Mateso Makali ya CCP Yanauimarisha tu Upendo Wangu kwa Mungu

26/01/2021

Na Li Zhi, Mkoa wa Liaoning

Mnamo mwaka 2000, nilikuwa na bahati nzuri ya kusikia injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu. Kwa kusoma maneno ya Mungu, nilipata kuelewa siri ya majina ya Mungu, fumbo laZ kupata mwili kwa Mungu, na ukweli juu ya mambo kama vile hatua tatu za kazi ya Mungu zinavyowaokoa wanadamu, na jinsi zinavyombadilisha, kumtakasa na kumkamilisha mwanadamu. Nilikuwa na hakika kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, na nilikubali kwa furaha injili ya ufalme wa Mungu. Baada ya hapo, nilijiunga kivitendo na maisha ya kanisa, na kueneza injili na kumshuhudia Mungu. Mnamo 2002, nilijulikana karibu na eneo langu kwa kuhubiri injili na kila mara nilikuwa katika hatari ya kukamatwa na polisi wa CCP. Sikuwa na chaguo ila kutoroka nyumbani kwangu ili niweze kuendelea kutekeleza wajibu wangu.

Serikali ya CCP daima imekuwa ikitumia simu kama njia ya kufuatilia na kuwakamata Wakristo, kwa hivyo sikuthubutu kuipigia familia yangu simu baada ya kuondoka nyumbani. Kufikia mwanzoni mwa mwaka 2003 nilikuwa nimejitenga na familia yangu kwa takribani mwaka mmoja, kwa hivyo nilienda nyumbani kwa mama mkwe wangu kumwona mume wangu kwa sababu nilikuwa nimewakosa sana. Alipogundua kuwa nilikuwa nimerudi ndugu mdogo wa mume wangu alimpigia mama yangu na kumwambia kwamba nilikuwa nyumbani kwa mama mkwe wangu. Lililonishangaza, saa tatu baadaye, polisi wanne kutoka katika Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa walikuja nyumbani kwa mama mkwe wangu katika gari la polisi. Punde walipoingia ndani ya nyumba, waliniambia kwa ukali, “Tunatoka katika Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa. Wewe ni Li Zhi, sivyo? Umekuwa kwenye orodha yetu ya washukiwa kwa takribani mwaka mmoja, na sasa tumekupata hatimaye! Unaandama na sisi!” Niliogopa sana; na nikamwomba Mungu moyoni mwangu bila kukoma: “Ee Mwenyezi Mungu! Serikali ya CCP inanikamata leo kwa idhini Yako. Lakini mimi ni mtu wa kimo kidogo, na nahisi woga na naogopa. Tafadhali niongoze na Unilinde, na unipe imani na nguvu. Haijalishi jinsi watakavyonitendea, nataka kukutegemea Wewe na niwe na ushuhuda. Afadhali niende gerezani kuliko kuwa Yuda na kukusaliti!” Baada ya kuomba, nilifikiria kuhusu maneno haya kutoka kwa Mungu: “Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Aidha, ni ishara ya Yeye ambaye hawezi[a] kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu). “Hiyo ni kweli,” niliwaza. “Mungu anashikilia mamlaka na Anatawala juu ya vitu vyote. Katika miaka michache iliyopita, serikali ya CCP imefanya yote iwezayo kuvuruga na kuzuia kueneza injili ya ufalme wa Mungu, na bado wale wa kila dini na dhehebu ambao wanamwamini Mungu kwa dhati na kuisikia sauti ya Mungu wamerejea mbele ya kiti Chake cha enzi kukubali wokovu Wake katika siku za mwisho. Ni wazi kutokana na hili kwamba hakuna nguvu inayoweza kusimamisha kazi ya Mungu, na hakuna mwanadamu anayeweza kuizuia. Ingawa sasa nimeanguka mikononi mwa polisi wa CCP, wao wenyewe wamo mikononi mwa Mungu, na nikiwa na Mungu ubavuni mwangu hakuna chochote cha kuogopa!” Maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu, na polepole nilianza kutulia.

Nilielekezwa kwenye chumba cha kuhojiwa baada ya kuwasili katika Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa. Polisi waliuchukua mkanda wangu, wakavua mavazi yangu, viatu na soksi, kisha wakanipekua. Baadaye, mmoja wa polisi alipigia kelele, “Wewe fanya tu haraka utuambie kila kitu unachojua. Umekuwa muumini kwa miaka mingapi? Ni nani aliyekuhubiria? Viongozi wa kanisa lako ni akina nani? Umewahubiria watu wangapi? Wewe hufanya nini kanisani?” Sikujibu maswali yake, mara moja nikamtia aibu na kumkasirisha, na akasema kwa sauti, “Usipoanza kuzungumza, basi tuna njia nyingi za kukufanya uzungumze!” Akisema hivi alinivuta kwa nguvu kutoka kwenye kiti hadi chini kwenye sakafu. Maafisa wawili waliikanyaga miguu yangu huku wengine wawili wakinipiga mgongoni kwa nguvu. Kichwa changu kilikuwa karibu kibamizwe chini kwenye sakafu na niliona vigumu kupumua. Mmoja wa polisi kisha alichukua penseli na akaitumia kuchorachora polepole kwa kurudia kwenye vichepe vya miguu yangu, akiniumiza na kunitekenya wakati huo huo. Haingevumilika; ilikuwa vigumu sana kupumua hivi kwamba nilikuwa karibu kukosa hewa, na hofu ya kifo ikanijia. Mmoja wao aliendelea kunitishia: “Je, utaongea au la? Usipoongea, tutakutesa hadi ufe!” Nilihisi hofu sana mbele ya mateso na vitisho vya genge hili la polisi; nilikuwa na wasiwasi kwamba wangenitesa hadi nife. Nilichoweza kufanya kilikuwa kuendelea kumwomba Mungu tu, nikimwomba Anipe imani na nguvu, na Anilinde ili niweze kuwa shahidi na kamwe nisiwe Yuda na kumsaliti. Baada ya kuomba, nilikumbuka maneno haya ya Mungu: “Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Nikitiwa moyo na maneno ya Mungu, mara moja nilihisi nguvu ikiongezeka ndani yangu, na nikagundua kuwa woga na hofu yangu ya kifo vilikuwa matokeo ya kudanganywa na Shetani. Serikali ya CCP ilikuwa ikitumaini bure kunipitishia katika mateso ya ukatili kama njia ya kunilazimisha nijisalimishe kwa nguvu zake za kidikteta, kunifanya nilisaliti kanisa na kuwa Yuda anayemsaliti Mungu kwa sababu niliogopa kufa au sikutaka kupitia maumivu yoyote. Singeruhusu kwa vyovyote njama za ujanja za Shetani zifanikiwe, na niliamua nitakuwa shahidi kwa Mungu hata kwa gharama ya maisha yangu mwenyewe. Polisi waliendelea kunitesa vivyo hivyo, lakini sikuhisi woga tena. Nilijua hapo kwamba ilikuwa ni Mungu aliyekuwa akinionyesha huruma na ulinzi Wake, na nilihisi shukrani kubwa Kwake.

Kisha maafisa wawili wa polisi walinifunga pingu kwenye kiti na kuniuliza kwa ukali maswali yale yale tena. Walipoona kwamba bado sikujibu, waliimarisha mateso. Walivuta mikono yangu ikanyooka mbali na mwili wangu na kisha wakaivuta kwa nguvu nyuma na juu nyuma yangu. Mara moja, ilihisi kana kwamba ingevunjika na maumivu yake ya kupasua yalinifanya nitoe jasho mwili mzima; sikuweza kujizuia ila kupiga unyende. Kisha waliinyanyua miguu yangu kwamba miguu yangu ilikuwa juu ya kichwa changu, na kisha wakaivuta miguu yangu pande tofauti. Uchungu wa kurarua ulinisababisha karibu nizirai. Moyoni mwangu, niliendelea tu kumwomba Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Naomba Unipe imani na nguvu na azimio la kuvumilia maumivu haya. Naomba uwe tegemeo langu thabiti linaloipa roho yangu nguvu. Haijalishi ni hila gani kundi hili la pepo linatumia kwangu, nitakutegemea Wewe kila wakati na kuwa shahidi.” Baada ya kuomba, wimbo wa maneno ya Mungu ulinitokea akilini mwangu: “Wakati wanapitia majaribu, ni kawaida kwa watu kuwa dhaifu, au kuwa na uhasi ndani yao, au kukosa uwazi juu ya mapenzi ya Mungu au njia yao ya kutenda. Lakini katika hali yoyote, lazima uwe na imani katika kazi ya Mungu, na usimkane Mungu, kama tu Ayubu. … Anachokamilisha kwa kufanya kazi kwa njia hii ni imani, upendo na matarajio ya watu. Mungu hufanya kazi ya ukamilisho kwa watu, nao hawawezi kuiona, hawawezi kuihisi; katika hali kama hizi imani yako inahitajika. Imani ya watu inahitajika wakati ambao kitu hakiwezi kuonekana kwa macho tu, na imani yako inahitajika wakati huwezi kuziachilia dhana zako mwenyewe. Wakati ambapo huna uwazi kuhusu kazi ya Mungu, kinachohitajika kutoka kwako ni kuwa na imani uchukue msimamo imara na kuwa shahidi. Wakati Ayubu alifikia hatua hii, Mungu alimwonekania na kuzungumza naye. Yaani, ni kutoka ndani ya imani yako tu ndipo utaweza kumwona Mungu, na wakati una imani Mungu atakukamilisha(“Majaribu Yanahitaji Imani” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu nyingi. Nilifikiria juu ya majaribio makubwa ambayo Ayubu alipitia, wakati mwili wake wote ulikuwa umejaa majipu machungu na akapitia maumivu makali. Na bado, licha ya maumivu yake, bado alikuwa na uwezo wa kutafuta mapenzi ya Mungu; hakutenda dhambi kwa maneno yake au kumkana Mungu, lakini badala yake alimtii Mungu na kulitukuza jina takatifu la Mungu. Ayubu alikuwa na imani ya kweli na uchaji kwa Mungu, na hiyo ndiyo maana aliweza kuwa shahidi kwa Mungu na kwamwaibisha kabisa na kumshinda Shetani—mwishowe, Mungu alitokea na kuzungumza naye. Shida na majaribu ambayo yalikuwa yamenipata sasa vilikuwa vimeruhusiwa na Mungu. Ingawa sikuelewa kikamilifu mapenzi ya Mungu na mwili wangu ulikuwa unapitia maumivu makali, lakini ni Mungu ndiye aliyekuwa na uamuzi wa iwapo ningeishi au kufa, na bila idhini Yake, polisi hawangeweza kuchukua maisha yangu bila kujali kiasi walichonitesa. Polisi hawa walionekana wa kutisha kwa nje, lakini mbele za Mungu walikuwa tu chui wa karatasi, zana tu mikononi mwa Mungu. Mungu alikuwa anatumia ukatili na kutesa kwao ili kuikamilisha imani yangu, na nilitamani kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu, kujikabidhi kikamifu mikononi Mwake, na kumtegemea Mungu kumshinda Shetani na kutowaogopa polisi tena.

Polisi walinitesa kwa kurudia. Kuona kwamba bado nilikuwa siongei, mmoja wa polisi alichukua kipiga mstari cheupe cha chuma cha takribani sentimita 50 na akaanza kunigonga nacho vibaya usoni. Sijui ni mara ngapi alinigonga nacho; uso wangu ulivimba na ulikuwa ukiwaka kwa maumivu. Nilichoweza kuona zilikuwa tu nyota zikitanda mbele ya macho yangu na kichwa changu kilikuwa kikivuma. Wawili kati ya polisi hao kisha walitumia visigino vya viatu vyao vya ngozi kunikanyaga kwa nguvu kwenye mapaja yangu. Kila pigo liliniacha nikiwa na maumivu makali. Katika mateso yangu, nilichoweza kufanya kilikuwa tu kumwita Mungu kwa dhati moyoni mwangu, nikimwomba Anilinde ili niweze kushinda mateso ya kikatili niliyopewa na polisi wa CCP.

Saa 2 asubuhi iliyofuata, mkuu wa Jeshi la Polisi wa Makosa ya Jinai aliingia katika chumba cha mahojiano. Aliposikia kwamba polisi hawakuweza kupata habari yoyote kutoka kwangu, alisema kwa ukali, “Unakataa kuongea, sivyo? Hmm! Tutaona kuhusu hilo!” Kisha akaondoka. Adhuhuri hiyo, ofisa mnene aliyekuwa na kitambulisho mkononi mwake alinijia na kuniuliza, “Je, unamjua mtu huyu?” Mara moja nikaona kuwa alikuwa ni dada wa kanisa kutoka kijiji kimoja kama mimi. Niliwaza: “Haijalishi chochote, ni lazima nisimsaliti dada yangu.” Na kwa hivyo, nilijibu, “Hapana, simjui.” Alikunja uso, na kuchukua kirungu cha mshutuko wa umeme kilichokuwa kimewekwa juu ya meza. Akikipunga mbele yangu, kwa kutishia akasema, “Wewe ni mkaidi. Tunajua wewe ni kiongozi kanisani, kwa hivyo kiri! Kuna washiriki wangapi kanisani kwako? Pesa za kanisa ziko wapi? Usiponiambia, nitakuonjesha kirungu hiki cha mshtuo wa umeme!” Nikiiangalia sura yenye nia mbovu ya yule afisa, nilihisi woga sana na haraka haraka nikasali sala ya kimya kwa Mungu. Wakati huohuo, nilikumbuka maneno ya Mungu: “Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 26). Yakiwa yamejaa mamlaka, maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu na mara moja nilihisi kama nilikuwa na kitu cha kutegemea. Niliwaza: “Mungu ni mwenye uweza, na haijalishi Shetani na pepo ni wakatili vipi, si wao pia wako mikononi mwa Mungu? Nikiwa na Mwenyezi Mungu kama tegemeo langu thabiti, sina chochote cha kuogopa!” Kwa hivyo nilijibu kwa kawaida, “Sijui chochote.” Polisi huyo mnene alisema kwa nia ya kudhuru, “Hiki ndicho unachopata kwa kutokujua chochote!” Alivyosema hili, aligusa pingu zangu kwa kirungu cha umeme na mshtuo wa umeme wenye nguvu ulipita katika mwili wangu mzima kwa wimbi la uchungu—maumivu hayo yalikuwa yasiyoweza kuelezeka. Yule polisi aliendelea kunishtua na kirungu hicho, na wakati nilikuwa karibu kushindwa kustahimili tena, muujiza ulitokea: Kirungu kiliisha nguvu ya umeme! Nilikuwa nimeshuhudia uweza na ukuu wa Mungu, na zaidi ya hayo nilikuwa nilipitia ukweli kwamba Mungu yuko nami kila wakati, akinilinda, akinichunga, na kujali kuhusu udhaifu wangu. Imani yangu ilikua na azimio langu la kuwa shahidi kwa Mungu liliimarishwa.

Baadaye polisi waliona kwamba bado sikunuia kuongea, na kwa hivyo kwa jozi walichukua zamu kunichunga. Hawakuniruhusu nile, ninywe au hata kulala. Wakati nilipoanza kusinzia, wangenipiga na kunigonga mateke, wakitumaini kwamba hili lingevunja dhamira yangu. Hata hivyo, Mungu alinielekeza kung’amua mpango wao wa ujanja na nikasali kimya kwa Mungu, nikaimba nyimbo akilini mwangu na kutafakari maneno ya Mungu na, kabla sijajua, nikawa mchangamfu. Polisi hawa, kwa upande wao, walikuwa wakinywa kahawa bila kukoma na bado walikuwa wamechoka sana hadi walishinda wakienda miayo. Mmoja wao alisema kwa mshangao, “Lazima awe na nguvu ya kimiujiza inayomfanya awe na nguvu, la sivyo, anapataje hizi nguvu zote?” Nikimsikia polisi huyo akisema hivi, nilisifu nguvu kuu za Mungu tena na tena, kwa maana nilijua vizuri moyoni mwangu kuwa yote haya yalikuwa chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, na kwamba ilikuwa ni nguvu ya maisha ya Mungu mwenyewe iliyonishikilia na kunipa imani na nguvu. Ingawa sikujua ni aina gani nyingine za mateso ya kikatili ambazo polisi walikuwa wananipangia, nilikuwa na imani ya kumtegemea Mungu kukabiliana na kuhojiwa kulikofuata, na niliamua: Sitawahi kujisalimisha kwa nguvu za kidikteta za Serikali ya CCP, lakini nitakuwa shahidi kwa Mungu!

Jioni ya siku ya tatu, mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jinai alinimiminia kikombe cha maji ya moto na, akijifanya kujali, alisema, “Usiwe mjinga sasa. Mtu mwingine ameshakusaliti tayari, kwa hivyo kuna maana gani ya kuvumilia haya yote kwa ajili ya watu wengine? Niambie tu kila kitu unachojua na naahidi kukuacha uende. Mwanao bado ni mchanga na anahitaji upendo wa mama yake. Unaweza kuwa na maisha mazuri, na bado unayapoteza ukiamini katika Mungu fulani! Mungu hawezi kukuokoa, lakini sisi tunaweza. Tunaweza kukusaidia kwa shida zozote ambazo unaweza kuwa nazo, na tunaweza kukusaidia upate kazi nzuri ukitoka hapa….” Nilipokuwa nikimsikiliza akiongea, sikuweza kujizuia ila kufikiria juu ya mwanangu mdogo, nikiwaza jinsi alivyokuwa tangu kukamatwa kwangu. Je, marafiki na jamaa wangu wasioamini wangemdhihaki? Wanafunzi wenzake shuleni wangemnyanyasa? Wakati tu nilikuwa naanza kudhoofika, Mungu alinipa nuru kwa kifungu cha maneno Yake: “Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 17). Nikiwa nimetiwa moyo na maneno ya Mungu, niligundua wazi kuwa Shetani alikuwa akitumia hisia zangu kwa familia yangu kunishawishi nimsaliti Mungu. Shetani alijua kuwa nilimpenda mwanangu zaidi ya wote na alikuwa anawatumia polisi kama msemaji wake kunishambulia na kunijaribu, na kufanya upendo wangu kwa mwanangu unisababishe niwasaliti ndugu zangu. Kwa hivyo ningekuwa Yuda anayemsaliti Mungu ambaye mwishowe angeishia kulaaniwa na kuadhibiwa na Mungu—Shetani ni mwenye nia za kudhuru na mwovu sana! Nilifikiria juu ya jinsi ambavyo singeweza kuwa na mwanangu kumtunza, lakini haikuwa hivyo kwa sababu serikali ya CCP ilikuwa adui wa Mungu, na kwa sababu inawatia nguvuni na kuwatesa Wakristo kwa hasira? Lakini polisi walikuwa wakisema kwamba ni kwa sababu niliamini katika Mungu. Kwa kusema hivyo, hawakuwa wanaugeuza ukweli na kuupotosha ukweli? Serikali ya CCP haina aibu na ni ovu sana! Na kwa hivyo, haijalishi kile ambacho polisi alisema, sikumjali hata kidogo. Kuona kwamba sikuweza kushawishiwa na mbinu zake zote, aliondoka kwa hasira. Chini ya mwongozo na ulinzi wa Mungu, nilikuwa nimeyashinda majaribu ya Shetani kwa mara nyingine.

Ilikuwa baada ya 2 usiku jioni hiyo wakati polisi huyo mnene alirudi na kirungu kikubwa cha mshtuomshtuo wa umeme mkononi na wadogo wake watatu wakimfuata. Walinipeleka kwenye chumba cha mazoezi na kunivua nguo zangu (wakiniacha tu na nguo zangu za ndani), kisha wakanifunga kwa kamba kwenye kinu cha kuendesha kwa miguu. Nikiangalia nyuso zao, kila mmoja mwenye nia mbaya kumliko mwingine, kuliniacha nikiwa mwoga sana na asiyejiweza, na sikujua mateso ya kikatili ambayo wangenipa baadaye au yangechukua muda gani. Nilihisi dhaifu sana wakati huo na nilianza kuwa na mawazo ya kifo. Lakini mara moja, nilijua kwamba mawazo haya hayakuwa sawa, na kwa hivyo kwa haraka nilimwomba na kumwita Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Unaujua moyo wangu, na sitaki kuwa Yuda anayekusaliti na kuingia katika historia kama msaliti. Lakini kimo changu ni kidogo sana, na nahisi uchungu na dhaifu katika mateso haya—naogopa kuwa sitaweza kustahimili na nitakusaliti. Ee Mungu! Naomba unilinde na kunipa imani na nguvu. Naomba uwe nami, niongoze na kunielekeza, na uniwezeshe kuwa shahidi katika mateso haya katili.” Baada ya kuomba, nilifikiria kuhusu maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Maneno ya Mungu yaliniletea faraja na kunitia moyo. Yaliniruhusu nielewe kwamba Mungu alikuwa akiruhusu mateso haya katili yanitendekee ili imani na upendo wa kweli viweze kuchovywa ndani yangu, ili niweze kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu kupitia mateso yangu, kutii mipango na mipangilio ya Mungu, na kuwa shahidi kwa kutegemea maneno ya Mungu bila kujali majaribu yangekuwa makubwa vipi au maumivu yangekuwa makali vipi. Nikiwa nimeelewa mapenzi ya Mungu, ujasiri na azimio la kupigana na Shetani hadi mwisho mchungu viliinuka ndani yangu, na nikafanya azimio hili: Haijalishi ni mateso yapi ninapaswa kupitia, natamani kuendelea kuishi, na bila kujali jinsi mateso yangu yanavyokuwa makubwa, nitamfuata Mungu mpaka pumzi yangu ya mwisho!

Wakati huohuo, yule polisi mnene, akiwa na sigara inaning’inia mdomoni mwake, alinijia na kuniuliza, “Utazungumza au la?” Kwa uthabiti, nikajibu, “Unaweza kunipiga hadi nife, lakini bado sijui chochote.” Kwa hasira, aliitupa sigara yake sakafuni, na akichemka kwa hasira, akakifinya kirungu cha umeme mgongoni mwangu na kwenye mapaja yangu tena na tena. Maumivu makali yalinifanya nitokwe na kijasho baridi mwili wangu wote, na niliendelea kulia kwa uchungu. Huku akikifinya kirungu kwangu, alitoa sauti kubwa, “Hiki ndicho unachopata kwa kutoongea! Nitakufanya upigie unyende, na tutaona utadumu kwa muda gani!” Maafisa wengine chumbani wakiwa wamesimama kando kando walicheka kwa nguvu na kusema, “Inakuwaje kwamba Mungu wako haji kukuokoa?" Walisema pia mambo mengine mengi ya kumkufuru Mungu. Kuona sura zao za mapepo, nilimlilia Mungu kwa dhati anipe imani na nguvu ili niweze kuvumilia uchungu na kuifuta tabasamu iliyo usoni mwa Shetani. Baada ya kusali, niliufunga kabisa mdomo wangu na nikakataa kutoa sauti nyingine bila kujali walivyonitesa. Walinipitishia umeme bila kukoma. Wakati kirungu kimoja cha umeme kiliishiwa na nguvu ya umeme, walikibadilisha na kingine, na niliteswa hadi akili yangu ikawaa na kifo kilionekana kuwa bora kuliko maisha. Sikuweza kusongesha hata msuli mmoja na waliponiona sitikisiki walidhani nimezirai. Walinitupia maji baridi kuniamsha na kisha wakaendelea kunipishia shoti ya umeme. Katika uchungu wangu, nilikumbuka maneno ya Mungu yanayosema: “Genge hili la washiriki jinai![1] Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu…. Wanatamani kuwa wa nguvu za ukuu duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu kiasi kwamba isiweze kusonga mbele kiasi kidogo na wanamfunga mwanadamu kwa mkazo kama wapo nyuma ya kuta za shaba na chuma cha pua. Baada ya kufanya dhambi mbaya sana na kusababisha majanga mengi sana, je, bado wanatarajia kitu tofauti na kuadibu? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)).

Nuru ya maneno ya Mungu iliniruhusu kuona wazi uso wa kweli wa serikali ya CCP. Inachukia ukweli na Mungu kabisa, na inaogopa kabisa maneno ya Mwenyezi Mungu kuenea kila mahali. Ili kudumisha utawala wake milele, inafanya kila iwezalo kuzuia injili ya ufalme wa Mungu isienee, na haizuiwi na chochote kukamata, kuwatesa na kuwanyanyasa wateule wa Mungu. Serikali ya CCP inatunyanyasa na kututesa sisi tunaoamini namna hii kwa sababu inataka kuharibu kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Inafanya hili katika jaribio la kumaliza kabisa imani ya kidini, kuwazuia watu kumwamini na kumfuata Mungu, na kuigeuza China kuwa eneo la kumkana Mungu, na hivyo kufanikisha nia yake ya wazimu ya kuwadhibiti watu wa China milele. Licha ya ukweli kwamba serikali ya CCP inatangaza kwa ulimwengu wa nje kwamba kuna “uhuru wa imani” na “raia wa China wanafurahia haki za kisheria,” kwa kweli, haya yote ni uwongo mtupu ulio wazi uliokusudiwa kudanganya, kutapeli na kuwafunga watu, na ni mipango ya kuficha njia zake ovu! Serikali ya CCP hutenda kwa ukaidi hutenda kinyume na mbingu, na kiini chake ni cha ibilisi Shetani, cha adui wa Mungu! Wakati huo huo, nililazimika kabisa kufanya azimio kimya kimya: Lazima nisiruhusu gharama kuu ambayo Mungu amenilipia iwe ilikuwa bure; lazima niwe na azimio na dhamiri, na haijalishi ni mateso gani katili ambayo bado napaswa kuvumilia, nitakuwa shahidi kwa Mungu daima. Wakati huo tu, hisia nzuri ya haki iliibuka ndani yangu, na nilimhisi Mungu kando yangu, akinipa nguvu. Baadaye, bila kujali jinsi polisi walivyonipitishia umeme, sikuhisi uchungu. Nilikuwa nimeshuhudia tena matendo ya ajabu ya Mungu; nilipata ufahamu wa kina sana wa uwepo wa Mungu, kwamba ni Mungu aliyekuwa akinilinda na kunichunga. Polisi walinitesa kwa saa nne lakini bado hawakupata habari yoyote kutoka kwangu. Wakikosa chaguo, hawangefanya chochote isipokuwa kunifungua kutoka kwenye kinu cha kuendesha kwa miguu. Sikuwa hata na chembe ya nguvu mahali popote mwilini mwangu na nikaanguka kwa kishindo sakafuni. Polisi wawili walinivuta hadi kwenye chumba cha kuhojiwa na kuniweka kwenye kiti, kisha wakanitia pingu kwenye bomba kuu la kupitisha joto. Kuwaona wakionekana walioshindwa kabisa, sikuwa na budi ila kutoa shukrani na sifa kwa Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Nimeuona uweza Wako na ukuu wako, na naona kwamba nguvu Yako ya maisha inaweza kushinda nguvu zingine zote. Shukrani ziwe kwa Mungu!”

Siku ya nne, polisi watano waliingia katika chumba cha kuhojiwa. Mmoja wao alibeba kirungu cha mshtuo wa umeme na kukifanya kitoe sauti kwa kupitisha umeme. Siku nyingi za mateso ya kikatili zilikuwa zimenijaza hofu kila nilipoona kirungu hicho kikitoa mwanga huo wa samawati. Afisa ambaye hakuwa amenihoji kabla ya siku hiyo alikuja na kusimama mbele yangu, akanifinya na kirungu cha mshtuo wa umeme na kusema, “Nasikia wewe ni mgumu sana. Leo, nitaona jinsi ulivyo mgumu hasa. Siamini kuwa hatuwezi kukupata. Utazungumza au la? Usipoongea, basi utakutana na hatima yako siku ii hii!” Nilimjibu, nikisema, “Sijui chochote.” Hili lilimwaibisha na kumpa hasira, na akanivuta kwa nguvu kutoka kwenye kiti hadi chini sakafuni na akanishikilia hapo. Polisi mwingine alisukuma kirungu cha umeme ndani ya shati langu, akipiga kelele alipokuwa akiushtua mgongo wangu kwa umeme, “Utaongea au la? Usipoongea, tutakuua!” Nikikabiliwa na ukatili wao na sura zao za kutisha, zenye ufisadi, sikuwa na budi ila kuingia katika hali ya hofu, na kwa haraka nikamlilia Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Tafadhali niongoze! Tafadhali nipe imani ya kweli na nguvu!” Polisi waliendelea kunipitishia nguvu ya umeme huku nikipiga unyende bila kukoma. Ilihisi kana kwamba damu yote mwilini mwangu ilikuwa ikikimbia kwenda kichwani mwangu, na iliumiza sana kwamba nililowa jasho na karibu nizirai. Kuona kwamba bado singeongea, polisi walianza kunilaani kwa hasira yao. Baadaye kidogo nilipokuwa karibu kuzirai, walininyanyua na kunifunga pingu kwenye kiti tena, ambapo baada ya hapo wawili walichukua zamu ya kunichunga kuhakikisha kuwa sikulala. Kufikia wakati huo, sikuwa nimekula chakula chochote, kunywa maji yoyote, au kulala kwa siku nne mfululizo usiku na mchana. Kuongezea kwa hilo mateso ya kikatili ambayo walikuwa wakinitesa, mwili wangu ulikuwa umefikia hali dhaifu zaidi. Nilikuwa na baridi na njaa, na maumivu ya kuwa na njaa na baridi kabisa yaliungana na maumivu ya kuwasha ya mwili wangu uliojeruhiwa—nilihisi kana kwamba maisha yangu yalikuwa yanakaribia mwisho. Katika hali yangu dhaifu zaidi, mstari wa maneno ya Mungu ulitokea akilini mwangu: “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu(Mathayo 4:4). Nikitafakari haya, nilielewa kuwa maneno ya Mungu tu ndiyo yaweza kuwa msaada wangu kuendelea kuishi katika hali kama hii, na wakati huo huo pia niligundua kuwa ni hali hii hasa ndiyo Mungu alikuwa anaitumia kukamilisha kuingia kwangu katika kipengele hiki cha ukweli. Nilipotafakari haya kwa kurudia, bila kujua nilisahau kabisa kuhusu mateso, njaa na baridi yangu.

Siku ya tano, polisi waliona kuwa nilisalia kimya kwa uthabiti, na wakaanza kunitishia kwa uonevu, wakisema, “Subiri tu hadi utakapokuwa umehukumiwa. Utapata miaka saba angalu, lakini bado kuna nafasi ya kuepuka hilo ukianza kuongea sasa!” Kisha nikamwomba Mungu kimya kimya: “Ee Mwenyezi Mungu! Polisi wa CCP wanasema watanihukumu kifungo cha miaka saba gerezani, lakini najua kuwa hawana uamuzi wa mwisho, kwa kuwa majaliwa yangu yamo mikononi Mwako. Ee Mungu! Ni afadhali kufungwa gerezani maisha yangu yote na kubaki kwenye njia ya kweli kuliko kukusaliti!” Baada ya hapo, polisi walijaribu kunishawishi nimsaliti Mungu kwa kumleta mume wangu asiyeamini katika Mungu. Aliponiona nimevaa pingu nikiwa na majeraha mwili wangu mzima, aliniambia kwa unyonge, “Nimeziona pingu kwenye runinga tu. Sijawahi kufikiria ningekuona nazo.” Nilipomsikia akisema hivi na kuona sura yake ya kusikitisha, nilimwomba Mungu haraka, nikimuuliza Anilinde ili nisije nikashikwa na mtego wa Shetani kwa sababu ya hisia zangu kwa familia yangu. Baada ya kusali, nikamwambia mume wangu kwa utulivu, “Namwamini Mungu, siibi vitu au kuwanyang’anya watu. Mimi huenda tu kwenye mikutano na kusoma maneno ya Mungu, na kujaribu kuwa mtu mwaminifu kama Mungu anavyotaka. Sijatenda jinai yoyote, lakini wanataka kunihukumu gerezani.” Mume wangu akajibu, “Nitakutafutia wakili.” Alipoona kwamba mume wangu hakujaribu kunifanya nitoe habari juu ya kanisa na ndugu zangu, lakini badala yake alikuwa anajitolea kuniajiria wakili, polisi walimtoa kwa fujo nje ya chumba hicho. Nilijua kuwa huyu alikuwa Mungu akinilinda, kwa sababu hisia zangu kwa familia yangu ni za kina sana, kama mume wangu angesema chochote kinachoonyesha kujali hali yangu ya mwili, sijui kama ningeweza kuendelea kuwa na nguvu. Ni mwongozo na ulinzi wa Mungu ndivyo viliniwezesha kushinda jaribio la Shetani.

Polisi waliona kwamba hawakuwa wamenipata na, wakiwa wamejaa hasira, wakasema, “Tutakudunga sindano baada ya dakika moja ambayo itakufanya uwe mwendawazimu. Halafu, tunakuacha uende, na hata hutaweza kufa!” Hili lilinifanya niwe na wasiwasi mwingi, na hofu ikanishika mara nyingine tena. Nilifikiria jinsi serikali ya CCP katili na uovu: Mara wanapomkamata mtu aliye na madaraka kanisani, na wakati bado hawawezi kupata chochote juu ya kanisa kutoka kwake baada ya kichapo na mateso ya chuki, wanamdunga kwa nguvu na dawa zinazompa wazimu na kumsababisha awe mwenye kuchanganyikiwa na akili—ndugu wengine wameteswa kikatili na kuadhibiwa kwa njia hii na serikali ya CCP. Moyo wangu ulianza kupiga kifuani mwangu nilipowaza hili, na nilijiuliza: “Je, kweli nitateswa na hawa askari jela wa CCP hadi nipoteze akili yangu na niishie kuzurura kama kichaa?” Kadiri nilivyofikiria kuhusu hili zaidi, ndivyo nilivyoogopa zaidi, na sikuweza kuzuia jasho baridi kutoka kwenye mwili wangu. Kwa haraka, niliomba na kumwita Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Askari jela wa CCP wanataka kunidunga sindano yenye dawa ili wanifanye niwe wazimu, na naogopa nitakuwa kichaa. Ee Mungu! Ingawa najua kuwa nastahili kuwa shahidi Kwako, nahisi mwoga na mwenye hofu sana sasa hivi. Ee Mungu! Tafadhali ulinde moyo wangu, na unipe imani ya kweli ili niweze kukuaminia maisha yangu na kifo changu, na kutii mipango na mipangilio Yako.” Wakati huo huo, maneno ya Bwana Yesu yalinijia mawazoni: “Msiwe na hofu ya wao wanaoua mwili, lakini hawana uwezo wa kuifisha roho: ila heri uwe na hofu ya yeye anayeweza kuiangamiza roho pamoja na mwili katika kuzimu(Mathayo 10:28). Maneno ya Bwana yalinipa imani na nguvu. “Ndiyo,” niliwaza. “Pepo hawa wanaweza kuua na kuumiza mwili wangu, lakini hawawezi kuiua au kuiumiza roho yangu. Bila idhini ya Mungu, sitakuwa kichaa hata kama wakinidunga na dawa hizo.” Kisha nikafikiria kuhusu maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Watu wanapokuwa tayari kuyatoa maisha yao, kila kitu huwa hafifu, na hakuna anayeweza kuwashinda. Ni nini kingekuwa muhimu zaidi kuliko uzima? Hivyo, Shetani anakuwa hawezi kufanya chochote zaidi ndani ya watu, hakuna anachoweza kufanya na mwanadamu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 36). Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, woga ambao nilihisi ndani mwangu ulipotea polepole na sikuhisi tena hofu hiyo. Badala yake, nilikuwa radhi kujiweka mikononi mwa Mungu na kujiwasilisha kwa ukuu wa Mungu iwe ningeishi au kufa, na ikiwa ningekuwa kichaa au punguani. Wakati huo huo, polisi alileta sindano na dawa hiyo, na kunitishia, akisema, “Utaongea au la? Usipoongea, nitakudunga na hii!” Mara moja bila woga, nikasema, “Fanya kile unachotaka. Kila kinachotokea kiko juu yako.” Kuona kwamba sikuogopa, alisema kwa ukatili, “Nenda ulete yenye virusi vya UKIMWI! Tutamdunga hiyo.” Wakati bado sikuonyesha hofu, alikaza meno yake kwa hasira, na kusema, “Wewe mkorofi. Wewe ni mgumu kuliko Liu Hulan!” Kisha akaitupa sindano kwenye meza. Nilihisi mwenye furaha kuu. Nikiwa nimeshuhudua jinsi maneno ya Mungu yalivyonielekeza kumdhalilisha Shetani kwa mara nyingine tena, sikuwa na budi ila kutoa sala ya shukrani kwa Mungu. Mwishowe, polisi waligundua kuwa hawangepata habari waliyotaka kutoka kwangu, kwa hivyo waliondoka kwa kukata tamaa.

Baada ya kujaribu kila wawezalo bila mafanikio, polisi hawakuwa na la kufanya ila kunipeleka kizuizini. Punde nilipofika huko, walinzi wa gereza waliwachochea wafungwa wengine, wakisema, “Yeye ni muumini wa Umeme wa Mashariki. Mkaribisheni ‘kwa moyo mkunjufu’!” Kabla hata ya kuwa na nafasi ya kujibu, wafungwa kadhaa walinikimbilia na kunivuta kwenye choo na kisha, baada ya kunivua nguo zangu, wakaanza kuniosha kwa maji baridi ya barafu. Kila chungu cha maji baridi niliyomwagiwa yalihisi kama jiwe likiugonga mwili wangu, yenye baridi ya barafu na uchungu, na nikawa na baridi sana hivi kwamba nilikuwa natetemeka kila mahali. Niliinama chini sakafuni, kichwa changu kikiwa mikononi mwangu, nikimwita Mungu tena na tena moyoni mwangu. Baada ya muda, mmoja wa wafungwa alisema, “Sawa, sawa, imetosha. Sitaki awe mgonjwa.” Wafungwa ambao walikuwa wakinipa adhabu hii walikoma tu walipomsikia mfungwa huyo akisema hivi. Alipogundua kuwa sikuwa nimekula kitu chochote kwa siku tano, wakati wa chakula cha jioni alinipa nusu ya mkate wa mahindi uliopikwa kwa mvuke. Nilikuwa najua kabisa kuwa huku kulikuwa kujali kwa Mungu kuhusu udhaifu wangu, na kumgusa mfungwa huyu anisaidie. Niliona kuwa Mungu alikuwa pamoja nami kila wakati, na kutoka moyoni mwangu nilimshukuru Mungu kwa rehema na wokovu Wake.

Ndani ya Kizuizi, niliishi pamoja na wafungwa wa kila aina nyingine. Kila moja ya milo yetu mitatu ilikuwa na kipande cha mkate wa mahindi uliochemshwa na vipande viwili vya ua la tanipu lililotiwa chumvi, la sivyo ilikuwa bakuli la supu ya kabichi iliyokuwa na wadudu wakielea ndani yake na kabichi kidogo sana. Mara moja kwa wiki, tulipewa chakula cha nafaka nzuri, ambacho bado kilikuwa mkate uliopikwa kwa mvuke kiwango cha ngumi—hakikushibisha kabisa. Kando na kukariri sheria za gereza, kila siku mahali hapo tulipewa vipimo vya kazi ya kutengeneza sanaa ya mikono ambavyo vilikuwa vigumu kutimiza. Kwa sababu mikono yangu ilikuwa imeharibiwa na pingu zilizokazika na ilikuwa imepitishiwa umeme kiasi kwamba nilipoteza hisia zote ndani yake, na juu ya hayo sanaa za mikono ambazo tulipaswa kutengeneza zilikuwa ndogo sana, singeweza kuzishikilia, na singeweza kukamilisha kazi yangu nyingi. Wakati mmoja, kwa sababu sikuwa nimemaliza kazi yangu, walinzi wa gereza waliwafanya wafungwa wengine wanitazame usiku kucha kunizuia nisilale. Pia niliadhibiwa mara kwa mara kwa kufanywa nishike doria, na niliruhusiwa kulala tu kwa saa nne usiku. Wakati huu, polisi wa CCP waliendelea kunihoji bila kukoma. Walikuwa hata wamemfanya mwanangu aniandikie barua, wakijaribu kunidanganya nimsaliti Mungu. Lakini chini ya ulinzi na mwongozo wa Mungu, niliweza kung’amua ujanja wa Shetani na kuwa shahidi wakati baada ya mwingine. Licha ya ukweli kwamba hawakuwa wameweza kupata chochote kinachoweza kuniweka hatiani, bado walinishtaki kwa “kuvuruga utaratibu wa umma” na kunihukumu miaka mitatu ya masomo upya kupitia kazi.

Mnamo Desemba 25, 2005, hukumu yangu ilitekelezwa kikamilifu na niliachiliwa. Baada ya kupitia mapigano haya kati ya haki na uovu, ingawa nilikuwa nimeteseka katika mwili na mawazo, bado nilikuja kuelewa ukweli mwingi, na nikaona wazi kiini kinachopinga Mungu, cha mapepo cha serikali ya CCP. Pia nilipata ufahamu fulani halisi wa uweza, ukuu, ajabu na hekima ya Mungu, na nilipitia kweli upendo wa Mungu kwangu na wokovu Wake. Wakati wale mashetani walikuwa wakinitesa na kuniadhibu, ni nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu kwa wakati unaofaa ndivyo vilikuwa msaada wangu thabiti na ndivyo vilivyonipa azimio na ujasiri wa kupigana na Shetani hadi mwisho kabisa. Wakati Shetani alikuwa akijaribu ujanja wa hila wa kila aina kunijaribu na kunishawishi nimsaliti Mungu, ni Mungu ndiye aliyetumia maneno Yake kwa wakati unaofaa kunitahadharisha na kunielekeza, na kufuta vumbi kutoka katika macho yangu ya kiroho ili niweze kung’amua njama za Shetani na kusimama kidete katika ushuhuda wangu; wakati wale pepo walinitesa vibaya hadi kifo kikaonekana kuwa afadhali na maisha yangu yalikuwa ukingoni, maneno ya Mungu yalikuwa msingi wa kupona kwangu. Yalinipa imani na nguvu kubwa, na yakaniwezesha kujiondoa kutoka katika mshiko ambao kifo kilikuwa nao kwangu. Vitu hivi vyote viliniruhusu kuona kweli asili ya Mungu iliyo nzuri na yenye fadhila—ni Mungu tu anayewapenda wanadamu zaidi. Serikali ya CCP, kwa upande mwingine, genge hili la Shetani na mapepo, linaweza tu kuwapotosha, kuwadhuru na kuwameza watu! Leo, mbele ya mashambulio makali yanayosababishwa kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu na serikali ya CCP, nimeazimia kwa uthabiti kabisa kumwacha shetani huyo mzee serikali ya CCP, kumpa Mungu moyo wangu, na kufanya bidii yangu yote kufuatilia ukweli na kutafuta kumpenda Mungu. Nitaeneza injili ya ufalme wa Mungu na kuwarudisha mbele za Mungu wale wote wanaomwamini Mungu kwa dhati, wanaotamani ukweli, na ambao wamedanganywa sana na serikali ya CCP, ili niweze kumlipa kwa kunifadhili na wokovu Wake!

Tanbihi:

1. “Washiriki jinai” ni wa namna moja na “kundi la majambazi.”

a. Maandishi asilia yanasema “ni ishara ya kutoweza.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp