939 Ishara ya Tabia ya Mungu

1 Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, tulizo kwa binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa binadamu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Aidha, ni ishara ya Yeye ambaye hawezi kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui, pamoja na ishara ya Yeye ambaye hawezi kukosewa (wala Hatavumilia kukosewa) na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanao uwezo au wanaoweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake.

2 Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na ni mwenye heshima kila wakati, ilhali mwanadamu siku zote ni wa chini, siku zote asiye na thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa wanadamu; mwanadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na kujitahidi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia kwa dhati kuendelea kuishi kwa wanadamu, ilhali mwanadamu kamwe hachangii kitu kwa ajili ya mwangaza au haki. Hata kama mwanadamu anajitahidi sana kwa muda, ni dhaifu sana kiasi cha kutoweza kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake mwenyewe na wala si kwa ajili ya wengine. Mwanadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mwenye ubinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo vya haki, vyema, na vya uzuri, huku naye mwanadamu ni yule anayerithi na kudhihirisha vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na uzuri, ilhali mwanadamu anaweza kabisa, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 938 Tabia Ya Mungu Ni Ya Juu na Tukufu

Inayofuata: 940 Tabia ya Haki ya Mungu ni Halisi na Dhahiri

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp