822 Jinsi ya Kushuhudia kwa Mungu ili Upate Matokeo ya Vitendo
Mnapokuwa na ushuhuda wa, mnapaswa kuzungumza hasa kuhusu jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwaadibu watu, ni majaribio yapi anayoyatumia kuwasafisha wanadamu na kubadilisha tabia zao. Mnapaswa pia kuzungumza kuhusu kiwango cha upotovu ambacho kimefichuliwa katika uzoefu wenu, kiasi ambacho mmestahimili na jinsi ambavyo hatimaye mlishindwa na Mungu; kiasi cha maarifa ya kweli ya kazi ya Mungu mlicho nacho, na jinsi mnavyopaswa kumshuhudia Mungu na kumlipiza kwa ajili ya upendo Wake. Mnapaswa kuweka umuhimu katika lugha ya aina hii, huku mkiisema kwa njia rahisi. Msizungumze juu ya nadharia tupu. Zungumzeni mambo halisi zaidi, zungumzeni kwa dhati. Hivi ndivyo jinsi mnavyopaswa kupitia. Msijiandae kwa nadharia zinazoonekana kuu, zilizo tupu katika juhudi la kujionyesha; kufanya hivyo kunawafanya muonekane wenye majivuno sana na msio na maana. Mnapaswa kuzungumza zaidi kuhusu mambo ya kweli na halisi kutoka kwa uzoefu wenu ambayo ni ya kweli na ya dhati; hili ndilo la manufaa zaidi kwa wengine, na ndilo linalowafaa zaidi kuona. Ninyi mlikuwa watu waliompinga Mungu zaidi na ambao waliegemea kumtii Yeye kwa kiasi kidogo zaidi, lakini sasa mmeshindwa—msisahau hilo kamwe. Mnapaswa kutenga tafakari na fikira nyingi kwa masuala haya kwa bidii. Vinginevyo mnaweza kufanya vitendo vya aibu na vya kipumbavu.
Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo