Kukimbia Kutoka katika “Tundu la Chui”

02/12/2019

Na Xiaoyou, China

Jina langu ni Xiaoyou na nina umri wa miaka 26. Nilikuwa Mkatoliki. Nilipokuwa mdogo, nilikwenda na mama yangu kanisani kuhudhuria Misa, kusoma Biblia, kwenda kukiri na kupokea Komunyo. Mama yangu alikuwa mwenye bidii sana katika imani yake. Mara nyingi angetoa chakula na vitu vingine mbalimbali kutoka nyumbani kwetu kupeleka kanisani, na pia angetoa pesa. Viongozi wa kanisa na watawa hasa walimpenda mama yangu. Walipomwona, wangemsalimia na kutabasamu na kuonyesha kujali kumhusu, na mara nyingi wangempigia mamangu simu kumuuliza ashiriki katika kila aina ya shughuli za kanisa na kusaidia katika kazi mbali mbali. Pia nilishiriki kwa bidii katika madarasa ambayo watawa walifundisha, na mimi na marafiki wangu wa kanisa hilo tungesoma Bibilia pamoja. Wakati huo, niliweza kuhisi furaha na amani iliyokuja kutokana na kuwa na Bwana kando yangu, na nilihisi mwenye furaha kila siku. Hata hivyo, kadiri muda ulivyosonga, imani ya marafiki wa kanisa langu ilizidi kuwa baridi na baridi. Roho yangu pia ilidhoofika na sikuweza kushika mafundisho ya Bwana. Mara nyingi nilikuwa nikitenda dhambi kisha ninakiri na baada ya kufunga ndoa, mimi na mume wangu tulihama kwenda katika sehemu nyingine ya nchi kwa ajili ya kazi.

Kufumba na kufumbua, ilikuwa Krismasi ya mwaka wa 2013, na nilikuwa na bahati nzuri ya kukutana na dada mmoja kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Aliniambia kuwa Bwana Yesu alikuwa amerudi tayari na kwamba Anatekeleza hatua mpya ya kazi Yake. Niliposikia hili, nilishangaa na nikasema kwa furaha, “Kweli? Bwana amerudi! Bwana alirudi lini? Bwana yuko wapi sasa hivi? Dada, niambie mara moja.” Dada alinipa ushirika, akisema, “Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerejea. Mwenyezi Mungu ameonyesha mamilioni ya maneno na Anatekeleza kazi Yake ya kuhukumu katika siku za mwisho. Amefichua ukweli wote ambao unaweza kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, ikiwa ni pamoja na hatua tatu za kazi ambayo Mungu hufanya ili kuwaokoa wanadamu, siri ya kupata mwili, siri ya Biblia, umuhimu wa majina ya Mungu, na mwisho na hatima ya wanadamu, kati ya wengine. Hili linatimiza maneno ya Bwana Yesu aliposema: ‘Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo’” (Yohana 16:12–13). Nilisikiliza kwa dhati ushirika wa dada huyo na nikawaza: “Sikutarajia kamwe kuweza kukaribisha kurudi kwa Bwana. Hili ni jambo zuri.” Baadaye, dada huyo alinishuhudia kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu na umuhimu wa majina ya Mungu. Akihofu kuwa singeelewa, yule dada alinipa vilinganisho na mifano. Alitoa ushirika kwa undani zaidi, kwa njia iliyokuwa yenye kueleweka na wazi. Kupitia katika ushirika wake, nilikuja kuelewa ukweli mwingi ambao sikuelewa hapo awali. Pia nilijifunza kuwa Bwana alikuwa amerudi ili kutekeleza kazi ya hukumu, kuadibu, kutakasa na kumkamilisha mwanadamu. Nilihisi kwamba inawezekana sana kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerea, na nilimwambia dada huyo kwamba nilitamani kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Baadaye, nilihudhuria mikutano na ndugu, na kwa pamoja tulisoma neno la Mungu, kuimba nyimbo na kucheza katika sifa kwa Mungu. Kila nilipokutana na kitu ambacho sikuelewa wakati nilikuwa nikisoma maneno ya Mungu, ndugu daima wangechukua jukumu la kushirikiana nami juu ya jambo hilo. Ushirika wao ulikuwa na nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na kuhudhuria mikutano nao kuliniruhusu nifurahie tena kazi ya Roho Mtakatifu. Nilihisi mwenye furaha sana. Katika familia hii kubwa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakukuwa na tofauti kati ya wa juu na wa chini au maskini na tajiri. Ndugu wote walikuwa wazi kwa kila mmoja na kila wakati walisema kile kilichokuwa mawazoni mwao. Ilipokuja katika kuishi maisha ya furaha, nilihisi kwamba haya yalikuwa halisi! Baada ya uchunguzi wa zaidi ya mwezi mmoja, nilikuwa nimesoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu na nikawa na hakika kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerejea. Nilihisi kuwa mwenye bahati nzuri sana, na wakati huo huo nilitaka kumwambia mama yangu na marafiki zangu kanisani habari hii njema.

Wakati wa Sikukuu ya msimu wa kuchipuka ya China, mimi na mume wangu tulirudi katika mji wetu. Baada ya kufika, mara moja nilitoa ushuhuda wa kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa mama yangu, lakini alikataa kuikubali bila kujali nilichosema. Nilihisi kusikitishwa na mwenye kutatizika sana. “Ni wazi, Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerejea,” nilifikiria. “Angewezaje kutokubali hili?” Kwa kuwa mama yangu hakukubali, sikuwa na chaguo ila kuacha mada hiyo. Wakati safari yetu ya kurudi nyumbani kwetu ilikuwa imekwisha, nilirudi mahali nilikokuwa nikifanya kazi. Nilihudhuria mikutano na ndugu zangu na kutenda kutimiza wajibu wangu kwa ajili ya kanisa. Wakati huo, roho yangu ilikuwa inabubujikwa na furaha na maisha yangu yalikuwa wamejawa na furaha na raha isiyo na kifani. Nilisoma katika maneno ya Mungu kuhusu jinsi Ayubu alivyopoteza mali zake zote na wana na binti katika majaribu, na jinsi mwili wake ulivyofunikwa na vidonda na bado alikuwa na uwezo wa kulisifu jina la Mungu na kuwa na imani ya kweli kwa Mungu. Na kisha kulikuwa na Ibrahamu, aliyeweza kutoa mwana wake wa pekee Isaka na kumrudisha kwa Mungu. Niliposoma juu ya mambo haya haswa, nilihisi kuguswa sana na imani na utii wao kwa Mungu, na mimi pia nilitaka kuwa mtu wa aina hii.

Wakati tu nilikuwa nahisi kuzama katika upendo wa Mungu, ghafla maisha yangu yaligeuka kuwa jinamizi. Siku moja mnamo Agosti 2014, mama yangu alinipigia simu ghafla na kusema kuwa binti yangu alikuwa mgonjwa mahututi. Moyo wangu ulishtuka niliposikia hili. “Binti yangu ni mchanga sana,” niliwaza, “Anawezaje kuwa mgonjwa mahututi?” Nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu binti yangu na nilihisi mfadhaiko mkubwa sana. Kwa hivyo nilienda mbele za Mungu na kuomba: “Ee Mungu, ni kwa idhini Yako kwamba hali hii imenifika. Ugonjwa wa binti yangu uko mikononi Mwako. Natamani kumkabidhi binti yangu Kwako. Tafadhali nipe imani ya kweli.” Nilihisi raha zaidi baada ya hapo. Mimi na mume wangu tulirudi nyumbani kwetu katika mji wetu kwa haraka. Tulipofika huko, nilishangaa kumwona binti yangu amelala kwa amani kitandani mwake. Nilitaka kumuamsha, lakini mama yangu akainua mkono wake kunikomesha na akasema kwa ukali, “Usimwamshe. Yuko sawa!” Ni hapo tu ndipo niligundua kuwa jamaa wangu wengi walikuwa wamekusanyika pale nyumbani kwangu, na nikagundua kuwa alikuwa amenidanganya nirudi nyumbani ili kujaribu kunizuia nisimwamini Mwenyezi Mungu. Nilifikiria: “Mungu ameniandalia hali hii leo. Lazima liwe jambo ambalo ni sharti nilipitie.” Kisha nikamuuliza mama yangu, “Mama, binti yangu yuko sawa. Mbona ulitudanganya turudi nyumbani?” Kabla sijamaliza kuongea, mama yangu alipatwa na hasira na kupiga kelele, “Nilienda kanisani na kuwauliza makasisi na viongozi wa kanisa. Walisema kwamba Umeme wa Mashariki ni hatari, na kwamba ukishajiunga nao kamwe huwezi kuliacha tena. Usiamini katika hilo tena. Ninafanya hili kwa ajili yako mwenyewe. Naogopa kwamba umechukua njia mbaya.” Mama yangu pia alirudia uwongo na hadithi mbaya zilizobuniwa na ulimwengu wa kidini dhidi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilipomsikiliza mama yangu akisema haya, niliwaza: “Imani yangu sio mbaya hata kidogo. Badala yake, ninaenda kwa mwendo sawa na kazi mpya ya Mungu. Mwenyezi Mungu ninayemwamini ni Bwana Yesu aliyerejea ambaye sasa hutekeleza kazi ya kuhukumu, kuadibu na kumtakasa mwanadamu. Nina hakika kabisa kwamba hii ndiyo njia ya kweli, kwa nini niiache? Makasisi na viongozi wa kanisa wanaposema, ‘Ukiamini katika Umeme wa Mashariki na ujiunge na kanisa lao basi kamwe huwezi kuondoka,’ huu ni uwongo na udanganyifu mtupu ulioandaliwa kuwadanganya watu. Nimehudhuria mikutano katika Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa zaidi ya miezi sita sasa na najua mengi zaidi kulihusu kuliko vile mnavyojua. Mlango wa Kanisa la Mwenyezi Mungu uko wazi kila wakati na watu wanaweza kuchagua kuondoka. Sio kama vile makasisi na viongozi wa kanisa wanavyosema hata kidogo. Ndugu wote wanakuwa na hakika juu ya njia ya kweli kwa kusoma maneno ya Mungu, wanapata lishe ya maisha na wamepata chemchemi ya maji yaliyo hai, na hiyo ndiyo sababu hawataki kuliacha kanisa hilo. Tunaposoma neno la Mwenyezi Mungu, roho zetu zinaridhika. Ni nani angependa kurudi kwenye kanisa lake la zamani lenye ukiwa na lililo tasa? Makasisi na viongozi wa kanisa hawajachunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho hata kidogo. Wao hawajasoma maneno ya Mwenyezi Mungu na zaidi ya hayo, hawajahudhuria mikutano katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wao wametegemeza madai yao kwa kitu gani? Si wanabuni tu uvumi usio na msingi?” Mamangu alipoona kwamba sikuwa najibu, alinijia kwa kishindo, akanizaba kofi mara kadhaa, na kujaribu kunilazimisha niseme vitu vya kumsaliti Mungu. Iliniumiza sana kumwona akiwa namna hii. Nilidhani kwamba isingekuwa kwa sababu ya uwongo uliobuniwa na makasisi na viongozi wa kanisa, basi kusingekuwa na namna ambavyo mama yangu angejaribu kunilazimisha kuiacha imani yangu kwa Mwenyezi Mungu. Kisha nikamwambia, “Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerejea. Kumwamini Mwenyezi Mungu ni sheria ya mbingu na dunia isiyoweza kubadilika, nami nitamwamini mpaka mwisho kabisa!” Mama yangu aliposikia nikisema hivi, uso wake ulijawa na hasira na macho yake yalikuwa mekundu kwa gadhabu. Aliniambia kwa sauti kubwa, “Mimi ndiye mama yako. Lazima unisikilize!” Kuona jinsi mama yangu alivyokuwa bila busara, niliamua kutosema chochote zaidi. Wakati huohuo, jamaa zangu pia walianza kunikosoa wote mara moja na walisema mambo mengi kujaribu kunifanya nimsaliti Mungu. Nilifikiria: “Tayari nimemkaribisha Bwana Yesu. Mungu ninayemwamini ni wa kweli na njia ninayoitembea ni njia sahihi. Sitamsaliti Mungu hata kidogo!” Nilitaka sana kuwashauri waichunguze kazi ya Mungu ya siku za mwisho na wasidanganywe na uvumi wa makasisi na viongozi wa kanisa wamshutumu na kumkataa Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, kwa kuona kwamba mtazamo wao ulikuwa wa chuki kwa ukweli na kwa Mungu, nilihisi kwamba hawangeukubali ukweli na hakungekuwa na maana yoyote bila kujali nilichosema, kwa hivyo sikuwaambia chochote zaidi. Baada ya muda mfupi, mamangu na jamaa zangu waliondoka pamoja. Hata hivyo, mamangu hakuwa ameniachilia bado, kwa kuwa alimwambia kakangu mdogo aje akae nyumbani kwangu. Kila siku, kakangu angeniangalia kana kwamba nilikuwa mahabusu na angenifuata kila nilikokwenda. Kwa namna hiyo tu, uhuru wangu wa kibinafsi ulikuwa umetoweka.

Siku mbili baadaye, mimi na familia yangu tulipokuwa tunakula chakula cha jioni, mama yangu aliingia ghafla. Alikuwa akitabasamu sikio hadi sikio na kuniambia kwa sauti ya upendo, “Xiaoyou, angalia ni nani aliyewasili hapa!” Usemi wa mama yangu na toni ya sauti yake vilinifanya nishangae ni mtu wa aina gani aliyekuja anayeleta mjibizo mkubwa hivyo kutoka kwake, na nilijua kuwa hakingekuwa kitu chochote kizuri. Wakati huohuo, kiongozi wa kanisa Liu na mwana parokia anayeitwa Wang walingia. Niliwasalimu kwa utulivu na kuwaalika waketi. Baada ya kumaliza kula, kiongozi wa kanisa Liu alinitazama, akatabasamu na kusema, “Xiaoyou! Tutaenda kwa mada moja kwa moja. Kulingana na mama yako, sasa unaamini katika Umeme wa Mashariki. Lazima nikwambie kwamba lazima uache kuliamini. Familia yako nzima imekuwa ya Kikatoliki kwa vizazi vingi. Huwezi kumwacha Bwana, la sivyo Atakuacha. Leo, tumekuja kukupa ushauri, lakini usipotusikiliza, basi hutakuwa na mtu wa kulaumu ila wewe mwenyewe wakati utakapofika na utashuka kuzimu. Xiaoyou, tunafanya hili kwa ajili yako mwenyewe. Fikiria juu ya ugonjwa wa mumeo. Asingepata nafuu isingekuwa kwa ajili ya mimi na mama yako kunaomba kwa Bwana kila siku. Ukiendelea kuamini katika Umeme wa Mashariki na ugonjwa wa mumeo urudi, basi hakuna mtu atakayefanya chochote kusaidia.” Kumsikiliza akisema mambo haya, moyo wangu ulikuwa ukipiga na sikuweza kujizuia ila kuhisi hofu kidogo. Niliwaza: “Mume wangu alikua mgonjwa mahututi na ingawa tulitumia pesa nyingi bado hakupata nafuu. Mwishowe, alikuwa bora tu kwa sababu ya sala zetu kila siku. Ikiwa mambo yako kama vile wanavyosema, na ugonjwa wa mume wangu urudi, ningefanyaje?” Wakati tu nilikuwa naanza kushindwa na udanganyifu wao, mstari wa maneno ya Mungu ulielea akilini mwangu:“ Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zote. daktari! “Mwenyezi Mungu ni daktari mwenye nguvu zote!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Nilifikiria kuhusu hili, ghafla niliamka na akili yangu ikawa wazi. “Hiyo ni kweli,” niliwaza. “Ninaamini katika Mwenyezi Mungu ambaye ni Bwana aliyerudi. Ikiwa mume wangu atakuwa mgonjwa tena liko mikononi mwa Mungu; siyo juu yao. Mungu ana mamlaka juu ya kila kitu, kwa hivyo kuna nini cha mimi kuogopa? Kwa vyovyote vile, ni Bwana aliyeponya ugonjwa wa mume wangu, si wao. Sikuwahi kufikiria kwamba wangejaribu kutumia ugonjwa wa mume wangu kunitishia nimsaliti Mungu, au kwamba wangejaribu kunifanya nimkatae na kumsaliti Mungu kwa hofu ya shida kutokea katika familia yangu. Jinsi gani walivyo wenye kudhuru kwa siri!” Nilipong’amua nia zao mbaya, sikuhisi chochote ila chukizo kwao, na sikutaka kuongea nao tena.

Kiongozi wa kanisa Liu alipoona kuwa nilisalia kimya, alisema kwa kejeli, “Inaonekana unasisitiza sana! Kufikia sasa ni sisi ndio ambao tumeongea leo, kwa hivyo tuambie msimamo wako ni upi!” Kwa kuwa walikuwa wamezungumza tu juu ya suala la ugonjwa wa mume wangu, nilihisi wasiwasi. Lakini nilipofikiria juu ya Mungu kushikilia mamlaka juu ya kila kitu, ghafla nilipata imani. Bila kujali kitakachotokea, singemsaliti Mungu. Nilipata ujasiri na kusema, “Acha niwaambie kwamba ninaamini katika Mwenyezi Mungu kwa uthabiti na sitaiacha imani yangu katika Mungu!” Mama yangu alinguruma, “Twendeni! Tutaenda kanisani kusali.” Baada ya kusema hayo, wote waliondoka kwa hasira. Kuona jinsi walivyoonekana wakali, sikuweza kujizuia ila kuhisi hofu kidogo. “Wanaenda kuomba,” niliwaza. “Je, watanilaani? Naweza kufanya nini?” Nikihisi nisiye na msaada, nilikuja mbele za Mungu na kuomba: “Ee Mwenyezi Mungu! Wote wameunda safu ya vita dhidi yangu na wananizingira, na ninahisi mpweke. Ee Mungu! Sijui la kufanya. Ninaogopa sana. Tafadhali niongoze!” Baada ya kumaliza kuomba, nilikumbuka maneno kadhaa ya Mungu: “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote vilivyo katika mazingira yanayo wazunguka vipo hapo kwa ruhusa Yangu, Mimi napanga yote. Oneni wazi na muridhishe moyo Wangu katika mazingira Niliyokupa. Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 26). Nikiwa na nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu, ghafla moyo wangu ulijawa na nuru: “Ndiyo! Mungu ndiye msaada wangu thabiti,” niliwaza. “Nikiwa na Mungu kando yangu, hakuna chochote cha kuogopa. Kiongozi wa kanisa na yule anayeitwa Wang walisema vitu hivyo ili kunifanya niogope kwamba nitakwenda kuzimu, niogope shida kutokea katika familia yangu, na kuogopa kwamba mume wangu angekuwa mgonjwa, na hivyo kumwacha Mungu. Ikiwa ninaogopa au nina hofu, basi hiyo haimaanishi kuwa nimeshindwa na njama za Shetani? Majaliwa, hatima ya mwisho na bahati nzuri na bahati mbaya kwangu na mume wangu sio kwa ajili ya mtu yeyote, sembuse makasisi na viongozi wa kanisa kuwa na usemi wowote katika hilo. Yote yamo mikononi mwa Mungu. Haina maana kwa wao kunishutumu na kunilaani.” Nikifikiria hili, nilihisi utulivu tena na sikuogopa hata kidogo. Kutoka moyoni mwangu, nilimsifu Mungu na kumshukuru Mungu kwa kunielekeza kwa maneno Yake, na kwa kunipa imani na nguvu ya kung’amua njama za Shetani ili nisisumbuliwe au kudanganywa na mama yangu au wengine.

Alasiri moja, nilipokuwa karibu kula chakula cha mchana na mtoto wangu, Dada Zhao na Dada Zhang kutoka katika kanisa langu la zamani walikuja kunisumbua. Dada Zhao alisema mambo kadhaa kunitishia, na kisha Dada Zhang, akiigiza kwa uzito sana, akasema, “Ni kweli. Tumekuwa na mawasiliano na watu kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu zamani, na ilikuwa karibu tudanganywe nao.” Nilipomsikia akisema hivi, nilikasirika. Nilijua kuwa ndugu zangu hawangeweza kujaribu kumdanganya mtu yeyote. Kila kitu walichokuwa wakisema kilikuwa uwongo na kashfa tu. Kwa hivyo, niliwauliza, “Waliwadanganyaje?” Dada Zhang alisema kwa sauti ya uzito, “Hakuna ambavyo ungejua. Walinipa kitabu!” Niliendelea na kumuuliza, “Niambie, kitabu walichokupa kilikuwa namna gani? Jina la kitabu hicho lilikuwa lipi? Kitabu hicho kilikuwa kinahusu nini?” Dada Zhang alionekana mwenye aibu, na baada ya kumunyamunya kidogo, mwishowe alijaribu kupuuzilia swali hilo, akisema, “Nimesahau.” Nilipomsikia akisema hivi, niliwaza, “Nyinyi ni watawa! Mnawezaje kuthubutu kutoa ushahidi wa uwongo na kujaribu kuweka mashtaka ya uwongo dhidi ya wengine? Mnawezaje kuwa na uchaji mdogo hivyo kwa Mungu? Je, ninyi kweli mnaamini katika Mungu? Hamwogopi kuadhibiwa na Mungu?” Baadaye, Dada Zhao aliniuliza tena, “Je, unaenda kazini?” Nilimjibu kwa uthabiti, “Ndiyo!” Kwa urafiki wa kujifanya, alinishauri, “Usiende kazini. Kukaa nyumbani na kumtunza mtoto wako ni bora zaidi!” Nilihisi kuchukizwa na unafiki wao, kwa hivyo nilianza kutoka nje ya chumba na nikasema, “Jishughulisheni na mambo yenu wenyewe.” Kuona kwamba majaribio yao ya kunisumbua yameshindwa, waliondoka wakiwa wamekata tamaa. Baada ya wao kuondoka, nilihisi mwenye kutatizika na mwenye huzuni sana. Nilifikiria juu ya jinsi kiongozi wa kanisa na watawa hawa walikuwa wameendelea kunijia na kunisumbua hivi karibuni, na walikuwa wakinikashifu, kunishambulia na kueneza uvumi juu ya Mwenyezi Mungu na ndugu zangu, au vinginevyo walikuwa wakieneza uwongo kunidanganya na kunitishia niwatii. Hata ingawa sikudanganywa nao na nilibishana na kupinga madai yao, kila wakati niliachwa nikiwa nimesumbuka sana na sikuweza kujituliza mbele ya Mungu na kusoma maneno ya Mungu. Ndugu yangu mdogo bado alikuwa akinichunga wakati wote vile vile. Nilihisi mwenye kufungwa kila niliposali, kuimba nyimbo na kusoma neno la Mungu, na nilihisi aliyekandamizwa sana. Kati ya mateso yangu, nilimwomba Mungu: “Mwenyezi Mungu! Kiongozi huyu wa kanisa na watawa hawa wamekuja kunisumbua muda baada ya muda. Ninahisi mwenye kutatizika na kukasirika sana. Hivi sasa, sijui jinsi ninavyopaswa kushughulika nao. Mungu mpendwa, naomba unipe nuru na uniongoze!”

Baada ya kusali, nilichukua kicheza MP5 changu na ikatukia tu kwamba niliona kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye ‘mwili imara,’ wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu). Baada ya kumaliza kusoma maneno ya Mungu, nilielewa mara moja. Ilibainika kuwa hawa makasisi na viongozi wa kanisa walikuwa wapinga Kristo wa kidini kweli ambao Mungu alikuwa akiwafunua katika maneno Yake. Hata ingawa walimwamini Bwana, hawakutafuta ukweli hata kidogo na hawakuwa na moyo unaomcha Mungu hata kidogo. Sio tu kwamba hawakuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho wenyewe, lakini pia walimkufuru Mungu, waliishutumu kazi mpya ya Mungu na wakabuni uvumi kumdanganya mama yangu ili anichape, anikashifu na kuniweka chini ya kifungo cha nyumbani. Kisha, walikuja nyumbani kwangu mara kwa mara wakijaribu kunisumbua, kunidanganya, kunihada na kunitishia. Kwa bahati nzuri, nikiwa na maneno ya Mungu yakinielekeza na kuniongoza, sikushindwa na njama zao, wala sikumsaliti Mungu. Mafarisayo pia walitumia aina zote za njia zinazodharauliwa kuwazuia watu wa kawaida wa Kiyahudi kukubali injili ya Bwana Yesu. Hata walitumia uwongo kuwadanganya watu, wakisema kwamba kazi ya Bwana Yesu ilivuka mipaka ya Agano la Kale na kwamba Yesu hakuwa Masihi aliyerejea. Hii ilisababisha watu wa kawaida wa Kiyahudi wawafuate Mafarisayo katika kumsaliti Bwana Yesu asiye na dhambi msalabani. Bwana Yesu aliwakemea kwa kusema, “Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie(Mathayo 23:13). Nililinganisha yale Mafarisayo walifanya na matendo ya makasisi, viongozi wa kanisa na watawa, na nikafikiria juu ya ushirika ambao ndugu zangu walikuwa wamenipa hapo zamani juu ya jinsi ya kutambua kiini cha Mafarisayo. Kisha nikaona wazi kuwa makasisi na viongozi wa kanisa kimsingi hawakuwa tofauti na Mafarisayo wa zamani hata kidogo. Ili kulinda hadhi yao na riziki zao, walikuwa wanatumia kila njia inayowezekana kunizuia kumwamini Mwenyezi Mungu. Waliogopa kwamba ningewahubiria mama yangu na familia yangu nzima kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na kwamba familia yangu ingeanza kumwamini Mwenyezi Mungu. Kisha hii ingepunguza idadi ya kundi lao na idadi ya michango wanayopokea kila mwezi ingepungua pia. Kweli wao ni watumishi waovu na wapinga Kristo ambao huiba matoleo kwa Mungu na ambao huwazuia watu kuingia katika ufalme wa mbinguni! Mara tu nilipoona kiini chao upinga Kristo, basi nilijua jinsi ya kushughulika na watu hawa. Waliamini katika Mungu na bado walimpinga Mungu na walikuwa maadui wa Mungu na, kwa hivyo, nilijua ilinilazimu niachane nao. Ingawa, kwa siku za hivi karibuni, nilikuwa nimepitia shida kutoka kwa usumbuaji wao, lakini nilikuwa na mwongozo na nuru ya maneno ya Mungu. Kwa kufanya kama foili[a] hasi kwa Mungu, waliniruhusu kukuza utambuzi na zaidi ya hayo, waliniruhusu kupata uzoefu fulani wa vitendo juu ya maneno ya Mungu. Nilijionea mwenyewe kuwa maneno ya Mungu ni ukweli, njia na uzima, na nilipata uhakika zaidi kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa kweli. Nilihisi mwenye furaha sana na mtulivu moyoni mwangu na nikafanya azimio kimya: Bila kujali jinsi Shetani anajaribu kunisumbua, sitawahi kumsaliti Mungu kamwe, na nimeazimia kuwa shahidi kwa Mungu na kumdhalilisha ibilisi Shetani!

Sikutarajia kwamba, baada ya siku mbili tu za amani, ningekumbana na kusumbuliwa na uonevu wa Shetani. Usiku mmoja, mama yangu, wajomba, shangazi wangu wachache pamoja na dadake bibi yangu walikuja kujaribu kunizuia nisimwamini Mwenyezi Mungu. Nilipoona wote wamekusanyika pamoja, nilikasirika sana. Nilifikiria, “Ninamwamini tu Mungu wa kweli. Kuna nini mbaya na hilo? Kwa nini hawakomi kuhusu jambo hili?” Dadake bibi yangu alisema kwa sauti ilikuwa ngeni, “Njoo, Xiaoyou. Twende nyumbani kumuona bibi yako.” Nilishangaa kumsikia akisema hivi na nikawaza: “Wamekuja kunipeleka nyumbani kwa mama yangu. Wanataka kunifungia ndani pamoja na bibi yangu aliyechanganyikiwa kiakili! Masikini, jamaa zangu wanawezaje kunifanyia hivyo? Wanawezaje kuwa wakatili hivyo?” Wakati tu nilikuwa nikifikiria hili, mama yangu alichukua kamba na kunikimbilia, akachuchumaa chini na kuanza kuifunga miguu yangu pamoja. Nilipatwa na wasiwasi sana. Nilisukuma mikono yake mbali na kupiga kelele, “Unafanya nini? Kwa nini unataka kunifunga?” Kuona haya, wajomba wangu wawili walinijia na kila mmoja wao akashikilia moja ya mabega yangu ili nisipinge. Wakati huo nilikuwa nimekaa kwenye sofa na sikuweza kusimama. Nilimlilia Mungu kwa haraka moyoni mwangu: “Ee Mungu! Wanajaribu kunifunga na kunichukua mbali. Wakifanikiwa, sitaweza kukuamini na sitaweza kulipata kanisa. Ee Mungu! Nipe imani na nguvu na Unifungulie njia!” Baada ya kumaliza kuomba, nilihisi nguvu ikiongezeka mwilini mwangu. Nilijitahidi na kupiga kelele, “Mnafanya nini? Niachilie niende!” Walipoona jinsi ninavyokuwa nikipinga vikali, waliniachilia. Nilihisi mwenye shukrani sana kwa Mungu. Niligundua kweli kwamba mtu akimtegemea Mungu kwa kweli, mtu atashuhudia matendo ya Mungu. Pia nilihisi kuwa Mungu yuko kando yangu, Akilinda na kunichunga kila wakati. Niliwaza: “Katika mazingira haya, lazima nimpe Mungu moyo wangu wa kweli na lazima nimwaibishe kabisa ibili Shetani.” Kwa hivyo niliwaambia kwa uthabiti, “Ikija kwa masuala mengine, nitawasikiliza. Hata hivyo, ikija kwa suala la kuamini katika Mungu nitamsikiliza Mungu pekee! Tayari nina uhakika kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana aliyerejea. Haijalishi mnavyojaribu kunilazimisha, sitatikiswa!” Mara tu nilipoazimia kumfuata Mungu, nilishuhudia matendo ya Mungu tena. Mmoja wa shangazi wangu alisema, “Msimfunge. Haitasaidia. Ninaona amefanya uamuzi kuhusu imani yake.” Ni wakati tu shangazi yangu alisema hivyo ndipo wote waligeuka na kuondoka kwa kukata tamaa. Baada ya wao kwenda, mara moja nilihisi mchovu na goigoi kimwili na kiakili. Sikuwa na nguvu yoyote. Nililala kitandani mwangu na kulala. Asubuhi iliyofuata, nilifikiria juu ya kile kilichotokea usiku uliopita kwa moyo mzito. Wakati nilifikiria kuhusu jinsi jamaa zangu walikuwa wakinitesa, sikuweza kujizuia ila kufikiria: “Ah, mama yangu na ndugu zangu wamedanganywa na uvumi unaosambazwa na makasisi na viongozi wa kanisa, na wanaendelea kujaribu kunishurutisha. Je, yote haya yataisha lini?” Kisha nikawaza kuhusu wakati nilipokuwa pamoja na ndugu zangu kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa moyo mmoja, tulikuwa tumefuatilia ukweli na kutimiza wajibu wetu, kila mtu alikuwa amesaidiana na kuungana mkono. Hakuna mtu aliyejaribu kumnyanyasa au kumkandamiza mtu mwingine yeyote, na hakukuwa na haja ya kuwa mwangalifu. Nilihisi huru na mwenye kuachiliwa, na nilihisi mwenye kuridhika na mtulivu kila siku. Lakini sasa nilikuwa nimefungiwa nyumbani kwangu, sikuwa na uhuru wowote, na nilikuwa naishi kila siku kwa wasiwasi. Sikuwahi kujua ni lini ndugu zangu au watu kutoka katika kanisa langu la zamani wangetokea. Hali ikiwa nzuri, wangenikosoa kidogo. Mbaya zaidi, walinitishia na kujaribu kuniogofya. Nilihisi uchungu na kukosa furaha sana. Nilitaka sana kurudi kwenye Kanisa la Mwenyezi Mungu na kuhudhuria mikutano, kuimba nyimbo na kumsifu Mungu pamoja na ndugu zangu.

Mara tu kufuatia tukio hili, kitu kilitokea ambacho kisichotarajiwa hata zaidi. Siku moja, mimi na mume wangu tulienda kufanya ununuzi. Baada ya kurudi nyumbani, nilitaka kusoma maneno ya Mungu kwenye chombo changu cha kucheza MP5 lakini sikuweza kukipata. Nilihisi mwenye wayowayo na wasiwasi. Niliwaza: “Kicheza MP5 changu kilienda wapi? Bila shaka nilikiacha nyumbani. Mbona siwezi kukipata?” Ghafla nilifikiria mama yangu lazima amekichukua. Nilikumbuka kuwa kuna siku moja mama yangu aliingia na akaniona nikisoma neno la Mungu kwenye kicheza MP5. Baada ya hapo, angekuja nyumbani kwangu na kupekua vitu vyangu. Nilikuwa na hakika kwamba sababu ya kicheza MP5 changu kutopatikana ni kwamba alikuwa amekichukua. Nikiwa na wazo hili, nilikasirika sana, na nikaenda nyumbani kwa mama yangu kwa kishindo. Nilipoingia, niliona kuwa mama yangu alikuwa akiongea na dadake bibi yangu. Nilimwendea na kumwambia, “Mama, ulichukua kicheza MP5 changu? Hicho ni changu. Ikiwa ulikichukua, nirudishe mara moja.” Nilishangaa kwamba mama yangu alikataa kata kata kwamba hakuwa amekichukua. Alinipa sura ya dharau, na nikasema kwa hasira, “Mimi huweka kicheza MP5 changu nyumbani. Hakuna mtu mwingine angeweza kukigusa. Wewe ndiye mtu wa pekee ambaye hupekua vitu vyangu mara kwa mara. Bila shaka ni wewe uliyekichukua. Nirudishie!” Akikabiliwa na mahojiano yangu, mama yangu akajibu kwa toni kali ya sauti, “Sitakirudisha kwako. Ni bora uende nyumbani kwani hatakipata kutoka kwangu kamwe!” Haijalishi nilisisitiza kiasi, hakunirudisha, kwa hivyo sikuwa na chaguo ila kwenda nyumbani mikono mitupu. Nikiwa njiani kurudi nyumbani, nilihisi vibaya sana. Nilifikiria: “Sina tena kicheza MP5 changu kwa hivyo siwezi kusoma maneno ya Mungu tena. Zamani, hata ingawa mama yangu na wengine walikuja kunisumbua, bado niliweza kusoma maneno ya Mungu na kuwa na mwongozo na uongozi wa maneno ya Mungu. Kama matokeo, niliweza kuelewa mapenzi ya Mungu na nikawa na imani na nguvu ya kuhimili mashambulio yao. Lakini sasa, sina tena kicheza MP5 changu! Nitafanya nini? Bila maneno ya Mungu, si mimi nimeisha?” Kadiri nilivyofikiria juu hilo ndivyo nilivyohisi kukosa tumaini zaidi, na roho yangu ikaingia katika uhasi. Nilihisi asiyejiweza kabisa. Katika wakati wangu dhaifu na wa kuvunja moyo zaidi, wimbo wa maneno ya Mungu ulielea akilini mwangu: “Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! … Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana(“Tafuta Kumpenda Mungu Bila Kujali Mateso Yako Ni Makubwa Vipi” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, nilielewa kuwa Mungu alikuwa anatarajia kuwa ningeweza kumshuhudia katika hali hii. Bila kujali jinsi mambo yalivyokuwa magumu, ilibidi niwe mwaminifu kwa Mungu hadi mwisho na nisipoteze imani kwa Mungu. Nilifikiria nyuma juu ya mateso yote niliyopitia, na nikagundua kuwa kila tukio lilikuwa vita katika ulimwengu wa kiroho. Shetani alikuwa akitumia njia za kila aina kunivunja kipande baada ya kipande. Hivi sasa, alikuwa ameninyang’anya “chakula cha maisha yangu ya kiroho” kwa hamu ya kuimeza roho yangu. Shetani kweli ni mwovu. Nilijua kuwa lazima nisishindwe na njama zake. Hata ingawa kicheza MP5 changu kilikuwa hakipo, bado nilikuwa na Mungu. Mungu bado angenipa nuru na kunielekeza, na niliamini kuwa mradi nimtegee Mungu kila wakati, Mungu angenisaidia kupita katika kila ugumu na shida. Bila kujali ni hali gani ningelazimika kukumbana nazo katika siku za usoni, mradi tu ningekuwa na pumzi moja iliyobaki mwilini mwangu, ningekuwa shahidi kwa Mungu. Maneno ya Mungu kwa mara nyingine yalinielekeza na yalinipa imani ambayo nilihitaji kuendelea.

Kwa kupitia mateso haya na shida tena na tena, nilishuhudia nguvu na mamlaka ya maneno ya Mungu. Kila wakati nilipokuwa hasi, dhaifu, mwenye kuchanganyikiwa na kufadhaika, maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu niliyohitaji na kunielekeza nione miradi ya Shetani na kusimama kama shahidi kwa Mungu. Wakati huo huo, niliweza kuona kuwa Mungu alikuwa kando yangu kila wakati, Akiwa kama msaada wangu na kunifungulia njia. Imani yangu kwa Mungu iliongezeka polepole na tamanio langu la kuachana na familia yangu liliongezeka. Nilijua kuwa nilipaswa kutoroka kutoka kwenye “tundu la chui” mara tu nilipoweza na kwenda kutafuta kanisa na ndugu zangu. Kwa hivyo nilimwomba Mungu na kumwaminia jambo hili, na nikamwomba Mungu aniongoze. Siku chache baadaye, niliweza kukwepa uchunguzi wa kaka yangu na nikaondoka nyumbani kwa mafanikio. Kwa mara nyingine tena, nilirudi katika Kanisa la Mwenyezi Mungu kuishi maisha ya kanisa na kutekeleza wajibu wangu kadiri ya uwezo wangu. Zaidi ya mwezi wa uchungu ulikuwa umefika mwisho hatimaye, na hisia za ukandamizaji na wasiwasi ndani ya moyo wangu zikatoweka kama moshi hewani. Namshukuru Mungu kwa kunielekeza kushinda ushawishi mwovu wa Shetani na kutoroka kutoka katika “tundu la chui,” na kwa mara nyingine tena kunielekeza kurudi kwa familia ya Mungu.

Tukio hili linabaki jipya katika kumbukumbu yangu kwa sababu wakati huo nilishuhudia wazi upendo na wokovu wa Mungu, na nikaona kwamba Mungu alikuwa kando yangu Akinilinda kila wakati, na kunizuia kudanganywa na kumezwa na Shetani. Wakati huo huo, tukio hili la ajabu pia liliniwezesha kukuza utambuzi wa makasisi, viongozi wa kanisa, na wengine. Walimshutumu na kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa hasira na walibuni uvumi na kutoa ushahidi wa uongo ili wanidanganye. Walitumia hila za kila aina kujaribu kunizuia kumfuata Mwenyezi Mungu. Wao ni vizuizi na vikwazo kwa sisi kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, kupokea wokovu wa Mungu na kupatwa na Mungu, nao ni pepo wa kishetani ambao wamekuja kuzitekeza roho za watu! Ilikuwa wakati huu ndipo mwishowe nilielewa maana ya kweli ya maneno yafuatayo ambayo Mwenyezi Mungu alinena: “Waumini na wasioamini hawalingani ila wanapingana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja). Niligundua kwamba hata kama makasisi, viongozi wa kanisa, watawa, washiriki wa kanisa langu la zamani na mama yangu walionekana kuamini katika Mungu kwa juu juu, hawakuielewa sauti ya Mungu na hawamjui Mungu. Walikataa kukubali kazi ya Bwana aliyerejea, na kwa hivyo Mungu haitambui imani yao. Machoni pa Mungu, wao ni wasioamini. Wao ni magugu yaliyofunuliwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho na kwa kweli, ni pepo na wapinga Kristo wanaompinga Mungu. Kwa kuongezea, pia niliona kwamba mateso kutoka kwa wanafamilia na kusumbuliwa na watu wa dini yote ni mashambulio yanayotoka kwa Shetani, na kwamba ni vita vikali vinavyopiganwa katika ulimwengu wa kiroho. Shetani alitaka kuwatumia watu hawa, matukio na vitu kunisumbua, kunisababisha niikane njia ya kweli, kumsaliti Mungu, kuingia ndani ya “kumbatio”, nipoteze nafasi ya kuokolewa na Mungu na kuangamizwa pamoja naye kuzimu. Hata hivyo, hekima ya Mungu inatekelezwa kwa msingi wa njama za Shetani. Kila mara Shetani aliponishambulia na kunisumbua, Mungu alinielekeza na kuniongoza katika kila hatua ili niweze kupitia maneno Yake, na kukuza utambuzi na ufahamu kupitia katika maneno Yake. Mungu pia aliikamilisha imani yangu Kwake, na Akaiwezesha imani yangu Kwake kuwa ya kweli, thabiti, na isiyo dhaifu tena. Namshukuru Mungu kwa kunielekeza na kunisaidia nielewe ukweli fulani kwa zaidi ya mwezi mmoja tu. Sasa najua tofauti kati ya wema na uovu, kati ya uzuri na ubaya. Imani yangu kwa Mungu imeimarishwa na nimesonga karibu zaidi na Mungu. Uchungu kweli ni baraka ya Mungu! Katika maisha yangu ya baadaye ya imani, natamani kupitia kazi zaidi ya Mungu na niko tayari kumfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho kabisa!

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kupenya Ukungu ili Kuona Mwanga

Na Xinxin, ChinaMimi ni mfanyakazi wa kawaida. Mwishoni mwa Novemba, 2013, mfanyakazi mwenza aliona kwamba mke wangu na mimi tungefanya...

Kuwa katika Hatari Kubwa

Nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Mchungaji na wazee hawajaacha kunisumbua na kuwashawishi...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp