sikuwa na huzuni kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, wala sikuwaogopa; badala yake, niliwadharau. Wakati watu hao walikuwa wakitangaza hukumu, nilisema kwa sauti ya chini: “Huu ni ushahidi kwamba serikali ya CCP inampinga Mungu!” Baadaye, maafisa wa usalama wa umma walikuja tu kuchunguza jinsi mtazamo wangu ulivyokuwa, na nikawaambia kwa utulivu: “Miaka tisa ni nini? Wakati utakapofika kwangu kutoka, bado nitakuwa mshiriki wa Kanisa la Mwenyezi Mungu; ikiwa huniamini, subiri tu na kuona! Lakini unapaswa kukumbuka, kesi hii wakati mmoja ilikuwa katika mikono yenu!” Mtazamo wangu kwa kweli uliwashangaza; waliinua vidole gumba vyao juu na kusema tena na tena: “Wewe ni wa kutamaniwa sana! Mwenye kutamaniwa sana! Wewe ni Dada Jiang kuliko Dada Jiang alivyo! Wakati utakapofika wa wewe kutoka nje, tutakusanyika tena na wewe utaalikwa!” Wakati huo, nilihisi kwamba Mungu alipata utukufu na moyo wangu ulipendezwa. Mwaka huo nilipohukumiwa, nilikuwa na umri wa miaka 31 tu.

Jela za China ni kuzimu duniani, na maisha ya muda mrefu ya gereza yalinifanya kuona kabisa unyama wa kweli wa Shetani na kiini chake cha kishetani ambacho kimekuwa adui kwa Mungu. Polisi wa China huwa hawafuati utawala wa sheria, lakini badala yake hufuata utawala wa uovu. Gerezani, polisi binafsi huwa hawawashughulikii watu, lakini huwachochea wafungwa kufanya vurugu ili kutiisha wafungwa wengine. Hawa polisi waovu pia hutumia mbinu za aina zote kuyafungia mawazo ya watu; kwa mfano, kila mtu anayeingia anapaswa kuvaa sare sawa za mfungwa zilizo na nambari maalum ya mfululizo, ni sharti anyolewe nywele zao kulingana na matakwa ya gereza, ni lazima avae viatu vilivyoidhinishwa na jela, anapaswa kutembelea vijia ambavyo gereza limemruhusu kutembelea, na anapaswa kutembea mwendo wa askari kwa kasi iliyoruhusiwa na gereza. Bila kujali kama ni majira ya kuchipua, majira ya joto, majira ya kupukutika kwa majani au majira ya baridi, ikiwa kuna mvua au kuna jua, au kama ni siku ya baridi kali, wafungwa wote wanapaswa kufanya kama walivyoamriwa bila ya uchaguzi wowote. Kila siku tulihitajika kukusanyika angalau mara 15 kupangwa na kuimba nyimbo za sifa kwa serikali ya CCP angalau mara tano; tulikuwa pia na kazi za kisiasa, yaani, walitufanya tujifunze sheria za gereza na katiba, na walitufanya kufanya mtihani kila baada ya miezi sita. Kusudi la hili lilikuwa ni kututia kasumba. Pia wangeyapima bila mpango maalum maarifa yetu ya masomo na sheria za jela. Polisi wa gereza walitutesa sio kiakili tu, wao pia walituharibu kimwili kwa unyama kamili: nilipaswa kufanya kazi ngumu kwa zaidi ya saa kumi kwa siku, kama tumesokomezwa pamoja na watu wengine mia kadhaa katika kiwanda chembamba tukifanya kazi za mikono. Kwa sababu kulikuwa watu wengi sana katika nafasi ndogo kiasi hicho, na kwa sababu kelele ya kutatanisha ya mashine ilikuwa kila mahali, bila kujali mtu alikuwa na afya kiasi gani, mwili wake ungepata uharibifu mkubwa kama angekaa hapo kwa muda. Nyuma yangu kulikuwa na mashine ya kutoboa matundu na kila siku ilitoboa mashimo mfululizo. Sauti ya kunguruma iliyopitisha ilikuwa isiyovumilika na baada ya miaka michache, nilipata ugonjwa hatari wa kutosikia. Hata leo hii sijapata nafuu. Kitu kilichokuwa kibaya zaidi kwa watu kilikuwa vumbi na uchafuzi wa mazingira katika kiwanda hicho. Baada ya kuchunguzwa, watu wengi walipatikana wakiwa wameambukizwa kifua kikuu na uvimbe wa koromeo. Aidha, kutokana na muda mrefu wa kukaa kitako hapo kufanya kazi ya mikono, ilikuwa haiwezekani kusogea hapa na pale na watu wengi waliambukizwa ugonjwa hatari wa bawasiri. Serikali ya CCP iliwachukulia wafungwa kama mashine za kutengeneza pesa; hawakuwa na mazingatio hata kidogo ya kama mtu aliishi au alikufa. Waliwafanya watu kufanya kazi tangu asubuhi na mapema mpaka usiku kabisa. Mara nyingi nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba sikuweza kuendelea kimwili. Haikuwa hii tu, nilipaswa pia nishughulike na aina zote za mitihani ya nasibu bali na kazi zangu za kila wiki za kisiasa, kazi za mikono, na kazi za umma, nk. Kwa hiyo, kila siku nilikuwa katika hali ya wasiwasi wa hali ya juu; hali yangu ya kiakili ilikuwa ikinyoshwa daima, na nilikuwa na wasiwasi zaidi kwamba singeweza kuwafikia wengine kama ningezembea hata kidogo, na kwa hiyo ningeadhibiwa na polisi wa gereza. Katika mazingira ya aina hiyo, kumaliza siku moja salama haikuwa kazi rahisi kufanya.

Ujana Usio na Majuto Yoyote

Nilipoanza tu kumaliza kifungo changu, sikuweza kustahimili aina hii ya kuharibiwa kikatili na polisi wa gereza. Aina zote za kazi ngumu ya mikono na shinikizo la kiitikadi lilifanya kupumua kuwe kugumu, sembuse kuwa ilibidi niwe na mawasiliano ya aina yote na wafungwa. Nilibidi pia kuvumilia dhuluma na matusi ya polisi wa kishetani wa gereza na wafungwa …. Niliteswa mara kwa mara na kuwekwa taabuni. Mara kadhaa, nilizama katika hali ya kukata tamaa, hasa nilipofikiria urefu wa hukumu yangu ya miaka tisa, nilihisi mshindo wa kutojiweza kwa kuhuzunisha na sikujua ni mara ngapi nililia—kiasi kwamba nilifikiria kujiua ili kujiweka huru kutoka kwa maumivu niliyokuwa nayo. Kila wakati nilipokuwa na huzuni kupita kiasi na sikuweza kujifadhili, ningeomba kwa haraka na kumlilia Mungu na Mungu angenipatia nuru na kuniongoza: “Bado huwezi kufa. Sharti ukaze ngumi yako na kuendelea kuishi kwa ari; lazima uishi maisha kwa ajili ya Mungu. Watu wanapokuwa na ukweli ndani yao basi wanakuwa na azimio hili na kamwe hawatamani kufa tena; kifo kinapokutisha, utasema, ‘Ee Mungu, siko radhi kufa; bado sikufahamu. Bado sijalipiza upendo Wako. Lazima nife baada tu ya kukujua Wewe vyema.’ … Ikiwa huelewi nia ya Mungu, na unatafakari tu kuhusu mateso yako, basi kadri unavyozidi kuyawaza, ndivyo unavyozidi kuhisi kusikitishwa, na kisha utakuwa mashakani na kuanza kuteseka mateso ya kifo. Ukiuelewa ukweli utasema, ‘Bado sijapata ukweli. Lazima nitumie rasilmali yangu kwa ajili ya Mungu sawasawa. Lazima niwe na ushuhuda mzuri wa Mungu. Lazima nilipize upendo wa Mungu. Baada ya hapo, haijalishi jinsi nitakavyokufa. Kisha, nitakuwa nimeishi maisha ya kutosheleza. Bila kujali ni nani mwingine anayekufa, sitakufa sasa; lazima niendelee kuishi kwa ushupavu.’(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalikuwa kama maono laini na latifu ya mama yangu akiutuliza moyo wangu mpweke. Yalikuwa pia kama baba yangu akitumia mikono miwili kuyafuta kwa uangalifu machozi kutoka kwa uso wangu kwa upendo. Moja kwa moja, mkondo wa vuguvugu na nguvu zilikurupuka kupitia moyo wangu. Ingawa nilikuwa nikiteseka kimwili katika jela la giza, kujaribu kujiua hakukuwa mapenzi ya Mungu. Singeweza kumshuhudia Mungu na pia ningekuwa kichekesho cha Shetani. Ingekuwa ushuhuda kama ningetoka hai kutoka gereza hili lenye pepo baada ya miaka tisa. Maneno ya Mungu yalinipa ujasiri wa kuendelea na maisha yangu na nikafanya azimio moyoni mwangu: Haijalishi matatizo gani yaliyo mbele yangu, kwa uangalifu nitaendelea kuishi; nitaishi kwa ujasiri na nguvu na hakika nitashuhudia kuridhika kwa Mungu.

Mwaka nenda mwaka rudi, kazi ya kuzidi kiasi ilisababisha mwili wangu kudhoofika hatua kwa hatua. Baada ya kukaa kitako kwa muda mrefu katika kiwanda ningeanza kutoa jasho maridhawa na bawasiri zangu zingevuja damu zilipokuwa kali vya kutosha. Kutokana na upungufu wangu mkali wa damu, mara kwa mara ningehisi kizunguzungu. Lakini gerezani, kumwona daktari si jambo rahisi kufanya; kama polisi wa gereza walikuwa wamefurahi, wangenipa dawa za bei nafuu. Kama hawakuwa na furaha, wangesema nilikuwa nikijifanya mgonjwa ili kuepuka kazi. Ningevumilia mateso ya ugonjwa huu na kuyazuilia machozi yangu. Baada ya kazi ya siku kutwa ningekuwa nimechoka kabisa. Niliukokota mwili wangu mchovu hadi kwa chumba changu kidogo cha gereza na nilitaka kupata mapumziko, lakini sikuwa hata na chembe ya ya nguvu ya kupata usingizi madhubuti: Ama polisi wa gereza walikuwa wakiniita katikati ya usiku kufanya kitu fulani, au niliamshwa na kelele ya kunguruma iliyopigwa na polisi wa gereza. … Mara kwa mara nilichezewachezewa nao na kuteseka vibaya sana. Aidha, nililazimika kustahimili kutendewa kinyama na polisi hawa wa gereza. Nilikuwa kama mkimbizi nikilala sakafuni au ushorobani, au hata kando ya choo. Nguo nilizoziosha hazikuwa kavu, lakini zilikuwa zimefungwa pamoja na nguo za wafungwa wengine ili kukaushwa. Kuosha nguo katika majira ya baridi kulikuwa kwa kukatisha tamaa hasa, na watu wengi waliambukizwa ugonjwa wa baridi yabisi kwa sababu ya kuvaa mavazi manyevu kwa vipindi virefu vya wakati. Gerezani, haikuchukua muda mrefu kwa watu wenye afya kuwa goigoi na bozi, wadhaifu kimwili au kujawa magonjwa. Mara kwa mara tulikula majani ya mboga ya zamani, yaliyokaushwa na ambayo yalikuwa yamepitwa na msimu. Kama ulitaka kula kitu bora zaidi, basi ulilazimika kununua chakula ghali huko gerezani. Ingawa watu walifanywa kujifunza sheria gerezani, hakukuwa na sheria huko; polisi wa gereza ndio waliokuwa sheria na kama mtu yeyote angewaudhi, walipata sababu ya kukuadhibu—hata kwa kiasi kwamba waliweza kukuadhibu bila sababu yoyote. Hata la kudharauliwa zaidi ni kwamba walichukulia waumini wa Mwenyezi Mungu kuwa wahalifu wa kisiasa, wakisema kuwa uhalifu wetu ulikuwa mbaya zaidi kuliko mauaji na kuchoma mali. Kwa hiyo, walinichukia hasa na walinidhibiti kikamilifu, na kunitesa kikatili sana. Aina hii ya tabia mbovu ni ushahidi usiobadilika wa tabia potovu ya CCP, upinzani kwa Mbinguni, na kuwa na uadui na Mungu! Baada ya kuvumilia mateso ya kikatili ya gereza, moyo wangu mara kwa mara ulijazwa na hasira ya haki: Ni sheria gani kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu hukiuka? Ni uhalifu gani kumfuata Mungu na kuitembea njia sahihi ya maisha? Wanadamu waliumbwa na mikono ya Mungu na kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu ni sheria ya mbingu na dunia; ni sababu gani serikali ya CCP iliyo nayo ya kuzuia kwa nguvu na kusumbua hili? Kwa dhahiri ni tabia yake potovu na upinzani kwa Mbingu; huwa inajiweka yenyewe dhidi ya Mungu katika kila kipengele, huwa inashikiza kitambulisho cha kupinga maendeleo kwa waumini wa Mwenyezi Mungu na hututesa kwa ukali na kutuharibu. Huwa inajaribu kuwaondosha waumini wote wa Mwenyezi Mungu kwa dharuba moja kali. Si huku ni kubadilisha weusi na weupe na kuwa mpinga maendeleo kikamilifu? Kwa hasira huipinga Mbingu na ina uhasama na Mungu; hatimaye ni lazima ipitie adhabu ya haki ya Mungu! Kila mahali kuna upotovu, lazima kuwe na hukumu; kila mahali kuna dhambi, lazima kuwe na adhabu. Hii ni sheria ya Mungu ya mbinguni iliyoamuliwa kabla, hakuna mtu anayeweza kuitoroka. Uhalifu muovu wa serikali CCP umepanda kwa anga, na itapitia maangamizo ya Mungu. Kama tu Mungu alivyosema: “Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga mwovu huyu, joka wa zamani mwenye chuki, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote. Mungu hatamsamehe hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote,[a] Atamwangamiza kabisa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)).

Katika gereza hili la pepo, nilikuwa duni kuliko mbwa wa kutangatanga machoni mwa polisi hawa maovu; hawakunipiga na kunikemea tu, lakini polisi hawa waovu mara kwa mara na kwa ghafla wangeingia kwa vishindo na kutawanya matandiko yangu na vitu vyangu vya kibinafsi kuwa takataka. Pia, wakati wowote ambapo ghasia fulani zilifanyika katika ulimwengu wa nje, watu walio gerezani ambao ni wasimamizi wa masuala ya kisiasa wangenitafuta na kudadisi maoni yangu kuhusu matukio haya na kwa kawaida wangenishambulia kuhusu ni kwa nini niliitembea njia ya kumwamini Mungu. Kila wakati nilipokabiliwa na aina hii ya kuhojiwa, ningekuwa na wasiwasi, kwa sababu sikujua mpango upi muovu waliokuwa nao kwangu. Moyo wangu daima ulikuwa ukimwomba Mungu kwa haraka na kulilia msaada na mwongozo kupitia wakati wa kilele cha hatari hii. Siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, dhuluma, unyonywaji, na ukandamizwaji viliniumiza kwa mateso yasiyosemeka: Kila siku nilipewa kazi ya mikono iliyozidi na majukumu ya kisiasa ya kuchusha, ya kuchosha, nilisumbuliwa pia na ugonjwa wangu na juu ya yote, nilidhoofika akili. Lilinifikisha kwenye ukingo wa kusambaratika. Hasa wakati nilipoona mfungwa wa makamo wa kike amejinyonga kutoka kwa dirisha usiku wa manane kwa sababu hakuweza kuvumilia mateso ya kinyama ya polisi hawa waovu, na mfungwa mwingine mzee wa kike aliyekufa kutokana matibabu ya ugonjwa wake yaliyocheleweshwa, nilizama katika shida zile zile zilizosonga na tena nikaanza kutafakari kujiua. Nilihisi kuwa kifo kilikuwa ndiyo aina bora ya faraja. Lakini nilijua kwamba huko kungekuwa kumsaliti Mungu na singeweza kufanya hivyo. Sikuwa na chaguo jingine lolote ila kuvumilia maumivu yote na kuitii mipango ya Mungu. Lakini mara tu nilipofikiri juu ya hukumu yangu ndefu, na kufikiri juu ya nilivyokuwa mbali na kupata uhuru, nilihisi kuwa hakuna maneno yaliyoweza kuelezea maumivu yangu na kukata tamaa kwangu; nilihisi kuwa sikuweza kuendelea kuhimili hili na kwamba sikujua ni muda gani ningeweza kusimama imara. Ni mara ngapi sikuweza kufanya chochote ila kujifunika kwa mfarishi wangu usiku wa manane na kulia, nikimuomba na kumsihi Mwenyezi Mungu na kumwambia Yeye kuhusu maumivu yote yaliyokuwa kwa mawazo yangu. Katika wakati wa maumivu yangu mengi na kutojiweza, niliwaza: Mimi ninateseka leo ili nipate kujitenga na upotovu na kupokea wokovu wa Mungu. Shida hizi ndizo ninazopaswa kupitia, na ambazo ni lazima nipitie. Mara tu nilipofikiria hili, sikuhisi uchungu tena; Badala yake, nilihisi kuwa kulazimishwa kuingia gerezani kwa sababu ya imani yangu kwa Mungu, na kupitia shida ili kupata wokovu lilikuwa jambo la thamani na umuhimu mkubwa mno; mateso haya yalikuwa ya thamani sana! Bila kujua, dhiki ya moyo wangu ilibadilika kuwa furaha na sikuweza kuzuia hisia zangu; nilianza kuimba bila kufungua mdomo wimbo wa uzoefu niliokuwa na uzoefu nao moyoni mwangu uitwao “Tuna Bahati Kukutana na Kuja kwa Mungu”: “Tuna bahati kukutana na kuja kwa mungu, twaisikia sauti Yake. Tuna bahati kukutana na kuja kwa mungu, tunahudhuria sikukuu ya Mwanakondoo. Tunamjua Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaona matendo Yake ya ajabu. Tunaelewa siri ya maisha ya mwanadamu, maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya thamani zaidi. Nani anaweza kuwa na bahati zaidi? Nani anaweza kubarikiwa zaidi? Mungu anatupa ukweli na uzima, lazima tuishi kwa ajili ya Mungu. Lazima tuishi kwa ajili ya Mungu. Lazima tuishi kwa ajili ya Mungu. Tunapata ukweli na tunashuhudia kwa Mungu ili kulipa upendo wa Mungu” (Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliurudia wimbo huo ndani ya moyo wangu na nilivyozidi kuimba ndani ya moyo wangu, ndivyo nilivyozidi kutiwa moyo; nilivyozidi kuimba, ndivyo nilivyozidi kuhisi kuwa nilikuwa na nguvu na furaha. Sikuweza kujizuia kuapa mbele ya Mungu: “Ee, Mwenyezi Mungu, ninakushukuru Wewe kwa faraja Yako na kunitumainisha ambavyo vimenisababisha kuwa tena na imani na ujasiri wa kuendelea kuishi. Umeniruhusu kujisikia kwamba Wewe kweli ni Bwana wa maisha yangu na Wewe ni nguvu ya maisha yangu. Ingawa nimefungwa mahali hapa pa kusikitisha sana, siko peke yangu, kwa sababu Umekuwa pamoja nami daima kupitia siku hizi za giza; Umenipa imani tena na tena na umenipa motisha kuendelea. Ee Mungu, kama ninaweza kutoka nje ya hapa siku moja na kuishi kwa uhuru, basi nitatimiza wajibu wangu na sitauumiza moyo Wako tena wala kujifanyia mipango mwenyewe. Ee Mungu, bila kujali jinsi siku zijazo zilivyo ngumu au zilivyo za shida, niko radhi kukutegemea Wewe kwendelea kuishi na nguvu!”

Gerezani, mara kwa mara nilikumbuka siku za nyuma tukiwa na ndugu zangu wa kiume na wa kike; huo ulikuwa wakati mzuri sana! Kila mtu alishangilia na kucheka, na pia tulikuwa na migogoro, lakini yote haya yalikuwa kumbukumbu nzuri. Lakini kila wakati nilipotafakari juu ya nyakati ambapo kwa uzembe nilifanya kazi zangu za zamani, nilihisi kuwa na hatia sana na mwenye kuwiwa. Nilifikiri juu ya migogoro niliyokuwa nayo na ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa sababu ya tabia yangu ya kiburi; nilihisi kuwa na wasiwasi hasa na mwenye kujuta. Kila wakati hili lilipotokea, ningeangua kilio na kimya kimya ningeimba wimbo mashuhuri katika moyo wangu: “Nimemwamini Mungu kwa miaka mingi lakini sijawahi kutenda wajibu wangu vizuri, nahisi majuto makuu sana moyoni mwangu. Nimefurahia upendo mwingi wa Mungu, lakini sijawahi kurudisha chochote. Mungu amenipa fursa nyingi sana kutenda, lakini nilizichukulia zote kwa njia ya hobelahobela, na badala yake kwa wazo moja nikatafuta hadhi, umaarufu na utajiri na kufanya mipango ya hatima yangu ya baadaye. Nikiwa nimejawa na tamaa kubwa, kweli sikujua aibu yoyote na nimepoteza muda mwingi mzuri. … Najuta sana—mbona sikugundua kwamba tabia ya Mungu ni yenye haki? Sijui kama toba yangu imechelewa sana, najuta sana. Sijui kama Mungu atanipa fursa nyingine, najuta sana” (“Ninajuta Sana” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Katika maumivu yangu na kujilaumu, mara kwa mara nilimwomba Mungu moyoni mwangu: Ee Mungu! Kwa hakika nimepungukiwa na Wewe mno; kama Utaliruhusu, niko radhi kutafuta kukupenda Wewe. Baada ya kuondoka gerezani, bado nitakuwa tayari kutimiza wajibu wangu na nitakuwa radhi kuanza tena! Nitaufidia upungufu wangu wa zamani! Wakati wa muda wangu gerezani, nilikuwa nimewakosa hasa wale ndugu wa kiume na wa kike niliokuwa nikiwasiliana nao asubuhi na usiku; kwa kweli nilitaka kuwaona, lakini katika gereza hili la pepo ambalo nilikuwa nimefungiwa, tamaa hii ilikuwa ombi lisilowezekana. Hata hivyo, mara kwa mara ningewaona ndugu hawa wa kiume na wa kike katika ndoto zangu; niliota kwamba tulikuwa tunasoma neno la Mungu pamoja na kuwasiliana ukweli pamoja. Tulikuwa na furaha na wachangamfu.

Ujana Usio na Majuto Yoyote

Wakati wa tetemeko kubwa la ardhi la Wenchuan la mwaka wa 2008, gereza tulimokuwa tulifungiwa ndani lilitetemeshwa na mimi nilikuwa mtu wa mwisho kuhama eneo hilo wakati huo. Katika siku hizo kulikuwa na mitikisiko midogo baada ya tetemeko ambayo haikusita. Wafungwa wote na polisi wa gereza waliogopa sana na kuwa na wasiwasi kiasi kwamba hawakuweza kuendelea. Lakini moyo wangu ulikuwa hasa mtulivu na imara, kwa sababu nilijua kwamba hili lilikuwa ni neno la Mungu likitimia; kulikuwa ni kuwasili kwa ghadhabu kali ya Mungu. Wakati wa tetemeko hilo moja katika miaka mia, neno la Mungu liliulinda moyo wangu daima; ninaamini kwamba maisha na kifo cha mwanadamu vyote vi mikononi mwa Mungu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya hivyo, niko radhi kuitii mipango ya Mungu. Hata hivyo, kitu cha pekee kilichonifanya kuhuzunika ni kama ningekufa, basi singepata tena fursa ya kutimiza wajibu wangu kwa Bwana wa viumbe, singekuwa na fursa tena ya kuufidia upendo wa Mungu, na singeweza kuwaona ndugu zangu wa kiume na wa kike. Lakini, wasiwasi wangu ulikuwa uliozidi; Mungu alikuwa nami daima na alinipa ulinzi mkubwa sana, ambao uliniruhusu kuendelea kuishi baada ya tetemeko la ardhi na kuishi kwa amani wakati wa tetemeko!

Mnamo Januari ya mwaka wa 2011, niliachiliwa mapema, ambako hatimaye kulimaliza maisha yangu ya utumwa gerezani. Katika kupata uhuru wangu, moyo wangu ulikuwa na msisimko mkubwa: Ninaweza kurudi kanisani! Ninaweza kuwa pamoja na ndugu zangu wa kiume na wa kike! Maneno hayakuweza kuelezea hali yangu ya kihisia ya akili. Kile ambacho sikutarajia ni kwamba baada ya kurudi nyumbani, binti yangu hakunijua, na jamaa na marafiki zangu walinitazama kwa mtazamo wa pekee; wote walijitenga nami na hawangeingiliana nami. Watu waliokuwa karibu nami hawakunielewa au kunikaribisha. Wakati huu, ingawa sikuwa gerezani nikidhulumiwa na kuteswa, mitazamo ya dharau, dhihaka, na kuachwa vilifanya kuwe vigumu kustahimili. Nilikuwa dhaifu na hasi. Sikuweza kujizuia kutafakari juu ya siku za nyuma: wakati tukio lilipotendeka, nilikuwa na umri wa miaka thelathini na mmoja tu; wakati nilipotoka gerezani, majira nane ya baridi na majira saba ya joto yalikuwa yamepita. Ni mara ngapi ambapo Mungu alikuwa amepanga watu, mambo na vitu wakati wa upweke wangu na kutojiweza ili kunisaidia; ni mara ngapi maneno ya Mungu yalinifariji katika maumivu yangu na kukata tamaa kwangu; Ni mara ngapi nilipotaka kufa Mungu alinipa uwezo wa kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi. ... Katika kipindi hicho cha miaka mirefu ya mchungu, ni Mungu aliyeniongoza hatua kwa hatua nje ya bonde la kivuli cha mauti hadi kuendelea kuishi kwa ushupavu. Katika kukabili shida hii sasa, nilikuwa hasi na dhaifu na nilikuwa nimemsikitisha Mungu. Kwa kweli nilikuwa mwoga na mtu asiyeweza ambaye alikuwa alikuwa na asante ya punda! Katika kufikiria hili, moyo wangu ulishutumiwa vikali; sikuweza kujizuia kufikiri juu ya kiapo nilichofanya na Mungu wakati nilipokuwa gerezani: “Kama ninaweza kutoka nje ya hapa siku moja na kuishi kwa uhuru, basi bado nitatimiza wajibu wangu. Siko tayari kuumiza tena moyo wa Mungu na sitajifanyia mipango mwenyewe tena!” Niliwazia kiapo hiki na kutafakari juu ya hali niliyokuwa nayo wakati nilipofanya kiapo kwa Mungu. Machozi yaliyatia ukungu kuona kwangu na polepole nikaimba wimbo mmoja: “Mimi mwenyewe niko radhi kumfuatilia Mungu na kumfuata Yeye. Sasa Mungu anataka kuniacha lakini bado nataka kumfuata Yeye. Iwapo Ananitaka au la, bado nitampenda Yeye, na mwishowe lazima nimpate Yeye. Ninatoa moyo wangu kwa Mungu, na haijalishi kile Yeye hufanya, nitamfuata Yeye kwa maisha yangu yote. Lolote litokealo, lazima nimpende Mungu na lazima nimpate Yeye; sitapumzika mpaka nimpate Yeye(“Nimeamua Kumpenda Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).

Baada ya muda wa ibada za kiroho na urekebishaji, kwa haraka nilitoka nje ya uhasi wangu chini ya kunurishwa kwa Mungu na nikajirudisha kwenye safu za kutimiza wajibu wangu.

Hata kama miaka bora zaidi ya ujana wangu ilitumika gerezani; katika miaka hii saba na miezi minne nilipopitia shida kwa sababu ya imani yangu katika Mungu, sina malalamiko na sina majuto, kwa sababu ninaelewa ukweli fulani na nimepitia upendo wa Mungu. Nahisi kuwa kuna maana na thamani kwa mateso yangu; hili ni jambo la pekee la utukufu na neema ambazo Mungu alinitengenezea, hili ni pendeleo langu! Hata kama jamaa na marafiki zangu hawanielewi, na hata kama binti yangu hanijui, hakuna mtu, jambo au kitu kitakachoweza kunitenga na uhusiano wangu na Mungu; hata kama nikifa, siwezi kumwacha Mungu. Upendo Safi Bila Dosari ndio wimbo niliopenda sana kuuimba gerezani; sasa, nataka kutumia matendo yangu halisi kutoa upendo safi zaidi kwa Mungu!

Tanbihi:

a. “Kiongozi wa uovu wote” inahusu ibilisi mkongwe. Kirai hiki kinaonyesha kutopenda kabisa.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Utajiri wa Maisha

Wang Jun Mkoa wa Shandong Kwa miaka mingi tangu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, mke wangu na mimi tumepitia hili...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp