Ufanisi

14/01/2020

Na Fangfang, China

Sote katika familia yangu tunamwamini Bwana Yesu, na wakati nilikuwa muumini wa kawaida tu katika kanisa letu, babangu alikuwa mmoja wa wafanyakazi wenza wa kanisa. Mnamo Februari mwaka wa 2004, nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na nikamhubiria injili ya ufalme dadangu mdogo zaidi punde baadaye. Mwanzoni nilikuwa napanga kushuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa babangu baada ya kujitayarisha na maneno na ukweli kiasi wa maneno ya Mungu. Lakini nilishangaa kuwa babangu aliposikia kwamba nilikuwa nimekubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, alishikwa na hasira, akijaribu kuvuruga na kuzuia imani yangu.

Jioni moja, babangu alikuja nyumbani kwangu kwa hasira na kuniambia kwa ghadhabu, “Singewahi kuamini kwamba ungeweza kupuuza ushauri wangu na ushauri wa kiongozi wetu wa kanisa na kuanza kuliamini Umeme wa Mashariki! Ni vyema uharakishe na uende nyumbani kwa kiongozi na utubu, na umwombe Bwana asamehe dhambi zako!” Nilijibu, “Baba, nimesoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu na kweli naamini kwamba ni sauti ya Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, na nina uhakika wa imani yangu. Enzi ya Neema tayari imeisha, na sasa tuko katika Enzi ya Ufalme. Mungu amekuja kufanya kazi mpya na kutupeleka katika karamu ya harusi ya Mwanakondoo. Je, si Biblia inasema, ‘Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo(Ufunuo 14:4)? Katika kumwamini Mwenyezi Mungu, nafuata nyayo za Mwanakondoo….” Lakini bila kujali nilichosema, babangu hakuwa na hamu ya kukisikia na aliendelea kusisitiza kunipeleke kumwona kiongozi wa kanisa. Mume wangu pia alijiunga naye katika kunishurutisha. Uso wa babangu uliniambia kwamba alikuwa amedhamiria kabisa kunirudisha katika kanisa langu la zamani. Niligundua kwamba hisia zilikuwa zikipanda na walikuwa wakiniwekea shinikizo sana, na sikuwa na budi ila kuhisi wasiwasi kiasi. Kwa hiyo nilimwomba Mungu kimoyomoyo na kutaka anilinde na kuniongoza. Kwa hakika, bila kuniacha niseme jambo jingine, babangu alimfanya mume wangu atupeleke sote kwa gari hadi pahali pa kukutana pa kanisa langu la zamani. Nilipoingia chumbani na kuona watu 60 ama 70 wakisubiri hapo—akiwemo dadangu mdogo zaidi, aliyeletwa hapo na mama mkwe wake—niligundua kwamba mkutano huu wote ulikuwa umepangwa kabla na kwamba wangetushambulia sisi wawili. Kila mtu katika chumba hicho alikuwa akinitazama mimi na dadangu kwa jinsi isiyo ya kawaida, na wengine wao walikuwa wakituelekezea vidole na kunong’onezana wao kwa wao. Kiongozi wetu mkubwa alitujia kwa haraka na mara moja akaanza kutuhimiza tuache kumwamini Mwenyezi Mungu. Kisha akaanza kuishutumu na kuikufuru kazi ya Mungu ya siku za mwisho bila kujizuia. Hata alisema uongo mwingi, kama vile, “Watu wanaojiunga na Kanisa la Mwenyezi Mungu hawawezi kuondoka kamwe, na wakiepa pua zao hukatwa na macho yao kutolewa….” Kwa kuzungumza uongo huu na kuchochea waumini, kiongozi aliwafanya babangu na mama mkwe wa dadangu wawe na hasira na hamaki zaidi, na walitufanya tufumbe macho yetu na kumtaka kiongozi atuombee. Ingawa nilichukizwa na kile walichokuwa wakifanya, na hatukusema chochote wakati kiongozi alikuwa akituombea, uongo ambao kiongozi alikuwa amesema tayari uliniathiri kwa kina.

Nilipofika nyumbani, bado niliweza kusikia huo uongo mbaya sana ukivuma masikioni mwangu na amani ya akili yangu ilivurugwa. Hata singeweza kumakinikia maneno ya Mungu. Nilifikiria kuhusu jinsi tayari nilikuwa nikiwasiliana na Dada Zhang wa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa muda fulani na jinsi alivyokuwa mwenye heshima na mwadilifu daima katika usemi wake na tabia yake. Dada Zhang pia alionyesha upendo mwingi sana kwa jinsi alivyoshiriki nasi na hakuwa jinsi kiongozi wa kanisa alivyoelezea hata kidogo. Lakini jambo muhimu kabisa lilikuwa kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yalikuwa ukweli, na yalijaa mamlaka na nguvu. Hakuna mwanadamu ambaye angeweza kuonyesha maneno kama hayo na nilidhani lazima yawe matamshi ya Mungu. Kwa hivyo mbona kulikuwa na uvumi mwingi sana wa kutisha kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu? Na kwa hiyo, niligaagaa na kugeuka kitandani usiku mzima, nisiweze kulala huku fikira zangu zikibadilika kutoka mema hadi mabaya na kwa mema tena, tena na tena. Siku iliyofuata nilihisi mwenye usingizi na mlegevu—niliyesumbuka kwa njia iliyokuwa ngumu kueleza—na sikutaka kufanya chochote. Dadangu mdogo zaidi alikuja kwangu, na punde ikawa dhahiri kwamba hakuweza kustahamili kushambuliwa na kiongozi na mama mkwe wake. Hakuthubutu tena kumwamini Mwenyezi Mungu na sasa alikuwa akinihimiza niachane na imani yangu katika Mwenyezi Mungu pia. Nilimwambia kwa wasiwasi, “Dada, najua una wahaka, na pia mimi nimekanganyikiwa na kufadhaika sana, kama wewe tu. Lakini nimefikiria juu ya shida hii sana, na pia kumwomba Bwana aniongoze, na kwa hiyo bila kujali kile ambacho kiongozi na wengine wanasema, kuna jambo moja ambalo tunaweza kuwa na uhakika nalo, na hilo ni kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu hayangeweza kamwe kusemwa na mwanadamu. Nina uhakika kwamba maneno haya ni sauti ya Mungu. Nimesoma ‘Kitabu Chafunguliwa na Mwanakondoo’ mara nyingi, na kitabu hiki kinafichua siri za mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita. Kusoma kitabu hiki kulinifunza kwamba kuna hatua tatu za kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu, na kwamba kazi ya hukumu kwa maneno ya siku za mwisho itamwokoa mwanadamu kabisa. Ni kazi ya hukumu pekee inayoweza kutuwezesha kuondoa pingu za asili yetu ya dhambi kwa kweli na kupata utakaso ili tuweze kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Maudhui ya kitabu yanakubaliana kabisa na unabii wa Bwana katika Biblia na yana ukweli ambao haupatikani katika Biblia. Ni Mungu tu ambaye angeweza kujua ukweli na siri hizi. Kwa hiyo hii ndiyo maana nina uhakika sana kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ndiyo sauti ya Mungu na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi ambaye tumemtamani sana! Dada, imani yetu si ya makosa. Chochote ufanyacho, usiiache njia ya kweli kwa urahisi hivyo!” Baada ya dadangu mdogo zaidi kuondoka, nilihisi huzuni sana na kuwaza: “Ni dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Ni kweli na sahihi sana. Kwa hivyo mbona kiongozi wa kanisa na familia yetu isituwache tumwamini?” Nilipokuwa tu nikifikiria hili, simu ya rununu ya mume wangu ililia. Ilikuwa babangu, na alitaka niende nyumbani kwake mara moja. Nilijua bila shaka kwamba babangu angenisumbua tena, kwa hiyo nilisema kwamba sikutaka kuenda, lakini mume wangu alinishika ghafla na kunivuta hadi kwenye gari. Nilipofika nyumbani kwa babangu, niliona kwamba dadangu mdogo zaidi na mama mkwe wake walikuwa hapo tayari. Aliponiona, uso wa babangu ukawa mgumu, na akasema, “Jana usiku kiongozi wa kanisa aliombea kusamehewa kwa dhambi zenu mbele za Bwana Yesu. Lakini hakuna kati yenu ambaye tayari amekiri dhambi zake na kutubu. Nimewaita ninyi wawili hapa leo ili muweze kusema sala ya toba kamili mbele za Bwana, na ili msiendelee kumwamini Mwenyezi Mungu tena….” Niliposikia hili, nilihisi kuchoka sana. Nilijiwazia: “Kwa kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho nafuata nyayo za Mwanakondoo na kukaribisha kurudi kwa Bwana. Kuna dhambi gani hapo? Sitasema uongo na kuzungumza upuzi kwa kujua.” Kwa kuona kuwa singesema sala ya toba, wazazi wangu na mama mkwe wa dadangu walianza kunishambulia. Walianza kumkashifu na kumkufuru Mwenyezi Mungu na kurudia kusema uongo huo mbaya ili kunilazimisha nikiri na kutubu. Kuwa na uongo huo wote akilini mwangu na familia yangu kunishambulia kila wakati kulinifanya nihisi kupungukiwa na pumzi, na nikaanza kuhisi kizunguzungu na dhaifu. Nilijiwazia: “Wakiendelea kunishurutisha kila siku, sitaweza kuwasiliana na ndugu wala sitaweza kusoma maneno ya Mungu vizuri. Sidhani nitaweza kuchukua njia hii maalum ya imani katika Mungu….” Wakati huo tu, wazazi wangu na huyo mama mkwe walinishika ghafla na kunilazimisha mimi na dadangu kufunga macho yetu na kutubu. Kuona jinsi walivyokuwa wakitenda kwa ujeuri kulinifadhaisha sana, na sikuweza kuzuia machozi kububujika machoni pangu. Nilipokuwa nikilia, nilimwomba Bwana: “Ee Bwana Yesu, najua kwamba Umerudi kama Mwenyezi Mungu, lakini sasa hivi sina ujasiri wa kukuamini. Nakuomba unisamehe na kusamehe dhambi zangu.” Baada ya kufika mahali hapa katika maombi yangu, nilikuwa nikilia sana kiasi kwamba singeweza kuendelea, na kwa hivyo maombi yangu yaliisha. Baada ya hayo, ghafla nilihisi mwenye akili chache sana, ujasiri wangu wote ukatoweka, na sikuweza kuhisi uwepo wa Mungu hata kidogo. Nilihisi mwenye mashaka sana, na nikamwambia dada yangu mdogo zaidi, “Kabla ya sala hiyo ya toba nilihisi kwamba bado nilikuwa na nguvu kiasi, lakini baada ya kuisema nilihisi kuchoka kabisa, kana kwamba Roho Mtakatifu ameniacha. Kwa kweli, kumwamini Mwenyezi Mungu ni kumfuata Bwana, na kwa kusema sala hiyo ya toba tumemsaliti Bwana.”

Ugomvi uliokuwa moyoni mwangu uliendelea baada ya mimi kufika nyumbani. Nilikuwa nimesoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu na nilikuwa nimetambua kwamba yalikuwa matamshi ya Mungu. Nilijua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi na kwamba kutomkubali kungekuwa kumsaliti Mungu, jambo ambalo lingenisababisha kukosa kupata wokovu, na pia kushutumiwa na Mungu. Lakini ikiwa ningesisitiza kumwamini Mwenyezi Mungu, basi kiongozi wa kanisa na babangu hakika wangeendelea kunisumbua na singekuwa na amani tena kamwe. Kweli nilihisi kwamba sikuwa na ujasiri wa kuvumilia katika imani yangu. Akili yangu ilikuwa katika machafuko, nilikumbana na ugumu kila nilipogeuka, na sikujua cha kufanya hata kidogo. Kichwa changu kilikuwa kikivuma, na nilihisi nilikuwa karibu kuharibikiwa akili. Nilimtaka Dada Zhang aje ili niweze kumrudishia kitabu cha maneno ya Mungu, na katika kufanya hivyo ningeweza kujiondolea maisha haya ya machungu.

Siku chache baadaye, Dada Zhang alikuja kwenye duka kunisaidia. Nilikuwa na wasiwasi sana, kwani nilikuwa na wahaka kwamba mume wangu angemuona na kumwambia babangu. Na kwa hiyo, kwa haraka, nilimweleza yote ambayo yalikuwa yametendeka katika siku chache zilizopita. Kisha niliharakisha kuchukua kitabu cha maneno ya Mungu ambacho nilikuwa nimeficha chini ya makasha machache ya bidhaa na kumpa. Nilimwambia, “Dada, wazazi wangu na mume wangu wananisumbua, na kiongozi na ndugu kutoka katika kanisa langu la zamani wananizuia sana kiasi kwamba nahisi kuchoshwa kabisa na wasiwasi. Siwezi kuvumilia tena, kwa hivyo tafadhali kichukue kitabu hiki.” Dada Zhang alinitazama, na kwa uaminifu mkubwa akasema, “Dada, tumekubali kazi mpya ya Mungu ya siku za mwisho, na kwa hivyo vurugu na mkazo huu kutoka kwa viongozi wa dini na familia kweli ni vita vinavyofanywa katika ulimwengu wa kiroho! Bwana Yesu alisema: ‘Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani: sikuja kuleta amani, bali upanga(Mathayo 10:34). ‘Na maadui wa mtu watakuwa wale wa kaya yake mwenyewe(Mathayo 10:36). Kutoka katika maneno ya Bwana tunaweza kuona kwamba Mungu kuja duniani kufanya kazi ya wokovu hakika kutaishia na vita katika ulimwengu wa kiroho. Hiyo ni kwa sababu watu wanaomwamini Mungu kweli na kupenda ukweli watamfuata Mungu watakaposikia matamshi ya Mungu. Hili hakika litachochea uhasama wa wale wote waliochoshwa na ukweli, wanaochukia ukweli, na wanaompinga Mungu. Kama matokeo, pande mbili—walio wema, ambao ni wa Mungu, na walio wabaya, ambao ni wa Shetani—zitafichuliwa na kila atatengwa kulingana na aina yake mwenyewe. Huu ni uweza na hekima ya Mungu! Zamani wakati Bwana Yesu alianza kwanza kufanya kazi Yake, watu wengi wa kawaida wa Kiyahudi ambao walisikia matamshi ya Bwana Yesu na kushuhudia nguvu Yake kuu walikuja kuamini kwamba Bwana Yesu alikuwa Masihi aliyekuwa ametabiriwa, na kwa hiyo wakamfuata. Lakini makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo wote, waliowaona watu wa kawaida wakiwaacha na kumfuata Bwana Yesu, walianza kubuni na kueneza uvumi mwingi ili kuwadanganya watu wa kawaida. Walisema kwamba Bwana Yesu alimtegemea Beelzebuli mfalme wa pepo kufukuza pepo, na kwamba Alikuwa mlafi na aliyependa kunywa mvinyo. Na Bwana Yesu alipofufuka, waliwahonga wanajeshi wa Kirumi kwa fedha kubuni na kueneza uvumi kwamba mwili wa Bwana Yesu ulikuwa umeibwa na wanafunzi Wake. Hizi ni baadhi za njia ambazo walijaribu kuwazuia watu kukubali wokovu wa Bwana Yesu. Na ni nini kilichofanyika mwishowe kwa Wayahudi wote walioamini kile ambacho viongozi wao wa dini walisema na hawakuthubutu kumfuata Bwana Yesu? Walipoteza wokovu wa Bwana, pia waliadhibiwa na kulaaniwa na Mungu: Israeli ilishindwa kwa karibu miaka 2000, na Wayahudi walienda uhamishoni duniani kote, ambapo wengi wao waliteswa na kuuawa. Haya yalikuwa matokeo mabaya sana yaliyosababishwa na wao kumsulubisha Bwana na kuikosea tabia ya Mungu vibaya. Leo, Mungu amepata mwili tena kufanya kazi Yake, na historia sasa inajirudia. Viongozi wa dini wa leo ni kama tu Mafarisayo wa zamani: Wanaona wazi uhalisi wa Mungu kuja kutenda kazi Yake, kuonyesha ukweli na kuwaokoa watu, lakini kwa sababu hawapendi ukweli wanakataa na kuishutumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Ili kulinda vyeo vyao na kuhifadhi riziki zao, wanabuni uvumi kumpinga na kumshutumu Mungu na kutumia uvumi huu kuwadanganya na kuwadhibiti watu. Hata wanatumia na kuwachochea watu wengine wasiojua kuwashurutisha waumini ambao wamekubali njia ya kweli, na wanajaribu kwa hasira kuwavuruga na kuwazuia watu kumrudia Mwenyezi Mungu, hivyo kuharibu nafasi ya mwisho ya watu ya wokovu. Dada, lazima tuweze kuona kwa uwazi hivi ni vita vya kiroho na kubaini njama za ujanja za Shetani.” Baada ya kusikia ushirika wa Dada Zhang, kila kitu kilikuwa dhahiri ghafla: Kutoka nyakati za zamani, njia ya kweli daima imeteswa na kweli nilikuwa katika vita vinavyoendelea vya kiroho! Viongozi wa kanisa langu la zamani walikuwa wakibuni uvumi na kushutumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na walikuwa wakinitesa na kunisumbua tena na tena ili kunikomesha kumwamini Mwenyezi Mungu, yote kwa sababu walichukia ukweli na walikuwa maadui wa Mungu, Ushirika wa dada huyo ulinisaidia kuelewa kwa nini vitu hivyo vilikuwa vikinitendekea, lakini bado nilihisi dhaifu sana na mwenye hofu sana kukiweka kitabu cha maneno ya Mungu. Nilijua kwamba babangu na wale wengine wangekuja nyumbani kwangu na kulalamika ikiwa ningekiweka na wangefanya maisha ya familia kuwa magumu kwangu, kwa hivyo nilisita kukiweka kitabu hicho. Kwa kuona kwamba nilikuwa katika hali ngumu, Dada Zhang alinipa nambari ya simu na kusema, “Dada, waonaje hivi—nitakichukua kitabu cha maneno ya Mungu nyumbani nami na kukuwekea salama. Wakati wowote unapohisi kukisoma, nipigie tu simu na nitakileta mara moja.” Nilikubali na kumsindikiza Dada Zhang hadi mlangoni. Wakati huo tu, mume wangu alikuja akikimbia na huku akimwelekezea Dada Zhang kidole, akasema kwa sauti. “Chukua kitabu hicho na uondoke, sasa hivi. Na usirudi tena, la sivyo nitakukaripia!” Huku nikimtazama Dada Zhang akiondoka na kutoweka, nilihisi fadhaa na huzuni sasa kwa njia ambayo ilikuwa ngumu kueleza.

Mwanzoni, nilidhani kwamba kumrudishia Dada Zhang kitabu cha maneno ya Mungu kungemaanisha kwamba babangu angeacha kunisumbua na kwamba maisha ya utulivu ambayo nilikuwa nayo awali yangeendelea. Kwa kweli, mambo yalitokea kuwa kinyume kabisa: Sikuhisi amani moyoni mwangu, lakini badala yake kweli nilihisi utupu usioelezeka humo, Nilikosa uhai katika chochote nilichofanya, na maneno ya Mwenyezi Mungu na nyimbo za maneno ya Mungu yaliendelea kuingia kichwani mwangu nyakati zote za mchana na usiku. Nilimjua Mwenyezi Mungu kuwa Bwana Yesu aliyerudi, na kwamba maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli; hata hivyo, mambo ambayo kiongozi wa kanisa aliniambia, na matukio ya babangu na wengine kunisumbua na kunishambulia pia yaliendelea kunijia akilini mwangu. Nilikuwa nikiteseka vibaya, na nilihisi kana kwamba nilikuwa nimeanguka ndani ya lindi kuu ambalo singeweza kujiondoa kwa kupanda. Sikuweza kula ama kulala vizuri, na nilihisi msongo sana, kana kwamba kichwa changu kilikuwa karibu kupasuka. Katikati ya uchungu huu wote, nilipiga magoti na kumsihi Mungu: “Ee Mungu, Mungu mmoja wa kweli aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote hai! Nina uchungu mwingi sana na nahisi kupotea sana sasa hivi. Najua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, lakini kimo changu ni kidogo sana na wakati wowote ninapofikiria kuhusu usumbufu na mashambulizi ninayopata kutoka kwa babangu, nahofia sana kukufuata. Ee Mungu, niko katika njia panda, nisiweze kufanya uamuzi. Sijui la kufanya, kwa hiyo tafadhali niongoze na unielekeze….” Wakati wa sala hiyo, bila kugundua, ghafla nilianza kufikiria maneno haya ya Mwenyezi Mungu: “Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. … Usiwe na hofu; kwa msaada Wangu, ni nani angeweza daima kuzuia barabara? Kumbuka hiki! Kumbuka!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 10). Maneno ya Mungu yalinipa mlipuko wa nguvu iliyotosha kuufanya moyo wangu wenye woga uwe wenye nguvu. “Ndiyo!” Nilifikiri. “Nikiwa na Mungu kama msaada wangu, kuna nini cha kuogopa kweli? Kwa kuwa tayari nimeamua kwamba hii ndiyo njia ya kweli, basi sipaswi kuzuiwa na mtu, tukio ama jambo lolote. Lazima nipenye katika nguvu za giza na kumfuata Mungu kwa azma thabiti. Kama muumini wa Mungu, ikiwa siwezi kukubali imani yangu ninapokabiliwa na nguvu katili za Shetani basi mimi ni muumini wa aina gani? Je, si najisalimisha tu kwa Shetani na kumsaliti Mungu?” Kisha nilikumbuka jinsi, katika ushirika wake, Dada Zhang alikuwa ameniambia kwamba usumbufu kutoka kwa familia yangu na kiongozi wa kanisa wote ulikuwa sehemu ya vita vya kiroho, na kwamba ningeamua kusimama nao, basi ningekuwa nikianguka hasa katika mtego mjanja wa Shetani. Hilo lingemaanisha kwamba ningepoteza kabisa nafasi yoyote ya kuokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kisha nilifikiria kuhusu mateso ya kiroho ambayo nilikuwa nimepitia tangu Dada Zhang achukue kitabu cha maneno ya Mungu. Nilihisi kwamba singeweza kukosa kuwa na Mungu maishani mwangu na kwamba kumwacha Mungu kulikuwa chungu zaidi kuliko kuachwa na familia na kanisa langu la zamani. Kwa hivyo nilichukua simu na kumpigia Dada Zhang, na kupanga mahali pa kukutana naye ili niweze kupata tena kitabu cha maneno ya Mungu.

Baada ya hapo, kila wakati ambapo mume wangu hakuwa nyumbani, ningechukua fursa ya kusoma maneno ya Mungu na kuimba nyimbo kwa shauku. Nilivyozidi kusoma maneno ndivyo nilivyoyafurahia zaidi, na nilivyozidi kuimba nyimbo, ndivyo nilivyohisi aliyepumzika na mwenye utulivu zaidi. Imani yangu ya awali ilirejeshwa, na maumivu na taabu yangu yote vikatoweka kama ukungu wa asubuhi. Nilihisi mara moja kwamba maneno ya Mungu yangeweza kuyaruzuku maisha yangu, na kwamba ningeweza kuishi bila chochote isipokuwa Mungu. Miezi mitatu baadaye, Dada Zhang alinipeleka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu kuhudhuria mikutano.

Bila kutarajiwa, mume wangu aligundua kuhusu mimi kuhudhuria mikutano katika Kanisa la Mwenyezi Mungu na kumwambia babangu. Jioni moja, nilikuwa kwa ghorofa ya juu niliposikia ghafla vurugu kubwa chini katika uga. Nilifungua pazia na kushikwa na woga nilipomwona babangu na wafanyakazi wenzake wa kanisa wanne ama watano wakikimbia ndani wakionekana tayari kuleta fujo. Moyo wangu ulianza kudunda, na kwa haraka nilipiga magoti na kumwita Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu, babangu amewaleta watu wa kanisa kunisumbua tena, na nina hofu sana. Ee Mungu, Unajua kimo changu ni kidogo, kwa hiyo tafadhali nipe imani na ujasiri….” Maneno haya ya Mungu yalinijia ghafla: “Lazima uwe na ushujaa Wangu ndani yako na lazima uwe na kanuni wakati unakabiliana na ndugu wasioamini. Lakini kwa ajili Yangu, si lazima pia usikubali kushindwa na nguvu zozote za giza. Tegemea hekima Yangu ili kutembea kwa njia kamili; usiruhusu njama za Shetani kuchukua umiliki. Weka juhudi zako zote katika kuuweka moyo wako mbele Zangu, nami Nitakufariji na kukuletea amani na furaha(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 10). Maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu, na sikuhisi mwoga na mwenye hofu tena. Niliwaza: “Bila kujali jinsi wanavyonisumbua sitaanguka katika mtego wa Shetani tena na kudanganywa nao. Niliumbwa na Mungu. Kuwa na imani katika Mungu na kumfuata Mungu ni sheria zisizobadilika za mbingu na dunia, na hakuna mtu aliye na haki ya kuingilia kati, hata watu walio karibu zaidi nami.” Kwa sababu hiyo, niliweza kuenda chini na kumsalimu babangu na wafanyakazi wenzake kwa njia ya utulivu. Punde waliponiona, wote walianza kuzungumza mara moja. Mfanyakazi mwenza wa kike miongoni mwao alikuwa na sura ya “masikitiko ya upendo” usoni mwake alipokuwa akisema, “Fangfang, wewe ni mtu mwerevu sana, kwa hivyo kwa nini huwezi kuelewa jinsi tunavyohisi? Sote tunakujali kwa dhati. Usiwe mkaidi sana. Kuja mbele za Bwana na utubu, sawa?” Kwa utulivu sana nilijibu, “Dada, hakuna yeyote kati yenu ambaye amesikiza mahubiri ya Umeme wa Mashariki, hakuna aliyesoma maneno ya Mwenyezi Mungu. Nawahimiza nyote mlichunguze vizuri na msimshutumu na kumpinga tu Mwenyezi Mungu bila kufikiria. Yote mnayohitaji kufanya ni kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kisha mtajua iwapo Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi ama la.” Akajibu, “Hatuthubutu kusoma kitabu hicho kwa sababu maudhui kweli yana uwezo mwingi sana wa kuwavutia watu ndani. Ni rahisi sana kuvutwa ndani.” Nikasema, “Ni hasa kwa sababu yale yote anayoonyesha Mwenyezi Mungu ni ukweli na kwa sababu maneno Yake ni sauti ya Mungu kiasi kwamba yana nguvu ya kuwatuliza watu. Ni maneno ya Mungu tu yaliyo na mamlaka na nguvu ya aina hii. Sababu ya watu kuvutiwa na maneno ya Mungu wanapoyasoma ni kwa ajili wanaweza kuelewa ukweli na kupata ruzuku ya maisha kutokana na kuyasoma. Ni nani anayeweza kuacha chemichemi ya maji hai ya uzima baada ya kuipata?” Hawakuwa na jibu ya hilo, lakini wakasema tu mambo mengi yaliyomkufuru Mwenyezi Mungu na kujaribu kunihofisha kwa kusema ningehukumiwa kuzimuni ikiwa singetubu. Kwa sauti ngumu, nikasema, “Mlilikashifu Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa kusema ‘Watu wanaojiunga na Umeme wa Mashariki hawawezi kuondoka kamwe, na wakiepa pua zao hukatwa na macho yao kutolewa.’ Hakuna chembe ya ushahidi wa kweli kwa madai kama hayo. Yote ni uvumi na kashfa mbovu! Nitafutieni mtu mmoja ambaye pua yake imekatwa ama macho yake kutolewa. Ikiwa hamwezi kutoa ushahidi wa kweli basi ninyi ni waongo wanaotaka tu kuwadanganya watu. Injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu tayari imeenea mbali katika nchi nzima ya Uchina, na kila mtu sasa amesikia kuihusu. Kuna angalau milioni chache ya Wakristo katika Kanisa la Mwenyezi Mungu sasa. Bila shaka, injili inapohubiriwa daima kuna watu fulani wanaochukia ukweli na ambao hawaukubali. Lakini mmewahi kumwona yeyote ambaye amekatwa pua ama kutolewa macho? Kungewahi kuwa na hata mmoja, vyombo vya habari vingeripoti hilo mara moja na lingekuwa kioja cha taifa. Mimi na dadangu tumekuwa tukisumbuliwa na nyinyi kwa makusudi hadi tukaacha imani yetu. Lakini tunaonekana kuwa sawa, sivyo? Mnasema uongo ili kuwadanganya watu. Kwa kumwamini Mwenyezi Mungu, nafuata nyayo za Mungu na kuchagua njia ya kweli. Sijafanya makosa yoyote, kwa hivyo sina lolote la kutubu. Imani yangu katika Mwenyezi Mungu haitawahi kuyumba, kwa hivyo ikiwa hamtaki kuamini hiyo ni sawa, lakini angalau msijaribu kunikomesha kuamini. Kuhusu mwisho wangu utakuwa upi, hakuna binadamu anayeweza kuamua, kwa sababu majaliwa ya kila mtu yako mikononi mwa Mungu. Ni kwa kuwa sambamba na kazi ya Mungu na kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho tu ndiyo watu watakuwa na hatima nzuri ya mwisho. Kwa hivyo msikuje kunisumbua tena.” Punde tu maneno hayo yalipotoka kinywani mwangu, babangu alisimama haraka na ghafla, na kwa sauti jeuri akatoa tishio hili: “Ukiendelea kumwamini Mwenyezi Mungu, basi wewe si binti yangu!”

Niliposikia tishio la babangu kuhitimisha uhusiano wetu nilifadhaika sasa, na kufikiri: “Ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu hakika ni kile ambacho Roho husema kwa makanisa. Kwa hivyo mbona usiusikize, lakini badala yake usikize uvumi na uongo unaoenezwa na viongozi wa kanisa? Unawezaje kuwa kama wao katika kunichukia kwa sababu ya kumwamini Mwenyezi Mungu, na hata kuwa tayari kukatiza uhusiano wetu?” Nilivyozidi kulifikiria, ndivyo nilivyozidi kuhuzunika, lakini ghafla nikafikiria kuhusu kifungu cha maneno ya Mungu: “Mungu aliumba dunia hii na kuleta mwanadamu, kiumbe hai ambaye alitia uhai ndani yake. Kisha, mwanadamu akaja kuwa na wazazi na jamaa na hakuwa mpweke tena. Tangu mwanadamu alipotua macho kwa mara ya kwanza katika dunia hii ya mali, ilibainika kuwa angeishi ndani ya utaratibu wa Mungu. Ni pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ndiyo hustawisha kila kiumbe hai katika ukuaji wake hadi kinapokomaa. Wakati wa mchakato huu, hakuna anayehisi kwamba mwanadamu anakua chini ya uangalizi wa Mungu, bali badala yake anaamini kwamba mwanadamu anafanya hivyo chini ya utunzaji wa upendo wa wazazi wake, na kwamba ni silika yake mwenyewe ya maisha ambayo inaongoza mchakato huu wa kukua kwake. Hii ni kwa sababu mwanadamu hajui aliyeleta maisha au yalikotoka maisha hayo, sembuse jinsi silika ya maisha husababisha miujiza(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu). Maneno ya Mungu yaliniwezesha kuelewa kwamba hata kama mwili wangu ulitoka kwa wazazi wangu, chanzo cha maisha yangu ni Mungu. “Bila zawadi ya Mungu ya maisha,” Nilifikiri, “mwili wangu ungekuwa tu kipande cha nyama inayooza, na ukweli kwamba niko hai leo ni kwa sababu ya utunzaji na ulinzi wa Mungu kabisa, vinginevyo ningemezwa na Shetani zamani. Mungu ndiye chanzo cha maisha yangu, sio wazazi wangu, na naweza kuvunja uhusiano wowote isipokuwa ule na Mungu. Wazazi wangu hawana hamu ya kutafuta ama kuchunguza kurudi kwa Bwana, pia wanaunga mkono viongozi wa kanisa kwa asilimia mia moja katika kukashifu na kuikufuru kazi ya Mungu na kujaribu kunilazimisha kumsaliti Mungu. Hili linathibitisha kwamba asili yao inampinga Mungu na iko katika uadui na Mungu, lakini sitatiwa doa na wao na kumpinga Mungu. Nitasimama upande wa Mungu, na hata wazazi wangu wakinikana, bado nitamfuata Mungu hadi mwisho kabisa, na nitasimama imara na kumshuhudia Mungu.” Kwa hiyo nilimwambia babangu, “Baba, inapofikia imani katika Mungu, namtii Mungu, sio watu, na sishawishiwi na hisia pia. Ikiwa kile ulichosema kingelingana na ukweli na mapenzi ya Mungu basi ningekusikiza. Lakini ukiniambia nimsaliti Mungu, basi sitawahi kufanya kile unachosema!” Walipoona jinsi mtazamo wangu ulivyokuwa mgumu, wote walitikisa vichwa vyao, wakasimama, na kuondoka wakionekana kuhuzunika. Wakati huo, nilihisi kwamba nilikuwa nimepata ushindi na sikuwa na budi ila kumsifu na kumshukuru Mungu moyoni mwangu: “Ee Mwenyezi Mungu, Wewe ni mwenye kudura sana. Ni maneno Yako yaliyonipa imani na ujasiri, na ambayo yalimletea Shetani kushindwa huku kamili na kwa aibu.”

Ingawa watu kutoka jumuia ya kidini hawakuja kunisumbua tena, kiongozi wa kanisa bado aliendelea kuwachochea wazazi wangu kunibughudhi. Kila siku chache wangekuja nyumbani kwangu kunihimiza nibadili mawazo yangu, na daima walisisitiza kwamba niende kwa kiongozi kutubu. Siku moja, wazazi wangu walikuja na babangu akajaribu kutumia vifungu visivyo na mantiki kutoka katika Biblia kunidanganya wakati mamangu alisimama kwa upande mmoja na kunisihi akilia niende kwa kiongozi kutubu. Ilinihuzunisha kweli kumwona mamangu akifadhaika sana. Nilifikiria kuhusu jinsi alivyompoteza mamake akiwa na umri wa miaka mitatu na kisha akadhulumiwa na mamake wa kambo. Alikuwa ameteseka sana maishani mwake na sasa alikuwa anazidi kuzeeka, na sikuwa binti mwenye upendo sana, hasa katika jinsi nilivyokuwa nikimfanya awe na wasiwasi sasa. Kisha nikaangalia uso wa babangu uliozeeka na nywele yenye mvi, na hilo lilinifanya nihuzunike zaidi, na punde nilikuwa ninalia. Nilipokuwa tu nikianza kudhoofika, nilifikiria kuhusu kifungu cha maneno ya Mungu: “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Maneno ya Mungu yalinisaidia kuelewa kwamba kwa nje ilionekana kana kwamba wazazi wangu walikuwa wakinisumbua, lakini katika ulimwengu wa kiroho ilikuwa Shetani aliyekuwa akiweka dau na Mungu. Ilikuwa kama wakati ambapo Ayubu alikuwa akipitia majaribio ya Mungu, na mke wake, aliyechukua nafasi ya mmoja wa wahudumu wa Shetani, alimwambia “Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe” (Ayubu 2:9). Lakini kwa sababu Ayubu alimwogopa Mungu na kuepuka maovu, alimkaripia mkewe, akimwita mwanamke mjinga na mkaidi; hakutenda dhambi kwa maneno yake. Alimshuhudia Mungu mbele za Shetani, na machoni pa Yehova Mungu alikuwa mtu mkamilifu. Sasa nilikuwa nikisumbuliwa na wazazi wangu, waliokuwa wameamini uongo wote dhahiri ambao viongozi walikuwa wakisema, na hili lilikuwa mojawapo ya majaribu ya Shetani pia. Shetani alijua kwamba nilijali kuhusu wazazi wangu sana na alikuwa akitumia fursa hiyo kujaribu kunipata. Shetani alikuwa akitumai bure kutumia huruma yangu kwa wazazi wangu kunifanya nimpinge na kumsaliti Mungu, jambo ambalo linaonyesha jinsi Shetani alivyo mwovu na mwenye kudhuru kwa siri! Lakini singemridhisha Shetani kwa kumfanya aone njama zake zikifua dafu. Singemsikitisha na kumhuzunisha Mungu, kwa hivyo niliamua kusimama upande wa Mungu. Kufuatia hilo, bila kujali kile walichosema wazazi wangu, jinsi walivyonihimiza, moyo wangu haukushawishika hata kidogo. Walipoona kuwa sikuguswa hata kidogo, wazazi wangu waliondoka, wakionekana kuhuzunika sana.

Siku nyingine baadaye, kiongozi wa kanisa alimwambia babangu asimame mbele ya washirika wote wa kanisa lao na kutangaza kwamba nilikuwa nimefukuzwa kutoka katika kanisa hilo. Kiongozi pia aliwafanya wazazi wangu wajitenge nami. Kama matokeo ya usumbufu kutoka kwa kiongozi wa kanisa na wazazi wangu, mume wangu alianza kunitesa kwa hasira. Kila wakati niliporudi nyumbani kutoka kutimiza wajibu wangu wa kanisa, angenichapa ama kunifokea matusi, na nyakati nyingine hata alinifungia nje ya nyumba. Angeiharibu skuta yangu ya umeme ama baiskeli yangu, na wakati mmoja hata alinipeleka kwenye kituo cha polisi. Alinitesa hadi nikahisi kuchoka kimwili na kuonekana kusawajika kabisa, na majirani wetu katika kijiji pia walianza kunidhihaki na kunikashifu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, roho yangu ilidhoofika na nikaanza kuhisi kwamba imani yangu katika Mungu ilikuwa ngumu sana. Sikujua jinsi ya kuendelea, na kwa hiyo mara nyingi nilipiga magoti mbele za Mungu na kuomba na kulia, nikimsihi Mungu anipe imani na nguvu. Na kisha, wakati mmoja, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi. Kama kufuata kwako ni bora kabisa Mungu Anapokubariki, lakini unarudi nyuma bila baraka Zake, si huu ni utakaso? Kwa sababu una uhakika kuwa njia hii ni ya kweli, lazima uifuate hadi mwisho; lazima udumishe ibada yako kwa Mungu. Kwa sababu umeona kuwa Mungu Mwenyewe amekuja duniani kukukamilisha, lazima umpe moyo wako Kwake kabisa. Haijalishi ni nini Anafanya, hata kama Anaamua tokeo lisilofaa kwako mwishowe, bado unaweza kumfuata. Hii ni kudumisha usafi wako mbele za Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu). Kutoka katika maneno ya Mungu nilikuja kuelewa kwamba, wakati wa siku za mwisho, Mungu atafanya kundi la watu kuwa washindi. Mungu atamruhusu Shetani awajaribu watu, na iwe ni ukandamizaji wa CCP, usumbufu kutoka kwa jumuiya ya kidini, kuachwa na jamaa, ama dhihaka na matusi yaliyopokewa kutoka kwa umma, sisi waumini lazima tupitie majaribu haya kwa vitendo, kwa sababu ni wale waumini tu wanaoweza kumtii Mungu, wabaki waaminifu kwa Mungu na kumshuhudia Mungu katika hali yoyote ndio watakuwa washindi ambao wamefanywa na Mungu. Mungu alikuwa amepanga hali hizi ngumu ili kunikamilisha, kuona ikiwa kweli nilikuwa na imani Kwake, na kuona ikiwa kweli nilikuwa mtu ambaye alimwamini hakika, ambaye alimtii kweli, na ambaye alikuwa mwaminifu Kwake kwa kweli. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, nilienda mbele za Mungu na kutoa ahadi hii: Bila kujali taabu ama ukandamizaji ninaokabili, nitamfuata Mungu kwa azma daima, nitatimiza wajibu wangu daima kama mmoja wa viumbe wa Mungu ili kumridhisha Mungu, na nitamshuhudia Mungu kwa ushindi mbele ya Shetani. Baada ya hapo, ingawa mume wangu aliendelea kunisumbua na kunivuruga kwa hasira, bado nilimwomba Mungu mara kwa mara, nilimtazamia Mungu, nilijitayarisha na maneno ya Mungu kila siku, na sikuhisi tena mateso yoyote moyoni mwangu. Mungu pia alinifungulia njia: Mume wangu aliadhibiwa na Mungu mara kadhaa kwa sababu ya kunitesa kwa wazimu sana, na baada ya hapo hakujaribu kunichapa ama kuharibu baiskeli yangu tena. Kupitia uzoefu huu, niliona uweza na ukuu wa Mungu na matendo Yake ya ajabu. Niliona kwamba hakuna nguvu yoyote ya giza inayoweza kupita mamlaka na uweza wa Mungu, na nilipitia mwenyewe ukweli kwamba alimradi tumtegemee Mungu kwa kweli na tukabili kila kitu kinachokuja kwa kutegemea maneno ya Mungu, basi Mungu atatufungulia njia mbele na Atatuongoza kushinda ushawishi mwovu wa Shetani. Baada ya kupitia mateso na usumbufu huu wote, ingawa mwili wangu ulikuwa umeteseka kiasi, bado nilihisi kwamba nilikuwa nimepata mengi sana. Imani yangu katika Mungu iliimarika na kuimarika, na hizi zote zilikuwa baraka za Mungu kwangu. Shukrani, Mwenyezi Mungu!

Mwaka mmoja baadaye, nilienda na Dada Zhang mahali pa kazi pa dadangu mdogo zaidi na tukaishuhudia kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwake tena. Dadangu aliikubali, na nilipomwona akichukua kitabu cha maneno ya Mungu, nilikuja kufahamu kwa kina jinsi ilivyo vigumu kwa mtu kuokolewa na Mungu. Hamu ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu ni ya kweli sana! Sikuweza kuzuia machozi ya shukrani kutiririka usoni mwangu, na moyo wangu ulichangamshwa na shukrani na sifa kwa Mungu! Mwaka wa 2016, mimi na dadangu mdogo zaidi tuliungana na kumhubiria injili ya ufalme dada yetu mwingine, na baada ya hapo, tuliweza kuwaleta jamaa wetu wengine mbele za Mwenyezi Mungu pia. Hili liliniwezesha kuona kwamba bila kujali jinsi viongozi wa dini walivyo na hasira katika kubuni uongo na kuvuruga na kuwasumbua waumini wa kweli, injili ya ufalme ya Mungu itaenea, na hakuna mtu anayeweza kuizuia. Wanakondoo wa Mungu hakika wataisikia sauti Yake na kurudi mbele ya kiti Chake cha enzi. Asemavyo Mwenyezi Mungu: “Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 19).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kupotea na Kurejea Tena

Na Xieli, MarekaniNilikuja Marekani kufanya kazi kwa bidii kama vile ningeweza kutafuta maisha yenye furaha na hali ya juu ya maisha....

Dhoruba ya Talaka Yazimwa

Na Lu Xi, Japani Mnamo mwaka wa 2015, rafiki yangu alinishawishi nianze kumwamini Mwenyezi Mungu. Baada ya kupokea kazi ya Mwenyezi Mungu...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp