Upendo wa Mungu Umeuimarisha Moyo Wangu

26/01/2021

Na Zhang Can, Jimbo la Liaoning

Katika familia yangu, kila mtu daima amekuwa akielewana na mwingine vizuri sana. Mume wangu ni mtu mwenye kufikiria wengine sana na anayejali, na mwanangu ni mwenye busara sana na daima huwaheshimu sana wazee wake. Aidha, tumekuwa wakwasi kabisa. Kinadharia, ningefaa kuwa mwenye furaha sana, lakini hali halisi haikutendeka kwa namna hiyo. Bila kujali jinsi mume wangu na mwanangu walivyonitendea vyema, na bila kujali jinsi tulivyokuwa wenye mali, hamna mojawapo ya hayo ambayo yangeweza kunifurahisha. Sikuweza kamwe kulala usiku kwa sababu nilianza kuwa na ugonjwa wa baridi yabisi na pia nilikuwa na tatizo baya la kukosa usingizi, ambalo lilisababisha kupunguka kwa mzunguko wa damu kwenye ubongo wangu na udhaifu wa jumla kwenye viungo vyangu. Maumivu makali ya magonjwa haya pamoja na shinikizo la siku zote la kuendesha biashara vilinisababisha niishi na mateso yasiyoelezeka. Nilijaribu kuyashinda kwa njia nyingi tofauti, lakini hakuna kitu ambacho kiliwahi kuonekana kufaulu.

Mnamo Machi mwaka wa 1999, rafiki mmoja alinihubiria injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Kupitia kusoma neno la Mungu kila siku, kuhudhuria mikusanyiko siku zote, na kushiriki pamoja na ndugu zangu, nilikuja kufahamu ukweli kiasi, nikapata habari kuhusu siri nyingi ambazo sikuzijua hapo awali, na nikawa thabiti katika imani yangu ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerejea. Nilisisimshwa sana na haya yote na kila siku nilikula neno la Mungu kwa shauku. Pia nijishughulisha na maisha ya kanisa, mara nyingi tukikusanyika, tukiomba, na kuimba nyimbo na kucheza ili kumsifu Mungu pamoja na ndugu zangu. Nilihisi hali ya amani na furaha moyoni mwangu na hamasa yangu na mtazamo wangu uliboreshwa kila siku iliyopita. Polepole lakini kwa hakika, nilianza kupona magonjwa mbalimbali niliyougua. Mara nyingi nilitoa shukrani na sifa zangu kwa Mungu kwa ajili ya maendeleo haya chanya maishani mwangu na nilitaka kueneza injili ya Mwenyezi Mungu kwa watu wengi hata zaidi ili wote waweze kupata wokovu wa Mungu. Muda mfupi baada ya hapo, kanisa lilinikabidhi wajibu wa kazi yake ya kueneza injili. Nilijiingiza katika kazi hii kwa bidii ya mchwa, lakini kitu kilitokea ambacho sikuwahi kufikiria …

Jioni ya Desemba 15, mwaka wa 2012, nilipokuwa tu nimemaliza kukutana na dada wanne na nilikuwa karibu kuondoka, tulisikia mlio mkubwa wa kupasuka mlango wa mbele ulipopigwa teke na kufunguliwa na polisi saba au wanane waliingia ndani ya chumba hicho kwa kishindo, wakitufokea: “Mtu yeyote asisonge, wekeni mikono yenu juu!” Bila kuonyesha hati yoyote, walianza kutupekua kwa nguvu, wakichukua ngawira kitambulisho changu na risiti ya mapatano ya kibiashara ya fedha za kanisa yuani 70,000. Walisisimka sana mara tu walipoona risiti hiyo na walianza kutusukuma na kutuvuta kwa nguvu hadi katika gari la polisi na kutupeleka kwenye kituo cha polisi. Katika kituo cha polisi, walichukua ngawira simu zetu za rununu, vifaa vya kuchesesha MP5 na yuani 200 pesa taslimu kutoka kwenye mifuko yetu. Wakati huo, walishuku kuwa mimi na mmoja wa akina dada hao tulikuwa viongozi kanisani, kwa hivyo usiku huo walituhamisha sisi wawili kwenda katika Kitengo cha Upelelezi wa Jinai cha Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa.

Tulipofika, polisi walitutenganisha na kutuhoji mmoja mmoja. Walinitia pingu kwenye stuli ya chuma kisha afisa mmoja alinihoji kwa ukali: “Je, ukweli kuhusu yuani hizo 70,000 ni gani? Ni nani alityetuma pesa hizo? Ziko wapi sasa? Kiongozi wa kanisa lako ni nani?” Nilimwomba Mungu wakati wote moyoni mwangu: “Mungu Mpendwa! Polisi huyu anajaribu kunilazimisha niwasaliti viongozi wa kanisa na nimkabidhi pesa za kanisa. Siwezi kuwa Yuda hata kidogo na kukusaliti. Ee Mungu! Niko tayari kujiweka mikononi Mwako. Ninakuomba Unipe imani, ujasiri na hekima. Bila kujali jinsi polisi watakavyojaribu kupata habari kutoka kwangu kwa kutumia nguvu, niko tayari kuwa na ushuhuda Kwako.” Kisha nikawaarifu kwa ushupavu: “Sijui!” Jambo hili lilimghadhibisha sana polisi huyo; alichukua sapatu kutoka chini na kuanza kunipiga kichwani kikatili huku akinikemea kwa hasira: “Jaribu tu kukaa kimya. Jaribu tu na umwamini Mwenyezi Mungu! Tutaona utaendelea kuamini kwa muda gani!” Uso wangu uliuma sana kwa uchungu kutokana na kichapo hicho na ulianza kuvimba haraka, na nilikuwa na maumivu makali ya kichwa. Polisi wanne au watano walichukua zamu ya kunipiga ili kunilazimisha niwaambie mahali ambapo pesa za kanisa zilikuwa zimehifadhiwa. Baadhi yao walipiga miguu yangu mateke, wengine walikamata nywele zangu kwa nguvu, wakizivuta na kuzitikisa huku na huko, na wengine walinizaba kibao mdomoni. Nilianza kutokwa na damu mdomoni, lakini walifuta tu damu na kuendelea kunipiga. Pia walinipiga kwa nguvu bila mpango kwa kutumia kirungu cha mshtuo wa umeme na, walipokuwa wakinipiga, walifoka: “Je, utazungumza au la? Sema ukweli!” Walipoona kwamba bado nilikuwa nikikataa kuzungumza, walinishtua kwa umeme kwenye kinena na kwenye kifua—maumivu yalikuwa makali sana. Moyo wangu ulikuwa ukipiga kwa nguvu, nilianza kuwa na tatizo la kupumua na nilikunjamana kuwa katika umbo la mpira, nikitetemeka. Ilihisi kana kwamba kifo kilikuwa kikinikaribia, hatua kwa hatua. Ijapokuwa niliufunga mdomo wangu na sikusema lolote, nilihisi dhaifu sana moyoni mwangu na nilifikiria kuwa singeweza kuvumilia kwa muda mrefu zaidi. Katikati ya mateso yangu, kamwe sikuacha kumwomba Mungu: “Ee Mungu! Ingawa nimeazimia kukuridhisha, mwili wangu ni dhaifu na hauna nguvu. Ninaomba Unijaze nguvu ili niweze kuwa shahidi Kwako.” Wakati huo, niliwaza ghafla jinsi Bwana Yesu alivyopigiliwa msumari msalabani, alipigwa vibaya na askari wa Kirumi: Alipigwa na kuraruliwa sana hadi akalowa damu nyingi, mwili Wake wote ulijawa na vidonda…, lakini hakusema hata neno moja. Mungu ni mtakatifu na hana hatia, lakini Alivumilia fedheha kubwa na maumivu makali na alikuwa tayari kusulubiwa ili awakomboe wanadamu. Nilijiwazia: “Ikiwa Mungu anaweza kutoa mwili Wake ili kuwaokoa wanadamu wapotovu, ninapaswa pia kupitia mateso ili kulipa upendo wa Mungu.” Baada ya kutiwa moyo na upendo wa Mungu, imani yangu ilirejeshwa na niliapa kwa Mungu: “Mungu Mpendwa, mateso yoyote yale Unayopitia, mimi pia sina budi kuyapitia. Sina budi kukinywa kikombe kile kile cha mateso kama Wewe. Nitatoa maisha yangu ili kuwa shahidi Kwako!”

Baada ya mateso haya kuendelea wakati mwingi wa usiku, nilikuwa nimepigwa kiasi kwamba hata wakia mmoja wa nguvu haukubaki mwilini wangu. Nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba sikuweza kudumisha macho yangu yakiwa yamefumbuka, lakini mara tu nilipoanza kufumba macho yangu, walinirushia maji. Nilikuwa nikitetemeka kwa ajili ya baridi. Kikundi hiki cha watu hawa wakatili waliponiona nikiwa katika hali hiyo, walinikemea kikatili: “Bado hutaki kuzungumza? Mahali hapa, tunaweza kukutesa mpaka ufe na hakuna mtu atakayejua kamwe!” Niliwapuuza. Mmoja wa askari hao waovu kisha alichukua ganda la mbegu za alizeti na kuzishinikiza kwenye ukucha wa kidole changu; hili lilikuwa la kuumiza kwa namna isiyovumilika na sikuweza kuzuia kidole changu kutetemeka. Kisha wakaanza kunirushia maji usoni pangu na kuyamwaga chini ya shingo langu. Maji hayo baridi kama barafu yalinipelekea kutetemeka kwa ajili ya baridi; nilikuwa na maumivu makubwa kabisa. Usiku huo, nilimwomba Mungu mfululizo, nikiogopa kwamba ikiwa ningemwacha, singeweza kuendelea kuishi. Mungu alikuwa karibu nami kila wakati na maneno Yake yalinitia moyo daima: “Watu wanapokuwa tayari kuyatoa maisha yao, kila kitu huwa hafifu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 36). “Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Maneno ya Mungu yalinipa nguvu nyingi mno. Nilijiwazia, “Hayo ni ya kweli, Mungu anatawala kwa ukuu vitu vyote na vitu vyote viko mikononi Mwake. Hata kama polisi wabaya watatesa mwili wangu hadi kufa, roho yangu iko chini ya udhibiti wa Mungu.” Kwa ajili ya msaada wa Mungu, sikumwogopa Shetani tena, sembuse kuwa tayari kuwa msaliti na kuishi maisha yasiyokuwa na maana ya kuridhisha tamaa za mwili. Kwa hivyo, niliapa kwa Mungu katika maombi: “Mungu Mpendwa! Ijapokuwa pepo hawa wanautesa mwili wangu, bado niko tayari kukuridhisha na kujiweka mikononi Mwako kikamilifu. Hata ikiwa inamaanisha kifo changu, nitakuwa shahidi Kwako na sitawahi kupiga magoti mbele ya Shetani!” Kwa ajili ya mwongozo wa maneno ya Mungu, nilijisikia nimejawa na matumanini na imani. Hata ingawa polisi walikuwa wakiumiza vibaya na kutesa mwili wangu na nilikuwa tayari nimeshinikizwa hadi kwenye upeo wa uvumilivu wangu, nikiwa na neno la Mungu likinihimili, ghafla nilihisi kuwa na maumivu madogo zaidi kuliko hapo awali.

Asubuhi iliyofuata, polisi hao waovu waliendelea kunihoji na pia walinitishia, wakisema: “Usipozungumza leo, tutakukabidhi kwenye kitengo maalum cha polisi—wana vifaa 18 tofauti vya mateso vinavyokusubiri huko.” Niliposikia kwamba wangenikabidhi kwenye kitengo maalum cha polisi, sikuweza kujizuia kujawa na hofu, nikijiwazia mwenyewe: “Polisi maalum kwa hakika ni wakatili zaidi kuliko watu hawa; je, nitawezaje kuendelea kuishi kupitia aina 18 tofauti za mateso?” Nilipokuwa tu nikiingia kwenye hali ya hofu, nilifikiria kuhusu kifungu kimoja cha neno la Mungu: “Mshindi ni nini? Wanajeshi wazuri wa Kristo lazima wawe jasiri na kunitegemea kuwa wenye nguvu kiroho; lazima wapigane kuwa wapiganaji na wapambane na Shetani hadi kufa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 12). Maneno ya Mungu yaliutuliza haraka moyo wangu uliokuwa na wayowayo na hofu. Yalinisaidia kugundua kuwa hivi ilikuwa vita vya kiroho na kwamba wakati ambao Mungu alitaka niwe shahidi ulikuwa umewadia. Nikiwa na Mungu akiniegemeza, hakukuwa na kitu cha kuogopa. Bila kujali polisi hao waovu walitumia mbinu gani za kuvuruga, ilinibidi nimtegemee Mungu ili niwe askari mzuri wa Kristo na kupigana na Shetani hadi kufa bila kuwahi kukubali kushindwa.

Alasiri hiyo, maafisa wawili waliosimamia maswala ya kidini kutoka katika Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa walikuja kunihoji: “Kiongozi wako wa kanisa ni nani?” Waliuliza. “Sijui,” nilijibu. Walipoona kwamba nilikataa kuzungumza, walibadilishana kati ya mbinu za upole na mbinu za ukatili. Mmoja wao alinipiga kikumbo begani mwangu kwa nguvu kwa ngumi yake huku huyo mwingine alianza kufoka nadharia za kipumbavu za kukana kuweko kwa Mungu ili kujaribu kunibembeleza: “Vitu vyote ulimwenguni vinatokea kwa njia ya kiasili. Unapaswa kuwa mwenye vitendo zaidi: Kumwamini Mungu hakutasaidia kutatua shida zozote katika maisha yako; unaweza tu kufanya hivyo kwa kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii. Tunaweza kukusaidia wewe na mwanao kupata kazi….” Niliendelea tu kuwasiliana kwa karibu na Mungu moyoni mwangu, na kisha nilifikiria kuhusu kifungu kimoja cha neno Lake: “Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 17). Maneno ya Mungu yalinipa nuru mara moja, yakiniwezesha kufahamu njama za hila za Shetani. Nilijiwazia: “Polisi huyu mwovu anajaribu kunidanganya kwa nadharia zake za kipumbavu na kunihonga na fadhila ndogo ndogo—sipaswi kudanganywa na hila za Shetani, na, hata zaidi, siwezi kumsaliti Mungu na kuwa Yuda.” Nuru ya Mungu iliniwezesha kugundua nia mbaya ya polisi, kwa hivyo bila kujali walitumia kwangu mbinu gani za upole au za kikatili, niliwapuuza tu. Usiku huo, nilisikia kwamba kuna mtu mwingine aliyekuwa akija kunihoji na kwamba alikuwa akidai kuwa nina rekodi ya uhalifu. Sikujua cha kutarajia au kile kitakachotokea, kwa hivyo nilichoweza kufanya tu ni kumwomba Mungu moyoni mwangu anipe mwongozo. Nilijua kuwa bila kujali ni aina gani za mateso na matatitzo niliyokuwa nikikabili, singemsaliti Mungu. Muda mfupi baadaye, nilipokuwa nimekwenda msalani, ghafla nilianza kuwa na mpapatiko wa moyo; nilipatwa na kizunguzungu na kuzirai sakafuni. Polisi waliposikia kulikuwa na tatizo, walikuja kwa mwendo wa kasi mara moja na kukusanyika karibu nami. Nilimsikia mtu akisema kwa husuda: “Mpeleke kwenye tanuu ya kuchoma maiti, mchome na umalize!” Hata hivyo, wakiogopa kwamba ningeweza kufa na kwamba wangelaumiwa kwa ajili ya kifo changu, waliishia kupiga simu kwenye huduma za dharura na kuleta gari la wagonjwa na kunipeleka hospitalini kwenda kukaguliwa. Ilitukia kwamba, hapo awali nilikuwa nimepatwa na mshtuko wa moyo na nilikuwa na iskemia ya moyo ya masazo. Kwa kuwa mahojiano yalihitajika kubatilishwa, walinipeleka kizuizini. Nilipoona sura zilizovunjika moyo kwenye nyuso za polisi hao waovu, nilifurahi sana—Mungu alikuwa amenifungulia njia, ili kwamba, kwa wakati huo, sikuhitajika kupitia mahojiano mengine. Kuweza kunusurika hali hiyo mbaya kuliniwezesha nishuhudie matendo ya Mungu; nilimshukuru na kumsifu Mungu kwa dhati.

Kwa siku kumi zisizo za kawaida zilizofuata, nikijua kuwa serikali ya CCP haingekata tamaa kabla ya kupata eneo la pesa za kanisa kutoka kwangu, nilimwomba Mungu kila siku, nikimwomba Alinde kinywa changu na moyo wangu, ili bila kwamba kujali chochote, ningesimama kidete upande wa Mungu na singemsaliti kamwe na kuiacha njia ya kweli. Siku moja baada ya maombi, Mungu alinipa nuru, Akiniwezesha kukumbuka wimbo mmoja wa maneno Yake: “Haijalishi kile ambacho Mungu anataka kutoka kwako, unahitaji tu kujitolea kikamilifu. Natarajia utaweza kuonyesha uaminifu wako kwa Mungu mbele Yake mwishowe, na maadamu unaweza kuiona tabasamu ya Mungu ya kupendeza Akiwa katika kiti Chake cha enzi, hata kama ni wakati wako kufa, lazima uweze kucheka na kutabasamu macho yako yanapofumba. Lazima umfanyie Mungu wajibu wako wa mwisho wakati wa muda wako hapa duniani. Zamani, Petro alisulubiwa juu chini kwa ajili ya Mungu; hata hivyo, unapaswa kumridhisha Mungu mwishowe, na utumie nguvu zako zote kwa ajili ya Mungu(“Kiumbe Aliyeumbwa Anapaswa Kuwa Chini ya Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliimba na kutafakari wimbo huo tena na tena moyoni mwangu na, kupitia maneno ya Mungu, nilikuja kufahamu mahitaji ya Mungu na matarajio Yake kwangu. Nilifikiria jinsi, kati ya viumbe wote ulimwenguni wanaoishi chini ya utawala wa Mungu, na kati ya watu wote wanaomfuata Mungu, ni idadi ndogo sana tu ndiyo inayoweza kweli kusimama mbele ya Shetani na kuwa na ushahidi kwa Mungu. Kwamba nilikuwa na bahati ya kutosha ili kukabili hali ya aina hii alikuwa Mungu akiniinua kwa njia ya kipekee, na ilionyesha neema Yake kwangu. Maneno haya kutoka kwa Mungu hasa yalinitia moyo sana: “Zamani, Petro alisulubiwa juu chini kwa ajili ya Mungu; hata hivyo, unapaswa kumridhisha Mungu mwishowe, na utumie nguvu zako zote kwa ajili ya Mungu.” Sikuweza kusita kumwomba Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Hapo zamani, Petro aliweza kusulubiwa juu chini msalabani kwa ajili Yako, akiwa na ushuhuda kwa upendo wake Kwako mbele ya Shetani. Na sasa, kukamatwa kwangu na chama tawala nchini China kuna nia Zako nzuri. Ingawa kimo changu ni kidogo sana na siwezi kamwe kufananishwa na Petro, ni heshima yangu kubwa kuwa na fursa ya kuwa shahidi Kwako. Niko tayari kuyakabidhi maisha yangu Kwako na nitakufa bila kusita ili kuwa shahidi Kwako, ili Upate faraja kupitia kwangu.”

Asubuhi ya tarehe 30 Desemba, Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa iliwatuma maafisa wengine kuja kunihoji. Mara tu nilipoingia kwenye chumba cha kuhojiwa, askari mmoja mwovu alinilazimisha nivue suruali yangu na koti langu lililojazwa pamba, na kuniambia: “Sasa dada yako mdogo na mtoto wako wamefungwa. Tunajua kuwa familia yako yote ni waumini. Tulikwenda mahali pa kufanyia kazi pa mumeo na kugundua kuwa ulianza kumwamini Mwenyezi Mungu mnamo mwaka wa 2008….” Maneno yake yalitumia udhaifu wangu mkubwa zaidi na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye hali yangu ya akili; sikuwahi kufikiria kwamba wangewakamata pia mwanangu na dada yangu. Ghafla nilipozidiwa na hisia, nilianza kuwa na wasiwasi juu ya ustawi wao na moyo wangu ulianza kuondoka kutoka kwa Mungu bila kukusudia. Nilijiuliza tena na tena: “Je, wanapigwa? Mtoto wangu anaweza kuvumilia utendewaji kama huo? …” Wakati huo huo, nilikumbuka kifungu kimoja cha neno la Mungu: “Hii ni kwa sababu daima Nineamini kwamba kiasi ambacho mtu lazima ateseke na umbali ambao lazima autembee kwenye kinjia yake yameamuliwa na Mungu, na kwamba hakuna yeyote anayeweza kumsaidia mwingine kweli(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia … (6)). Maneno ya Mungu mara moja yalinigeuza kutoka katika hali yangu yenye mhemuko na yaliniwezesha kugundua kuwa njia ya imani ya kila mtu imeamuliwa kabla na Mungu. Kila mtu anapaswa kuwa shahidi kwa Mungu mbele ya Shetani—je, si jambo hilo litakuwa baraka kubwa kwao kuwa mashahidi kwa Mungu mbele ya Shetani? Baada ya kufikiria haya, niliacha kuwa na wasiwasi na sikuhangaika tena kwa ajili yao; nilihisi kwamba nilikuwa tayari kuwakabidhi kwa Mungu na kumwacha Mungu atawale na kufanya utaratibu Wake. Wakati huo huo, askari mwingine alisema majina ya dada wengine kadhaa na kuniuliza iwapo niliyatambua majina hayo. Niliposema kuwa sikutambua majina yoyote, aliruka kutoka kwenye kiti chake, akanivuta kwa hasira hadi kwenye stuli ya chuma iliyokuwa karibu na dirisha, alinitia pingu kwenye stuli hiyo, na akafungua dirisha haraka ili kwamba hewa baridi iliyotoka nje ikaanza kunipuliza. Kisha alianza kunirushia maji baridi huku akinitukana kwa maneno machafu kabla ya kunipiga kikumbo usoni kwa sapatu mara kadhaa mfululizo. Alinipiga vibaya sana kiasi kwamba nilianza kuona vimulimuli, masikio yangu yaliwangwa na damu ilidondoka kutoka mdomoni mwangu.

Usiku huo, baadhi ya polisi walinihamisha hadi kwenye chumba baridi zaidi; madirisha yalijawa kabisa na barafu. Walivua nguo zangu zote kwa nguvu na kunilazimisha niketi, nikiwa uchi kabisa, kwenye stuli ya chuma karibu na dirisha. Walitia mikono yangu pingu nyuma ya mgongo kwenye sehemu ya stuli ya kuegemea ili kwamba nisiweze kusonga hata kidogo. Mmoja wa askari waovu aliniambia kwa sauti ya kikatili, ya husuda: “Hatubadilishi mbinu zetu za uchunguzi kulingana na jinsia.” Alifungua dirisha alipokuwa akiyasema haya na upepo wa baridi ulinikumba; ilihisi kama mwili wangu ulikuwa ukikatwa nakshi na visu vingi. Nilipokuwa nikitetemeka kwa ajili ya baridi, nilisema kupitia meno yaliyotatarika: “Siwezi kuwekwa wazi kwa baridi ya aina hii, nina ugonjwa wa baridi yabisi wa baada ya kujifungua.” Alijibu kikatili, “Oh hili litashughulikia ugonjwa wako wa baridi yabisi vizuri! Utapata ugonjwa wa kisukari na ugonjwa wa figo pia wakati haya yanapofanyika! Bila kujali utaona madaktari wangapi, hutapona kamwe!” Kisha, alimwagiza mtu fulani alete ndoo iliyojaa maji baridi na akanishurutisha nitumbukize miguu yangu ndani. Kisha aliniamuru, “Usiruhusu hata tone moja la maji liruke kutoka kwenye ndoo hiyo.” Alinirushia maji mengine baridi mgongoni mwangu kisha akapepeza mgongo wangu kwenye kadibodi. Halijoto ilikuwa digrii –4 Farenhaiti: maji yale baridi sana yalinigandisha kiasi kwamba niliinua miguu yangu bila kufikiri kutoka kwenye ndoo, lakini afisa mmoja akailazimisha kurudi ndani mara moja na akanikataza kuisogeza tena. Nilihisi baridi sana kiasi kwamba mwili wangu wote ulikaza sana na sikuweza kuacha kutetemeka. Ilihisi kana kwamba damu ilikuwa imeganda ndani ya mishipa yangu. Walisisimka kuniona nikiwa katika hali hiyo, na waliangua kicheko cha kutisha sana huku wakinidhihaki kwa kusema: “Unashirikiana nasi vizuri!” Nilichukia genge hili la pepo na hayawani wakatili kwa kiasi kikubwa; nilikumbushwa ghafla juu ya video iliyoigiza pepo za jehanamu ambazo ziliwatesa watu kwa kujifurahisha, na kupata raha kutokana na kuteseka kwa wengine. Hawakuwa na hisia na ubinadamu, wakifahamu ukatili na mateso tu. Askari hawa waovu hawakuwa tofauti na pepo hao wa jehanamu—kwa kweli, walikuwa hata wabaya zaidi. Kwa kipindi cha siku moja na usiku mmoja, walikuwa wamenizaba makofi usoni mara nyingi mno, wakijaribu kunilazimisha kutoa wazi habari kuhusu pesa za kanisa. Uso wangu ulipovimba kutokana na kichapo chao, walipaka barafu ili kupunguza uvimbe na kisha wakaendelea na kichapo chao. Isingekuwa kwa ajili ya ulinzi wa Mungu, ningekuwa nimekufa muda mrefu kabla ya hapo. Maafisa hao waovu walipoona kuwa bado sikuwa tayari kuzungumza, walianza kunishtua kwenye mapaja na kinena changu kwa kirungu cha umeme. Kila waliponishtua, mwili wangu wote ungesukasuka na kukaza kwa ghafla kwa maumivu. Kwa sababu walikuwa wamenitia pingu kwenye stuli ya chuma, haingewezekana kukwepa, kwa hivyo ilinibidi tu nipokee kichapo, kukanyagwa, na fedheha yoyote mbaya waliyotoa. Maneno hayawezi kueleza maumivu makali ambayo nilikuwa nikiyapata, na bado, kupitia hayo yote, polisi hao walicheka tu kwa kishindi. Hata ya kutisha zaidi, askari mdogo alitumia vijiti viwili vya kulia kubana chuchu yangu na kisha kuipopotoa kwa nguvu awezavyo. Iliumia sana kiasi kwamba nilikuwa nikipiga mayowe kwa sauti kubwa sana. Pia waliweka chupa ya maji baridi kama barafu katikati ya miguu yangu dhidi ya kinena changu na kisha kulazimisha maji yaliyokuwa na poda ya wasabi ndani ya pua langu. Kijishimo changu chote cha pua kiliunguza na joto la kuunguzia lilionekana kunipata hadi kwenye ubongo wangu. Sikuthubutu kuvuta pumzi. Polisi mwingine mwovu alivuta mkupuo wa sigara kutoka kwa sigara yake na kupuliza moshi huo kwenye pua yangu, akisababisha niwe na mfuatano wa kukohoa. Kabla ya kupata nafasi ya kupumzika, mwingine aliangusha stuli ya mbao na kuweka miguu yangu juu yake ili nyayo za miguu yangu ziwachwe wazi. Kisha akachukua fimbo ya chuma na kupiga nyayo za miguu yangu yote mara nyingi. Iliumiza sana kiasi kwamba nilidhani miguu yangu itavunjika; nilipiga mayowe tena na tena kwa ajili ya maumivu. Muda mfupi baadaye, nyayo za miguu yangu zilikuwa zimevimba na kuwa nyekundu. Polisi hao waovu walinitesa bila kupunguza ukali. Moyo wangu ulikuwa ukipiga kwa nguvu sana na nilidhani kuwa nilikuwa nimechungulia kifo. Kisha walinipa aina ya dawa ya moyo ya kienyeji ya Kichina inayofanya kazi haraka, na mara tu nilipoanza kupata nafuu, walianza kunipiga tena na kunitishia, wakisema: “Usipozungumza, tutakugandisha na kukupiga hadi ufe! Kwa kweli, hakuna mtu atakayejua! Usiposema ukweli leo tunaweza kuendelea kutumia wakati pamoja kwa siku chache zaidi na tuone ni nani anayeweza kudumu kuliko mwingine. Tutamleta mumeo na mtoto wako ili waone jinsi unavyofanana sasa na ikiwa bado hutatuambia, tutahakikisha kwamba wote wawili wamefukuzwa kazini mwao!” Hata walinitania kwa kejeli, wakisema: “Humwamini Mungu? Je, kwa nini Mungu wako haji kukuokoa? Nadhani Mungu wako si mkuu hata hivyo!” Nilidharau genge hili la hayawani wenye uadui, waovu na wakatili kwa moyo wangu wote na roho yangu yote. Ilikuwa vigumu sana kuhimili mateso ya ukatili na hata vigumu zaidi kustahimili kashfa zao kwa Mungu. Kwa hivyo, nilimwomba Mungu nikiwa tayari kufanya lolote, nikimsihi Anilinde, Anijaze imani, nguvu na nia ya kuvumilia mateso, ili niweze kusimama kidete. Wakati huo huo, maneno ya Mungu yalitokea akilini mwangu: “Katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Nilijiwazia: “Hayo ni kweli! Mapenzi ya Mungu ni kwamba niwe shahidi Kwake mbele ya Shetani, kwa hivyo ninapaswa kuvumilia maumivu haya yote na dhihaka hii yote ili kumridhisha Mungu. Hata kama nina pumzi moja tu iliyobaki, sina budi kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu, kwani jambo hilo ndilo hufanyiza ushuhuda wenye nguvu na mkubwa sana, na hili ndilo litamtia aibu ibilisi mzee.” Nikiwa na mwongozo wa neno la Mungu, nilihisi hali mpya ya kujiamini na imani ndani ya moyo wangu. Nilikuwa tayari kushinda nguvu za giza; hata kama ilimaanisha kifo changu, ilinibidi nimridhishe Mungu wakati huo. Kisha nikakumbuka wimbo wa kanisa: “Nitampa Mungu upendo na uaminifu wangu na kukamilisha misheni yangu ya kumtukuza Mungu. Nimeazimia kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu, na kamwe kutoshindwa na Shetani. Eh, kichwa changu kinaweza kupasuka na damu kutiririka, lakini ujasiri wa watu wa Mungu hauwezi kupotea. Ushawishi wa Mungu umo moyoni, ninaamua kumwaibisha Shetani Ibilisi. Maumivu na shida vimeamuliwa kabla na Mungu, nitastahimili aibu ili kuwa mwaminifu Kwake. Kamwe sitamsababisha Mungu alie au kusumbuka tena” (“Ninatamani Kuona Siku ya Utukufu wa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). “Hiyo ni kweli!” Nilijiambia. “Sipaswi kuridhisha tamaa za mwili wangu. Alimradi fursa ipo kwangu ya kumfedhehesha Shetani na kuuletea moyo wa Mungu faraja, niko tayari kutoa maisha yangu kwa Mungu.” Mara tu nilipokuwa shupavu katika nia yangu, bila kujali jinsi pepo hao walivyonitesa au kujaribu kunidanganya na njama zao za hila, nilimtegemea Mungu moyoni mwangu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Maneno ya Mungu yalinipa nuru na kuniongoza kutoka moyoni, yakinipa imani na nguvu, na kuniwezesha kuushinda udhaifu wa mwili wangu. Polisi waovu waliendelea kunitesa kwa baridi: Walisugua vipande vya barafu kwenye mwili wangu wote, na kunisababisha niwe baridi sana na mwenye kutetemeka kiasi kwamba nilihisi kana kwamba nilikuwa nimefungiwa kwenye pango la barafu. Meno yangu yalitatarika kwa sauti kubwa na ngozi yangu iligeuka kuwa rangi ya bluu na zambarau. Takribani mwendo wa saa nane usiku, baada ya kuteswa hadi nikatamani kifo, sikuweza kujizuia kuanza kuwa dhaifu kwa mara nyingine tena. Kwa ajili sikujua ni muda gani ningehitaji kuvumilia mateso hayo, niliweza tu kumwomba Mungu tena na tena moyoni mwangu: “Mungu Mpendwa, mwili wangu ni dhaifu sana na siwezi kuvumilia kwa muda mrefu zaidi. Tafadhali niokoe!” Shukrani ziwe kwa Mungu kwa kujibu maombi yangu; nilipokuwa tu siwezi kuvumilia tena, polisi waovu waliamua kubatilisha mahojiano yao kwa sababu hayakuwa yakitoa matokeo yoyote.

Wakati fulani baada ya saa nane alasiri mnamo tarehe 31 Desemba, polisi wabaya walinirudisha kwenye seli yangu. Niliviliwa na kupigwa kutoka utosini hadi vidoleni. Mikono yangu ilikuwa imevimba kama baluni; yote ilikuwa ya rangi ya samawati na ya zambarau. Uso wangu ulikuwa umevimba kwa theluthi moja kubwa kuliko saizi yake ya kawaida, ulikuwa wa rangi ya kijani ya kibuluubuluu, mgumu kugusa, na ulikuwa umekufa ganzi kabisa. Sehemu nyingi kwenye mwili wangu zilikuwa na majeraha ya moto kutokana na kushtuliwa kwa umeme. Kulikuwa na zaidi ya wafungwa ishirini kwenye seli wakati huo, na walipoona jinsi nilivyokuwa nimeteswa na pepo hao, wote walilia. Baadhi yao hata hawakuthubutu kuniangalia, na mwanachama mdogo wa Chama cha Kikomunisti alisema: “Nitakapotoka hapa nitaondoa uanachama wangu.” Mwakilishi wa kisheria aliniuliza, “Je, watu waliokupiga wanafanya kazi katika kituo kipi? Majina yao ni yapi? Niambie, nitachapisha kila kitu kwenye tovuti za nje na kuwaweka wazi. Wanasema kwamba China ni mahali penye huruma, lakini huruma iko wapi katika jambo hili? Huu ni ukatili mtupu!” Taabu yangu ilichochea hasira ya wafungwa wengi, na ghafla wakasema kwa hasira: “Sikuwahi kufikiria Chama cha Kikomunisti kinaweza kuwa katili kiasi hiki—siamini kuwa wamefanya vitendo danganyifu hivi. Kumwamini Mungu ni jambo zuri, kunawazuia watu kufanya makosa. Je, si wanasema kwamba China ina uhuru wa dini? Hakika huu sio uhuru wa dini! Nchini China, ikiwa una pesa na uwezo, basi una kila kitu. Wahalifu wa kweli bado wako huru na hakuna mtu anayethubutu kuwakamata. Wafungwa waliohukumiwa kifo huachiliwa huru mara tu watakapowalipa wafanyikazi wa serikali. Hakuna haki au usawa wowote katika nchi hii! …” Wakati huo, sikuweza kujizuia kukumbuka maneno haya kutoka katika maneno ya Mungu: “Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)). “Je, mnalichukia kwa kweli lile joka kuu jekundu? Mnalichukia kwa kweli? Mbona Nimewauliza mara nyingi? Mbona Nimewauliza swali hili, mara tena na tena? Kuna picha gani ya joka kuu jekundu katika mioyo yenu? Picha hiyo kwa kweli imeondolewa? Hamchukulii kwa kweli kama baba yenu? Watu wote wanafaa kuona nia Yangu katika maswali Yangu. Sio kuwafanya watu wawe na hasira, au kuchochea uasi kati ya mwanadamu, au ili mwanadamu agundue njia yake mwenyewe, bali ni kuwawezesha watu wote wajifungue kutoka kwa minyororo ya lile joka kuu jekundu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 28). Maneno ya Mungu yalikuwa faraja kubwa sana kwangu. Sikuwahi kufikiria kwamba asili ya ukatili, mbovu, na ya Shetani ya serikali ya CCP inaweza kuwekwa wazi kupitia mateso ya kikatili niliyoyapitia, kwamba hii inaweza kuwaruhusu wasioamini kuona serikali ya CCP kwa jinsi ilivyo kwa kweli, na kusimama pamoja ili kumchukia na kumwacha yule ibilisi mzee. Kwa kweli hii ilikuwa kazi ya hekima na uweza wa Mungu. Hapo zamani, nilikuwa ninaona CCP kama jua kubwa nyekundu, kama mwokozi wa watu, lakini baada ya kuathiriwa na adhabu na mateso ya kinyama ya serikali ya CCP, mtazamo wangu juu yake umebadilika kabisa. Kwa kweli niliona kutojali kwake kabisa kuhusu maisha ya mwanadamu, jinsi inavyowadhulumu kikatili wateule wa Mungu, jinsi inavyopinga Mbingu, na jinsi ni roho muovu anayefanya makosa makubwa—ni kupata mwili kwa ibilisi na pepo anayempinga Mungu. Mungu ni Bwana wa uumbaji, na wanadamu ni viumbe walioumbwa. Ni kawaida na haki kuamini katika Mungu, lakini serikali ya CCP inatunga mashtaka ya uwongo ili kuwakamata na kuwatesa bila sababu harabu wafuasi wa Mungu, wakitamani sana kumwangamiza kila mfuasi wa Mungu aliyebaki. Kwa kufanya hivyo, wameweka wazi kabisa asili yao ya kikatili ya njia zao za kumchukia Mungu na za kumchokoza Mungu. Serikali ya CCP ikitumika kama foili, asili ya wema na upendo wa Mungu ilionekana wazi zaidi kwangu. Mungu alipata mwili mara mbili na, katika visa vyote viwili, Amevumilia kupitia mateso na matatizo makubwa na pia kukimbizwa na ibilisi. Lakini, kupitia hayo yote, Mungu alivumilia akiwa kimya mashambulio na mateso yote, akifanya kazi Yake ili kuwaokoa wanadamu. Upendo wa Mungu kwa wanadamu kweli ni mkubwa! Wakati huo, nilikidharau kikundi hicho cha pepo kwa moyo wangu wote na roho yangu yote na nilijuta kweli kwamba hapo zamani sikukuwa nimefuatilia ukweli kwa bidii au kutimiza wajibu wangu wa kulipa upendo wa Mungu. Nilijiwazia kwamba ikiwa, siku moja, nitanusurika kutoka mahali hapo nikiwa hai, nitajitolea hata zaidi kutimiza wajibu wangu na kumwacha Mungu apate moyo wangu.

Baadaye, polisi waovu walinihoji mara nne zaidi. Hawakuweza kupata habari yoyote kutoka kwangu, kwa hivyo walitunga tu shtaka la “kuvuruga amani ya umma” na kuniachilia kwa dhamana ya mwaka mmoja, iliyowekwa yuani 5,000, nikisubiri kesi. Mwishowe niliachiliwa mnamo tarehe 22 ya Januari, mwaka wa 2013, baada ya familia yangu kuniwekea dhamana. Baada ya kurudi nyumbani, kila nilipoona barafu kwenye madirisha moyo wangu ungeanza kupiga kwa kasi. Uwezo wangu wa kuona ulipungua kwa kiasi kikubwa, ugonjwa wangu wa baridi yabisi ulizidi kuwa mbaya zaidi, na nilianza kuwa na tatizo la figo. Nilihisi baridi kila wakati, nilishikwa na hofu mara kwa mara, nilikufa ganzi mikono yote miwili, uso wangu ulikuwa umeambua safu ya ngozi, na mara nyingi nilikuwa na maumivu yasiyovumilika kwenye upande wa ndani wa mapaja yangu hadi kiwango ambacho yangeweza kuniamsha kutoka usingizini. Haya yote yalikuwa ushahidi wa mateso ya pepo hao.

Upendo wa Mungu Umeuimarisha Moyo Wangu

Baada ya kupitia mateso dhalimu ya kinyama ya serikali ya CCP, ingawa nilikuwa nimepitia kila aina ya mateso ya mwili, nilimkaribia Mungu zaidi katika uhusiano wangu na Mungu, nikapata uelewa zaidi wa vitendo wa hekima, uweza, upendo na wokovu wa Mungu, na kuimarisha azimio langu la kumfuata Mwenyezi Mungu. Niliamua kumfuata Mungu katika maisha yangu yote na kutafuta kuwa mtu anayempenda Mungu. Kupitia mateso ya kikatili ya serikali ya CCP, nilijionea mwenyewe upendo, utunzaji na ulinzi wa Mungu. Kama neno la Mungu halingeniongoza kila hatua njiani, likinipa nguvu na imani, singeweza kamwe kuvumilia maumivu yote makali na mateso yote ya kikatili ambayo nilipata. Kupitia uzoefu wangu wa hali hii ya kipekee, nilikuja kuona kikamilifu kwamba serikali ya CCP ni ibilisi Shetani tu anayempinga Mungu, na kumchokoza Mungu. Katika juhudi yake ya kuigeuza China kuwa nchi inayomkana Mungu na kutwaa madaraka ya ulimwengu, inafanya lolote iwezalo na inafanya lolote chini ya uwezo wake kumfukuza Mungu katika ulimwengu huu. Inawakimbiza, inawakamata na kuwatesa kwa wayowayo wale wanaomfuata Mungu kwa lengo la kuwaondoa wafuasi wote wa Mungu, ikiwaondoa wote katika mtego wake na, kwa kufanya hivyo, kukomesha kazi ya Mungu kabisa. Serikali ya CCP kweli ni mbovu sana! Ni mnyama tu wa Shetani ambaye anawameza watu kikamilifu—ni nguvu ya giza ya Shetani, potovu, inayokataa mbinguni, inayozuia haki na inayowezesha uovu. Nchini China, serikali ya CCP inawaruhusu wahalifu ambao wanakandamiza na kuwadhulumu watu wema wa kawaida kuwa huru, hata kuwapa mgao katika nguvu za kisheria na za kisiasa. Wanasuhubiana na kutangatanga na majambazi na wakora wakishiriki katika ukahaba, kamari na biashara za dawa za kulevya; wao hata husaidia kulinda masilahi yao. Ni wafuasi wa Mungu tu ambao hutembea kwa njia sahihi maishani ndio serikali ya CCP inawachukulia kama adui wake, inawakandamiza na kuwakamata kwa utukutu, na kuwatesa kikatili hadi kiwango ambacho familia za waumini wengi zimevunjwa, wapendwa wanatawanyika na kupotea, na hawawezi kurudi nyumbani. Wengi wao hawawezi kutulia, lakini hawana budi kuishi maisha ya uzururaji mbali na nyumbani. Bado wengine wanateswa kikatili na hata wanapigwa hadi kiwango cha kupooza au kufa kwa sababu ya kumwamini Mungu. … Ni dhahiri kabisa kuwa serikali ya CCP ni ibilisi Shetani, mkatili wa kinyama, muuaji wa mwanadamu. Mwishowe, hataepuka adhabu ya haki ya Mungu kwa ajili ya dhambi kubwa ambazo amefanya. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alisema zamani sana: “Kiota cha pepo hakika kitachanwachanwa na Mungu, na mtasimama kando ya Mungu—nyinyi ni wa Mungu, na sio wa milki hii ya watumwa. Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga mwovu huyu, joka wa zamani mwenye chuki, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote. Mungu hatamsamehe hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote,[1] Atamwangamiza kabisa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)). Haki ya Mungu inastahili sifa na shukrani na ataondoa na kuangamiza ufalme wa Shetani. Ufalme wa Mungu utaanzishwa hapa duniani na utukufu wa Mungu utaenea kote ulimwenguni!

Tanbihi:

1. “Kiongozi wa uovu wote” inahusu ibilisi mkongwe. Kirai hiki kinaonyesha kutopenda kabisa.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Upendo wa Mungu Hauna Mipaka

Na Zhou Qing, Mkoa wa ShandongNimepitia taabu ya maisha haya kikamilifu. Sikuwa nimeolewa kwa miaka mingi kabla ya mume wangu kufariki, na...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp