660 Wimbo wa Washindani

1 Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu yu nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; binadamu utaguswa vipi? Mmeona na macho yenu hali ya mwanadamu; hakika bado hamna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii?

2 Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu.

3 Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawakumbuka, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao.

4 Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kuzitafuta ahadi mlizofanyiwa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya katika utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtasimama imara na thabiti katika nchi ya Sinimu. Kupitia katika mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaonyesha utukufu Wangu katika ulimwengu mzima.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 19” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 659 Wale Wanaoshuhudia Katika Taabu ni Washindi

Inayofuata: 661 Wafuasi wa Kweli wa Mungu Wanaweza Kusimama Imara Katika Majaribio

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp