Mungu Anielekeza Kuushinda Ukatili wa Pepo

26/01/2021

Na Wang Hua, Mkoa wa Henan

Mimi na binti yangu sote tu Wakristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Tulipokuwa tukimfuata Mungu, mimi na binti yangu sote tulikamatwa na kuhukumiwa na serikali ya CCP kuadilishwa tena kupitia kazi. Nilihukumiwa kifungo cha miaka mitatu, na binti yangu akahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja. Ingawa nilipatwa mara kwa mara na mateso na dhuluma ya kikatili na serikali ya CCP, kila nilipojikuta nikikata tamaa na kuwa hatarini, Mungu alikuwapo, Akinilinda, Akinihifadhi na kunifungulia njia kwa siri. Ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyonipa ujasiri na motisha ya kuendelea kuishi, yaliyonielekeza kuyashinda maumivu ya kuteswa kikatili, na yaliyonisaidia kuvumilia miaka mitatu kwenye gereza hilo baya mno. Katikati ya dhiki, nilishuhudia upendo na wokovu wa Mwenyezi Mungu, na nikapitia mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu. Ninahisi kuwa nimefadhiliwa kwa kupata mengi sana, na nimeazimia kumfuata Mungu kwa uthabiti na kutembea katika njia sahihi maishani.

Kabla ya kumwamini Mungu, niliendesha biashara. Nilikuwa hodari katika kufanya hivyo na nilipata kiasi kizuri cha pesa. Lakini nilipokuwa nikijishughulisha na kujipatia kipato, pia nilipata mabadiliko ya maisha kwa ukamilifu. Sikulazimika tu kufikiria sana jinsi ya kupata pesa siku baada ya siku, lakini pia nililazimika kukumbana na ukaguzi wa kila aina kutoka kwa kila idara za serikali. Nililazimika kuhusika katika mazungumzo ya uwongo siku nzima na kuwa mnafiki katika mahusiano yangu na wengine. Nilihisi kuwa njia hii ya maisha ilikuwa yenye kuumiza na ya kuchosha, lakini sikuwa na chaguo lingine. Ilipofikia tu kiwango ambacho nilikuwa nimechoka kabisa kihisia na kimwili kutokana na kazi, niliikubali injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Niliona kuwa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu yanafichua siri za maisha na kufunua chanzo cha maumivu yote ya wanadamu, pamoja na ukweli wa wanadamu kupotoshwa na Shetani. Pia yanamwonyesha mwanadamu njia ya nuru anayohitaji kufuata katika maisha yote, na mara moja moyo wangu uliyapenda maneno ya Mungu. Kwa yakini, nilikuwa na hakika kuwa hii ilikuwa kazi ya Mungu wa kweli, na kwamba imani katika Mungu ilikuwa ndiyo iliyokuwa njia sahihi pekee katika maisha. Nilihisi kuwa mwenye bahati nzuri sana kuweza kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, nami nilifikiria kuhusu watu wote ulimwenguni ambao walikuwa kama mimi, ambao walikuwa wakiishi maisha matupu, ambao hawakuweza kupata mwelekeo katika maisha yao, na ambao walihitaji wokovu wa siku za mwisho wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo nilitamani kuhubiri injili ya siku za mwisho kwa watu wengi zaidi wanaoutafuta ukweli, ili watu wengi zaidi waweze kupata wokovu wa Mungu. Huku nikichochewa na upendo wa Mungu, kila nilipozungumza juu ya kazi ya Mungu au wokovu Wake, sikuweza kusema kiasi cha kutosha, na niliweza kupata watu halisi wanaoutafuta ukweli kwa kuwahubiria—nilisisimka. Wakati huo, binti yangu alikuwa amehitimu tu katika shule ya upili. Aliona jinsi ambavyo nilikuwa na furaha baada ya kuanza kumfuata Mwenyezi Mungu, na pia akaona kwamba ndugu wote ambao walikuja nyumbani kwetu walikuwa safi na wema, kwamba wote walikusanyika ili kuzungumza kwa uwazi, kuimba nyimbo, na kucheza, na kwamba kila wakati kulikuwa na uchangamfu mwema na wenye furaha ya ajabu sana. Kwa hiyo, alianza kutamani maisha haya na alitaka sana kumwamini na kumfuata Mungu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, tuliendesha biashara wakati wa mchana, na kisha tukasali pamoja, tukasoma maneno ya Mungu pamoja, tukajifunza nyimbo pamoja na tukashiriki juu ya ufahamu wetu kuhusu maneno ya Mungu wakati wa usiku; maisha yetu yalijawa furaha.

Tulipokuwa tu tukihisi kuzamishwa na kutiwa ukunjufu na upendo wa Mungu, bila kutarajia, kucha la pepo wa serikali ya CCP lilitushambulia sisi wawili na kutusababishia maumivu ya jinamizi na yenye kuhuzunisha sana—ulikuwa wakati ambao sitasahau kamwe. Ilikuwa mnamo Desemba 7, mwaka wa 2007, binti yangu alikuwa akifua nguo nyumbani, nami nilikuwa nikijitayarisha kwenda kutekeleza wajibu wangu kwa kanisa, wakati polisi watano au sita waliignia ghafla. Mmoja wao alisema kwa sauti kubwa, “Ninyi ni waumini wa Mwenyezi Mungu! Na aidha, mnazunguka mkiwahubiria wengine!” Kisha akamwashiria binti yangu na kuwaambia polisi wengine wawili, “Mchukueni kwanza!” na binti yangu alichukuliwa mara moja na wale polisi wawili. Kisha polisi waliobaki wakaanza kupekua nyumba yangu yote, wakichakura masanduku na makasha na hata kuangalia kila mfuko wa nguo zetu. Muda si muda, vitanda na sakafu vilifunikwa na vitu, na hata walikanyaga vitandani kote kwa viatu vyao vya ngozi. Mwishowe, walichukua vitabu vya maneno ya Mungu, diski kadhaa, vifaa viwili vya kuchezesha CD, vifaa viwili vya kuchezesha MP3, yuani 2000 pesa taslimu na jozi ya pete za dhahabu. Kisha wakanisukuma na kuniweka kwenye gari la polisi. Niliwauliza, nikitaka wanieleze, “Tumevunja sheria gani kwa kumwamini Mungu? Mbona mnatukamata?” Kwa mshangao wangu, walitangaza bila haya mbele ya watu wote waliokuwa wakitazama, “Kuwakamata ninyi waumini wa Mungu ni kazi yetu!” Niliudhika. Hawakuwa “Polisi wa Umma.” Walikuwa tu genge la majambazi, wahuni na jamii ya wahalifu wenye kazi ya kuwasaka watu wenye haki!

Tulipofika katika Ofisi ya Usalama wa Umma, nilifungwa pingu na kuongozwa hadi kwenye chumba cha mahojiano. Nilipoona jinsi walivyoonekana wakali, sikuwa na budi kuogopa, nami nikawaza: “Sasa kwa kuwa nimeangukia mikononi mwa pepo hawa na wamepata vitabu vingi vya maneno ya Mungu na diski nyumbani kwangu, bila shaka hawataniruhusu niende sasa. Nikishindwa kustahimili mateso yao na kuwa Yuda, basi nitajulikana wakati wote kama msaliti aliyemsaliti Mungu!” Nilimwomba Mungu kimya kimoyomoyo, nikimwomba Anilinde na kuniongoza. Wakati huo huo, nilifikiri juu ya maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako). Maneno ya Mungu yalinifanya nigundue kuwa tabia Yake yenye haki haivumilii kosa lolote, na kwamba Mungu hawapendi wale wanaomsaliti. Kisha nikafikiria maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Kutoka kwa nje, wale walio na mamlaka wanaweza kuonekana kuwa waovu, lakini msiogope, kwa kuwa hii ni kwa sababu mna imani kidogo. Almuradi imani yenu ikue, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 75). “Ndiyo!” Niliwaza. “Sipaswi kuwaogopa. Bila kujali jinsi kundi hili la polisi wabaya lilivyo hatari, bado wapo mikononi mwa Mungu, na bila idhini ya Mungu hawawezi kuumiza nywele kichwani mwangu hata wakiwa wabaya jinsi gani.” Maneno ya Mungu yalinipa imani na ujasiri, na kwa hivyo nilimwahidi Mungu: “Ee Mungu! Wakati Wako wa kunijaribu umefika. Natamani kushuhudia kwa ajili Yako, nami ninaapa juu ya maisha yangu kutokuwa Yuda kamwe.” Baada ya kumaliza ombi langu, moyo wangu ulitulia zaidi. Wakati huo, mmoja wa polisi wabaya ambaye alionekana kama kiongozi kati yao, alinikaripia, akisema, “Wewe mwanamke mjinga! Kuna vitu vingi ambavyo ungefanya, lakini bila shaka uliona ni vyema kumfanya binti yako pia amwamini Mungu, siyo? Yeye ni mrembo. Angeweza kuchuma makumi ya maelfu ya yuani kwa kujiuza kwa wanaume wakwasi, lakini anamwamini Mungu kama mjinga! Tuambie sasa, ulianza kumwamini Mungu lini? Ni nani aliyekuingiza? Ulitoa wapi vitabu hivyo?” Nilipomsikiliza akipayuka nilikasirika. Sikuweza kuamini kwamba afisa wa serikali aliyesemekana kuwa mwenye heshima angeweza kusema mambo ya kudharaulika na ya aibu kama hayo! Machoni pao, mtu kuuuza mwili wake ni jambo zuri, na hata wanawatia watu moyo wafanye vitu vibaya kama hivyo. Lakini sisi ambao tunamwamini Mungu na kumwabudu Mungu, na kutafuta kuwa watu waaminifu, tunapachikwa jina la wahalifu ambao hutenda vibaya, na tunakuwa walengwa wa kusakwa na kukamatwa vikali. Kwa kutenda hivi, si wanaunga mkono uovu, wakikandamiza wema na kuzuia haki? Serikali ya CCP ni mbovu na potovu sana! Nilipoona jinsi walivyoendelea kuzungumza upuuzi mtupu kama huo na hawakusikia mantiki yoyote, nilijua kwamba haikuwezekana kuwafanya waelewe, na kwa hivyo nilinyamaza kimya. Walipoona kwamba nilikataa kuongea, walinisindikiza hadi kwenye gari la polisi na kunitishia, wakisema, “Tumepata ushahidi mwingi sana nyumbani kwako kiasi kwamba ikiwa hutashika adabu na kutuambia kila kitu, tutakuvuta nje upigwe risasi!” Nilipowasikia wakisema hivi, sikuweza kujizuia kuogopa, nami nikawaza: “Watu hawaweza kufanya chochote. Wakinipiga risasi kwa kweli, basi sitamwona tena binti yangu.” Kadiri nilivyozidi kufikiri juu ya hilo, ndivyo nilivyozidi kuhuzunika, nami nilimwomba Mungu moyoni mwangu bila kukoma, nikimwomba Aulinde moyo wangu na kuniondolea woga na wasiwasi niliokuwa nao ndani yangu. Wakati huo huo, nilikumbuka maneno ya Mungu: “Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu. Ni kitu gani kilichopo ambacho hakiko mikononi Mwangu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 1). “Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Wakati huo, kila kitu kilikuwa wazi: “Ndiyo,” niliwaza. “Maisha yangu na maisha ya binti yangu yamo mikononi mwa Mungu, na Mungu ndiye mwenye kauli ya mwisho kuhusu iwapo tutaishi au kufa. Pepo hawa wa Shetani hawana udhibiti juu ya kudura zetu. Bila idhini ya Mungu, hakuna mtu ambaye angeweza hata kufikiria kuchukua maisha yetu. Shetani hivi leo anajaribu kutumia udhaifu wangu kunitishia na kuniogopesha, akitarajia kunifanya nidangayike na hila yake ya kijanja na kujisalimisha kwake. Lakini sitamruhusu anidanganye. Ikiwa nitakufa au kuishi, niko tayari kutii, kwa kuwa ni heri nife kuliko kumsaliti Mungu.” Nilipofikiria kuhusu jambo hili, papo hapo nilipata azimio la kupigana na Shetani hadi mwisho kabisa, na sikuhisi tena hofu au woga.

Polisi walinipeleka kizuizini. Mara tu nilipoelekezwa ndani ya uwanja, maafisa wa marekebisho walinipekua kwa fujo na kuniamuru nivue viatu na nguo zangu. Kisha walinilazimisha nisimame katika uwanja uliokuwa baridi kwa karibu dakika 30. Nilihisi baridi sana kiasi kwamba sikuweza kusimama bila kuanguka, mwili wangu wote ulitetemeka kwa nguvu, na meno yangu yalitatarika bila kukoma. Walipoona kwamba hawakuwa wamepata chochote kutoka kwangu, mmoja wa maafisa wa marekebisho alinipeleka kwenye seli, na akamchochea mkuu wa wafungwa katika seli hiyo pamoja na wafungwa wengine, akisema, “Huyu ni muumini wa Mwenyezi Mungu....” Mara tu aliposema hivyo, wafungwa walinivamia na kunilazimisha niivute suruali yangu chini hadi kwenye vifundo vya miguu yangu na kisha kuivuta juu tena. Walinilazimisha nifanye hivi tena na tena huku wote wakinicheka. Baada ya kuchokozwa na kufedheheshwa, mkuu wa wafungwa alinilazimisha nijifunze jinsi ya kutengeneza vitu kutokana na manyoya ya ndani ya kuku. Lakini kwa kuwa kazi hii ilihitaji ustadi na mazoezi fulani, sikuwa bado nimekuwa stadi katika siku ya pili, na kwa hivyo mkuu wa wafungwa alichukua fimbo ya mwanzi na akaipiga mikono yangu kikatili. Mikono yangu ilipigwa hadi ikafa ganzi kutokana na maumivu, na sikuweza hata kubana manyoya ya kuku. Niliposonga ili niyaokote manyoya yaliyokuwa yameanguka sakafuni, mkuu wa wafungwa alisimama juu ya mkono wangu na kuusindika chini kwa mguu wake, jambo ambalo lilisababisha maumivu makali kwenye vidole vyangu, kana kwamba vilikuwa vimekatwa. Hata hivyo, hakuwa bado amemalizana na mimi, kwani alichukua fimbo yake ya mwanzi tena na kunigonga kichwani nayo mara kadhaa hadi nikapata kizunguzungu na macho yangu yakawa na ukungu. Mwishowe, alisema kwa ukali, “Adhabu yako itakuwa kufanya kazi ya zamu ya usiku wa leo. Utahojiwa kesho na polisi, kwa hivyo lazima ufanye kazi ya kesho leo. Usipoifanya yote, kesho usiku nitakulazimisha usimame usiku kucha!” Wakati huo, nilihisi masikitiko na huzuni isiyoelezeka. Nilifikiria jinsi ambavyo tayari sikuweza kuvumilia, pamoja na polisi waovu kuungana na wafungwa kuniumiza kwa njia hii, kwa hivyo nilipaswaje kufaulu katika siku zijazo? Katika dhiki, nililia kwa ajili ya dhuluma katika hayo yote, machozi yakitiririka usoni mwangu, nami nikamwambia Mungu kimyakimya, nikamwambia kuhusu shida zangu: “Ee Mungu! Ninapokabiliwa na dhihaka na mateso yaliyotolewa kwangu na kundi hili la majinamizi, nahisi mpweke sana, nisiyejiweza na mwenye woga, na sijui nitakavyofaulu. Tafadhali niongoze na Unifanye niwe thabiti.” Baada ya kuomba, Mungu alinifanya nifikiri kuhusu kifungu cha maneno Yake ili yanipe nuru: “Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu). Nilipata faraja sana kutoka kwa maneno ya Mungu, nayo yaliniwezesha kuelewa mapenzi ya Mungu. Mungu hutumia kuzingirwa na mateso ya Shetani ili kumkamilisha mwanadamu, kumwezesha mwanadamu kuepuka ushawishi wa Shetani ili tuweze kufanywa na Mungu kuwa washindi na kuingia katika ufalme Wake. Katika nchi hii ya giza na mbaya inayotawaliwa na CCP, watu wanaruhusiwa tu kutembea katika njia ya uovu na sio njia sahihi. Kusudi la CCP la kufanya hivi ni kuwapotosha watu sana kiasi kwamba hawawezi tena kutofautisha uovu na haki au mema na mabaya, kuwafanya watu watetee uovu na kuiacha haki, hadi mwishowe waangamie pamoja nayo kwa sababu ya kumpinga Mungu. Mtu anaweza tu kuwa mshindi wa kweli kwa kutosalimu amri kwa masharti anaposhambuliwa kutoka pande zote na ushawishi mwovu, kwa kuishikilia imani yake, bidii na upendo mbele za Mungu, na kuwa shahidi kwa ajili ya Mungu, na kwa kufanya hivi tu ndipo mtu anaweza kumwaibisha Shetani na kumwezesha Mungu kupata utukufu. Kisha nilimwomba Mungu: “Ee Mungu! Unawatumia pepo hawa wa Shetani wakuhudumie ili kuijaribu imani yangu na kunipa nafasi ya kukushuhudia. Kwa kufanya hivi, Unaniinua, nami ninaamini kuwa kila kitu kinachonitokea sasa kimepangwa na Wewe, na kwamba Wewe huchunguza kila kitu kwa siri. Natamani kuwa shahidi kwa ajili Yako na kukuridhisha katika jaribio hili. Ninakuomba tu Unipe imani na nguvu, na azimio la kuvumilia mateso, ili bila kujali ni mateso gani ninayoweza kukabili, nisianguke au kupotea!”

Saa 9 asubuhi ya siku ya tatu, polisi walinipeleka katika chumba cha mahojiano. Wakiitahabibu simu ya binti yangu, walianza kunihoji. “Ujumbe kwenye simu hii ulitumwa na wewe. Ulimwambia binti yako kuwa utanunua nyumba, kwa hivyo inaonekana kana kwamba una pesa.” Polisi hawa waovu walistahili kudharauliwa kweli—walifanya kila wawezalo katika jitihada yao ya kuchukua kila senti kutoka kwangu. Nilimjibu, “nilikuwa namtania tu.” Sura ya yule polisi ilibadilika ghafla na, akichukua daftari, alianza kunipiga nalo kichwani na usoni mwangu kwa nguvu mpaka nikahisi kizunguzungu na uso wangu ukawasha kwa maumivu. Akiwa ameyakaza sana meno yake kwa ukali, alisema, “Tuambie! Pesa zako ziko wapi? Usipotuambia kila kitu, tutakuburuta nje na kukupiga risasi! La sivyo utahukumiwa kifungo cha miaka kati ya minane hadi kumi!” Nilisema sikujua chochote. Polisi mrefu na wa kuvutia alikasirika, akanijia na, huku akishika blauzi yangu kwa nyuma, akanivurumisha yadi kadhaa kwenye sakafu. Kisha akaanza kupiga kichwa, mgongo na miguu yangu kikatili, akisema alipokuwa akifanya hivyo, “Hii ndio thawabu yako kwa kutokiri! Unasema hujui chochote, lakini ni mpumbavu tu anayeweza kukuamini! Usipotwambia tunachotaka kujua, basi nitakupiga hadi ufe leo hii!” Nilikereza meno yangu na kuvumilia maumivu hayo, nikimwita Mungu moyoni mwangu bila kukoma: “Ee Mungu! Pepo hawa ni waovu sana. Tafadhali Nipe nguvu ya kushinda adhabu yao na Unilinde ili niweze kuwa shahidi kwa ajili Yako.” Wakati huo, nilifikiria kuhusu maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Wanajeshi wazuri wa Kristo lazima wawe jasiri na kunitegemea kuwa wenye nguvu kiroho; lazima wapigane kuwa wapiganaji na wapambane na Shetani hadi kufa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 12). “Kama unayo pumzi moja tu, Mungu hatakuacha ufariki(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu, na yalinipa ujasiri wa kushinda mamlaka ambayo kifo kilikuwa nayo juu yangu. Nilihisi upendo wa Mungu wakati huo nami nikaona kuwa Mungu alikuwa karibu nami kila wakati. Nilifikiria: “Kadiri mnavyozidi kunipiga kwa jinsi hii, ndivyo ninavyozidi kuona tabia zenu halisi kama adui wa Mungu. Hata kama nitakufa, sitajisalimisha kwenu kamwe. Kama mnafikiria nitawahi kumsaliti Mungu, fikirieni tena!” Mara moja nilihisi mwili wangu wote ukilegea baada ya kufikiria hivi. Walibadilishana kati ya kunipiga na kunihoji asubuhi hiyo, na alasiri walinilazimisha nipige magoti kwenye sakafu ngumu iliyokuwa baridi sana. Walinitesa siku hiyo nzima hadi usiku, na mwishowe nilikuwa nimepigwa sana kiasi kwamba mwili wangu wote uliuma kwa namna isiyovumilika nami sikuwa na nguvu ya kusimama. Waliona kwamba hawakuweza kupata chochote kutoka kwangu kwa kunihoji, kwa hivyo walinisindikiza hadi kizuizini.

Kule kizuizini, afisa wa marekebisho mwenye moyo mgumu hakuniruhusu kamwe nile chakula cha kutosha lakini alinizidishia kazi. Alinilazimisha kufanya kazi kwa zaidi ya saa 15 kila siku, na kama singeimaliza kazi yote, basi angemfanya mkuu wa wafungwa anitese. Kwa sababu nilikuwa nimeanza tu kufanya kazi hii na sikuwa naifanya kwa haraka sana, mkuu wa wafungwa alichukua nyundo ya chuma niliyotumia katika kazi yangu na akanigonga kichwani nayo. Uvimbe mkubwa ulitokeza mara moja kichwani mwangu, baada ya hapo alinipiga mateke na kunichapa hadi nikawa na maumivu makali katika mwili wangu wote na damu ikachuruzika kutoka kinywani mwangu. Kwa sababu ya kukumbwa na mateso ya kikatili kama hayo, sikuwa na budi kumfikiria binti yangu. Tangu alipokamatwa, sikujua pepo woavu walikuwa wakimpa mateso gani, sembuse jinsi alivyokuwa akiendelea gerezani. Wakati uo huo, nilisikia ukemi wa ghafla ukitoka kwenye seli ya wanaume iliyokuwa karibu na yangu, na mmoja wa wanawake katika seli yangu akasema, “Humu ndani, kumuua mtu ni kama kumuua mdudu. Mmoja wa wafungwa wa kiume hakuweza kuvumilia mateso hayo kwa hivyo akakimbilia milimani nyuma ya gereza. Polisi walipompata, walimpiga hadi akafa kisha wakaiambia familia yake kwamba alikuwa amejiua. Hivyo tu, yote yaliishia kufichwa.” Hadithi hii iliniogofya, nami nilihisi kuwa na wasiwasi hata zaidi kumhusu binti yangu. Alikuwa ametimia umri wa miaka 19 tu na hakuwa amewahi kuteseka maisha yake yote, sembuse kupitia dhiki yoyote ya aina hii. Pepo hawa ambao wanaweza kumuua mtu bila kujali walikuwa na uwezo wa kufanya kitendo chochote cha kustahili dharau ambacho mtu angeweza kufikiria, na sikujua kama binti yangu angeweza kuvumilia mateso na ukatili wa pepo hawa. Kwa sababu sikujua kama binti yangu alikuwa hai au alikuwa amekufa, nilihisi uchungu sana, na hata katika ndoto zangu usiku niliona mandhari mabaya ya kuteswa kwake na pepo hao. Niligutuka mara nyingi kutoka ndotoni, na kisha ningefadhaika kiasi kwamba singeweza kulala tena usiku kucha.

Siku iliyofuata, afisa wa marekebisho alipata kisingizio cha kusema kwamba sikuwa nikifanya kazi kwa bidii kiasi cha kutosha na akanipiga usoni bila sababu hata kidogo. Alinipiga kwa nguvu sana kiasi kwamba uso wangu ukawasha na masikio yangu yalikuwa yanawangwa. Hata hivyo, hiyo haikumtosha kwani alinipigia kelele, “Siamini kuwa hatuwezi kukurekebisha humu, kwa hivyo nitakupa ladha ya ‘chombo cha kutesea chenye misumari ya vyuma’!” Kisha alitoa agizo na wengine watano au sita wakaja na kuzikata nywele zangu nyingi kiasi kwamba sikufanana nami tena. Kisha walinishikilia chini na kunilazimisha nivae kifaa cha mateso cha kutisha zaidi katika gereza lote—“chombo cha kutesea chenye misumari ya vyuma.” Waliweka kizingo cha chuma kichwani mwangu, kimoja kwenye kila mkono na tena kwenye kila mguu, ambavyo viliunganishwa pamoja na ufito wa chuma. Mara nilipofungwa kwa vifaa hivi vya mateso, sikuweza hata kusimama, lakini nililazimika kuegemea ukutani. Afisa wa marekebisho alinilazimisha nivae vifaa hivi vya mateso kila siku kuanzia saa 11 hadi usiku wa manane (nililazimika kusimama kwa saa 19 kamili), na kumwamuru mkuu wa wafungwa, akisema, “Mchunge kwa niaba yangu. Akijaribu kulala, mpige teke!” Mkuu wa wafungwa baadaye alinichunga kila siku na hakuruhusu nifunge macho yangu kwa sekunde moja. Kwa sababu vizingo hivi vilikuwa vya chuma na vilikuwa katika mwili wangu wote, nilihisi kama kwamba vilikuwa vikizuia mzunguko wangu wa damu. Niliishia kutoweza kabisa kuyafumbua macho yangu, na kwa hivyo mkuu wa wafungwa alinitusi na, wakati mmoja, alinipiga mateke vile vile. Mwili wangu wote ulianza kutetemeka na nilivumilia maumivu kwa shida. Wakati wa kulala usiku ulipofika, wafungwa wanne waliniinua kwenye bodi kubwa niliyokuwa nikifanyia kazi mchana, na asubuhi iliyofuata walikuja na kunishusha chini. Kwa siku hizo chache, kulikuwa na dhoruba mbaya ya theluji nje, na hali ya hewa ilikuwa ya baridi sana. Ili kunitesa, yule afisa wa kuchukiza wa marekebisho alinifanya nivae vizingo hivi vya chuma kwa siku saba mchana na usiku. Sikuweza kula, kunywa, au kwenda msalani pekee yangu. Nilipolazimika kwenda chooni, wafungwa wengine ambao hawakuwa wamemaliza kazi yao walilazimika kunisaidia. Wafungwa wote walikuwa na shughuli kila siku, na kwa hivyo kila waliponilisha, walifanya hivyo ovyovoyo, na walinipa maji ya kunywa mara chache sana. Kwa kweli niliteseka kutokana na njaa na baridi, na kila siku ilionekana kama muda mrefu sana. Kila alfajiri waliponishusha kutoka kwenye bodi hiyo kubwa, nilihisi uchungu sana, bila kujua jinsi ningeweza kuvumilia siku nyingine. Nilitamani tu kuwe usiku, na ingekuwa vizuri kwangu ikiwa jua halingechomoza tena. Kwa sababu vizingo vya chuma vilikuwa vizito sana, siku ya pili ambayo nililazimishwa kuvivaa, mikono yangu ilivimba na ikawa myeusi na zambarau, na ngozi ilionekana kana kwamba ilikuwa karibu kupasuka. Mwili wangu wote ulikuwa umevimba kama puto, na uvimbe bado haujapungua kabisa hata baada ya miezi kumi. Niliteseka sana wakati huo kiasi kwamba kifo kilionekana kuwa bora kuliko uhai, na nilikuwa katika upeo wa uvumilivu wangu wa maumivu. Kwa hivyo, nilimsihi Mungu katika ombi: “Ee Mungu! Kwa kweli siwezi kuvumilia mateso haya. Sitaki kuishi lakini siwezi kufa pia. Ninaomba tu Uchukue pumzi yangu ya uhai, kwa kuwa sitamani kuishi dakika moja zaidi.” Nilipokuwa tu nikimwomba Mungu ombi hili lisilo na busara, nikitamani kufa kama njia ya kuepuka uchungu wangu, nilifikiria kuhusu maneno ya Mungu yasemayo: “Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani…. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! … Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). “Kwa kuwa wewe ni binadamu, unapaswa kujitumia kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso! Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu na Petro. … Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale mnaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (2)). Maneno ya Mungu yalitua juu ya moyo wangu uliokauka kama umande mtamu. “Ndiyo,” niliwaza. “Huu ni wakati ambapo Mungu ananihitaji nimshuhudie. Nikifa kwa sababu siko radhi kupitia maumivu, si hilo litanifanya niwe mwoga? Ingawa sasa ninapitia ukatili na mateso mikononi mwa pepo hawa, si ni jambo la maana na la kufaa kabisa kuweza kushuhudia kwa ajili ya Mungu na kuitwa mwenye haki na Mungu? Nimemfuata Mungu kwa miaka hii yote na nimefurahia neema nyingi sana na baraka nyingi sana kutoka Kwake, kwa hivyo, leo, ninapaswa kumshuhudia Mungu mbele ya Shetani—ni heshima yangu kufanya hivyo. Nitashikilia maisha bila kujali nitateseka kiasi gani au jinsi hali itakavyokuwa ngumu kiasi gani, ili moyo wa Mungu uridhike.” Maneno ya Mungu yalizindua moyo wangu na roho yangu na kuniwezesha nielewe mapenzi Yake. Sikutamani tena kufa, lakini badala yake nilitamani tu kuvumilia uchungu wowote na kutii utaratibu na mipangilio ya Mungu. Mwishowe, siku saba, usiku na mchana, za adhabu ya mwili zilikamilika. Nilikuwa nimeteswa hadi karibu nife, ngozi kwenye visigino vyangu ilikuwa imebambuka na safu baada ya safu ya ngozi iliyo kandokando ya mdomo wangu ilikuwa imebambuka. Baadaye nilimsikia mfungwa wa kiume katika seli iliyokuwa karibu na yangu akisema, “Mfungwa wa kiume mwenye nguvu na afya wa umri wa miaka thelathini hivi amekufa chini ya mateso hayo.” Niliposikia haya, niliendelea kumshukuru Mungu moyoni mwangu, kwani nilijua kuwa sikuwa nimenusurika kwa sababu tu nilikuwa na bahati, lakini kwa sababu ya mwongozo na ulinzi wa Mungu. Ni maneno ya Mungu yaliyojaa nguvu ya maisha ambayo yaliniwezesha kuvumilia, la sivyo, kwa ajili ya umbile langu dhaifu la kike, ningekuwa nishakufa kutokana na mateso.

Baada ya mateso hayo ya kikatili, kwa kweli nilishuhudia kudura ya Mungu na, hata zaidi, nilipata kufahamu jinsi ambavyo sina nguvu. Wakati wa jaribio hilo, sikuweza hata kujitunza, lakini bado nilikuwa na wasiwasi juu ya iwapo binti yangu angeweza kusimama imara au la—si nilikuwa tu na wasiwasi juu ya mambo ya fikira zangu mwenyewe? Kudura ya binti yangu ilikuwa mikononi mwa Mungu na wasiwasi wangu juu yake haungeweza kumsaidia hata kidogo. Ulichofanya ilikuwa ni kumpa Shetani nafasi ya kunifikia na kunifanya niweze kudhuriwa na udanganyifu na madhara yake. Vitu vyote hupangwa na kuratibiwa na Mungu, na nilijua wakati huo kwamba ninapaswa kumkabidhi binti yangu kwa Mungu na kumtegemea, nikiamini kwamba, ikiwa Mungu anaweza kuniongoza kupitia shida hii, Atakuwa pia akimuongoza binti yangu kupitia wakati huu mbaya. Na kwa hivyo, nilimwomba Mungu na nikatafakari kuhusu maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Mbona usiwakabidhi mikononi Mwangu? Je, hunisadiki vya kutosha? Au ni kwamba unahofia Nitafanya mipango isiyofaa juu yako? Mbona daima wewe huwa na wasiwasi kuhusu familia yako ya mwili? Wewe huwatamani sana wapendwa wako! Je, Ninamiliki nafasi fulani moyoni mwako?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 59). Maneno ya Mungu yalirekebisha hali yangu. “Hiyo ni kweli,” niliwaza. “Shida ambazo watu hupitia na maumivu wanayoyapitia yote huamuliwa kabla na Mungu. Mateso ambayo binti yangu anayapitia yameruhusiwa na Mungu yamfike. Ingawa huenda sielewi na sijui kinachomtokea, hayo yote ni kwa ajili ya upendo wa Mungu kwa hakika, kwani upendo Alio nao Mungu kwa mwanadamu ndio upendo halisi na wa kweli zaidi. Natamani kumkabidhi binti yangu kwa Mungu ili Amtawale na kumfanyia mipango, nami niko tayari kutii yote yatokayo kwa Mungu.” Nilipoacha tu mambo haya yote na nikawa tayari kutii mipango ya Mungu, nilimwona binti yangu mahakamani. Aliniambia kwa siri kuwa Mungu alikuwa Amemwongoza kushinda dhiki na mateso kadhaa, na kwamba alikuwa ameshuhudia baraka za Mungu: Mungu alikuwa amewagusa wafungwa wengine wakwasi wamsaidie, wengine wakimpa nguo na wengine wakimnunulia vitu vya kula na kunywa; mkuu wa wafungwa alipokuja kumdhulumu kwa kisingizio hafifu, mtu fulani alimtetea. Hizi ni baadhi tu ya baraka ambazo Mungu alimpa binti yangu gerezani. Kupitia uzoefu huu, binti yangu alipata ufahamu fulani juu ya kazi ya ajabu na ya busara ya Mungu, na akaja kufahamu kwamba upendo wa Mungu hauwezi kuelezwa kamwe. Nilifurahia mno kusikia mambo haya kutoka kwake, na macho yangu yakajaa machozi ya shukrani kwa Mungu. Katika binti yangu, niliona tena mamlaka makuu na matendo ya kushangaza ya Mungu, nami nikaona kwamba Mungu amekuwa Akituongoza daima na kutulinda sote ili tuweze kupitia dhiki na mateso haya. Kwa hivyo, imani yangu katika Mungu iliimarishwa hata zaidi.

Kwa siku zilizofuata, afisa wa marekebisho hakuzingatia ukweli kwamba mwili wangu ulikuwa umevimba na kuuma lakini aliendelea kunilazimisha nifanye kazi. Muda si muda, nilichoka sana kiasi kwamba niliishia kupata majeraha mengi mapya juu ya yale yaliyokuwepo, na sehemu ya chini ya mgongo wangu iliuma sana hata sikuweza kusimama wima. Niliposogea au kugeuka, ningehisi maumivu ya kuchoma katika kila mfupa na kila kiungo mwilini mwangu, kana kwamba yote vilikuwa vikipasuliwa, na kwa hivyo ikawa vigumu kulala usiku. Licha ya haya, afisa wa marekebisho bado hakuniacha, lakini badala yake alifanya mkuu wa wafungwa anidhulumu kila alipopata fursa. Kwa sababu sikuwa na pesa za kuwanunulia vitu vya kula, mkuu wa wafungwa alinipiga teke kwa nguvu katika sehemu ya chini ya mwili wangu, ambapo nilikwepa bila kufikiria na nikajaribu kujificha. Kuvunjika moyo kwake kuligeuka na kuwa ghadhabu naye akanipiga mateke na kunikanyaga bila kujizuia. Kwa kuwa mafuta hayakutumiwa kupika chakula tulichokula, mara nyingi nilifunga choo, na nilitumia muda mrefu kuchutama chooni, wangenitukana na kuniadhibu kwa kunilazimisha niondoe choo kwenye ndoo kwa zaidi ya siku kumi. Walitafuta sababu yoyote isiyo na msingi ili kuniadhibu kwa kunifanya nichukue zamu ya wengine na kulinda usiku kucha. Walisema pia kuwa nilitumia malighafi nyingi nilipokuwa nikifanya kazi, na kwa hivyo walinitoza faini ya yuani 50. Afisa wa marekebisho alitumia fursa hiyo kunipeleka ofisini, na kujaribu kunishawishi kwa kusema, “Ikiwa unaweza kuniambia ni nani mwingine ambaye uliamini katika Mungu pamoja naye, nitamsihi mkuu wa mahakama apunguze kifungo chako, na pia hatutakutoza faini ya hii yuani 50.” Polisi hawa waovu walikuwa na njama nyingi sana za hila zenye siri, wakibadilisha kati ya mbinu zenye huruma na ziziso za hurumu, na wakijaribu kila mkakati ambao wangeweza kufikiria ili kunifanya nimsaliti Mungu, lakini yote ikawa bure! Nilikataa ahadi yake.

Mnamo Agosti 25, mwaka wa 2008, serikali ya CCP ilinishtaki kwa “kujiunga na shirika la Xie Jiao na kuzuia utekelezaji wa sheria” na kunihukumu kifungo cha miaka mitatu ya kuadilishwa tena kupitia kazi. Kisha walinisindikiza hadi kwenye Kambi ya Wanawake ya Wafanyakazi ya Mkoa ili nitumikie kifungo changu. Binti yangu alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja wa kuadilishwa tena kupitia kazi, alikuwa atumikie kifungo hicho katika kituo cha uzuizi cha mtaa.

Baada ya wiki mbili gerezani, walinzi wa gereza walitaka kuwatenganisha wafungwa wawe katika vikundi tofauti vya kazi. Nilikuwa nimesikia habari kuwa kazi iliyofanywa na wafungwa wazee ilikuwa nyepesi kidogo, nami nilifikiria jinsi mwili wangu ulivyokuwa umeharibiwa vibaya, na karibu kuangamia humo kizuizini, na jinsi ambavyo sikuwa na nguvu ya kufanya kazi ngumu ya mwili tena. Nilimwomba Mungu kuhusu jambo hili, nikimwomba Anifungulie njia. Ikiwa kwa kweli Alinihitaji niendelee kupitia hali ya aina hiyo, basi nilikuwa tayari kutii. Namshukuru Mungu kwa kusikia maombi yangu, kwani bila shaka nilipelekwa kwenye kikundi cha kazi cha wafungwa wazee. Kila mtu alisema hili likikuwa jambo la ajabu, lakini nilijua vyema moyoni mwangu kwamba haya yote yalikuwa yamepangwa na Mungu, na kwamba Mungu alikuwa Akinionyesha huruma kwa ajili ya udhaifu wangu. Katika kundi la wafungwa wazee, walinzi wa gereza walizungumza kwa furaha, “Yeyote atakayefanya kazi kwa bidii na kujitahidi atapunguziwa adhabu yake. Hatumtapendelea mtu yeyote….” Niliwaamini waliposema haya, nikidhani kwamba walinzi wa hapa walikuwa bora zaidi kuliko maafisa wa marekebisho wa kule kizuizini. Na kwa hivyo, nilijitosa katika kazi hiyo na nikaishia kuwa mmoja wa wafanyikazi kumi hodari zaidi ya karibu watu 300. Hata hivyo. Ilipofika wakati wa kutangaza orodha ya watu ambao vifungo vyao vilipaswa kupunguzwa, walinzi wa gereza walipanga tu kupunguza vifungo vya wale waliopenda kupigana na waliowanunulia zawadi—kifungo changu hakikupunguzwa hata kwa siku moja. Mfungwa mmoja alifanya kazi kwa bidii mno ili apunguziwe kifungo chake, lakini alishangaa walinzi wa gereza waliposema tu, “Tunapaswa kumzuilia mtu aliye na uwezo kama wewe hapa siku zote!” Niliposikia hivi, nilijichukia kwa ajili ya ujinga wangu, kwa kutoelewa kiini kikatili na cha kinyama cha serikali ya CCP, na kwa kuzuzuliwa sana na uwongo wao. Kwa kweli, Mungu alisema zamani: “Anga iliyo juu ya jamii ya binadamu ni nzito sana, ni yenye giza na huzuni, bila hata dalili ya uwazi, na ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, kiasi kwamba anayeishi ndani yake hawezi hata kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake au jua anapoinua kichwa chake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi). Nilipolinganisha ufunuo wa maneno ya Mungu na ukweli wa uhalisi, niliona mwishowe kwamba serikali ya CCP ni mbovu na chafu sana tu kuanzia juu mpaka chini na haina usawa au haki hata kidogo. Wale polisi waovu waliweza tu kuwadanganya na kuwaghilibu watu kwa uwongo na hawakuweza kabisa kututendea kama wanadamu. Kwao, wafungwa walikuwa tu vyombo vya kuchuma pesa—kadiri wafungwa walivyozidi kuwa na uwezo, ndivyo walivyozidi kutokuwa na uwezekano wa kupunguziwa vifungo vyao. Walinzi wa gereza walitaka watu wawahudumie wakati wote na kufanya kazi kama nyumbu ili waweze kuchuma pesa nyingi hata zaidi kutoka kwao. Ili kuongeza mazao ya kazi, polisi waovu hawangeturuhusu hata twende msalani, na mara kadhaa sikuweza tu kuvumilia nami nilikojoa kwenye suruali yangu. Kwa sababu nilijitokeza kwa sababu ya kiasi cha kazi nilichoweza kumaliza, kikundi kikuu cha kazi kilipanga kunihamisha ili niwe “mwongozaji wa mwendo.” Nilikuwa tayari nimeziona sura zao mbaya waziwazi, nami nilijua kuwa kama ningehamishwa basi bila shaka wangenishinikiza zaidi ili nifanye kazi kwa bidii hata zaidi. Niliogopa kuhamishiwa, na kwa hivyo nilimwomba Mungu bila kukoma: “Ee Mungu! Najua huu ni mtego ambao pepo wameniwekea, lakini hakuna njia ya kuutoroka. Tafadhali nipe suluhisho.” Kwa mshangao wangu, baada ya kuomba ombi hili, licha ya hali ya hewa kuwa joto mikono yangu ilianza kuwa baridi na vidole vyangu vikashikamanana kuwa samawati. Afisa wa marekebisho wa timu kuu ya kazi alisema nilikuwa nikijifanya naye akawalazimisha wengine wawili wanibebe hadi ghorofani ili nifanye kazi. Nilimlilia tu Mungu kwa kukata tamaa, matokeo yake yakiwa kwamba niliishia kuanguka kutoka ghorofa ya tatu hadi ghorofa ya pili. Walipoona hivi, waliogopa, na kwa hivyo walinirudisha nijiunge na kikundi cha kazi cha wazee. Baadaye, niligundua kuwa kwa kweli mwili wangu haukuwa umejeruhiwa hata kidogo—kwa mara nyingine nilimshuhudia Mungu akinilinda.

Humo gerezani, waumini katika Mwenyezi Mungu wamepachikwa jina la wafungwa wa kisiasa na pepo wa CCP hutuchunga kila wakati, kumaanisha kuwa hata hatuna haki ya kuongea. Ikiwa ningeongea na mtu, walinzi wa gereza wangeona na kisha kutuhoji kuhusu kile tulichokuwa tukisema. Wakati wa usiku, walimfanya mkuu wa wafungwa anichunge ili kuona kama nilikuwa nikijadili mambo ya imani na watu wengine. Wakati wowote mtu yeyote katika familia yangu aliponitembelea, walinzi wa gereza walinilazimisha nijifunze kusema maneno kadhaa ambayo yalimkashifu Mungu, na kama singeyasema basi wangekatiza mazungumzo yangu na familia yangu kwa makusudi (jambo ambalo lilimaanisha kuwa ningekuwa na muda mfupi zaidi wa kuzungumza nao). Kwa sababu nilijua kuwa kusema mambo kama hayo kungemkosea Mungu, wakati wowote nilipokumbana na hali hii, nilimwomba Mungu kimyakimya, na kusema, “Ee Mungu! Huyu ni Shetani anayejaribu kunijaribu. Tafadhali Nilinde na Unizuie nisiseme chochote kinachoweza kuikosea tabia Yako.” Kwa sababu sikuwahi kusema chochote walichotaka niseme, hakukuwa na kitu ambacho walinzi wa gereza wangefanya kuhusu jambo hilo mwishowe.

Miaka mitatu gerezani ilinisababisha nione waziwazi tabia halisi ya serikali ya CCP. Inatenda kwa njia moja mbele ya watu na kisha kwa njia nyingine sirini; kwa ulimwengu wa nje, inasifu “uhuru wa dini,” lakini sirini ya inaitesa na kuikatiza kazi ya Mungu katika kila njia inayowezekana, na inawakamata waumini wa Mungu kwa hasira, inawafanya watu wakiri kupitia mateso, na kuwanyanyasa kikatili. Inatumia mbinu zenye kustahili dharau zaidi zinazoweza kufikirika ili kuwalazimisha watu wamkatae Mungu, wamsaliti Mungu na kujisalimisha kwa mamlaka yake ya kidikteta ili kufanikisha malengo yake maovu ya kuwakomesha na kuwadhibiti watu wakati wote. Wanadamu waliumbwa na Mungu na wanapaswa kumwabudu Mungu. Lakini serikali ya CCP inafanya yote iwezayo kutoa maanani kuja kwa Mungu, inawazuia watu kumwamini Mungu, kuhubiri injili na kumshuhudia Mungu, na kwa kufanya hivyo inafunua kabisa kiini chake kiovu ambacho ni kipotovu na kinachokwenda kinyume na mbinguni. Baada ya kupitia mateso na dhiki hii, ingawa mwili wangu ulipata maumivu kiasi, sina malalamiko na majuto, kwa kuwa nimepata mengi sana kutoka kwa Mungu. Nilipokuwa nikihisi kuwa dhaifu na asiye na nguvu, ni Mungu aliyenipa imani na nguvu tena na tena, Akiniwezesha kupata azimio la kupigana na Shetani hadi mwisho kabisa; nilipohisi kusikitika na kuhuzunika, mwenye huzuni na kukata tamaa, ni Mungu aliyetumia maneno Yake kunifariji na kunitia moyo; nilipokuwa karibu kufa, ni maneno ya Mungu ambayo yalinipa motisha ya kuendelea kuishi na ujasiri wa kuendelea kuishi; kila nilipokuwa katika hatari, Mungu aliunyoosha mkono Wake wa wokovu wakati ufaao hasa, Akinilinda, Akinisaidia kuepuka hatari na kuniokoa niwe salama. Kupitia uzoefu huu, sikuja tu kuona waziwazi kiini cha ibilisi Shetani cha kumpinga Mungu, na kuja kumchukia sana na kikamilifu kabisa, lakini wakati huo huo, pia nilikuja kupata ufahamu kiasi wa kweli kuhusu matendo ya Mungu ya ajabu, pamoja na upendo na wokovu wa Mungu. Nilikuja kuthamini kwa kweli wema na unyenyekevu wa Kristo na mateso aliyovumilia ili kuwaokoa wanadamu, na imani yangu na upendo wangu kwa Mungu vilizidishwa.

Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, kwa sababu pepo wa CCP walizua chuki baina yetu, marafiki na familia yangu wote walinikataa na kuniepuka. Hata hivyo, ndugu zangu kanisani, wote walinishughulikia na kunitunza, na walinipa kila kitu nilichohitaji ili kuanza maisha tena—kwa kufanya hivi, walinipa hisia ya ukunjufu ambayo ingekuwa vigumu sana kupata mahali popote pengine. Namshukuru Mungu kwa kuniokoa: Bila kujali barabara iliyo mbele ilivyo ngumu jinsi gani, nitamfuata Mungu hadi mwisho kabisa na kutafuta kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana ya kumlipiza kwa ajili ya upendo Wake.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp