Ukingoni mwa Kifo, Mwenyezi Mungu Alikuja Kunisaidia

26/01/2021

Na Wang Cheng, Mkoa wa Hebei

Wakati wangu kama muumini wa Bwana Yesu Kristo, niliteswa na serikali ya CCP. Serikali ilitumia “uhalifu” wa imani yangu katika Bwana Yesu kama sababu ya kunipa wakati mgumu na kunitesa. Waliamuru hata maafisa wa jeshi wa kijijini wazuru nyumbani kwangu mara kwa mara ili kudadisi desturi zangu za imani. Mnamo mwaka wa 1998, nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Niliposikia maneno ya Muumba yakinenwa na Yeye binafsi, nilifurahi na kuguswa kwa njia ambayo siwezi hata kueleza. Kwa sababu ya kutiwa moyo na upendo wa Mungu, niliamua: Nitamfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho kabisa, bila kujali lolote. Wakati huo, nilihudhuria mikutano kwa bidii na kueneza injili, jambo ambalo kwa mara nyingine lilivuta macho ya serikali ya CCP. Wakati huu, mateso yao kwangu yalikuwa mabaya zaidi kuliko hapo awali. Yalizidi kuwa mabaya kiasi kwamba sikuweza kutekeleza imani yangu kwa kawaida katika nyumba yangu mwenyewe na nililazimika kuondoka nyumbani kwangu ili kutekeleza wajibu wangu.

Mnamo mwaka wa 2006, nilikuwa na jukumu la kazi ya kuchapisha vitabu vya maneno ya Mungu. Wakati mmoja wakati wa kusafirisha vitabu, ndugu wachache na dereva wa kampuni ya uchapishaji kwa bahati mbaya walikamatwa na polisi wa CCP. Nakala zote elfu kumi za Neno Laonekana katika Mwili ambazo zilikuwa ndani ya lori zilichukuliwa ngawira. Baadaye, dereva aliwasaliti zaidi ya ndugu wengine kumi na wote walikamatwa mfululizo. Tukio hili lilisababisha vurumai kuu katika mikoa miwili na kesi hiyo ilisimamiwa moja kwa moja na serikali kuu. Serikali ya CCP ilipogundua kuwa nilikuwa kiongozi, walitumia mali yote, wakisambaza jeshi la polisi wenye silaha kuchunguza maeneo yote ya kufanyia kazi yaliyohusiana na kazi yangu. Walichukua ngawira magari mawili na gari moja la mizigo kutoka kwa kampuni ya kuchapisha ambayo tulifanya nayo kazi na pia kufuja RMB 65,500 kutoka kwa kampuni hiyo kando na RMB zaidi ya 3,000 walizoiba kutoka kwa ndugu ambao walikuwa ndani ya lori siku hiyo. Aidha, polisi hao pia walikuja kuchunguza nyumba yangu mara mbili. Kila wakati walipokuja, walibomoa mlango wa mbele, wakaponda na kuvunja mali yangu na kufudikiza nyumba yangu yote. Walikuwa wabaya zaidi kuliko kundi la majahili wanaozurura! Baadaye, kwa sababu serikali ya CCP haikuweza kunipata, walikusanya majirani, marafiki na jamaa zangu na kuwahoji kuhusu mahali nilipokuwa.

Nililazimika kutoroka kwenda nyumbani kwa jamaa aliyekuwa mbali sana ili kuepuka kukamatwa na kuteswa na serikali ya CCP. Sikufikiri kabisa kuwa polisi wa CCP wangeendelea kunifuatilia mbali sana ili kunikamata. Hata hivyo, usiku wa siku ya tatu baada ya kufika nyumbani kwa jamaa yangu, kikosi maalum cha takribani maafisa 100 kilijumuisha kitengo cha polisi kutoka mji wa nyumbani wakishirikiana na polisi wa jinai wa eneo hilo na polisi wenye silaha waliizingira kabisa nyumba ya jamaa yangu na kisha kunitia mbaroni na kuwakamata jamaa zangu wote. Nilizingirwa na maafisa zaidi ya kumi wa polisi wenye silaha, wote wakiwa na bunduki iliyolenga kichwa changu, wakipiga kelele kwa hasira, “Ukisonga tu utakufa!” Halafu, maafisa wachache wa polisi walinirukia na wote wakaanza kujaribu kutia pingu mikono yangu nyuma ya mgongo wangu. Walivuta mkono wangu wa kulia hadi juu ya bega langu kisha wakaelekeza mkono wangu wa kushoto nyuma ya mgongo wangu na kuuvuta mkono wangu kwa nguvu kuelekea juu. Waliposhindwa kutia mikono yangu pingu, walinikanyaga mgongoni na kuvuta kwa nguvu zaidi hadi mikono yangu ikakutana kwa nguvu. Uchungu huo mkali zaidi ulizidi kiasi ambacho ningevumilia, lakini bila kujali jinsi nilivyosema kwa sauti, “Siwezi kuvumilia uchungu,” maafisa hawakuonyesha wasiwasi, na kile nilichoweza kufanya ni kumwomba Mungu anipe nguvu. Walitwaa RMB 650 kutoka kwangu na kisha wakanihoji kwa ukali kuhusu mahali ambapo kanisa lilihifahdi pesa zake, wakidai niwape pesa zote. Nilighadhabika kabisa na nikajiwazia kwa dharau, “Wanajiita ‘Polisi wa Umma’ na ‘walinzi wa maisha na mali za watu,’ lakini sababu ya wao kutuma kikosi kikubwa kama hiki maalum cha askari kwenye uwindaji wa watu wa masafa marefu ili kunikamata sio tu ili kuzuia kazi ya Mungu, bali pia kupora na kuiba fedha za kanisa! Polisi hawa waovu wana tamaa ya pesa isiyoridhika kamwe. Wao hupiga bongo sana na hufanya kila linalowezekana kujaza makasha yao. Ni nani anayejua wamefanya vitendo vingapi visivyokuwa na busara wakifuatilia mali au wameharibu maisha ya watu wangapi wasiokuwa na hatia ili kujitajirisha wenyewe?” Kadiri nilivyozidi kufikiria juu ya hayo, ndivyo nilivyozidi kuwa na hasira, na nilijiapia kwamba ni afadhali nife mapema kuliko kumsaliti Mungu. Nilijiapia kwamba nitapambana na pepo hawa hadi mwisho kabisa. Mmoja wa maafisa alipoona jinsi nilivyokuwa nikiwaangalia kwa hasira na ukimya, alikuja na kunipiga kofi mara mbili usoni, jambo lililosababisha midomo yangu kuvimba na kutoa damu nyingi. Hata hivyo, kwa kutoridhika na hilo, polisi wale wabaya walifuatilia kwa kunipiga kwa ukatili kwenye miguu na kunitukana hadi nikaanguka chini. Waliendelea kunipiga mateke kama mpira wa kandanda nilipokuwa nikilala ardhini hadi, baada ya kipindi fulani cha wakati, mwishowe nikazimia. Nilipoamka, tayari nilikuwa ndani ya gari nikielekea nyumbani kwangu. Walikuwa wamenifunga kwa mnyororo mkubwa wa chuma ambao uliunganisha shingo yangu na vifundo vyangu hivyo sikuweza kuketi wima, lakini nililazimika kuangalia chini, nikiwa nimekunjamana kama kijusi, nikiegemezwa kwa shida na kifua na kichwa changu. Maafisa walipoona kuwa nilikuwa na uchungu uliokuwa dhahiri, waliangua kicheko cha sauti kubwa na kusema kwa kinaya, “Acha tuone ikiwa Mungu wako anaweza kukuokoa sasa!” Pamoja na maneno mengine ya kufedhehesha. Nilielewa waziwazi kuwa sababu ya wao kunitendea kwa njia hii ni kwa kuwa nilikuwa muumini wa Mwenyezi Mungu. Ni kama tu Mungu alivyokuwa amesema katika Enzi ya Neema: “Ikiwa dunia ikiwachukia, ninyi mnajua ya kwamba ilinichukia mimi kabla iwachukie ninyi(Yohana 15:18). Kadiri walivyozidi kunidhalilisha, ndivyo nilivyozidi kuona kiini chao cha shetani kama maadui wa Mungu na asili yao mbaya ya kumchukia Mungu, jambo ambalo lilinifanya niwadharau hata zaidi. Wakati huo huo, nilimwita Mungu kila wakati, nikisali, “Mwenyezi Mungu mpendwa! Kwa kweli ni kwa nia Yako nzuri kwamba umeniruhusu nikamatwe na polisi, na niko tayari kukutii. Leo, ingawa mwili wangu wa nyama una maumivu, niko tayari kushuhudia Kwako ili kumwaibisha ibilisi wa zamani. Sitamtii kwa hali yoyote. Ninaomba kwamba Unipe imani na hekima.” Baada ya kumaliza ombi langu, nilifikiria kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Uwe na utulivu ndani yangu, kwa maana Mimi ni Mungu wako, Mkombozi wenu wa pekee. Mnatakiwa kutuliza mioyo yenu nyakati zote, mkae ndani yangu; Mimi ni mwamba wako, msaidizi wenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 26). Maneno ya Mungu yalinipa nguvu na azimio kuu hata zaidi. Mungu hutawala kwa ukuu juu ya vitu vyote na maisha ya mwanadamu na kifo kiko mikononi Mwake. Nikiwa na Mwenyezi Mungu kama tegemeo langu thabiti, sikuwa na chochote cha kuogopa! Baada ya hili, nilikuwa nimefanya upya imani yangu na njia ya kutenda, na nilikuwa tayari kukabili mateso ya kikatili ambayo yalinisubiri.

Wakati wa kusindikizwa kwa muda wa saa 18 kurudi nyumbani kwangu, nilishindwa kuhesabu ni mara ngapi nilipoteza fahamu kwa sababu ya maumivu, lakini hakuna hata mmoja wa wale polisi ambaye aliyeonyesha kujali hata kidogo. Tulipofika mwishowe, ilikuwa imepita saa nane usiku. Nilihisi kana kwamba damu yote mwilini mwangu ilikuwa imeganda—mikono na miguu yangu yote ilikuwa imevimba na kufa ganzi na sikuweza kusonga. Nilimsikia mmoja wa polisi akisema, “Nadhani amekufa.” Mmoja wao alichukua mnyororo wa chuma na kuuvuta chini kwa nguvu, na hivyo kusababisha makali ya menomeno kuung’ata mwili wangu. Nilianguka ghafla na kwa vurumai nje ya gari na kuzirai kwa mara nyingine tena kutokana na maumivu. Polisi walinipiga teke mpaka nilipoamka na kisha wakasema kwa sauti kuu, “Ala! Unajaribu kujifanya kuwa umekufa, eh? Mara tutakapopumzika, utakipata!” Kisha wakanikokota kwa nguvu sana hadi kwenye seli ya waliohukumiwa kifo na, walipokuwa wakiondoka, walisema, “Tuliandaa seli hii hasa kwa ajili yako.” Wafungwa kadhaa walisumbuliwa kutoka usingizini mwao nilipokuwa nikivutwa ndani na niliogopa sana jinsi walivyonikodolea macho kiasi kwamba nikajikunyata kwenye kona, nikiogopa kusonga. Nilihisi kana kwamba nilikuwa nimeingia katika jahannamu ya aina fulani duniani. Wakati wa mapambazuko, wafungwa wengine wote walinizingira, wakinitazama kana kwamba nilikuwa mgeni. Wote walinivamia, wakiniogopesha sana kiasi kwamba nikachutama papohapo. Rabsha hiyo ilimuamsha mkuu wa wafungwa—alinitazama mara moja na kusema bila huruma, “Mfanyieni mtakavyo, ila msimpige hadi afe.” Wafungwa wale walimjibu mkuu wa wafungwa kama kwamba alikuwa ametoa amri. Walikwenda mbele, tayari kunipiga. Nilijiwazia, “Sasa utakipata. Polisi walinikabidhi kwa wafungwa hawa waliohukumiwa kifo wawafanyie kazi yao chafu—wananielekeza kwa kifo changu kwa kudhamiria.” Nilihisi mwoga kabisa na asiyejiweza, na nilichoweza kufanya ni kumwaminia Mungu maisha yangu na kukubali mipangilio Yake. Nilipokuwa tu nikijikaza kwa ajili ya kupigwa, kitu cha kushangaza kilitokea: Nilimsikia mtu akipiga kelele kwa haraka, “Acheni!” Mkuu wa wafungwa alinijia akikimbia, akaniburuta na akanitazama kwa kile kilichoonekana kama dakika kadhaa. Niliogopa sana kiasi kwamba hata sikuthubutu kumtazama. “Mtu mzuri kama wewe anajikutaje mahali kama hapa?” aliuliza. Nilipomsikia akiongea nami, nilimwangalia kwa ukaribu na nikagundua kuwa alikuwa rafiki wa rafiki ambaye nilikutana naye wakati mmoja hapo zamani. Kisha aliwahutubia wale wafungwa wengine, akisema, “Huyu mtu ni rafiki yangu. Mtu yeyote akimgusa, lazima utanijibu!” Baadaye, alienda haraka kuninunulia chakula na kunisaidia kupata vitu vya matumizi ya usafi na vitu vya kawaida ambavyo ningehitaji gerezani. Baada ya hapo, hakuna hata mmoja wa wafungwa wengine aliyethubutu kunionea. Nilijua kuwa kila kitu kilichokuwa kimetokea ni matokeo ya upendo wa Mungu na kwamba ulikuwa mpango wa Mungu wa busara. Mwanzoni, polisi walikuwa wametaka kutumia wafungwa wengine kunitesa bila huruma, lakini hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu angemgusa mkuu wa wafungwa ili anisaidie kukwepa tatizo hili. Niliguswa mpaka nikalia na sikuweza kujizuia kulia kwa kumsifu Mungu moyoni mwangu, nikisema, “Mungu mpendwa! Shukrani Kwako kwa kunionyesha huruma Zako! Ni Wewe uliyenisaidia kupitia rafiki huyu wakati ambapo nilikuwa na woga mkubwa zaidi, nisiye na msaada na dhaifu, Ukaniwezesha kushuhudia matendo Yako. Ni Wewe ambaye huhamasisha vitu vyote vikuhudumie ili wale wanaokuamini waweze kufaidi.” Wakati huo, imani yangu katika Mungu ilikua thabiti hata zaidi, kwa sababu mimi binafsi nilikuwa nimepitia upendo Wake. Ingawa nilikuwa nimetupwa katika tumbo la mnyama, Mungu hakuniacha. Nikiwa na Mungu kando yangu, kulikuwa na nini cha kuogopa? Rafiki yangu alinifariji, akisema, “Usiwe na huzuni. Bila kujali ulichofanya, usiwaambie neno, hata jambo hilo likikusonga sana. Lakini lazima ujiandae kiakili, na ujue kwamba, kwa kuwa wamekuweka hapa na kundi la wafungwa waliohukumiwa kifo, hawatakuachilia kwa urahisi.” Kutoka kwa maneno ya rafiki yangu nilihisi hata zaidi kuwa Mungu alikuwa akinielekeza kila wakati na kwamba alikuwa ameongea kupitia mwenzangu katika seli kunionya kuhusu yale yatakayokuja. Nilijitayarisha kikamilifu kiakili na nikajiapia kimyakimya: Bila kujali jinsi wale pepo watakavyonitesa, sitamsaliti Mungu asilani!

Siku ya pili, polisi zaidi ya kumi wenye silaha walifika na kufuatana nami kutoka kizuizini kana kwamba nilikuwa mfungwa aliyehukumiwa kifo hadi kwenye eneo la mbali huko mashambani. Mahali waliponipeleka palikuwa eneo lenye ukuta mrefu na uwanja mkubwa ambao ulilindwa sana na polisi wenye silaha. Bango lililokuwa kwenye mlango mkuu lilisema, “Kituo cha Mafunzo ya Mbwa wa Polisi.” Kila chumba kilijazwa vifaa vya aina tofauti vya kutesea watu. Ni kana kwamba walikuwa wamenileta kwa mojawapo ya maeneo ya serikali ya CCP ya mahojiano na mateso. Nilipokuwa nikitazama kando yangu, niliogopa sana na nilitetemeka kwa hofu. Wale polisi wabaya walinifanya nisimame kimya katikati ya uwanja na kisha wakaachilia mbwa wanne wakubwa sana na walioonekana kuwa wakali kutoka kwenye kizimba cha chuma, wakanielekezea na kuamuru mbwa hao wa polisi waliofunzwa vizuri, wakisema, “Nendeni mkaue!” Mara moja, mbwa walinishambulia kwa nguvu kama kundi la mbwa mwitu. Niliogopa sana kiasi kwamba niliyafumba macho yangu kwa kuyabana. Masikio yangu yalianza kuwangwa na sikuwa na mawazo yoyote—wazo la pekee lililokuwa kichwani mwangu lilikuwa, “Ee Mungu! Tafadhali niokoe!” Nilimwomba Mungu msaada bila kusita, na baada ya karibu dakika kumi, niliwahisi mbwa wakiuma nguo zangu. Mbwa mmoja mkubwa sana alisimama mabegani mwangu, akaninusanusa na kisha akauramba uso wangu, lakini kamwe hakuniuma. Nilikumbuka ghafla hadithi ya Biblia ambapo nabii Danieli alitupwa ndani ya shimo la simba wenye njaa kwa sababu alimwabudu Mungu, lakini simba hawakumdhuru. Kwa sababu Mungu alikuwa naye, Mungu alimtuma malaika kuyafunga mataya ya simba. Ghafla, hisia kuu ya imani ilijaa ndani yangu na ikaondoa woga wote moyoni mwangu. Nilikuwa na hakika kabisa ya kwamba yote hupangwa na Mungu na maisha ya mwanadamu na kifo viko mikononi mwa Mungu. Mbali na hilo, ikiwa ningeumwa na mbwa wakali hadi kufa kwa ajili ya imani yangu katika Mungu na kuwa mfiadini, hii ingekuwa heshima kubwa na bila shaka singekuwa na malalamiko. Wakati ambapo sikuzuiwa tena na hofu ya kifo na nilikuwa tayari kutoa maisha yangu ili kushuhudia kwa Mungu, nilishuhudia tena nguvu za Mungu na matendo ya muujiza. Wakati huu polisi waliwakimbilia mbwa kwa jazba, wakipiga kelele, “Ua! Ua!” Hata hivyo, ghafla ilikuwa kana kwamba mbwa hawa waliofunzwa kwa kiwango cha juu hawakuweza kuelewa amri za mabwana zao. Yote waliyofanya ni kurarua nguo zangu kidogo tu, kuuramba uso wangu kisha kutoweka. Baadhi ya polisi waovu walijaribu kuwazuia mbwa na kuwatuma wanishambulie tena, lakini mbwa hao ghafla waliogopa na kutawanyika katika pande zote. Polisi walipoona yaliyotokea, wote walishangaa na kusema, “Ajabu sana, hakuna mbwa yeyote ambaye amemuuma!” Nilikumbushwa ghafla kuhusu maneno ya Mungu kama yafuatavyo: “Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yake yote yanatazamwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu). “Mungu aliumba kila kitu, na hivyo yeye hufanya viumbe wote kuwa chini ya utawala wake, na kujiwasilisha kwenye utawala wake; Yeye ataamuru kila kitu, ili kila kitu kiwe mikononi mwake. Vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, pamoja na wanyama, mimea, mwanadamu, milima na mito, na maziwa—vyote ni lazima vije chini ya utawala Wake. Vitu vyote mbinguni na ardhini lazima zije chini ya utawala Wake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea). Kutoka kwa uzoefu wangu mwenyewe, nilikuwa nimeona katika maisha halisi jinsi vitu vyote–bila kujali ikiwa vina uhai hai au vimekufa—vyote vipo chini ya mipangilio ya Mungu na vyote husonga na kubadilika kwa sababu ya mawazo ya Mungu. Niliweza kuponea bila kuumia baada ya kushambuliwa na mbwa wakubwa wa polisi kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa amefunga midomo yao na akafanya wasithubutu kuniuma. Nilitambua kabisa kuwa hili lilikuwa limetokea kupitia nguvu kubwa ya Mungu na kwamba Mungu alikuwa amefunua moja ya matendo Yake ya muujiza. Iwe ni wale polisi majambazi, au mbwa wa polisi waliofunzwa, wote walilazimika kutii mamlaka ya Mungu. Hakuna anayeweza kuchukua nafasi ya mamlaka ya Mungu. Kwamba nilikuwa nimeanguka mikononi mwa serikali mbovu ya CCP na nilikuwa nimepata jaribio sawa na lile la nabii Daniel bila shaka ilikuwa sababu kwa Mungu alikuwa ameamua kuninua na kunipa neema Yake. Kupitia kushuhudia matendo makuu ya Mwenyezi Mungu, nilikuja kuwa na imani kuu hata zaidi Kwake na nikaapa kupigana na ibilisi hadi mwisho kabisa. Niliapa kumwamini na kumwabudu Mungu milele na kumletea utukufu na heshima!

Polisi waliposhindwa kufikia lengo lao kwa kutumia mbwa wa shambulio, walinileta kwenye chumba cha mahojiano. Walinining’iniza ukutani kwa pingu zangu na papo hapo nikahisi maumivu makali kwenye vifundo vya mikono yangu, kana kwamba mikono yangu ilikuwa karibu kukatwa kabisa. Matone makubwa ya jasho yalianza kudondoka kutoka usoni pangu. Hata hivyo, wale polisi majambazi hawakuwa wamemaliza bado, na walianza kunipiga mateke ya kikatili na kunipiga ngumi. Waliponipiga, walifoka kwa hasira, “Acha tuone ikiwa Mungu wako anaweza kukuokoa sasa!” Walibadilishana kunipiga—mmoja wao alipochoka, mwingine alianza moja kwa moja. Walinipiga hadi nikafunikwa na majeraha makubwa na michubuko kutoka kichwani hadi kwenye vidole na nilikuwa nikitokwa na damu sana. Usiku huo, bado hawakuwa wamenishusha chini kutoka ukutani na hawakuniruhusu niyafumbe macho yangu. Walikuwa wamewateua wasaidizi wawili waliokuwa na bunduki ya umeme ya kushtua. Kila nilipofumba macho yangu, walinishtua kwa umeme ili kunizuia kulala. Walinitesa usiku kucha kwa njia hii. Wakati ambapo mmoja wa wasaidizi alikuwa akinipiga, alinikodolea macho ya mviringo na madogo na kusema kwa sauti kubwa, “Watakapokupiga mpaka uzirai, nitakupiga mpaka uamke tena!” Kwa sababu ya nuru ya Mungu, nilijua kabisa kuhusu kile kilichoendelea: Shetani alikuwa akijaribu kutumia aina zote za mbinu za mateso ili kunifanya nijiaibishe. Lengo lilikuwa kunitesa hadi moyo wangu uvunjike na nipoteze uwezo wa kudhibiti akili yangu, wakati huo naweza kutoa habari ambayo walikuwa wakitafuta. Kisha wangewakamata watu wa Mungu walioteuliwa, wangevuruga kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na kupora na kutwaa mali ya Kanisa la Mwenyezi Mungu ili kutajirisha makasha yao wenyewe—hizi zilikuwa tamaa za kupita kiasi za asili yao ya kinyama. Nilikereza meno yangu na kustahimili maumivu. Nilijiapia kwamba singeridhiana nao hata kama ilimaanisha kuuawa kwa kutiwa kitanzi. Asubuhi iliyofuata, alfajiri, bado hawakuonyesha dalili yoyote kwamba wangenishusha chini na tayari nilikuwa nimechoka kabisa; nilihisi kana kwamba ni bora zaidi iwapo ningekufa, na sikuwa tena na utashi wa kuendelea. Kitu ambacho ningeweza kufanya ni kumwita Mungu kwa ajili ya msaada, na kuomba, “Ee Mungu! Ninajua kwamba ninastahili kuteseka, lakini mwili wangu ni dhaifu sana na kwa kweli siwezi kudumu muda mrefu zaidi. Wakati ambapo ningali ninapumua na nina fahamu, nataka kukuomba Usindikize nafsi yangu kutoka katika dunia hii. Sitaki kuwa Yuda na kukusaliti.” Nilipokuwa tu karibu kuchanganyikiwa, neno la Mungu lilinipa nuru na kuniongoza: “‘Kuja katika mwili wakati huu ni sawa na kuanguka katika tundu la duma.’ Hii ina maana kwamba kwa sababu awamu hii ya kazi ya Mungu imemfanya Mungu kuja katika Mwili na kuzaliwa katika makazi ya joka kuu jekundu, hata kuliko awali, Anakumbwa na hatari kubwa kwa kuja duniani wakati huu. Anachokabiliana nacho ni visu na bunduki na kumbi za starehe; Anavyokabiliana navyo ni vishawishi; Anaokutana nao ni umati wa watu wenye sura za wauaji. Ana hatari ya kuuawa wakati wowote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (4)). Mungu ndiye mkuu kabisa wa viumbe wote na mwenye mamlaka—kuja chini kati ya waliopotoka sana zaidi ya wanadamu wote ili kutuokoa tayari ilikuwa aibu kubwa, lakini pia Alilazimika kuvumilia kila aina ya mateso kutoka kwa serikali ya CCP. Mateso ambayo Mungu amepitia kwa kweli ni makubwa sana. Ikiwa Mungu amevumilia haya maumivu na mateso yote, kwa nini singejitoa mhanga kwa ajili Yake? Sababu pekee ya mimi bado kuwa hai ni kwa ajili ya ulinzi na utunzaji wa Mungu, ambao bila kuwa nao ningekuwa nimeteswa na kundi hili la pepo hadi kufa hapo zamani. Katika lile pango la pepo, ingawa wale wakatili walitumia kila mbinu waliyokuwa nayo kunitesa kwa ukatili, lakini Mungu alikuwa na mimi, na kila niliposhinda kipindi kimoja cha mateso nilishuhudia matendo ya muujiza ya Mungu, na pia wokovu na ulinzi Wake. Nilijiwazia, “Mungu amenitendea mengi sana, ninapaswaje kuufariji moyo Wake? Kwa kuwa Mungu amenipa nafasi hii leo, ninapaswa kuendelea kuishi kwa ajili ya Mungu!” Wakati huo, upendo wa Mungu ulizindua tena dhamiri yangu na nilihisi kabisa kwamba lazima nimridhishe Mungu bila kujali lolote. Nilijitamkia kwa dhati, “Ni heshima yangu kuteseka pamoja na Kristo leo!” Walipoona kwamba bado sikuwa nikizungumza na sikuwa nikiomba msamaha, lakini wakiogopa kwamba huenda nikafia mahali hapa bila kufumbua habari yoyote na wangewakosea wakubwa wao, polisi wabaya waliacha kunipiga. Baada ya hapo, nilining’inizwa ukutani kwa pingu zangu na kuachwa hapo kwa siku nyingine mbili

Wakati huo, kulikuwa na baridi kali, nilikuwa nimelowa chepechepe, nguo zangu zilikuwa nyembamba sana na hazikuzuia baridi, sikuwa nimekula kwa siku kadhaa na nilihisi njaa na baridi—sikuweza kwa kweli kuvumilia tena. Wakati tu nilipokuwa karibu kuchanganyikiwa, kundi hilo la polisi majambazi walitumia hali yangu pungufu kubuni njama nyingine ya siri: Walimleta mwanasaikolojia ajaribu kunitia kasumba. Alisema, “Bado wewe ni mchanga na unahitaji kuwasaidia wazazi wako na watoto wako. Baada ya kuletwa, waumini wenzako, na haswa viongozi wa kanisa lako, hawajajishughulisha hata kidogo na bado unatesekea humu kwa ajili yao. Hufikirii kuwa huku ni kuwa mjinga? Polisi hawa hawakuwa na budi kukutesa….” Nilipokuwa nikisikiliza uongo wake, niliwaza moyoni mwangu, “Kama ndugu zangu wangekuja kuniona hapa, si huko kungekuwa sawa na kujisalimisha? Unasema tu hivi ili kunidanganya, kueneza ugomvi kati yangu na ndugu zangu, na kunifanya nimwelewe visivyo, nimlaumu na kumwacha Mungu. Sitadanganyika!” Baada ya hapo, waliniletea chakula na kinywaji, wakijaribu kunibembeleza kwa ukarimu wao ulioonekana. Nilipokabiliwa na “wema” wa ghafla wa polisi hawa majambazi, moyo wangu ulimshikilia Mungu kwa karibu hata zaidi, kwa sababu nilijua kuwa nilikuwa dhaifu sana wakati huo, na Shetani alikuwa tayari kunishambulia ghafla wakati wowote fursa zilipojitokeza. Uzoefu wangu wakati huo uliniruhusu nibaini kiini cha serikali ya CCP. Bila kujali jinsi ilivyojifanya kuwa na wema na kujali, kiini chake kiovu, cha kupinga maendeleo na cha shetani hakikubadilika. Mkakati wa ibilisi wa “ubadilishaji kupitia huruma ya upendo” ulifunua tu zaidi undani wa udanganyifu na ulaghai wake. Shukrani kwa Mungu, kwa kunielekeza kubaini njama ya hila ya Shetani. Mwishowe, mwanasaikolojia aliambulia patupu na alitikisa kichwa chake, akisema, “Siwezi kupata chochote kutoka kwake. Yeye ni mkaidi sana, kadhia isiyoleta matumaini!” Kwa hilo, aliondoka akiwa na huzuni. Nilipoona Shetani akikimbia kwa ajili ya kushindwa, moyo wangu ulijawa na furaha isiyoelezeka!

Wale polisi waovu walipoona kuwa mbinu zao zenye huruma zimeshindwa, walifunua tabia zao halisi moja kwa moja, kwa mara nyingine wakanining’iniza ukutani siku nyingine nzima. Usiku huo, nilipokuwa nikining'inia huko nikitetemeka kwenye baridi, mikono yangu ikiwa na maumivu kiasi kwamba nilihisi kana kwamba ingevunjika, nilijiwazia kwa mapayo yangu kwamba huenda kwa kweli nisiokoke. Wakati huo huo, maafisa kadhaa waliingia na nikaachwa tena nikijiuliza ni aina gani ya mateso waliyoniwekea tayari. Nilimwomba Mungu tena katika udhaifu wangu, nikisema, “Ee Mungu, Unajua kuwa mimi ni dhaifu na kwa kweli siwezi kuvumilia tena. Tafadhali chukua maisha yangu hivi sasa. Ni afadhali nife kuliko kuwa Yuda na kukusaliti. Sitaruhusu hila za kijanja za pepo hawa zifaulu!” Polisi walitia tahabibu marungu yao ambayo yalikuwa na urefu wa chini ya mita moja, na wakaanza kupiga viungo vya miguu na nyayo zangu. Wengine kati yao walicheka sana walipokuwa wakinigonga, wengine walijaribu kunijaribu, wakisema, “Si wewe ni mpenzi mkubwa tu wa adhabu. Hujafanya uhalifu wowote mkubwa, hujamuua mtu yeyote au kuchoma mali yoyote kwa makusudi. Tuambie tu kile unachojua na tutakushusha.” Wakati ambapo bado sikuweza kuzungumza, walighadhabika sana na wakapiga kelele, “Unafikiri kuwa polisi hawa wengi waliosimama mbele yako hivi sasa wote hawawezi kumudu? Tumewasaili wafungwa wengi waliohukumiwa kifo mahali hapa na daima wao hutukiria, hata ikiwa hawajafanya chochote kibaya. Tunapowaambia wazungumze, wao huzungumza. Ni nini kinachokufanya ufikirie kuwa wewe ni tofauti nao?” Baadhi yao kisha walinijia na kuanza kufinya na kupinda miguu na kiuno changu hadi nilipofunikwa na michubuko. Katika sehemu nyingine walinifinya kwa nguvu sana hata zikatoa damu. Baada ya kuning’inizwa ukutani kwa muda mrefu sana, tayari nilikuwa dhaifu sana, na hili lilizidisha uchungu uliotokana na vichapo vyao vingi sana hadi kufikia kiwango ambacho nilitamani kifo changu mwenyewe. Wakati huo, nilikuwa nimevunjika kabisa—sikuweza kuvumilia tena na mwishowe nikatokwa na machozi. Machozi yalipotiririka, mawazo ya usaliti yalitokea akilini mwangu: “Labda napaswa tu kuwaambia kitu. Ilimradi nisimtie ndugu yeyote taabani, hata wakinishtaki au kuniua, basi na iwe hivyo!” Genge lile la polisi waovu liliponiona nikilia, walicheka kwa sauti kubwa na, huku wakiwa wamejiridhisha wenyewe kikamilifu, wakasema, “Ikiwa ungekuwa umesema jambo mapema zaidi, tusingelazimika kukupiga jinsi hiyo.” Walinishusha na kunilaza chini. Wakanipa maji na wakaniruhusu nipumzike kwa muda mfupi. Kisha wakachukua kalamu na karatasi ambayo ilikuwa imeandaliwa tokea mwanzo na wakajiandaa kurekodi taarifa yangu. Wakati tu nilipokuwa nikiingia katika jaribu la Shetani na nilikuwa karibu kumsaliti Mungu, maneno ya Mungu yalitokea waziwazi akilini mwangu kwa mara nyingine tena: “Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako). Katika maneno ya Mungu, niliona tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa lolote na matokeo ya kumsaliti Mungu. Niligundua pia uasi wangu mwenyewe. Imani yangu katika Mungu ilikuwa dhaifu sana na sikuwa na ufahamu wa kweli juu Yake, sembuse kuwa mtiifu Kwake kwa kweli. Kwa hivyo, nilikuwa na hakika ya kumsaliti Mungu. Nilifikiria jinsi Yuda alikuwa amemsaliti Yesu ili kupata sarafu thelathini tu na jinsi, hivi sasa, nilikuwa tayari kumsaliti Mungu kwa ajili ya raha na utulivu wa muda mfupi. Isingekuwa nuru ya maneno ya Mungu ya wakati ufaao, ningekuwa mmoja wa wasaliti wa Mungu wa kulaaniwa wakati wote! Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, niliona kwamba Mungu alikuwa amefanya mipango bora zaidi kadiri iwezekanavyo. Nilijiwazia, “Mungu akiniruhusu niteseke au nife, niko tayari kutii na kuweka maisha yangu na kifo mikononi mwa Mungu. Sina kauli katika jambo hilo. Hata nikiwa na pumzi moja tu iliyobaki, lazima nijitahidi kumridhisha Mungu na kuwa shahidi Kwake.” Wakati huo, nilikumbuka wimbo wa kanisa: “Kichwa changu kinaweza kupasuka na damu kutiririka, lakini ujasiri wa watu wa Mungu hauwezi kupotea. Ushawishi wa Mungu umo moyoni, ninaamua kumwaibisha Shetani Ibilisi” (“Ninatamani Kuona Siku ya Utukufu wa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilipokuwa nikijiimbia wimbo huu kimoyomoyo, imani yangu iliimarishwa tena, na nikaamua kwamba iwapo ningehitajika kufa, ingekuwa kwa ajili ya Mungu. Bila kujali lolote, singekubali kushindwa na ibilisi huyo wa kale, serikali ya CCP. Walipoona kwamba nililala tu sakafuni bila kusonga, polisi wabaya walianza kunijaribu wakisema, “Mateso haya yote yanafaa? Tunakupa fursa ya kufanya kitendo kizuri hapa. Tuambie kila kitu unachojua. Hata usiposema chochote, tuna ushuhuda wote wa mashahidi na ushahidi ambao tunahitaji kukutia hatiani.” Nilipoona jinsi ambavyo pepo hawa wala watu walikuwa wakijaribu kunifanya nimsaliti Mungu na kuwasaliti ndugu zangu ili kuharibu kazi ya Mungu, sikuweza tena kuzuia hasira iliyojaa ndani yangu na nikawajibu kwa sauti kubwa, “Ikiwa tayari mnajua kila kitu, basi nadhani hamna sababu ya kunihoji. Hata kama ningejua kila kitu singewaambia!” Polisi walijibu kwa hasira, wakisema kwa sauti, “Usipokiri, tutakutesa hadi ufe! Usifikirie kuwa utatoka hapa ukiwa hai! Tuliwafanya wafungwa wote waliohukumiwa kifo wazungumze, unafikiri kuwa wewe ni sugu kuwaliko?” Nilijibu, nikisema, “Sasa kwa kuwa mmenifunga, sina mpango wa kuondoka nikiwa hai!” Bila kusema neno lingine, polisi walinirukia kwa nguvu na kunipiga moja kwa moja tumboni. Niliumwa sana kiasi kwamba nikahisi kana kwamba matumbo yangu yalikuwa yamekatwa vipande viwili. Kwa hayo, maafisa waliobaki wote walinijia na kunipiga mpaka nikazimia... Nilipopata fahamu, niligundua kuwa walikuwa wamenining’iniza kama hapo awali, lakini wakati huu walikuwa wamenining’iniza juu hata zaidi. Mwili wangu wote ulikuwa umevimba na sikuweza kuongea, lakini kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, sikuhisi maumivu hata kidogo. Usiku huo, maafisa wengi waliondoka na wale wanne waliopewa kazi ya kunilinda walikuwa wamelala fofofo. Ghafla, pingu zangu zilifunguka kimuujiza na nikaanguka sakafuni bila kishindo. Wakati huo, nilipata fahamu tena na ghafla nikawaza jinsi Petro alivyokuwa ameokolewa na malaika wa Bwana wakati wa kufungwa kwake. Minyororo ilianguka kutoka kwa mikono ya Petro na lango la chuma la seli yake likajifungua lenyewe. Ilikuwa kwa ukuzaji na neema kuu ya Mungu kwamba niliweza kupitia matendo ya Mungu ya muujiza kama Petro. Nilipiga magoti chini mara moja na kutoa sala ya shukrani kwa Mungu, nikisema, “Mungu mpendwa! Asante kwa rehema Yako na utunzaji Wako mwema. Asante kwa uangalifu Wako kwangu usio na mwisho. Maisha yangu yalipokuwa hatarini na kifo kilipokuwa karibu, Ulinilinda sirini. Ni nguvu Yako kuu iliyonilinda na kuniruhusu kushuhudia tena matendo Yako ya ajabu na utawala mkuu. Nisingepata uzoefu huu mwenyewe, nisingeweza kuamini kwamba hii ni halisi!” Kupitia mateso yangu, nilikuwa tena nimeshuhudia wokovu wa Mungu na nilihuswa sana na kujawa na ukunjufu usio na kikomo. Nilitaka kuondoka mahali hapo, lakini niliumia sana kiasi kwamba sikuweza kusonga na nikalala pale pale sakafuni na kulala hadi nilipoamshwa alfajiri kwa kupigwa teke. Polisi wabaya waliponiona nikilala sakafuni, walianza kubishana kati yao, wakijaribu kuhakikisha ni nani aliyenishusha. Polisi wale wanne ambao walikuwa na jukumu la kunilinda usiku kucha wote walisema kwamba hawakuwa na funguo za pingu zangu. Wote walisimama kando ya pingu hizo wakikodoa macho kabisa—wote walitazama pingu mmoja baada ya mwingine, lakini hawakuweza kupata alama zozote za ufa kwazo. Waliniuliza jinsi pingu zilivyokuwa zimefunguka na nikasema, “Zilijifungua!” Hawakuniamini, lakini moyoni mwangu nilijua: Hii ilikuwa nguvu kuu ya Mungu, na ilikuwa moja ya matendo Yake ya muujiza.

Baadaye, walipoona kwamba nilikuwa dhaifu sana kiasi kwamba huenda ningekufa wakati wowote, polisi waovu hawakuthubutu kunining’iniza tena, na kwa hivyo walibadili na kutumia mbinu tofauti ya kutesa. Walinikokota hadi ndani ya chumba na kunifanya niketi kwenye kiti cha mateso. Kichwa na shingo yangu ilifungwa kwa kibanio cha chuma na mikono yangu na miguu yote ilifungwa ili nisiweze kusogeza musuli. Moyoni mwangu, nilimwomba Mungu, nikisema, “Ee Mungu! Yote yako chini ya utawala Wako. Tayari nimeshinda majaribu kadhaa ya kufa kupona na sasa najikabidhi Kwako tena. Niko tayari kushirikiana na Wewe kuwa shahidi na kumfedhehesha Shetani.” Baada ya kumaliza maombi yangu, nilihisi shwari, utulivu, na bila woga hata kidogo. Wakati huo, mmoja wa maafisa alibonyeza swichi ya umeme, na wadogo wote wakatazama kwa kushika pumzi ili kuona jinsi nitakavyotiwa umeme. Wakati ambapo sikuonyesha hisia hata kidogo, walikwenda kuangalia muunganisho wa umeme. Wakati ambapo bado sikuonyesha hisia, waliweza tu kutazamana bila kuamini, wasiweze kuamini macho yao. Mwishowe, mmoja wa wadogo alisema, “Labda kuna dosari katika unganisho katika kiti cha mateso.” Baada ya kusema hayo, alinijia na mara mkono wake uliponigusa, alipiga unyende—mshtuko wa umeme ulimrusha nyuma mita moja kamili na akaanguka chini, akilia kwa uchungu. Wale vikaragosi kumi na wawili au zaidi walipoona kilichotokea, wote walitishika na kutoka ndani ya chumba kwa haraka. Mmoja wao alitishika sana kiasi kwamba aliteleza na kuanguka ardhini kwa kishindo. Muda mrefu ulipita kabla ya wadogo kuja kunifungua, wakitetemeka kwa hofu ya kushtushwa wenyewe. Katika nusu saa nzima ambayo nilifungiwa kwenye kiti cha mateso, sikuhisi mkondo wowote wa umeme hata. Ilikuwa kama kwamba nilikuwa nikiketi kwenye kiti tu cha kawaida. Nilikuwa nimeshuhudia tena nguvu kubwa ya Mungu na nikapata utambuzi wa kina kuhusu uzuri Wake na wema Wake. Hata kama ningepoteza kila kitu nilichokuwa nacho, pamoja na maisha yangu, alimradi Mungu alikuwa pampoja nami, nilikuwa na kila kitu nilichohitaji.

Baada ya hapo, polisi waovu kisha walinirudisha kizuizini. Nilifunikwa kutoka kichwani hadi kwenye vidole na makato, michubuko na majeraha, mikono na miguu ilikuwa imevimba sana—nilikuwa dhaifu kabisa na hata sikuweza kusimama, kukaa chini au hata kula. Nilikuwa karibu kabisa kuzimia. Wafungwa wengine waliohukumiwa kifo waliokuwa kwenye seli waliarifiwa kuwa sikuwa nimemsaliti mtu yeyote, walinitazama kwa mtazamo mpya na wakasema huku wakisifu, “Wewe ndiye shujaa halisi, sisi ni mashujaa bandia!” Hata walishindana kunipa chakula na nguo za kuvaa.... Polisi wabaya walipoona jinsi Mungu alivyofanya kazi ndani yangu, hawakuthubutu tena kunitesa na hata waliondoa pingu na minyororo yangu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, hakuna mtu aliyethubutu kunihoji tena. Licha ya hayo, polisi bado hawakuwa wamekufa moyo, na kwa hivyo, ili kupata habari juu ya kanisa kutoka kwangu, walijaribu kushawishi wafungwa wengine wanifanye nikubali kushindwa. Walijaribu kuwachochea wafungwa wengine kwa kusema, “Wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu wanapaswa kupigwa!” Hata hivyo, jambo la kushngaza ni kwamba, mmoja wa wafungwa ambaye alikuwa muuaji alisema, “Sitawahi kufanya kile unachosema. Sio tu kwamba sitampiga, ila pia hakuna mtu kwenye seli hii atakayempiga! Sote tuko hapa ndani kwa sababu mtu mwingine alitusaliti. Kama kila mtu angekuwa mwaminifu kama mtu huyu, hakuna yeyote kati yetu ambaye angehukumiwa kifo.” Mfungwa mwingine aliyehukumiwa kifo alisema, “Sote tulikamatwa kwa sababu tulifanya vitu vibaya sana na kwa hivyo tunastahili kuteseka. Lakini huyu mtu ni muumini wa Mungu na hajafanya uhalifu, lakini mateso yenu yamemfanya akaribie kutotambulika!” Mmoja baada ya mwingine, wafungwa wote waliongea dhidi ya dhuluma ambazo nilikuwa nimezipitia. Walipoona kile kilichokuwa kikiendelea, polisi hawakutaka mambo yasiweze kudhibitiwa na kwa hivyo hawakusema kitu kingine, lakini waliondoka tu kwa huzuni. Wakati huo, nilifikiria kifungu kutoka kwa Biblia, ambacho kinasema, “Moyo wa mfalme umo mikononi mwa Yehova, kama mito ya maji: Anaugeuza popote Atakapo” (Mithali 21:1). Niliposhuhudia jinsi Mungu alivyokuwa amewagusa wale wafungwa wengine ili waje kunisaidia, nilikuwa na imani kuu kuwa haya yote yalikuwa matendo ya Mungu na imani yangu Kwake ilikua thabiti zaidi!

Mkakati mmoja ulipokosa kufaulu, polisi hao wabaya walibuni njama nyingine. Wakati huu, walimfanya mlinzi wa kituo cha uzuizi anipe kazi ngumu zaidi: Nililazimishwa kutengeneza magombo mawili kamilifu ya pesa za karatasi kwa siku (pesa za karatasi ni sehemu ya utamaduni wa Wachina ambapo watu huchoma pesa ili kuwapa babu zao waliokufa. Gombo moja la pesa za karatasi limetengenezwa na karatasi 1,600 za jaribosi za bati na mabomba 1,600 ya karatasi ya kushika moto kwa pamoja. Mzigo wangu wa kazi ulikuwa mara mbili ya wafungwa wengine na, wakati huo, mikono na miguu yangu ilikuwa katika maumivu yasiyovumilika kiasi kwamba nilishindwa kuinua au kushikilia chochote. Kwa hivyo hata ikiwa ningefanya kazi usiku kucha, singemaliza kazi yangu. Polisi walitumia kutoweza kwangu kukamilisha kazi yangu kama kisingizio cha kunipa adhabu ya kutandikwa katika kila aina ya njia. Walinilazimisha nioge kwa maji baridi wakati ambapo halijoto ilikuwa digrii -4 za Farenhaiti; walinifanya nifanye kazi hadi usiku wa manane au kusimama nikilinda na, kwa sababu hiyo, sikupata usingizi wa zaidi ya saa tatu kamwe kwa kila usiku. Ikiwa singemaliza kazi yangu kila siku, wangewakusanya wafungwa wote kutoka katika seli yangu, kututoa nje, kutuzingira na bunduki zao zikiwa mikononi na kutufanya tuchutame chini mikono yetu ikiwa nyuma ya vichwa vyetu. Ikiwa mtu yeyote hakuweza kukaa kwa namna ile, wangemshtua kwa kirungu cha umeme. Wale askari waovu walitumia kila njia waliyoweza kuwafanya wafungwa wengine wanichukie na kunidhulumu. Baada ya kukabiliwa na hali hii, nilichoweza kufanya ni kuja mbele za Mungu katika sala: “Mpendwa Mungu, najua kuwa polisi hawa waovu wanawachochea wafungwa wengine kwa kusudi la kuwafanya wanichukie na wanitese ili nikusaliti. Hivi ni vita vya kiroho! Ee Mungu! Bila kujali jinsi wafungwa wengine watakavyonitendea, niko tayari kutii katika mipangilio na mipango Yako na naomba kwamba Unipe azimio la kuvumilia mateso haya. Natamani kuwa shahidi Kwako!” Baada ya hapo, nilishuhudia tena matendo ya Mungu. Sio tu kwamba wale wafungwa waliohukumiwa kifo hawakunichukia, bali hata walipanga mgomo kwa niaba yangu na kuwataka maafisa wapunguze mzigo wangu kwa nusu. Mwishowe, polisi hawakuwa na budi kukubali madai ya wafungwa.

Ijapokuwa walilazimika kupunguza mzigo wangu wa kazi kwa nusu, polisi wale bado walikuwa na hila nyingine za siri. Siku chache baadaye, “mfungwa” mpya aliwasili kwenye seli. Alikuwa mwema sana kwangu, alininunulia chochote nilichohitaji, akanipatia chakula, akaulizia hali yangu ya afya na pia akauliza ni kwa nini nilikuwa nimekamatwa. Mwanzoni, sikujali jambo hili na nikamwambia kwamba mimi ni muumini wa Mungu na nilikuwa nimekamatwa kwa ajili ya kuchapisha vifaa vya dini. Aliendelea kuniuliza juu ya maelezo bayana ya kazi yangu ya kuchapisha vitabu na, nilipoona jinsi alivyoendelea kunihoji kwa maswali, nilianza kuhisi wasiwasi na nikamwomba Mungu nikisema, “Mungu, mpendwa, watu, vitu na hali zote zinazotuzingira zinaruhusiwa na Wewe. Ikiwa mtu huyu ni mtoa habari aliyetumwa na polisi, ninaomba kwamba Unifunulie utambulisho wake wa kweli.” Baada ya kumaliza sala yangu, nilikaa kimya mbele za Mungu na kifungu cha maneno Yake kikaingia akilini mwangu: “Salia mtulivu mbele Yangu na kuishi kwa mujibu wa neno Langu, na kwa hakika utasalia macho na kutumia utambuzi katika roho. Shetani atakapofika, utaweza kujikinga dhidi yake mara moja, na pia kuhisi kuja kwake; utahisi wasiwasi halisi katika roho yako” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 19). Nilitafakari juu ya maswali ambayo “mfungwa mpya” alikuwa ameniuliza na nikagundua kuwa yote yalikuwa hasa kuhusu yale ambayo polisi walikuwa wametaka kujua kutoka kwangu. Wakati huo, ilikuwa kana kwamba nilikuwa nimeamka kutoka ndotoni: Hii yote ilikuwa moja ya njama za polisi waovu na mtu huyu alikuwa mtoa habari. “Mfungwa” aliona kuwa nilikuwa nimekaa kimya ghafla na akaniuliza ikiwa nilikuwa nikihisi vizuri. Nilisema nilikuwa nikihisi vizuri halafu, kwa ukali na kwa haki, nikamwambia, “Acha nikuepushe na kujisumbua nikujulishe kwamba unapoteza wakati wako. Hata kama ningejua kila kitu, singekuambia!” Wafungwa wengine wote walisifu tabia yangu, wakisema, “Sote tunaweza kujifunza kutoka kwenu ninyi waumini. Mna uhodari wa kweli!” Mtoa habari hakuweza kufikiria chochote cha kuijibu na, siku mbili baadaye, aliondoka kimyakimya.

Niliendelea kudumu kwa mwaka mmoja na miezi minane kizuizini. Ingawa hao polisi majambazi walibuni kila njia inayowezekana kufanya maisha yawe magumu kwangu, Mungu aliwagusa wafungwa waliohukumiwa kifo wanitunze. Mkuu wa wafungwa alihamishwa baadaye na wafungwa wakanichagua kama mkuu mpya wa wafungwa. Kila mara wafungwa walipoingia taabani, nilijitahidi sana kuwasaidia. Niliwaambia, “Mimi ni mmoja wa waaminifu wa Mungu. Mungu anataka tuwe na ubinadamu. Ingawa tumefungwa gerezani, alimradi tu hai, lazima tuishi kwa mfano wa binadamu.” Baada ya kutoa kauli hii, wafungwa waliohukumiwa kifo waliacha kuwadhulumu wafungwa wapya. Jina “seli namba 7” lilikuwa limewaogofya wafungwa, lakini, chini ya umiliki wangu, ilikuwa seli ya kistaarabu. Wafungwa wote walisema, “Watu hawa wanaotoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu ni kundi zuri. Ikiwa tutawahi kutoka hapa, bila shaka tutamwamini Mwenyezi Mungu!” Uzoefu wangu kizuizini ulinikumbusha hadithi ya Yusufu. Wakati wa kufungwa kwake huko Misiri, Mungu alikuwa pamoja naye, Mungu alimpa neema, na kila kitu kilikwenda kwa utaratibu kwa Yusufu. Wakati huu, yote niliyokuwa nimefanya ni kutenda kwa mujibu na matakwa ya Mungu na kutii mipangilio na mipango Yake. Kwa hivyo Mungu alikuwa na mimi na aliniwezesha kuzuia maafa kila zamu mara kwa mara. Nilimshukuru Mungu kwa dhati kwa neema aliyonipa!

Baadaye, bila ushahidi hata mdogo kabisa, serikali ya CCP ilibuni mashtaka ya uwongo na kunihukumu kifungo kisichobadilika cha miaka mitatu, mwishowe wakaniachilia tu mnamo mwaka wa 2009. Baada ya kutoka gerezani, polisi wa eneo hilo walinilinda kwa karibu sana na wakanihitaji niwe chini ya amri yao wakati wote. Kila tendo langu likawa chini ya udhibiti wa serikali ya CCP na sikuwa na uhuru wowote wa kibinafsi. Nililazimika kuukimbia mji wangu na kutimiza wajibu wangu mahali pengine. Aidha, kwa sababu nilikuwa mmoja wa waaminifu wa Mungu, serikali ya CCP ilikataa kushughulikia rekodi za usajili wa kaya ya familia yangu (hadi leo, rekodi za usajili wa wanangu wawili bado zinaendelea kushughulikiwa). Hii ilinidhihirishia waziwazi hata zaidi kuwa maisha chini ya utawala wa serikali ya CCP ni ya mateso. Sitawahi kamwe kusahau mateso mabaya ambayo serikali ya CCP ilinipa. Ninaidharau kwa uhai wangu wote na ni heri nife kuliko kuwa mtumwa wayo. Ninaikana kabisa!

Uzoefu huu umenipa ufahamu mkuu zaidi kumhusu Mungu. Nimeshuhudia uweza Wake na hekima Yake na kiini cha wema Wake. Nimeona pia kuwa bila kujali serikali mbovu ya CCP inawatesa wateule wa Mungu kiasi gani, inasalia tu kuwa kitu cha utumishi na foili[a] ya kazi ya Mungu. Serikali ya CCP ni audi na daima itakuwa adui wa Mungu aliyeshindwa. Mara nyingi, ulinzi wa kimuujiza wa Mungu uliniokoa wakati wa kukata tamaa, ukiniruhusu niondokane na fumbato la makucha ya Shetani na kupata maisha tena ukingoni mwa kifo; mara nyingi sana, maneno ya Mungu yalinifariji na kunihuisha, na yakawa msaada na tegemeo langu nilipokuwa dhaifu zaidi na bila matumaini, yakiruhusu niushinde mwili wangu na kuponyoka fumbato la kifo; na mara nyingi, nilipokaribia kufa, nguvu ya Mungu ilinisaidia na kunipa nguvu ya kuendelea kuishi. Ni kama jinsi maneno ya Mungu yanavyosema, “Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung’aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko makubwa, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu wa kweli!

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp