Kupenyeza Mzunguko Uliokazwa wa Shetani

09/01/2020

Na Zhao Gang, China

Kulikuwa na baridi kali Novemba iliyopita huko Kaskazini Mashariki mwa China, hakuna theluji iliyoanguka chini iliyoyeyuka, na watu wengi waliokuwa wakitembea nje walikuwa baridi sana hivi kwamba walishindilia mikono yao ndani ya makwapa yao na kutembea kwa uangalifu, miili kama imeinama. Juzi asubuhi mapema upepo ulikuwa unavuma kutoka kaskazini magharibi, wakati mimi, shemeji yangu na mkewe na karibu ndugu kumi na wawili tulikuwa tumeketi nyumbani mwangu kwenye kitanda chenye joto. Kila mtu alikuwa na nakala ya Biblia kando yake, na mikononi mwao kila mtu alikuwa na nakala ya kitabu cha maneno ya Mungu, Hukumu Huanza na Nyumba ya Mungu. Dada wawili kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu walikuwa wanashiriki kuhusu ukweli juu ya hatua tatu za kazi ya Mungu. Dada hao wawili walikuwa wakichora picha za hatua hizo tatu za kazi walipokuwa wakishiriki: “Kazi ya Mungu kwa ajili ya wokovu wa wanadamu inaweza kugawanywa katika hatua tatu. Kutoka kwa Enzi ya Sheria hadi Enzi ya Neema na kisha Enzi ya Ufalme, kila hatua ya kazi ni ya juu zaidi na ya maana zaidi kuliko hatua ya awali. Kazi inayofanyika katika siku za mwisho ni hatua ya mwisho ya kazi, ambayo kwayo Mungu anaonyesha maneno ili kumhukumu na kumtakasa mwanadamu….” Tuliamkia kwa vichwa vyetu tulipokuwa tunasikiliza, na mioyo yetu ilijawa na nuru: Nani angeweza kufikiri kwamba mpango wa usimamizi wa Mungu kwa ajili ya wokovu wa wanadamu ungekuwa wa siri nyingi! Mbali na Mungu Mwenyewe, nani mwingine angeweza kuzungumza kuhusu siri za hatua hizi tatu za kazi ya Mungu kwa wazi? Hii kweli ni kazi ya Mungu! Tulishirikiana hadi jioni ya siku iliyofuata, na kundi letu lote lilionyesha nia ya kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.

Baada ya hapo, dada hao wawili kisha walishiriki juu ya ukweli kuhusu umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu, na sisi wengine sote tulisikiliza kwa makini wakati ghafla kiongozi wetu wa kanisa Wang Ping alitokea. Punde alipoingia nyumbani, alielekeza kidole chake kwa dada hao wawili kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu na akaniuliza: “Je, hawa wawili wanafanya nini?” Nilizungumza waziwazi: “Hawa ni Dada Zhang na Dada Mu—” Lakini kabla hata nimalize kuzungumza, alisema kwa sauti ya hasira, “Dada Zhang na Dada Mu ni nani? Ninaweza kuona wao ni wahubiri wa Umeme wa Mashariki, wao ni wezi wa kondoo….” Baada ya Wang Ping kumaliza kuzungumza, sote tuliketi hapo kwa mshangao. Nilijiwazia mwenyewe: “Dada Wang Ping karibu kila mara ameongea kuhusu kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda na kuhusu kuwapenda adui zetu; kwa nini ni kwamba leo anakuja hapa akisema mambo yasiyo ya busara? Kwa nini anawahukumu na kuwashutumu dada hawa wawili?” Nilikuwa nafikiria kuhusu jambo hili wakati nilimsikia Dada Zhang akimwambia Wang Ping kwa utulivu, “Dada, hakuna malengo yaliyofichika katika kuja kwetu hapa leo. Bwana Yesu tayari amerejea. Tunataka tu kuwaenezea injili ya Mungu ya siku za mwingi” Wang Ping alimkatiza Dada Zhang na akafoka: “Bwana amerejea? Hata wale kati yetu ambao hutumikia kama viongozi hatujui chochote kuhusu kurudi kwa Bwana, kwa hivyo ninyi mnawezaje kujua chochote kuhusu hilo? Hiyo haiwezekani! Bwana Yesu alisema: ‘Wote ambao wamewahi kuja kabla Yangu ni wakwepuzi na wezi: lakini kondoo hawakuwapa masikio(Yohana 10:8). Ninyi wawili mnapasa kuondoka hivi sasa na kamwe msije hapa tena.” Nilipomsikia Wang Ping akisema hivi nilihisi kero sana ndani mwangu: Mahubiri yake kwa kawaida huwa yenye busara na yenye majadiliano mazuri; inawezekanaje kuwa anaweza kuwa asiye na huruma kwa ghafla? Kwa hiyo nilimwuliza Wang Ping: “Dada Wang, muda umeisha. Unataka waende wapi? Bwana anatufundisha kwamba lazima tuwapende adui zetu, sembuse hawa dada wawili ambao wanamwamini Mungu. Kama tunawatendea hawa wawili kwa namna hii, hatuwezi kufanana na waumini katika Bwana kwa vyovyote—” Lakini kabla sijaweza hata kumaliza kile nilichokuwa nikisema Wang Ping kwa wasiwasi aliushika mkono wa mke wa shemeji yangu na kumwambia yeye na mumewe: “Kama Zhao Gang hawataki wanawake hawa wawili waondoke basi acha twende. Msiwasikilize tena!” Kisha aliwashikilia wawili hao na kutoka nje.

Baada ya wao kuondoka Dada Mu alitugeukia na kuuliza: “Ndugu, ninyi nyote mnahisije kuhusu tukio ambalo tumeshuhudia tu sasa hivi? Hebu tujadili hili pamoja.” Ndugu wote walinigeukia, bila mtu yeyote kusema neno. Nikasema wazi: “Dada, kupitia usomaji wetu wa neno la Mwenyezi Mungu katika siku hizi mbili zilizopita, na kwa kusikiliza ushirika wako, ninaamini kabisa kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Hata hivyo, mambo ambayo Wang Ping alisema sio bila sababu. Hata hivyo, yeye ni kiongozi wetu na amekuwa na imani katika Bwana kwa muda mrefu. Anaifahamu Biblia vizuri na amekuwa akijishughulisha daima kwa ajili ya Bwana. Kama Bwana amerejea, anapaswa kuwa wa kwanza kujua.” Dada Zhang alijibu kwa upole, akisema: “Watu wanaamini kwamba kurudi kwa Mungu lazima kwanza kufunuliwe kwa viongozi ambao kisha watawaambia waumini juu yake, lakini kweli kuna msingi wowote katika maneno ya Bwana katika fikira ya aina hii? Je, inapatana na ukweli na uhalisi wa kazi ya Mungu? Bwana Yesu alisema: ‘Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). ‘Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa(Ufunuo 2:7). Bwana Yesu anatuambia wazi kwamba Atakapokuja, hakika Atatamka maneno na kuonyesha ukweli, na kwamba wote wanaosikia sauti ya Mungu na kisha kuutafuta na kuukubali watakaribisha kurejea kwa Bwana na kuinuliwa juu mbele za Mungu. Je, Bwana alisema kwamba angempa kiongozi yeyote nuru na maarifa ya kuja Kwake atakaporudi? La, Hakusema hivyo. Kwa hivyo, maoni haya waliyo nayo watu yanawapotosha na kuwafadhaisha watu tu, na wakimsubiri Bwana awape nuru kufuatana na taarifa hii, basi wanangojea mwisho uje kwa kukaa tu. Acha tuangalie inavyosema katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu alisema: ‘Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?). Kutoka katika maneno ya Mungu tunatambua kuwa, katika suala la kuja kwa Bwana, watu wakishikilia dhana na mawazo yao wenyewe na wasitafute ukweli au kuzingatia kusikia sauti ya Mungu, lakini badala yake wasubiri tu Mungu awape nuru, basi kamwe hawataweza kukaribisha kurudi kwa Bwana. Ni wale tu wanaojali kusikiliza sauti ya Mungu ndio wanaoweza kukaribisha kuonekana kwa Bwana. Kwa kweli, hakuna hata mtu mmoja kati ya watu waliomfuata Bwana Yesu katika Enzi ya Neema aliyepewa nuru na Mungu kabla ya kumfuata Yesu. Walimsikia mtu mwingine akimshuhudia Bwana Yesu, au walisikia Bwana akizungumza au Akihubiri, na walimfuata tu baada ya kuitambua sauti ya Bwana. Ingawa Petro alipata nuru ya Mungu na kumtambua Bwana Yesu kuwa Kristo na kuwa Mwana wa Mungu, hilo lilifanyika tu baada ya kumfuata Bwana Yesu kwa muda; ni baada tu ya kupata ufahamu fulani kumhusu Bwana kutoka katika maneno na kazi Yake ndipo alipata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu—huu ni ukweli. Sasa katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu mwenye mwili anaonyesha ukweli, na kufanya kazi ya kuhukumu, kutakasa na kuwaokoa wanadamu. Watu wengi wanamkubali na kumfuata Mwenyezi Mungu, lakini hakuna hata mmoja kati yao ambaye alipata nuru ya Mungu kabla ya kumfuata Yeye. Mungu ni mwenye haki na hakika Hampendelei mtu yeyote. Mungu anafurahia katika watu wenye moyo safi walio na kiu ya kutafuta ukweli. Ni kama Bwana Yesu alivyosema: ‘Wamebarikiwa wale walio na njaa na kiu ya haki: kwa kuwa watapewa shibe(Mathayo 5:6). ‘Heri wenye moyo safi; kwa kuwa hao watamwona Mungu(Mathayo 5:8). Mwenyezi Mungu pia alisema: ‘Mungu anawatafuta wanaomtaka Yeye ajitokeze. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, wale ambao hawajasahau agizo Lake na wanatoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Yake, na hawampingi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Hii inatuwezesha kuona kwamba, mradi tu mwanadamu anapenda ukweli na kuwa kiu ya ukweli, bila kujali kama ana hadhi yoyote au la, bila kujali ni kiasi gani anachoelewa kuhusu Biblia, Mungu atampa nuru na kumwongoza, na Atamaruhusu mwanadamu kusikia sauti Yake na kushuhudia kuonekana Kwake. Kama wale wanaohudumu kama viongozi wanadhani kwamba Mungu lazima kwanza Awape nuru Anaporudi, basi hii inaonyesha kwamba hawana ufahamu wowote wa kazi ya Mungu and hawajui tabia ya Mungu ya haki. Inafichua pia kwamba wao ni wenye majivuno sana. Inasema katika neno la Mwenyezi Mungu: ‘Na kwa hivyo Nasema kwamba wale ambao “wanaona kwa wazi”. Mungu na kazi Yake ni wasioweza kufanikisha chochote, wao wote ni wenye kiburi na wapumbavu. Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Wale wasemao daima, “Mungu hafanyi kazi kwa njia hii ama ile” au “Mungu yuko hivi ama vile”—je hawa wote si wenye kiburi?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Uweza na hekima ya Mungu ni vya kina kwa kiasi kisichoweza kupimika. Watu ni viumbe wadogo tu. Mawazo yetu na fikira zetu finyu, kwa hivyo tunawezaje kuelewa kazi ya Muumba? Kwa hiyo, tunapongojea Bwana arudi, tunapaswa kuwa na uchaji kwa Mungu katika mioyo yetu na kutafuta na kuchunguza kwa uangalifu. Hatupaswi kutumia mawazo na dhana zetu wenyewe kumzuilia Mungu na kumhukumu Mungu kiholela, kwa kuwa hili litaikosea tabia ya Mungu, na pia litaharibu nafasi zetu za kupokea wokovu.”

Baada ya kusikia maneno ya Mungu, nilielewa kuwa sisi sio muhimu sana mbele ya Mungu, wasio muhimu hata zaidi ya mchwa. Aidha, tumepotoshwa na Shetani hadi tumejaa tabia potovu ya kiburi na majivuno. Tunapenda daima kutegemea mawazo na dhana zetu kumzuilia Mungu, na wakati wowote kazi ya Mungu haipatani na dhana zetu, sisi hata humkana Mungu, kumshutumu Mungu na kumpinga Mungu. Inaonekana kama mtu hafahamu ukweli na hana chembe hata moja ya uchaji kwa Mungu ndani ya moyo wake, basi atathubutu kufanya chochote anachotaka. Ni hatari sana! Hii ilinifanya nikumbuke kwamba Bwana Yesu wakati mmoja alisema: “Asante, Ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu Umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na busara, na ukayafichua kwa watoto wachanga. Ndiyo, Baba: kwani ndilo lililokupendeza(Mathayo 11:25-26). Mpaka leo ndipo nimeona kwamba kweli hivi ndivyo mambo yalivyo! Ufunuo wa maneno ya Mungu na ushirika wa Dada Zhang viliniruhusu nitambue kwamba wazo hili kwamba “viongozi wanapaswa kuwa wa kwanza kupokea nuru kuhusu ufahamu wa kuja kwa Bwana anaporudi” ni uongo na upumbavu, halipatani na ukweli kabisa, na linatokana na mawazo na dhana za mwanadamu kabisa. Kwa kweli, wale tu ambao wana kiu ya ukweli na hutafuta sauti ya Mungu ndio watakuwa na fursa ya kupokea kazi ya Mungu na uongozi Wake na kuletwa mbele za Mungu. Hili lilinipa ufahamu mpya wa haki na uhaki wa Mungu. Shukrani ziwe kwa Mungu!

Mapema asubuhi siku ya tatu, baada ya Dada Zhang na Dada Mu kuondoka, ndugu yangu Guan, mfanyakazi mweza kutoka ngazi za juu za kanisa letu, alinijia na kuuliza: “Ndugu Zhao, nilisikia kwamba ninyi wawili sasa mnaamini katika Umeme wa Mashariki?” Nilimwambia kwa dhati: “Ndiyo, nimeikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, kwa sababu kupitia maneno ya Mwenyezi Mungu nimekuja kuelewa ukweli mwingi ambao sikuelewa hapo awali, kama vile mafumbo ya hatua Zake tatu za kazi na umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu. Naona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ‘ambalo Roho aliyaambia makanisa’ kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo.” Ndugu Guan alinitazama na kusema, “Ndugu Zhao, kwa kweli unaenda kufuata yale ambayo watu hawa wanaamini? Unajua wao ni watu wa aina gani?” Nilisema, “Ninaona kwamba wote wa asili nzuri ya binadamu na kwamba wanashirikiana kuhusu ukweli kwa uwazi sana. Kila kitu wanachojadili kinahusiana na ukweli wa kazi ya Mungu. Kwa kweli nimepata mengi katika siku hizi mbili zilizopita.” Ndugu Guan aliniambia kwa hasira, “Unawezaje kuwa mkaidi sana? Waebrania 6:6-8 kinatuambia: ‘Wakianguka baadaye, kuwafanya wawe wapya tena hata wakitubu hakutawezekana; kwa sababu wao wenyewe wamemsulubisha Mwana wa Mungu tena, na kumwaibisha Yeye kwa wazi. Kwa kuwa nchi ambayo hunywa mvua inayoinyeshea mara nyingi, na hutoa mboga kwa sababu ya wale wailimayo, hupokea baraka kutoka kwa Mungu: Lakini ile itoayo miiba na magugu hukanwa, na iko karibu na laana; ambayo hatima yake ni kuchomwa.’ Wewe ni mhubiri, unafurahia neema nyingi ya Bwana, lakini siyo tu kwamba huwaongozi tu ndugu kumwamini Bwana, bali unawaongoza waondoke kanisani kwetu. Huogopi kuadhibiwa? Usipobadilika, utapoteza ulinzi wa Bwana, na hutaishi maisha yenye furaha. Magonjwa yako ya awali yatarudi tena, na watoto wako wawili hawatakuwa na kazi nzuri….”

Baada ya ndugu Guan kuondoka, nilihisi hofu kidogo, na nilifikiria: Mambo aliyosema yanaonekana kuwa na busara fulani kwayo, kwa hivyo napaswa nifanye nini kama imani yangu katika Mwenyezi Mungu inanifanya nipoteze neema ya Bwana? Nilipofikiria kuhusu hili nilihisi moyo wangu ukiwa dhaifu, kwa hiyo nikapiga magoti na kumwomba Mungu hivi: “Mwenyezi Mungu! Maneno ya Ndugu Guan yamenifanya nihisi dhaifu kiasi. Mungu! Je, mambo aliyosema kweli ni ya kweli au la? Sijui cha kufanya sasa....” Nilipokuwa nikimwomba Mungu, mke wangu alirudi, na nikamwambia kuhusu kilichokuwa kimetokea tu. Baada ya kusikia haya, alisema kwa hofu, “Je, hicho ndicho alichosema kweli?” Nilitikisa kichwa changu kwa kukubali, na mke wangu akasema kwa wasiwasi, “Amekuwa kiongozi mkuu ambaye amemwamini Bwana kwa miaka mingi, na anaifahamu vizuri sana Biblia. Sidhani kwamba angesema uongo. Kama itakuwa kweli kama anavyosema basi tunapaswa kufanya nini?” Wakati huo tu, mimi ghafla nilifikiria kuhusu ukweli wa hatua tatu za kazi ya Mungu ambazo Dada Zhang na Dada Mu walikuwa wameshiriki kuhusu: Kazi ya Mungu kwa wokovu wa wanadamu imegawanywa katika hatua tatu, lakini hatua zote tatu za kazi zinafanywa na Mungu mmoja. Nilipokuwa nafikiria kuhusu hili, ghafla ikawa wazi kwangu, na nikamropokea mke wangu: “Kile ambacho Ndugu Guan alisema hakionekani kuwa sahihi. Alisema kuwa kwa kukubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho tunaiacha njia ya Bwana na kumsaliti Bwana Yesu, lakini maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo tumekuwa tukiyasoma siku hizi chache zilizopita kwa kweli ni sauti ya Mungu na Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi. Kwa kumfuata Mwenyezi Mungu, sisi kwa kweli tunafuata nyayo za Mwanakondoo. Sisi ndio mabikra wenye busara. Kwa nini Bwana atuadhibu? …” Tulikuwa katikati ya ushirika kuhusu hili wakati Dada Zhang na Dada Mu waliingia …

Mke wangu aliwaambia akina dada hao kile ambacho Ndugu Guan alisema alipokuja nyumbani, na Dada Zhang akaniuliza jinsi nilivyohisi kuhusu jambo hili lolote. Kwa hiyo niliwaambia akina dada hao kuhusu udhaifu niliokuwa nimehisi na kuhusu ufahamu ambao nilikuwa nimeufikia. Dada Zhang akatabasamu, akisema: “Shukrani ziwe kwa Mungu! Huu ni ufahamu safi, na hii ni nuru na mwongozo wa Mungu!” Mke wangu aliuliza, akiwa amechanganykama, “Kwa kuwa hatujapotoka, kwa nini Ndugu Guan anasema mambo hayo? Yeye ni kiongozi mkuu ambaye amemwamini Bwana kwa miaka mingi!” Nilimwangalia mke wangu na kusema: “Anatutaka tu turudi katika kanisa letu la zamani!” Dada Zhang alitabasamu, akisema: “Hivi sasa, yote tunayoweza kuona ni kuonekana kwao kwa nje, lakini hatujaangalia katika kiini cha asili yao! Bwana Yesu wakati mmoja alisema: ‘Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie(Mathayo 23:13). ‘Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, nyinyi wanafiki! Kwani nyinyi ni kama makaburi yaliyopakwa rangi nyeupe, ambayo kwa nje yanaonekana mazuri sana, lakini ndani yake mna mifupa ya wafu, na yenye uchafu wote(Mathayo 23:27). Ukitazama kwa kuonekana kwao kwa nje, Mafarisayo walikuwa waaminifu sana katika utumishi wao kwa Mungu. Katika mawazo ya watu, Mafarisayo walikuwa watumishi waaminifu kwa Mungu, na ndio walikuwa viongozi wa kidini waaminifu zaidi. Hata hivyo, wakati Bwana Yesu alikuja kutekeleza kazi Yake, asili ya Mafarisayo ya kumpinga Mungu ilifunuliwa. Ilikuwa ni Mafarisayo hawa ambao walipinga na kuishutumu kazi ya Bwana Yesu. Walibuni kila aina ya uvumi na kutoa ushuhuda wa uongo kuwadanganya watu wa kawaida. Walisema kwamba Bwana Yesu alikuwa Amewafukuza pepo kupitia kwa Beelzebuli, mkuu wa mapepo. Na mara Bwana Yesu alipofufuliwa siku tatu baada ya kusulubiwa msalabani, waliwahonga askari kueneza uvumi kuhusu mwili wa Bwana Yesu kuibwa na wanafunzi Wake, miongoni mwa vitu vingine. Mafarisayo walibuni kila aina ya uongo na kutumia mbinu zote walizokuwa nazo kuwazuia watu kutotafuta na kuichunguza njia ya kweli. Lengo lao lilikuwa kuzuia kazi ya Mungu ili waweze kuwa na umiliki wa milele juu ya watu waliochaguliwa na Mungu. Ingawa walionekana kuwa waaminifu kwa nje, kwa kweli walikuwa wapinga Kristo ambao walichukia ukweli na waliosimama kama maadui kwa Mungu. Bwana Yesu alisema alipowafunua na kuwahukumu: ‘Ninyi nyoka, nyinyi kizazi cha nyoka, mnawezaje kuepuka laana ya jahanamu?(Mathayo 23:33). Kwa hivyo, hebu sasa tufikirie kulihusu: Je, hawa viongozi wa kidini wa leo ni tofauti na Mafarisayo?” Akina dada hao waliniambia nisome kifungu cha neno la Mwenyezi Mungu: “Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye ‘mwili imara,’ wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu). Dada hao walitupa ushirika wa kina kulingana na maneno haya ya Mungu, wakichanganua vitendo vyote vya viongozi wa kidini pamoja na kiini cha asili yao, mpaka hatimaye nilikuja kutambua kwamba wanatusumbua na kutuzuia bila kukoma kumwamini Mwenyezi Mungu, na hata kututishia na kutuogofya, si ili kutulinda, lakini badala yake ili waweze kutawala juu ya wateule wa Mungu, ili tuweze kuwaabudu na kuwasujudia kana kwamba wao Mungu. Hivyo kwa kweli, wao ni kama Mafarisayo tu. Wote ni wapinga Kristo ambao huchukia ukweli na wanamkataa Mungu. Mungu amekuja kutuokoa, lakini wanafikiria kila kiwezekanacho kutuzuia kukubali kazi ya Mungu na kutuzuia kusoma maneno ya Mungu. Je, si wao wanatuvuta chini kwenda Jahannamu kwa kufanya hivi? Kwa kweli wao ni wabaya sana! Isingekuwa kwa sababu ya maneno ya Mwenyezi Mungu kufunua kiini cha jinsi watu hawa wanavyompinga Mungu na kupigana na Mungu juu ya mwanadamu, basi ningekuwa karibu kudanganywa na ujanja wao, kuharibu nafasi yangu ya kupata wokovu wa kweli. Wakati huo tu, mke wangu alisema kwa mshangao: “Inaonekana kwamba wamekuja hapa kutudhuru! Watu hawa hawatakoma mpaka watuvute chini hadi Jahannamu! Sitaamini tena kile wanachosema.”

Dada Mu kisha alitusomea kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Kisha Dada Zhang akaanza kufanya ushirika: “Kupitia katika maneno ya Mungu tunaweza kuona kwamba, chochote kinachotutendekea, ingawa kutoka nje kinaweza kuonekana kufanywa na mwanadamu, kwa kweli ni Shetani anayeanzisha vita na Mungu kwa siri. Ni kama tu wakati ambapo Ayubu alijaribiwa na Shetani. Mke wake alimwomba amwache Yehova, lakini Ayubu aliweza kung’amua udanganyifu wa Shetani. Alitegemea imani yake kwa Mungu na kusimama kama shahidi kwa Mungu, na Ayubu alimkemea mkewe kwa kuwa mwanamke mjinga na mkaidi. Uzoefu wa Ayubu hutujulisha kwamba, kwa kila mtu ambaye Mungu anataka kumwokoa, Shetani atamjaribu mara kwa mara na kumvuruga na kutumia mbinu zote zilizopo kumshambulia ili amwache Mungu na kumsaliti Mungu, na hatimaye kupoteza nafasi yake ya kupata wokovu wa kweli. Kwa kuwa Shetani anataka kutudhibiti na kumwangamiza mwanadamu milele, kwa kweli hataki mwanadamu apate wokovu wa Mungu!” Dada Mu pia alitoa ushirika: “Ni kweli. Mara kwa mara, Shetani huwatumia viongozi kutushambulia na kututishia, akiwa na lengo la kutufanya tumkane Mungu, kumsaliti Mungu na kuiacha njia ya kweli. Huu ni udanganyifu wa Shetani. Lazima tuweze kuona wazi vita hivi vinavyoendelea katika ulimwengu wa kiroho.” Baada ya kusikiliza ushirika wa dada hawa wawili, nilitafakari juu ya mambo kwa muda, kisha nikasema, “Kwa hiyo Shetani anaanzisha vita na Mungu, na ni kupitia kwa mambo ambayo viongozi wanasema ndiyo Shetani hutushambulia pale tulipo dhaifu, na anataka tuiache njia ya kweli na kumwacha Mungu kwa sababu ya woga wetu! Hakika Shetani ni mdanganyifu!” Kisha mke wangu pia alisema, “Shetani ni mbaya sana! Kama hatungesikiliza maneno ya Mungu na ushirika wako, basi tungewezaje kujua kwamba huu ulikuwa mmoja wa mipango ya Shetani?” Nilisema kwa furaha, “Sasa kwa kuwa tunaelewa mambo haya, tunahitaji kumtegemea Mungu kupenyeza mzunguko uliokazwa wa Shetani, kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na kumwaibisha Shetani kwa vitendo vyetu vya utendaji!” Dada Zhang kisha akasema kwa furaha: “Ndugu, dada, kuanzia sasa kuendelea tuje pamoja mara kwa mara na kushirikiana kuhusu neno la Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo tunaweza kujitayarisha na ukweli zaidi ili siku moja tuweze kuwa na uhakika kuhusu kazi ya Mungu katika siku za mwisho na kuweka msingi katika njia ya kweli, nakisha hatutasumbuliwa na kila namna ya uvumi na udanganyifu wa wazi wa Shetani” Nilisema: “Vema! Ingekuwa bora kama ungeweza kuja kushiriki nasi mara kwa mara.” Dada Mu alitabasamu na kusema, “Basi hilo ndilo tutakalofanya.”

Mapema asubuhi siku chache baadaye, nilitoka kitandani na kuangalia nje ya dirisha na kuona kwamba kulikuwa na theluji kubwa iliyoanguka, na nikaanza kusugua mikono yangu pamoja bila kufahamu. Kisha, nilivaa kofia ya uzi na glavu za pamba na nikaenda ugani ili kufagia theluji. Nilipokuwa nimemaliza, nilirudi ndani na kufungua sehemu ya juu ya jiko ili kuweka moto wakati mke wangu alipokuwa akisafisha nyumba. Wakati huu ndugu mkubwa wa mke wangu na mkewe waliingia, na mara tu shemeji yangu alipoingia, alisema kwa sauti ya wasiwasi: “Kiongozi Wang na Mfanyakazi mwenza Guan walikuja hapa na kuwanenea mambo mengi, mngekosaje kuyasikiliza? Walituuliza hasa tuje hapa leo ili tujaribu kuwashawishi tena. Msiamini katika Umeme wa Mashariki tena. Ni viongozi wetu wanaowajibikia maisha yetu!” Baada ya kumsikia akisema hivi, nilisema kwa uthabiti: “Kama kwa kweli wanawajibikia maisha yetu, basi wanapaswa kutuongoza kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, na kukaribisha kurudi kwa Bwana!” Mke wangu kisha akasema waziwazi: “Wanafanya hivi kwa ajili yetu? Wanaogopa kwamba sote tukimwamini Mwenyezi Mungu basi hakutakuwa na mtu aliyeachwa wa kuwasikiliza.” Shemeji yangu alikasirika kwa namna fulani baada ya kusikia hili na kusema, “Nyote wawili mnawezaje kusema mambo kama hayo? Hawajamtaka mfanye kitu kingine chochote. Je, hawawataki tu mrudi kanisani? Nisikilize. Mnafikiria kwamba naweza kuwadhuru wakati familia zetu zina uhusiano wa karibu sana?” Ndugu wa mke wangu aliendelea, “Fikiria kuhusu jinsi nilivyokutendea kwa miaka. Unajua tumekutendea kiasi gani? Je, kweli una moyo wa kujitenga na sisi? Je, huhisi hatia?” Baada ya kuwasikia wawili hao wakisema mambo haya, nilihisi mwenye hasira sana, na niliwaza: “Kwa kweli wametusaidia sana, na sasa wanaona kwamba tunasisitiza kumfuata Mwenyezi Mungu. Hakika wanahisi kukwazika sana, lakini ni nini kinachoweza kufanywa? Wanaweza kuniambia niache njia ya kweli na kumsaliti Mungu, lakini haiwezekani kwangu kufanya hivyo, kwa maana najua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu. Lakini nikisisitiza kumwamini Mwenyezi Mungu, basi wao watafikiria nini kunihusu? Je, watasema kuwa sina shukrani?” Nilihisi hasirawakati huo tu, kana kwamba moyo wangu ulikuwa ukivutwa katika mielekeo miwili tofauti. Nilimwomba Mungu kwa kimya, nikimwomba Anipe suluhisho. Ghafla, nilifikiria juu ya maneno haya ya Mungu: “Mambo huwatokea watu wakati Mungu anawataka wasimame imara katika ushuhuda wao Kwake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Kisha nikatafakari juu ya maneno ambayo Dada Zhang na Dada Mu walikuwa wameshiriki nami siku chache kabla: Kila kitu kinachokufanyikia kinahusiana na mapambano ambayo yanapiganwa katika ulimwengu wa kiroho, na ni Shetani anayepigana vita na Mungu. “Leo ndugu ya mke wangu na shemeji yangu walijaribu kutumia uhusiano wetu ili kutuhimiza tumsaliti Mungu na kurudi kwenye dini yao, lakini hii ni moja ya mbinu za Shetani. Kama ningemsaliti Mungu ili kulinda hisia zangu za faragha, basi huko kungekuwa kweli kukosa shukrani na kungeonyesha kwamba ninakosa dhamiri. Kama sitaki kumkosea shemeji yangu, basi napaswa kushiriki naye injili ya Mungu ya siku za mwisho ili yeye pia apate fursa ya kupokea wokovu wa Mungu. Hii ndiyo njia pekee ya kuonyesha huruma ambayo ni lazima niwe nayo.” Nilipokuwa nafikiria kuhusu hili moyo wangu ulijawa na mwanga ghafla, na nikasema: Ndugu, shemeji, najua kwamba ninyi wawili mmekuwa wema kwangu, na kwa sababu ya hili ninahitaji kuwaambia kwamba Mwenyezi Mungu kwa kweli ni Bwana Yesu aliyerudi. Ni kwa kufuata kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho tu ndiyo tutaweza kupata wokovu wa Mungu! Vinginevyo, imani yetu katika Bwana miaka hii yote ingekuwa ya bure, na hatutapata kitu! Hebu niwasomee kifungu cha maneno ya Mungu, na baada ya kuyasikia mtajua kama maneno haya ni ukweli au la, na kama ni matamko ya Mungu au la Nilikichukua kitabu changu cha maneno ya Mungu na nilikuwa karibu tu naanza kukisoma wakati shemeji wangu alisimama na kusema kwa huzuni, “Tulikuja hapa leo kujaribu kuwashawishi, lakini badala ya kubadilisha mawazo yenu, mnajaribu hata kueneza injili hii kwetu, lakini hatutawasikiliza.” Baada ya kusema haya, alimchukua mumewe na kuondoka kwa kishindo kwa hasira.

Niliwafuata mpaka ugani hadi nilipofika kwenye njia ya kuingia, lakini niliona kwamba walikuwa wameshafika mbali. Nikihisi nisiye na msaada, nilisimama pale nikitikisa kichwa changu. Ilikuwa ni wakati huu ndipo niliona kwamba hali ya hewa ilikuwa imekuwa shwari, na kwamba mwanga wa joto ulikuwa unaangaza juu ya msonobari ulioko nje ya uga. Theluji iliyokuwa imekusanyika kwenye msonobari huo ilianza kuyeyuka, kana kwamba wakati huo huo mti ulikuwa tu umepitia ubatizo. Kinyume na theluji iliyoifunika ardhi, mti huo mrefu ulionyooka ulionekana wa kijani kibichi hasa. Nilihisi furaha sana, kana kwamba, kama vile msonobari huo, mimi pia nilikuwa nimepitia ubatizo wa upepo na theluji, na nilikuwa nimekua kutokana na rutubisho ya jua. Nilijua kwamba ilikuwa ni maneno ya Mungu ambayo yalikuwa yameniongoza kupita katika mzunguko uliokazika na kuwa na ushuhuda Kwake. Shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu!

Iliyotangulia: Ufanisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mwamko wa Roho Aliyedanganywa

Na Yuanzhi, BraziliNilizaliwa katika mji mdogo huko Kaskazini mwa China na mnamo 2010, nikafuata jamaa kwenda Brazili. Hapa nchini Brazili,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp