Kijani Kidogo cha Nyasi Kilichokua Miongoni mwa Mikwamba

24/12/2019

Na Yixin, Singapuri

Katika Novemba ya mwaka wa 2016 nilifahamiana, kupitia Facebook, na Ndugu wa kiume, Lin, na kina Dada Zhang na Xiaoxiao wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Waliunganisha baadhi ya unabii katika Biblia, kufanya ushirika nami na kuwa na ushuhuda wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Kufanya kwao ushirika na ushuhuda kulinifanya kuelewa kwamba Mwenyezi Mungu anafanya kazi ya kuwahukumu na kuwatakasa watu kupitia kwa maneno kwa misingi ya kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu. Mwenyezi Mungu anatamani kuwaokoa wanadamu kabisa kutoka kwa nguvu za Shetani na kutuondolea tabia yetu ya upotovu ili tusiasi tena dhidi ya Mungu na kumpinga Mungu lakini badala yake tuwe watu wanaomtii na kumwabudu Yeye kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu nilikuja kuelewa kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho itafichua ngano yote na magugu, kondoo na mbuzi, wanawali wenye hekima na wanawali wajinga, ili kwamba kila kimoja kitaishia na aina yake mwenyewe na wema utatuzwa ilhali uovu utaadhibiwa. Nilitambua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu ambako nilikuwa nikisubiri na kwa furaha niliikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.

Siku moja, Dada Zhu kutoka dhehebu langu la asili aliniuliza bila kutarajiwa kile kilichokuwa kikinipa shughuli nyingi siku za karibuni, na hivyo nikamwambia kuwa nilikuwa nikichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Dada Zhu alikuwa na mambo mengi mabaya ya kusema kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu na pia alimkufuru Mwenyezi Mungu. Alinihimiza nisijihusishe nalo kwa vyovyote. Nikasema: “Nimekuwa nikiwasiliana na baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa muda sasa na nimefurahia kubadilishana mawazo nao. Wana njia mpya na ya wazi ya kushiriki ukweli na nimeelewa ukweli mwingi kwa kuwasikiliza. Nimekua sana, na kunufaika sana, na bila shaka hawako ulivyowasifia kuwa. Na maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya vitendo sana na yametatua fadhaa nyingi nilizohisi kuhusu masuala fulani. Maneno hayo yameyapa maisha yangu riziki na yamenionyesha njia ya vitendo …” Baada ya kuona kwamba mtazamo wangu ulikuwa usiokubali kushindwa, Dada Zhu alibadilisha suala hilo na kuniuliza kama ningemwambia Dada Yun—aliyetuhubiria injili ya Bwana—kuhusu uchunguzi wangu katika kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Nikamwambia: “Bado kuna vitu vingi ambavyo sivielewi, lakini nitakapomaliza kuichunguza nitamwambia kila mtu kile nimegundua.” Akakubali kwamba ni lazima niwe na ufahamu mzuri kabla ya kusema chochote kwa Dada Yun.

Kwa hiyo nilishangaa siku 5 baadaye bosi wa duka la urembo nilikofanya kazi aliponijia na kusema: “Yixin, Yun ameniuliza nikuombee. Kwa hakika, sijui jinsi ya kuomba lakini nitafanya liwezekanalo …” Niliposikia hayo mara moja nilitambua kuwa Dada Zhu alikuwa amemwambia Dada Yun kuhusu uchunguzi wangu katika kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Nilihisi kwamba Dada Zhu hakuwa ametenda kwa tabia ya maadili sana, na nilikasirika naye kiasi. Nilihisi kwamba alikuwa amenidanganya na kunisaliti, na nikaanza kuhisi kwamba hata ndugu zangu wa kiume na wa kike katika Bwana hawakuwa waaminifu … lakini nilipokuwa tu nikifikiria hivi bosi wangu, bila kushauriana nami kuhusu cho chote, alivuta nadhari ya wenzangu takribani dazani moja katika duka hilo la urembo na kuwaambia kuwa sikuwa Mkristo mzuri na kwamba niliitembea njia ya kukengeuka. Aliendelea kusema vitu vingi vya kulihukumu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Haya yote yalitokea kwa haraka sana kiasi kwamba sikujua jinsi ya kujibu, na nilifadhaika sana. Kwa hiyo nilijiombea kimya kimya: “Bwana, wamesikia kwamba umerejea kwa hiyo ni kwa nini hawana haja na uchunguzi? Kwa nini wanasikiliza uvumi wa mtandaoni tu na kusema mambo hayo yote yanayokupinga na kukuhukumu? Mwenyezi Mungu ameelezea ukweli mwingi sana, hivyo si hilo linathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ni kurudi Kwako? Kwa nini wanapinga sana kuamini kwangu katika Mwenyezi Mungu? Inaweza kuwa ni mimi ambaye nina makosa? Ee Bwana, sijui cha kufanya. Tafadhali niongoze na kunielekeza …”

Siku nyingine baadaye, nikamwambia Ndugu Lin kilichokuwa kimetokea siku hiyo. Ndugu Lin akanitafutia vifungu viwili vya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Shetani daima anagugumia maarifa ambayo wanadamu wameshikilia kunihusu mioyoni mwao, na daima, kwa meno na makucha wazi, akishiriki kwa maumivu ya mwisho ya mapambano yake ya kifo. Je, unataka kukamatwa na mipango yake danganyifu wakati huu? Unataka, wakati awamu ya mwisho ya kazi Yangu imekamilika, kukata maisha yako mwenyewe? Hakika bado hunisubiri Nisambaze huruma Yangu mara moja tena? Kutaka kunijua ni jambo muhimu, lakini hupaswi pia kupuuza kuwa makini kwa mazoezi halisi. Nafichua ufahamu kwako moja kwa moja kwa maneno Yangu, kwa matumaini kwamba utaweza kuukubali mwongozo Wangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 6). Ndugu Lin alifanya ushirika juu ya vifungu hivi kwa njia hii: “Tunaweza kuona kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba kile kilichokutokea kilikuwa ni vita vya kiroho na ulikabiliwa na majaribu ya Shetani. Katika siku za mwisho, Mungu amekuwa mwili wa mwanadamu ili kuongea na kuwaokoa watu. Kutoka kwa maneno ya Mungu tunaweza kuuelewa ukweli, kuijua kazi ya Mungu, kuijua tabia ya Mungu, na kumtelekeza kabisa Shetani na kurudi kwa Mungu. Tunaweza kupata wokovu na kupatwa na Mungu. Shetani daima hufuata nyuma ya Mungu ili kujaribu na kuivunja na kuivuruga kazi ya Mungu. Shetani humtumia yeyote anayeweza kubuni uvumi ili kumkashifu na kumhukumu Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, na kutuzuia kuja mbele ya Mungu. Viongozi wa kidini na wakana Mungu walio katika vyeo vya mamlaka ni mfano halisi wa Shetani, na kila wakati Mungu anapokuwa mwili duniani ili kufanya kazi Yake wao humpimga na kumhukumu Yeye, kuvuruga kazi Yake, na kuwazuia watu kumfuata Yeye. Bwana Yesu alipofanya kazi Yake, makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa wakati huo walipewa jukumu na Shetani kufanya lolote waliloweza ili kuihukumu na kuipinga kazi Yake. Walieneza uvumi wa uongo, wakafanya ushuhuda wa uwongo, na kumkashifu na kumkufuru Yeye. Walidai kwamba Bwana Yesu alikuwa akiwafukuza pepo kupitia Beelzebuli; walisema kuwa Bwana Yesu alikuwa akiwashawishi wananchi wa mahali palepale wasilipe kodi kwa Kaisari; waliwahonga askari fulani kutoa ushahidi wa uongo ukisema kwamba Bwana Yesu hakuwa amefufuka na kwamba mwili Wake ulikuwa umechukuliwa kwa siri na wanafunzi Wake. Wakati Mungu wa siku za mwisho alipokuwa mwili ili kufanya kazi Yake mpya, serikali ya Kikomunisti ya China, ambayo inajaribu kugeuza China kuwa nchi ya wakana Mungu, pamoja na wachungaji wengi na wazee wa kanisa ambao wanataka kulinda riziki zao na hadhi yao, walianza kueneza uongo mwingi na ushuhuda wa uongo kuhusu Mwenyezi Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu ili kuwahadaa, kuogofya na kuwazuia watu kuichunguza na kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Watu wengi ambao hawauelewi ukweli, na hawawezi kutambua vizuri, bila kufikiria huamini uvumi huu na kufuata amri za Shetani kwa kueneza uongo huu unaowasumbua wengine na kuwazuia kukubali njia ya kweli. Watu kama hao huwa washiriki waovu ya Shetani ambao humpinga Mungu. Kwa hiyo, lazima tugundue asili ya kweli ya serikali ya Kikomunisti ya kukana Mungu, ambayo ni adui wa Mungu, na tugundue asili ya kweli ya wachungaji hao na wazee wa kanisa ambao huwazuia watu kuichunguza kazi ya Mungu, kwa kuwa wao ni Mafarisayo wa nyakati zetu. Lazima tuone kwamba uvumi wote kwa mtandao ni sehemu ya hila ya Shetani ili kutuzuia kurudi kwa Mungu. Ikiwa tunataka kuchunguza njia ya kweli, basi tunapaswa kusikiliza tu maneno ya Mungu na hakika hatupaswi kusikiliza uvumi wa Shetani kabisa. Hivi ndivyo tutakavyoweza kusimama upande wa Mungu wakati wa vita vya kiroho na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na sio kunyakuliwa na Shetani …”

Ushirika wa Ndugu Lin unisaidia kuzielewa asili za uvumi huu. Sasa ninaelewa kuwa madhumuni ya Shetani katika kueneza uvumi na kuvuruga na kuweka vikwazo mbele yangu ni kunizuia kupata wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Baada ya kufikiri zaidi juu ya jambo hili, nilitambua kwamba watu hawa ambao walikuwa wakinishambulia hawakuwa wamesoma kamwe maneno ya Mwenyezi Mungu, hawakuwa wamechunguza kamwe kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na walikuwa wakisikiliza tu uvumi kwa ujinga na kumpinga na kumhukumu Mwenyezi Mungu. Mawazo yao yamevurugwa kabisa na Shetani na wanafuata amri za Shetani na kumpinga Mungu bila hata kulijua. Mtu mwenye hekima kwanza angeyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu kwa uangalifu sana na kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kufikia uamuzi. Lakini imani katika Mungu ni jambo kubwa, na pia niliogopa kuchukua njia mbaya, hivyo bado nilikuwa na wasiwasi kiasi katika moyo wangu. Baada ya kurudi nyumbani kutoka kazini, nilimwomba Bwana nikiwa na machozi machoni mwangu: “Ee Bwana, nimepotea sana na kuchanganyikiwa, lakini sitaki kuwa muumini kipofu katika kile wanachosema wengine. Ninataka kutenda kulingana na nia Yako, kwa hiyo tafadhali nielekeze na kuniongoza.” Nililala, na wakati fulani usiku wa manane nilikuwa na hisia isiyoeleweka, hisia ya usingizi kwamba kitu fulani kilikuwa kikinigandamiza. Nilijitahidi kuyafungua macho yangu lakini sikuweza. Nilipotambua kwamba kujitahidi kulikuwa bure, nilipaaza sauti kwa haraka: “Niokoe Bwana Yesu!” Nilipaaza sauti mara mbili lakini halikufaulu. Bado niliweza kukihisi kile kitu kikinigandamiza. Nilichanganyikiwa nisijue cha kufanya, na niliogopa sana. Ghafla, nilifikiria kuhusu Mwenyezi Mungu, na nikapaaza sauti mara mbili, “Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu!”, kisha nikaamka mara moja. Baada ya kuamka, nilikuwa bado nimeshtuka kidogo, na ilinichukua muda kabla ya kujiruhusu kuwaza kwa utulivu. Niliwaza juu ya ni kwa nini kuliita jina la Bwana Yesu hakukufua dafu ilhali kuita “Mwenyezi Mungu!” kuliniamsha mara moja. Kisha nikakumbuka kuwa Ndugu Lin alikuwa ameniambia kuwa Mungu ana jina kwa kila enzi na baada ya Mungu kufanya kazi mpya kwa kila enzi Roho Mtakatifu hulilinda lile jina kwa enzi mpya. Hivyo kwa waumini kupata sifa ya Mungu, utunzaji, na ulinzi wanapaswa kuomba wakitumia jina la Mungu kwa enzi mpya. Katika enzi hii, Bwana Yesu tayari amerejea na anatumia jina la Mwenyezi Mungu kutamatisha Enzi ya Neema na kufungua Enzi ya Ufalme. Wakati wa siku za mwisho, jina la Mungu ni Mwenyezi Mungu, hivyo tunapoomba tunapaswa kutumia jina hili vinginevyo Mungu hatutusikiliza. Ni hapo nilipotambua kuwa ndoto yangu haikuwa ya hiari, lakini alikuwa ni Mungu akisikiliza sala zangu na kunipa ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu. Asante Mungu! Baada ya kutambua jambo hili, moyo wangu ulijaa nguvu na sasa nilikuwa na ujasiri wa kukabiliana na mashambulizi ya maneno kutoka kwa bosi wangu na wenzangu.

Siku iliyofuata kazini mwangu bosi mara nyingine tena alimwambia kila mtu kwamba nilikuwa nikielekea kwa njia mbaya na pia alisema mambo mengi yaliyomkufuru Mwenyezi Mungu. Kumsikiliza kulinifanya nikasirike sana, kwa hiyo nikamwuliza: “Sisi ni waumini katika Mungu. Kwa nini huyapelelezi maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu na kutafuta nia ya Mungu badala ya kumhukumu na kumkufuru bila kufikiria? Kwa kweli unamwogopa na kumheshimu Mungu moyoni mwako?” Baada ya kusema haya yote niliondoka kwa hasira. Muda mfupi baadaye bosi wangu alikuja kunitafuta na kuniambia kuwa sikupaswa kumkasirikia. Nikasema: “Sikutaka kukasirika lakini hukupaswa kuyasema mambo hayo. Maneno ambayo hukufuru, kupinga, na kumuhukumu Mungu siyo mambo ambayo sisi waumini katika Mungu tunapaswa kuyasema kamwe, kwa sababu humkosea Yeye. Kuangalia kutoka kwa mtazamo wako, inaweza kuonekana kuwa unafanya tendo zuri kwa kunisisitizia nibadilishe mawazo yangu. Lakini mimi ni mtu mzima, na hufikiria mambo kwa busara. Suala la kama Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu ni kitu ambacho nimetafutia maarifa na kukichunguza. Si kitu ambacho nimeamua kuamini tu kwa vyovyote vile. Tafadhali heshimu uamuzi wangu, na usijaribu kuniwekea mipaka au kunizuia kutafuta maarifa kukihusu na kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho.” Bosi wangu kisha akaniuliza kama nilikuwa nimetazama vipindi vyovyote vya televisiheni au kusoma uvumi wowote kwa mtandao kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nikajibu: “Mambo hasi daima hutoka kwa Shetani. Ninachokisoma ni maneno ya Mwenyezi Mungu, na ninachokitazama ni filamu, video za kwaya, na video za muziki zilizotungwa na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Huwa sitazami kile unachokitazama. Kanisa la Mwenyezi Mungu haliwaruhusu washirika wake kufanya vitendo viovu, ambacho ni kinyume kabisa na kile mnachosema. Mwenyezi Mungu hutuhitaji tuwe watu waaminifu na wenye busara ambao wana ubinadamu na dhamiri njema.” Baada ya kusikiliza kile nilichokuwa niseme bosi wangu aliduwaa, na hivyo aliondoka akikaa kama asiyejua jinsi ya kunishughulikia.

Baada ya hayo, bosi wangu alianza kunionea na hata akaanza kusema mambo ya kunikejeli. Nilijua kwamba alikuwa anajaribu kunilazimisha kuiacha imani yangu kwa Mwenyezi Mungu. Siku moja, ghafla akaniambia: “Yun anataka kuzungumza nawe wakati atarudi kutoka kwa safari yake ya biashara.” Niliposikia hilo nilifadhaika na kuchanganyikiwa kidogo. Niliwaza: “Kwa waziwazi atajaribu kunizuia kumwamini Mwenyezi Mungu. Nilikuwa Mkristo baada ya kumsikiliza Dada Yun akihubiri na yeye ni mteja mashuhuri sana katika duka letu la urembo, hivyo ikiwa nitamkosea basi bosi hatafurahia na nitakuwa na matatizo mengi hata zaidi naye wakati wa baadaye.” Siku ya kurudi kwa Dada Yun ilipokaribia nikawa na fadhaa na hofu zaidi. Siku moja adhuhuri, nilikuwa nimekaa katika chumba cha watu mashuhuri nikimwomba Mungu. Nilikuwa nimemaliza sala yangu tu simu yangu ilipolia. Ilikuwa ni bosi wangu: “Yun anakuja hivi punde. Mpodoe uso.” Sikuwa na nia ya kufanya hivyo lakini hakuna njia ambayo ningeweza kukataa. Niliporudi kwa chumba cha kupodoa uso nikacheza nyimbo za neno la Mungu zilizorekodiwa ili kujituliza katika uwepo wa Mungu. Nilipokuwa nikisikiliza wimbo “Nimedhamiria Kumpenda Mungu Kwa Moyo Wangu” nilisikia mistari hii: “Napenda Ufungue macho ya roho yangu, napenda Roho Wako auguse moyo wangu, ili mbele Yako nivuliwe hali zote za kutoonyesha hisia, na nisishurutishwe na mtu yeyote, jambo, au kitu; nauweka moyo wangu wazi kabisa mbele Yako, ili nafsi Yangu yote ijitoe mbele Yako, na Uweze kunijaribu vile Utakavyo. Sasa, siwazii matarajio yangu, wala sifungwi na kifo. Kwa kuutumia moyo wangu ambao unakupenda, napenda kutafuta njia ya uzima(Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Maneno ya Mungu yalinipa ujasiri, na hatua kwa hatua nilianza kujihisi mtulivu na mwenye busara zaidi na zaidi. Naam: Sipaswi kuzuiwa na mtu yeyote, jambo, au kitu wakati wa kuchagua njia ya kweli. Kwa kuwa tayari nimeamua kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu basi ni lazima nikae nalo bila hata chembe ya shaka au kusita. Jinsi bosi wangu huniona na kunitendea na jinsi uhusiano wangu na Dada Yun unavyoendelea yote yako mikononi mwa Mungu. Napaswa kujiondolea wasiwasi wangu na kuitii mipango ya Mungu. Kwa hiyo, nilikwenda kukabiliana na hali hiyo kwa ujasiri.

Dakika chache baadaye, Dada Yun akawasili. Niliomba kimya kimya kwa Mungu: “Mwenyezi Mungu, ninaogopa kwamba atasema jambo ambalo hukukufuru, kukupinga, kukushutumu na kukushamblia Wewe. Pia ninahofia kwamba atabishana nami. Tafadhali nisaidie na kunilinda, Mungu.” Mawanzoni, Dada Yun alizungumzia tu safari yake ya biashara nchini Israeli na jinsi ilivyofanikiwa. Hatimaye, hata hivyo, yeye alileta mada kwa njia ya kuzungazunguka: “Katika siku za mwisho kuna Makristo wengi wa uongo na manabii wa uongo ambao hujaribu kuwadanganya watu …” Sikutaka kumsikia akisema kitu chochote ambacho kingemkufuru Mwenyezi Mungu hivyo nilimkatiza kwa kusema: “Naam, Bwana alitukumbusha kwa njia hii ili tuweze kujilinda dhidi ya Makristo wa uongo ambao humuiga Bwana Yesu kwa kuonyesha ishara na miujiza. Lakini nia ya Bwana ni kutufanya tukuze utambuzi, sio kututaka tukatae kuwaasikiliza watu wote wanaoeneza injili ya kurudi kwa Bwana. Bwana Yesu alisema: ‘Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Bwana atatuongoza kwa njia ya kweli, kwa hiyo hatupaswi kuwa na wasiwasi juu ya kupotoshwa na Makristo wa uongo wa siku za mwisho lakini pia tuzingatie kurudi kwa Bwana wakati wa siku za mwisho. Alimradi tumtafute Bwana basi tutapata onyesho la Bwana kwa sababu ametuambia kwamba kondoo wa Mungu wanaweza kuisikia sauti ya Mungu.” Lakini Dada Yun hakusikiliza kile nilichokisema na alirudia tu mambo kuhusu Makristo wa uongo kuwadanganya watu wakati wa siku za mwisho na kwamba ningepaswa kuwa mwangalifu zaidi. Kisha akasema mambo zaidi juu ya jinsi Kanisa la Mwenyezi Mungu lilivyo baya. Sikumjali, na alipoona kuwa singejibu akaacha kuzungumza.

Lakini bosi wangu bado hakufurahi kuhusu kuamini kwangu katika Mwenyezi Mungu na aliendelea kunionea na kunishambulia mbele ya wenzangu. Katika kipindi hiki, ndugu wa kiume na wa kike kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu walikuwepo daima ili kufanya ushirika na kushiriki maneno ya Mungu nami ili nipate kuelewa nia za Mungu. Pia waliniambia kwamba Mungu ni mtakatifu, na kwamba wakati Mungu aliwaumba wanadamu alitupa hiari, uhuru wa kuchagua. Walisema kwamba Mungu huwa hamlazimishi yeyote kufanya chochote kamwe bali huonyesha ukweli ambao hututolea riziki na kutusaidia kuelewa nia Zake na kutofautisha wema na uovu. Ni sawa na wakati Mungu alipomwambia Adamu na Hawa kwamba wangeweza kula matunda kutoka kwa mti wowote katika bustani ya Edeni isipokuwa matunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa sababu kama wangefanya hivyo bila shaka wangekufa! Hilo lilionyesha kuwa Mungu kimsingi ni mkarimu katika kuwapa wanadamu uhuru wa kuchagua, na ni Shetani pekee ambaye huwadhibiti na kuwalazimisha watu, kwa sababu Shetani ni muovu. Kwa hiyo, kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ni uamuzi wa kila mtu, na hakuna mtu anayelazimishwa kuikubali. Ndugu wa kiume na wa kike walipata kifungu cha maneno ya Mungu: “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. … Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Mawasiliano na wao yalinisaidia kukielewa kifungu hiki zaidi kidogo. Sasa nilielewa kwamba bila kujali kilichonitokea, daima kilikuwa kimeidhinishwa na Mungu. Mungu alikuwa akitumia hali hizi kunijaribu ili kuona kama nilikuwa na imani halisi Kwake na kunifanya nikuze utambuzi. Mungu alitaka nione wazi kile kitokacho Kwake na kile kitokacho kwa Shetani, na majaribio yalikuwa kunifanya nijifunze kumtegemea Mungu na kumtazamia Yeye, kumshuhudia Mungu kama Ayubu, na hivyo kumuaibisha Shetani.

Kwa uongozi kutoka kwa maneno ya Mungu na msaada wa ndugu wa kiume na wa kike, niliweza kuielewa vizuri zaidi njia ya kweli. Nilikuwa na uhakika kwamba sikuwa katika njia isiyofaa kwa kumfuata Mwenyezi Mungu lakini nilikuwa nikifuata nyayo za Mwanakondoo. Ndugu wa kiume na wa kike kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu walikuwa wakishiriki nami ukweli na nia za Mungu. Walikuwa wakifanya ushirika kwa kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu, na chote Mungu anacho na alicho. Hawakujaribu kunilazimisha kuamini chochote, lakini badala yake walinisaidia kujifunza jinsi ya kutambua kila aina ya sauti ili nifanye maamuzi yangu mwenyewe kwa uhuru. Lakini Dada Yun na bosi wangu waliamini uvumi wote uliokuwa mtandaoni, na hawakusita kusema chochote kilichompinga na kumkufuru Mungu ili kunishurutisha na kunizuia kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nilipokosa kuyakubali maoni yao walianza kunionea, kunidhihaki, na kunishambulia kwa maneno. Lakini niliona wazi kwamba kila kitu walichosema na kufanya kilitoka kwa Shetani, kwa kuwa kuwaonea, kuwashurutisha, na kushambulia watu ni vitendo vitokavyo kwa Shetani. Nilimshukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kuona mara moja yule atokaye kwa Mungu na yule atokaye kwa Shetani. Sasa nilihisi kuwa kulikuwa na uangavu katika maisha yangu na kwamba uzito mkubwa ulikuwa umeondolewa kutoka kwa moyo wangu. Nilikuwa na shukrani sana kwa Mungu kwa kupata mwili katika umbo la mwanadamu wakati wa siku za mwisho na kuonyesha ukweli mwingi ili kila wakati niliposumbuliwa niliweza kutafuta usaidizi wa maneno ya Mungu na kuzielewa nia Zake na kupata njia ya kutenda. Nilihisi kubahatika kwamba kwa njia ya riziki iliyotolewa na maneno ya Mungu niliweza kukua, kidogo kidogo!

Mwanzoni, nilidhani kuwa jambo zima lilikuwa limefikia kikomo, hivyo nilishangaa msururu mpya wa mashambulizi ulipoanza. Siku moja, nilikuwa nimemaliza tu kumpodoa mteja mmoja bosi wangu alipokuja na kunipeleka kwa chumba cha pili. Tulipofika kwa mlango aliniambia kuwa Dada Yun alikuwa huko akinisubiri. Niliingia, na nilipoona kwamba Dada Yun na Mchungaji Liu na mkewe walikuwa hapo mara moja nilikuwa na hofu kidogo kwa sababu sikujua ni nini walichotaka kufanya. Kwa haraka niilimwomba Mungu kimya kimya: “Mungu, wamekuja kuzungumza nami tena. Tafadhali nilinde na unisaidie kwa kunipa majibu ya hekima kwa yale watayoyasema.” Baada ya kuomba, sikuwa na hofu tena, na nilishangaa kama walikuwa wamekuja kunilazimisha nimwache Mwenyezi Mungu. Na kama ningekataa, ningepoteza kazi yangu? Lakini nilikumbuka kuwa kila kitu kilikuwa mikononi mwa Mungu na kwamba mipango ya Mungu ilikuwa ya kufaa daima, hivyo hata kama ningepoteza kazi yangu singemwacha Mwenyezi Mungu.

Mchungaji aliniuliza wakati nilipoanza kumwamini Bwana, na kisha akasema mambo mengi kuhusiana na imani katika Bwana. Kisha akaniuliza: “Je, unajua kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu? Je, bado unawasiliana nao? …” Kisha akasema vitu vingi vilivyomkufuru Mwenyezi Mungu na kwa uongo kulifanya Kanisa la Mwenyezi Mungu kuwa lenye makosa. Nilikasirika kumsikiliza, na nikasema: “Kwa nini ni kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu mnalolizungumzia si sawa na lile ambalo nimekuwa nikiwasiliana nalo na kujua kitu kulihusu? Sote tumeona mambo mtandaoni. Nilichokiona ni maneno ya Mwenyezi Mungu na filamu na video zilizotungwa na Kanisa la Mwenyezi Mungu, na pia ushuhuda wa maandishi wa ndugu wa kiume na wa kike. Nimeangalia pia baadhi ya propaganda hasi, lakini yote niliyoyaona yalikuwa ni uvumi na uongo mwingi usio na msingi. Bila kujali ni uvumi upi wameshindwa kutoa hata chembe ya ushahidi wa kuaminika ili kuunga mkono. Ama wao hubuni mambo bila ya matayarisho au kuchukua uongo uliopo na kuutia nakshi na kisha kuuenea kote zaidi. Huu wote ni uongo wa Shetani, kwa hiyo siuamini na sina haja nao. Ni vipi kwamba mnaamini tu uvumi hasi lakini hata hamtazami kamwe maneno ya Mungu kwa tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu? Hakuna hata mmoja wenu anayesoma maneno ya Mwenyezi Mungu, wala hamchunguzi kazi ya Mungu ya siku za mwisho, lakini mnaihukumu jinsi mnavyopenda. Je, hilo ni jambo sahihi la kufanya?” Mchungaji hakujibu swali langu moja kwa moja lakini badala yake alisema: “Kanisa la Mwenyezi Mungu limepanuka haraka sana, na wamekuwa wakienda kwa makanisa mengine kwa bidii ili kuwaiba washirika wao. Ukishikilia kumwamini Mwenyezi Mungu, basi hatuwezi kuwa wazuri kwako. Tutawaambia ndugu wote wa kiume na wa kike katika kanisa letu kwamba sasa unamwamini Mwenyezi Mungu, hivyo wakati ujao utakapokuja kwa mkusanyiko wa waumini wetu watafikiri umekuja kuwaiba na watakosa kukuthamini.” Kisha akajaribu kutumia ushuhuda wa uongo ili kuniogofya lakini hakuna kitu alichokisema kiliniathiri. Kwa kweli, nilihisi kuwa na ujasiri zaidi na kusema: “Mambo haya unayoyazungumzia, wewe mwenyewe uliyaona yakitokea? Au umefanya uchunguzi wa kina na kupata ushahidi thabiti? Una ushahidi gani kwamba washirika najumuia wa Kanisa la Mwenyezi Mungu walifanya haya yote? Ushahidi uko wapi? Unachukua tu uvumi na ushuhuda wa uongo ulioenezwa na CCP na jumuiya ya kidini ili kumhukumu Mwenyezi Mungu na kwa uongo kulifanya Kanisa la Mwenyezi Mungu kuwa lenye makosa. Je, huna wasiwasi kwamba utahukumiwa na Bwana, kama vile tu Mafarisayo walivyohukumiwa?”

Pia nikasema: “Bwana Yesu alitabiri hili juu ya kurudi Kwake, ‘Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki(Luka 17:25). Hili linamaanisha nini? Kwa sasa, jumuiya nzima ya kidini na serikali pinga Mungu ya Kikomunisti ya China inafanya inalowezekana kuipinga na kuihukumu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Je, si hili linatimiza utabiri wa Bwana? Je, si upinzani na hukumu ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa dunia ya dini ni sawa na ule upinzani wa Mafarisayo wa Kiyahudi na hukumu ya Bwana Yesu? Mafarisayo walimkataa Bwana Yesu na wakakataa kwamba alikuwa Masihi aliyekuwa akirudi, lakini wanafunzi wa Bwana waliweza kutambua kwamba Bwana Yesu alikuwa Masihi aliyetabiriwa katika unabii na hivyo wakamfuata Yeye. Katika wakati wetu, tuna hali sawa na hiyo. Wachungaji na wazee wa kanisa hawakubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na hata humpinga na kumhukumu Mwenyezi Mungu, lakini kondoo wazuri katika madhehebu mbalimbali wanaweza kutambua sauti ya Mungu katika maneno ya Mwenyezi Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu. Hali iko hivi jinsi gani? Bwana Yesu alisema kwamba kondoo wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu, na kwamba kurudi kwa Mungu kungewatenganisha kondoo na mbuzi. Nimemwamini Bwana kwa muda mfupi tu, na siielewi Biblia vizuri sana, kwa hiyo sijui jinsi Bwana atakavyowatenganisha kondoo na mbuzi. Mchungaji Liu, umekuwa kwa seminari na umekuwa mchungaji kwa miaka mingi sasa. Labda ungekuwa na hisani kunielezea hilo?” Mchungaji Liu alinitazama kwa hasira, kwa sababu ilikuwa dhahiri kwamba hakujua jinsi ya kunielezea jambo hili. Yote aliyosema ni: “Sisi waumini hupata uzima wa milele kwa sababu tumebatizwa.” Kwa hiyo nikasema: “Unasemaje? Kupata uzima wa milele ni rahisi hivyo?! Kwa hiyo kila mtu ambaye ameekuja kanisani mwenu na kubatizwa ataingia katika ufalme wa mbinguni? Je, hilo linakubaliana na kile Bwana alichosema? Je, wote ni watu wanaomtendea Bwana kwa mioyo ya kweli? Je, wote huyatii mapenzi ya Baba wa mbinguni? Kila mahubiri katika kanisa hutaja kutoa sadaka, lakini Bwana hakusema kuwa kutoa sadaka ni sawa na kumpenda Bwana. Kwa hiyo kumpenda Bwana ni nini?” Mchungaji Liu alijibu: “Kusoma Biblia sana, kuomba sana ni kumpenda Bwana.” Ingawa sikujua kile kumpenda Bwana kwa hakika kilimaanisha, nilijua kuwa ulikuwa upuuzi mtupu kusema kuwa kusoma Biblia na kuomba ni kumpenda Bwana. Mafarisayo walisoma Biblia na waliomba sana, lakini inaweza kusemwa kwamba walimpenda Bwana? Kama walimpenda Bwana, kwa nini walimkufuru na kumhukumu Yeye, na kumtundika Yeye msalabani? Ilionekana kwangu kwamba mchungaji hakuelewa kile kumpenda Bwana kilimaanisha kamwe. Wachungaji huenda wakaelewa maarifa ya kibiblia na nadharia za kiteolojia lakini hiyo haina maana kwamba wanauelewa ukweli! Lakini niliweza tu kujilaumu kwa kuwa sikuwa na utambuzi wa kutosha na niliwaheshimu mno.

Nilipotambua jambo hili, sikuona haja ya kuendelea kujadiliana na Mchungaji Liu, hivyo niliacha kuzungumza. Lakini mchungaji alikuwa na mengine ya kusema: “Je, unajua kwamba wanasema kwamba Bwana amerejea akiwa mwili wa mwanamke kufanya kazi?” Baada ya kusikia hilo nilihisi kwamba ilinibidi kujibu: “Lile umbo analolichukua Bwana Anaporudi na kuwa mwili ili kufanya kazi ni shughuli ya Mungu. Sisi ni wadogo, viumbe wadogo walioumbwa na Mungu, kwa hiyo tunawezaje kutengeneza sheria za kazi ya Mungu? Inasema katika Biblia: ‘Ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?’ (Warumi 11:34). Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: ‘Mwanadamu hafai kufafanua kazi ya Mungu; zaidi ya hayo, mwanadamu hawezi kufafanua kazi ya Mungu. Katika macho ya Mungu, mwanadamu ni mdogo kushinda mchwa, kwa hivyo mwanadamu atawezaje kuelewa kazi ya Mungu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Mungu ni Muumba wa vitu vyote na hekima ya Mungu inazidi kila kitu, hivyo kwa hali yoyote Mungu afanyavyo kazi Yake Yeye hana haja ya kuwasiliana nasi wanadamu kwanza!” Kuona kwamba hawakuwa na shauku hata chembe katika kutafuta na kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, lakini walitaka tu kutafuta makosa na kutafuta fursa ya kumshambulia na kumkufuru Mungu na kunizuia kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, niliamua kutoendelea na mazungumzo hayo. Swali langu la mwisho kwao lilikuwa: “Mlifikiria kamwe jinsi kuja kwenu leo katika duka hili la urembo kugeathiri kazi yangu hapa?” Kwa mshangao wangu mkubwa, mchungaji alidanganya bayana: “Bosi wako hajui mazungumzo haya yanahusu nini.” Kama ningemsikia akisema hivyo kabla ningeshangaa sana kwamba mchungaji huyu—mtu ambaye huwahubiria na kuwafundisha watu na anayeijua Biblia vizuri sana—angeweza kusema uongo kama huo usiojificha. Lakini baada ya kuwasikia tu wakibuni uongo uliomkufuru Mungu, sikushangaa kamwe. Kwa dhahiri ilikuwa kawaida sana kwao kusema uongo. Sikuweza kujizuia kufikiria maneno ya Bwana Yesu: “Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na mtatimiliza tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo, na hakudumu katika ukweli, kwa sababu ukweli haupo ndani yake. Anaponena uwongo, anazungumza yaliyo yake mwenyewe: kwani yeye ni mwongo, na baba wa uwongo(Yohana 8:44). Katika moyo wangu nikamwambia Mungu maneno haya: “Asante, Mungu! Umeruhusu tukio hili linijie leo ili nipate kuona kwamba hawana ufahamu wa ukweli. Umeniruhusu nione kwamba wao ni waongo ambao hueneza uongo bila haya na kuwadanganya watu. Wao ni Mafarisayo wenye unafiki.” Sikuwa na kitu zaidi cha kuwaambia na nilitaka kuondoka mara moja.

Kuona kwamba sikujisikia kuendelea na mazungumzo, Dada Yun aliniambia: “Yixin, unapaswa kuwafikiria watoto wako na wazazi.” Nikajibu: “Wote ni wazima na sote tunajihisi kuwa na amani na salama. Ninamwamini Mungu mmoja wa kweli, Muumba wa vitu vyote. Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu. Mungu ni Mungu anayewapenda na kuwaokoa watu, na kwa baraka na uongozi wa Mungu familia yangu itafanya vyema zaidi na zaidi.” Mchungaji na Dada Yun walitaka kuniombea, lakini nikakataa. Hivyo Mchungaji Liu alikamilisha kwa onyo: “Ikiwa hutaliacha Kanisa la Mwenyezi Mungu basi utatenganishwa na kanisa letu!” Niliwaza: “Na kanisa likoje siku hizi? Ni kama hekalu wakati Bwana Yesu alipoanza kazi Yake kwanza: pango la wezi. Mikutano haitoi riziki yoyote ya kiroho, kwa hiyo kuna nini hapo kwangu kukikosa?” Nimekwisha kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na nimefuata nyayo za Mwanakondoo na kuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ninapewa maji yaliyo hai ya uzima yaliyotolewa na Kristo na ninafurahia malezi ya uso kwa uso na kulishwa kutoka kwa Mungu. Hakuna mtu mwenye bahati zaidi kuniliko, na Kanisa la Mwenyezi Mungu sasa ni nyumba yangu ya kweli.

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “Kila kitu ambacho kimepangwa sasa ni kwa lengo la kutoa mafunzo kwenu ili kwamba mkue katika maisha yenu, kuzifanya roho zenu ziwe na makali na zenye ncha, kuyafungua macho yenu ya kiroho na kuwafanya mtambue mambo yanayotoka kwa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). Ninashukurani kwa Mungu kwa kunionea huruma na kutumia machafuko ya nguvu za kidini ili nipate kukuza utambuzi. Niliona jinsi wale wachungaji walivyojaa uongo, jinsi wanavyoipinga na kuihukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, jinsi hawana chembe ya woga au heshima kwa ajili ya Mungu. Niliona jinsi mikusanyiko ya waumini wao wanavyoshikilia njia zao za dhambi, jinsi wanavyofuata bila kufikiria mielekeo na mitindo ya ulimwengu wa kimwili, jinsi wanavyodanganyana, na jinsi walivyopungukiwa na uchaji Mungu. Yote haya yalinithibitishia kuwa jumuiya ya kidini haikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tena, kwamba ilikuwa imegubikiwa katika giza na ilikuwa chini ya udhibiti wa Shetani. Wakati huo huo, niliweza kuona kwamba ndugu wa kiume na wa kike wa Kanisa la Mwenyezi Mungu wanatafuta ukweli na maarifa ya Mungu kupitia uongozi katika maneno ya Mungu. Wakati wanakabiliwa na shida, huwa wanatafuta kutumia maneno ya Mungu ili kutatua matatizo yao na halafu ni ukweli kabisa, maneno ya Mungu, na Roho Mtakatifu akishika madaraka. Maneno ya Mwenyezi Mungu hayawezi kurejeshwa, na kile kilichosemwa kitafanyika. Hakuna mtu anayeweza kuzuia kile ambacho Mungu anataka kutimiza, na huu ni ukweli usioweza kukanwa! Maneno ya Mwenyezi Mungu kweli ni ukweli, na Mwenyezi Mungu ndiye onyesho la Bwana wa uumbaji. Sasa niko tayari kumfuata Mwenyezi Mungu kwa maisha yangu yote!

Iliyotangulia: Kupotea na Kurejea Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ufanisi

Na Fangfang, China Sote katika familia yangu tunamwamini Bwana Yesu, na wakati nilikuwa muumini wa kawaida tu katika kanisa letu, babangu...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp