37 Hatuwezi Kuacha Kuimba Nyimbo za Upendo kwa Mungu

Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi,

ndivyo tumpendavyo zaidi!


Tunaimba juu ya kupata mwili kwa Mungu.

Tunainuliwa mbele ya kiti Chake,

na hatutazami mbinguni tena,tukitamani.

Mwenyezi Mungu yuko uso kwa uso nasi.

Atuchunga kwa ukweli,

kando yetu, wa kweli na halisi.

Tunafurahia maneno Yake kila siku.

Kuelewa ukweli kuna utamu sana.


Moyo wetu umejaa upendo kwa Mungu,

kwa kuwa tunauona uso Wake wa kupendeza.

Tunaimba na kucheza kwa sifa,

hakuna maneno ya kuelezea kupendeza Kwake.


Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi,

ndivyo tumpendavyo zaidi!


Twaimba juu ya hukumu ya haki ya Mungu.

Maneno Yake yatutakasa na kutuokoa,

yakifichua asili ya kishetani ya mwanadamu

na ukweli wa upotovu wa mwanadamu.

Maneno Yake hutakasa

tabia zetu za kishetani,

yakitufanya tuwe watu wapya.

Tumetupa nguvu za Shetani.

Tunaona upendo wa Mungu ni wa kweli.

Haki Yake ni ya kupendeza,

utakatifu Wake ni mtamu sana.

Hatuwezi kumpenda vya kutosha.


Hivyo tunamsifu Mungu; hatuwezi kuzuia hisia zetu.

Hakuna kinachoweza kuja kati yetu na Mungu.


Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi,

ndivyo tumpendavyo zaidi!


Neno la Mungu latawala katika maisha ya ufalme.

Tunaishi katika nuru.

Kupata ukweli kumetuweka huru.

Tunamwabudu Mungu kwa moyo, kwa uaminifu.

Tumekuwa wandani Wake,

tukimtumikia kwa uaminifu.


Tunambebea mzigo, tukitimiza wajibu wetu kweli,

daima tukiendelea kwenye njia ya kumpenda Mungu.


Sasa tunaweza kumpenda na kumtii Mungu,

kuishi kwa ajili Yake, hii ndiyo furaha kubwa zaidi.

Mwenyezi Mungu, tunakusifu!

Tunakuabudu milele!


Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi,

ndivyo tumpendavyo zaidi!

Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi,

ndivyo tumpendavyo zaidi!

Iliyotangulia: 36 Sifunini Kurejea kwa Mungu Sayuni

Inayofuata: 38 Maisha ya Kanisa Huleta Furaha Kuu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki