Kuwa katika Hatari Kubwa

28/12/2019

Nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Mchungaji na wazee hawajaacha kunisumbua na kuwashawishi wazazi wangu wanizuie pia. Ninahisi udhaifu kidogo na sijui jinsi ya kushinda haya. Ee, Ndugu Zhang, nilisikia kwamba ulitatizwa na mchungaji fulani kwa njia hii hii mara baada ya kukubali hatua hii ya kazi ya Mungu. Je, ulishindaje hilo?

Maneno ya Mungu yalinielekeza katika kila hatua. Mnamo 2005, muda mfupi baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, nilishiriki injili na ndugu mmoja kutoka kanisa langu la zamani. Kisha alasiri moja, Mchungaji Li na mfanyakazi mwenza Wang walifika nyumbani kwangu. Moyo wangu ulikuwa ukipapa. Nilijiuliza, “Wamekujia nini? Je, wanajua kwamba nimemkubali Mwenyezi Mungu? Washiriki wengine wa kanisa walipomkubali Mwenyezi Mungu, walizua uvumi, wakawatisha na kushawishi familia zao zipinge imani yao. Je, watatumia mbinu za aina gani dhidi yangu?” Wanangu wawili waliwasili baadaye kidogo. Nilishangaa. Watoto wangu walikuwa wamesema kwamba walikuwa na shughuli nyingi, hivyo kwa nini wote wawili waje leo? Je, Mchungaji Li alikuwa amepanga hayo? Niligundua kwamba walikuwa wamejiandaa kwa ajili ya haya mapema. Nilimwomba Mungu mara moja: “Ee Mungu, sijui watanijaribu kwa kutumia mbinu gani. Kimo changu ni kidogo sana kiasi kwamba sijui jinsi ya kukabiliana na jambo hili. Tafadhali niongoze na Unisaidie ili nisalie imara katika njia ya kweli.” Nilitulia zaidi baada ya kuomba.

Wakati huo huo, Mchungaji Li alitabasamu na kusema, “Ndugu Zhang, nimesikia kwamba umekubali Umeme wa Mashariki sasa. Je, hiyo ni kweli? Bila kujali Umeme wa Mashariki lina ukweli kiasi gani, hatuwezi kulikubali. Sote tumemwamini Bwana kwa miaka mingi na tumemfanyia kazi ya kuhubiri. Sote tunajua kwamba Bwana Yesu alisulubiwa na kuwa sadaka ya dhambi, ambayo ilituokoa kutokana na dhambi zetu. Lazima tutetee jina na njia ya Bwana wakati wote. Hatuwezi kumwamini Mungu mwingine. Kwa kumwacha Bwana Yesu na kumwamini Mwenyezi Mungu, je, humsaliti Bwana?”

Nilitulia na kusema kwa upole, “Mchungaji Li, lazima tusiwe na upendeleo na tuwe na busara. Lazima tufuate ushahidi na tusilishutumu kiholela. Hujachunguza njia ya Umeme wa Mashariki au kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo unawezaje kuamua kuwa ninamsaliti Bwana kwa kukubali Umeme wa Mashariki? Je, unajua ukweli unatoka wapi? Je, unajua ni nani anayeonyesha ukweli? Bwana Yesu alisema, ‘Mimi ndiye njia, ukweli na uhai(Yohana 14:6). Mungu ndiye chanzo cha ukweli. Unawezaje kusema kwamba bila kujali Umeme wa Mashariki lina ukweli kiasi gani, hatuwezi kulikubali? Je, huko si kupinga ukweli na kumpinga Mungu kwa makusudi? Je, sisi hata ni waumini wa Bwana?” “Nimesoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu hivi karibuni, na nimeona kwamba yote ni ukweli na kwamba yanafichua ukweli na siri nyingi. Masumbuko yangu yote niliyokuwa nayo katika miaka mingi ya kuamini imetatuliwa kupitia maneno ya Mwenyezi Mungu. Naamini kwa uthabiti kuwa Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu. Kumfuata Mwenyezi Mungu ni kukaribisha ujio wa Bwana!” “Mnasema kwamba kumwamini Mwenyezi Mungu ni kumsaliti Bwana Yesu. Je, hiyo inakubaliana na ukweli? Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi, watu wengi sana waliondoka hekaluni ili wamfuate. Je, hiyo inamaanisha kwamba walimsaliti Yehova Mungu?” “Ingawa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi ilikuwa tofauti na kazi ambayo Yehova Mungu alifanya ya kutoa sheria, na jina la Mungu lilibadilika pia, Bwana Yesu na Yehova ni Mungu mmoja. Kwa kumwamini Bwana Yesu, hawakuwa wakimsaliti Yehova Mungu, bali walikuwa wakifuata nyayo za Mwanakondoo na kupata wokovu wa Mungu.” “Kwa kweli, wale ambao walimwamini Yehova Mungu bali hawakumkubali Bwana Yesu ndio waliokuwa wakimwacha Mungu na kumsaliti.” “Kazi ya Mwenyezi Mungu ni tofauti na ya Bwana Yesu na jina la Mungu limebadilika, lakini Wao ni Mungu mmoja. Mungu hufanya tu kazi tofauti katika enzi tofauti. Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, ambayo ilikuwa tu kusamehe dhambi zetu. Hakutatua asili ya wanadamu yenye dhambi. Hii ndiyo sababu Aliahidi kwamba Atakuja tena kufanya kazi ya hukumu. Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho akionyesha ukweli ili kutuhukumu juu ya msingi wa kazi ya Bwana ya ukombozi ili kutatua tabia zetu za kishetani na asili yetu yenye dhambi na kutuokoka kikamilifu kutokana na dhambi ili tuweze kupatwa na Mungu. Kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu yanatimiza kabisa unabii wa Bwana Yesu.” “Kumwamini kwangu Mwenyezi Mungu si kumsaliti Bwana Yesu. Ni kufuata nyayo za Mwanakondoo. Je, kumwamini Bwana Yesu bila kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku ya mwisho hakutatufanya tuwe tu kama Mafarisayo, ambao walimwamini tu Yehova Mungu na wakamkataa Bwana Yesu? Ni watu kama hao wanaompinga na kumsaliti Bwana!” “Mnapaswa kuchunguza vizuri kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na mjionee wenyewe kama maneno Yake ni sauti ya Mungu. Msiihukumu wala kuishutumu kiholela, la sivyo, mnaweza kushutumiwa kwa kumpinga Bwana!”

Mchungaji Li alionekana kuwa na wasiwasi sana, kwa hivyo mfanyakazi mwenza Wang alilainisha mambo upesi: “Tunapinga Umeme wa Mashariki na hatutaki washiriki wetu wahusike nao ili tulinde kanisa na kulichunga kundi la kondoo. Je, Bwana anawezaje kutushutumu kwa ajili ya hilo? Mchungaji Li anahisi kwamba anawajibikia maisha yako. Hataki uchukue njia ambayo si sawa! Umekuwa mfanyakazi mwenza na umelifanyia kanisa mambo mengi sana. Kila mtu anakuheshimu na kukuamini. Wote watasikitika sana ukiondoka na kwenda kumwamini Mwenyezi Mungu!” Mchungaji Li aliingilia mazungumzo hayo upesi, “Mfanyakazi mwenza Wang amesema ukweli. Umefanya kazi kwa bidii miaka hii yote. Litakuwa jambo la kusikitisha sana kuondokea sifa ambayo umejipatia! Rudi. Kila mtu anakungojea. Kanisa letu limeanzisha makao ya kustaafu, tumeungana na makundi ya kidini ughaibuni na yanatupa msaada wa kifedha. Ukirudi, tutakupa gari mara moja. Kama ungependa kusimamia makao ya kustaafu au kulisimamia kanisa, au kuendelea kusimamia fedha za kanisa, hayo yote ni juu yako.”

Kadiri nilivyozidi kuwasikiliza, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba kulikuwa na tatizo. Waumini wanawezaje kusema jambo kama hilo? Nilikumbuka jinsi Shetani alivyomjaribu Bwana Yesu katika Biblia: “Tena, Ibilisi akampeleka hadi kwenye mlima mrefu sana, na kumwonyesha falme zote za dunia, na fahari yao; Na akasema kwake, Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu” (Mathayo 4:8-9). Je, mambo hayo yote waliyokuwa wakisema hayakuleta hisia ile ile na hayakusemwa kwa sauti ile ile kama ya Shetani? Niliwaza, “Huu ni ujanja wa Shetani!” “Wananishawishi niache njia ya kweli kwa kutumia hadhi na pesa ili nimsaliti Mwenyezi Mungu. Wanajaribu kuninasa na kuniangamiza!” Nilikuwa muumini kwa zaidi ya miaka 10 na nilikuwa na bahati nzuri sana ya kukaribisha kurudi kwa Bwana. Nilijua kwamba sikupaswa kudanganywa na Shetani na kumsaliti Bwana. Kwa hivyo nilisema, “Nimesikia sauti ya Mungu na nikapata njia ya uzima wa milele. Nachagua kumfuata Mungu. Maneno yenu hayatanibadilisha nia. Sitamwacha Mwenyezi Mungu.”

Kisha binti yangu akaanza kulia akisema, “Baba, nisikilize tu kidogo! Mama aliaga dunia hivi karibuni. Tumeteseka kiasi cha kutosha. Ukiamini Umeme wa Mashariki na ufukuzwe kanisani, kina ndugu watajitenga nasi pia!” Nilichukia kumwona binti yangu akilia vile. Mapambano makali yaliibuka ndani yangu. “Nikikubali kujiunga tena na kanisa, sitadharauliwa na nitasalia na cheo changu, lakini huko kutakuwa kumfungia Bwana mlango. Huo utakuwa usaliti mkubwa!” Hakukuwa na uchaguzi uliokuwa rahisi. Katikati ya maumivu haya, nilimlilia Mungu kimyakimya: “Ee Mwenyezi Mungu, nipo katika hali ya mtanziko. Tafadhali nipe imani na nguvu ili niepuke kusumbuliwa, na ili niweze kuwa na msimamo na kukufuata kwa uthabiti.” Baadhi ya maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo nilikuwa nimeyasoma siku chache kabla ya hayo yalinijia akilini wakati huo: “Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo(Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa nguvu na kunitahadharisha kuwa nilihitaji kutenda utambuzi. Ujanja wa Shetani ulisababisha yale niliyokabiliwa nayo siku hiyo. Shetani alikuwa akitumia hadhi na uhusiano wa kifamilia kujaribu kunishawishi, kunishambulia na kunivuruga mawazo kwa lengo la kunifanya nimsaliti Mungu. Sikunaswa na mtego wa Shetani! Niliwaambia watoto wangu, “Nimechunguza jambo hili na ni dhahiri kabisa. Mwenyezi Mungu ni Mungu wa kweli na maneno na kazi Yake ndiyo njia ya kweli. Tumekuwa tukitamani sana kuja kwa Bwana miaka hii yote. Sasa kwa kuwa Amekuja na Anaonyesha ukweli kwa ajili ya kazi Yake ya hukumu, hatuna budi kuendelea sawa na kazi Yake na kukubali hukumu na utakaso wa Mungu ili tuweze kuepuka maafa na tuingie katika ufalme wa Mungu. Hatupaswi kuogopa kukataliwa na wengine, bali tuogope kuondolewa na Bwana na kukosa nafasi ya kunyakuliwa. Wakati huo, tutakuwa tukilia na kusaga meno yetu katika maafa makubwa!” “Mnapaswa kuangalia maneno ya Mwenyezi Mungu. Mtasikia sauti ya Mungu ndani ya maneno hayo. Kisha mtathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Kristo wa siku za mwisho!” Watoto wangu waliacha kusisitiza suala hilo, na nikashukuru kimyakimya kwa ajili ya mwongozo wa Mungu.

Hawakuweza kubadili mawazo yao, lakini waliondoka kwa hasira. Walirudi siku chache baadaye kunishawishi kwa kutumia ndoa iliyokuwa na uwezo wa kufanyika. Mchungaji Li alisema, “Umepoteza mke wako, binti yako ameolewa na mara nyingi mwanao hayupo karibu. Hakika ni vigumu sana kwako kukaa peke yako. Kwa kweli, unapaswa kuwa na mtu hapa atakayekupikia. Dada Wang kanisani pia hana mwenzi. Yeye ni tajiri, anapendwa sana na mwenye shauku katika imani yake. Je, halitakuwa jambo zuri iwapo ninyi wawili mtaungana, muishi pamoja na kumtumikia Bwana pamoja?” Dada Wang alinipigia simu jioni hiyo na aliendelea kunihimiza nisiamini katika Umeme wa Mashariki. Alisema pia kwamba iwapo nilipungukiwa na pesa za harusi ya mwanangu, nilihitaji tu kumwambia. Nilikanganyikiwa sana niliposikia haya. Mke wangu alipokuwa mgonjwa kitandani, binti yetu alipata ajali ya gari alipokuwa akimletea dawa. Ajali hiyo ilifanya alazwe hospitalini. Dada Wang alikuja kumtunza mke wangu na binti yangu. Nilimshukuru sana kila mara. Je, nitamsononesha Dada Wang nisipokubali ushauri wake? Lakini kwa kukubaliana naye ili kulinda uhusiano wetu nitakuwa nikimsaliti Bwana. Nilihangaika sana na nikamwomba Mungu mara nyingi. Nilikanganywa na jambo hilo kwa muda kidogo, halafu nikamkatalia kwa uangalifu mno.

Siku moja, Mchungaji Li alinijia nilipokuwa nikifanya kazi mashambani. Alisema, “Ndugu Zhang, iwapo hutajifikiria, fikiri kuhusu watoto wako. Mwanao amechumbia na familia nzima ya mchumba wake inamwamini Bwana. Wakigundua kuwa unamwamini Mwenyezi Mungu, je, bado watamruhusu aolewe katika familia yako? Je, hilo halitaathiri vibaya ndoa ya mwana wako? Unapaswa kufikiria hilo zaidi.” Niliposikia hilo, niliwaza, “Unanitisha kwa kutumia harusi ya mwanangu ili kunizuia nisifuate njia ya kweli. Jambo hilo linastahili dharau!” Nilisema waziwazi, “Imani yangu katika Mwenyezi Mungu ni wajibu wangu mwenyewe. Haihusiani kabisa na harusi ya mwanangu. Mbali na hilo, iwapo harusi yake itafaulu, hilo limo mikononi mwa Mungu. Nimebaini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi na nitamfuata mpaka mwisho. Watoto wangu hawaelewi, lakini siku moja wataelewa.” Mwanzoni nilidhani kwamba Mchungaji Li alikuwa akiongea tu, lakini ajabu ni kwamba, kwa kweli alikuwa akitumia jambo muhimu kama hili kunifanya nimsaliti Mwenyezi Mungu.

Nilikwenda kwenye duka la mwanangu la kutia weko siku chache baadaye. Alikunja uso wake na kusema, “Baba, mchumba wangu alisema kwamba Mchungaji Li alikwenda kutembelea familia yake na aliwaambia kwamba unaamini katika Umeme wa Mashariki. Alisema kwamba usipoacha kuamini, harusi haitafanyika.” Nilipigwa na butwaa na nikaghadhabika. Mchungaji Li alikuwa akitumia ndoa ya mwanangu kunitisha kwa kweli. Je, muumini wa Bwana anawezaje kufanya jambo kama hilo linalostahili dharau? Nilihisi vibaya nilipomwona mwanangu akiwa amekata tamaa sana. Zilikuwa zimesalia siku 18 kabla ya tarehe ya harusi. Je, itavunjika kwa njia hiyo kwa kweli? Machozi yalijaa machoni mwangu. Aliendelea, “Baba, alisema pia kwamba ana masharti matatu ya kufunga ndoa. Kwanza ni kuvunja uhusiano wetu wa baba na mtoto. Pili ni kukosa kukutunza katika uzee wako. Tatu ni kuvunja uhusiano wote wa kifamilia. Mama yangu hayupo tena nasi. Tafadhali acha kuamini katika Umeme wa Mashariki kwa ajili ya familia yetu.” Kusikia maneno ya mwanangu na kuona uso wake ukiwa umejaa uchungu kuliumiza sana moyo wangu. Kwa sababu tu nilimwamini Mwenyezi Mungu, hawa wachungaji walikuwa wakinitendea kama adui, wakimlazimisha mwanangu avunje uhusiano nami. Jambo hilo linachukiza! Nilimwambia mwanangu, “Mwanangu, wewe ni mtu mzima sasa na huhitaji nikutunze. Mimi ni mkongwe. Nataka tu kutenda imani yangu na kumfuata Mungu katika siku zangu zote. Natumai kwamba unaelewa.” Baada ya hayo, niligeuka na kutoka dukani. Kule nyumbani, nilikuja mbele za Mungu kuomba: “Mwenyezi Mungu! Mchungaji anatumia kila hila kunisumbua na kunionea. Mwanangu atavunja uhusiano wote na mimi. Ninahisi dhaifu sana hivi sasa. Tafadhali niongoze na Unipe imani.”

Ndugu Lin kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu alikuja kwangu siku iliyofuata na nikamwambia kilichokuwa kikiendelea. Alinisomea kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu. “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. … Kila kitu wafanyacho watu kinawahitaji kulipa gharama fulani katika juhudi zao. Bila taabu ya kweli, hawawezi kumridhisha Mungu, hata hawakaribii kumridhisha Mungu, na wanarusha tu maneno matupu!(Neno Laonekana katika Mwili). Alipozungumza juu ya vita vya kiroho katika muktadha wa maneno haya kutoka kwa Mungu, nilielewa kwamba tunapozuiwa, kusumbuliwa na kuonewa na wachungaji, inaweza kuonekana kana kwamba hayo yanafanywa na watu, lakini kwa kweli, ni Shetani anayejaribu kutuvuruga. Kila Mungu anapofanya kazi, Shetani huwa pale akiingilia. Shetani huchukia kazi ya Mungu ya kuokoa wanadamu, kwa hivyo yeye hutumia mbinu na hila za aina yote kuwazuia watu ili wasimfuate Mungu, ili kuwapeleka watu kuzimuni pamoja naye. Mchungaji Li na wale wengine walijaribu kunizuia ili nisifuate njia ya kweli na walinisumbua mara kwa mara, wakisema kwamba watanipa gari, wataniruhusu nisimamie pesa za kanisa au makao ya kustaafu. Pia waliahidi kunitafutia mke. Wakati ambapo hayo hayakufaulu, walitumia harusi ya mwanangu kunitisha. Walijaribu kutumia vitisho na hongo. Jambo hilo lilikuwa baya na bovu sana.

Ndugu Lin alishiriki ushirika zaidi: “Bwana Yesu alipoonekana na kufanya kazi, viongozi wa imani ya Kiyahudi walichukia ukweli na kumchukia Mungu. Walijua vizuri kwamba njia ya Bwana Yesu ilikuwa yenye mamlaka. Mbali na wao kukataa kuichunguza, pia walimpinga, wakamshutumu na kumkufuru vikali. Walifanya kila waliloweza kuwazuia watu ili wasimfuate na wakashiriki katika kusulubiwa Kwake. Walifanya hivi kwa sababu waliogopa kwamba wangepoteza hadhi na riziki yao iwapo watu wangemfuata Bwana Yesu. Kama ilivyoandikwa katika Biblia, ‘Kisha makuhani wakuu na Mafarisayo walikonga baraza, na wakasema, Tufanye nini? Kwani mtu huyu anatenda miujiza mingi. Tukimwacha hivi peke yake, watu wote watamsadiki: nao Warumi watafika na kuichukua nafasi yetu na taifa letu. … Hivyo kuanzia siku hiyo walishauriana pamoja ili wamuue’ (Yohana 11:47, 48, 53). Mungu amekuja katika siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu. Wachungaji wa dini wanajua kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, lakini hawatafuti wala kuyachunguza. Wao hata humpinga na kumshutumu vikali na huwazuia wengine kumfuata Yeye. Je, kiini chao kina tofauti gani na cha Mafarisayo ambao walimpinga Bwana Yesu?” “Bwana Yesu aliwashutumu na kuwalaani wanafiki hao zamani. Bwana Yesu alisema, ‘Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie(Mathayo 23:13). ‘Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko(Mathayo 23:15). Maneno ya Mwenyezi Mungu pia yanafunua kiini na chanzo cha upinzani wa viongozi wa dini kwa Mungu.” Mwenyezi Mungu anasema, “Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye ‘mwili imara,’ wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?(Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, nilielewa vyema zaidi asili ya kishetani ya viongozi wa dini ya kuchukia ukweli na kumpinga Mungu. Wao humpinga na kumlaani Mwenyezi Mungu kwa ghadhabu na huwatesa kina ndugu wanaoshuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa sababu wanataka kuendelea kuwatawala kondoo wa Mungu milele. Wanataka kondoo wa Mungu wawe wao na wawadhibiti kwa uthabiti. Wao huwazuia waumini kufanya kile wasichoweza kufanya—kuingia katika ufalme wa Mungu. Wanaenda kuzimuni na wanawapeleka wengine humo pamoja nao. Wao kwa kweli ni kundi la pepo wabaya! Nisingejionea juhudi za wachungaji hao za kunizuia, isingekuwa Mungu mwenye mwili kuonekana na kufanya kazi katika siku za mwisho, kuwafunua watumishi hao waovu na wapinga Kristo wanaojificha makanisani, nisingeona kamwe kiini chao cha kishetani cha kumpinga Mungu. Ningekuwa nimepotoshwa na kuangamizwa nao bila kujua. Niliona sura zao mbaya na za kinafiki na imani yangu ya kumfuata Mwenyezi Mungu ikaimarika.

Niliendelea kushiriki injili na kina ndugu kutoka kanisa langu la zamani. Tulipokuwa mkutanoni asubuhi moja, Mchungaji Li na wafanyakazi wenzake walikuja nyumbani kwangu tena, na akasema, “Tumekwambia mara nyingi kwamba uache Umeme wa Mashariki. Mbali na kukataa kusikiliza, pia unawaiba kondoo wangu na kuwahubiria Umeme wa Mashariki. Je, unataka kweli kushindana nami?” Nilisema, “Mchungaji Li, si sawa kusema hivyo. Kanisa ni la Mungu na kondoo ni Wake pia. Wewe ni mchungaji tu. Unawezaje kusema kwamba kondoo ni wako?” “Ninashiriki injili na kina ndugu ili waweze kusikia sauti ya Mungu na kurudi mbele ya kiti Chake cha enzi. Jambo hili ni sawa na sahihi. Kwa nini ulizuie? Watu wote wanahisi kwamba wao ni dhaifu na hasi. Roho zao zina kiu na zimo gizani. Hawapati riziki yoyote ya maisha. Mwenyezi Mungu ametamka maneno na kutupa njia ya uzima wa milele. Kwa nini hutaki watu wayasome? Kwa nini uwanyime watu haki na uhuru wao wa kuchunguza njia ya kweli? Kwa kuwazuia kuchunguza, je, huwaachi wafe kwa sababu ya kiu na kuwaacha wakiwa wamekwama katika dini? Je, huko ni kuwa mtumishi mzuri au mtumishi mwovu?” Uso wa Mchungaji Li ulibadilika mara moja na akasema kwa sauti kuu na kwa ghadhabu, “Naona kwamba huwezi kusaidika. Ikiwa hutatufuata katika imani yako, subiri tu, utaadhibiwa kuzimuni!” Nilisema, “Huwezi kuamua iwapo nitaenda kuzimuni. Hujui hata jinsi ya kutambua sauti ya Bwana au kumkaribisha. Unawezaje kuwaongoza wengine kwenda katika ufalme Wake?” “Kristo wa siku za mwisho pekee ndiye lango letu la kuingia katika ufalme wa mbinguni. Nimepata njia ya uzima wa milele kupitia Kwake. Mungu ndiye anayewajibikia maisha yangu upo, si wewe.” Waliondoka kwa huzuni baada ya mimi kusema hivyo. Hakuna mtu aliyekuja kunisumbua tena.

Nilipata utambuzi kiasi juu ya ujanja wa Shetani baada ya kushinda vita hivi vya kiroho. Niliona pia kuwa wachungaji na wazee katika dini ni Mafarisayo wanafiki tu, na kwamba wao ni wapinga Kristo ambao humkana na kumpinga Kristo. Niliondokana kabisa na shutuma zao. Maneno ya Mwenyezi Mungu yaliniongoza katika kila hatua ya kumshinda Shetani na kusimama kidete kwenye njia ya kweli. Ninamshukuru Mungu kwa kweli! Ninapokumbuka yote niliyopitia, yote yalikuwa jaribio kubwa. Nilikuwa katika hali hatari sana. Nisingekuwa na mwongozo wa maneno ya Mungu, nisingeweza kubaini ujanja wa Shetani. Kama ningefuata mwili na kukubali kumtii Shetani na kutoka kwenye njia sahihi, huo ungekuwa usaliti mkubwa kwa Mungu. Ningekuwa nimekosea tabia ya Mungu na kupoteza kabisa nafasi yangu ya wokovu. Kwa kweli nilikuwa katika hatari kubwa! Ninashukuru sana kwa ulinzi na wokovu wa Mungu!

Kusikia hadithi yako kumenipa utambuzi kiasi. Sasa najua jinsi ya kuwakabili wachungaji wa kanisa. Shukrani kwa Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kupotea na Kurejea Tena

Na Xieli, MarekaniNilikuja Marekani kufanya kazi kwa bidii kama vile ningeweza kutafuta maisha yenye furaha na hali ya juu ya maisha....

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp