46 Ni Mwenyezi Mungu Pekee Awezaye Kumwokoa Mwanadamu

1 Matendo ya Mwenyezi Mungu yalivyo makuu! Ni ajabu iliyoje! Jinsi gani ilivyo ya kushangaza! Tarumbeta saba zinatoa sauti, ngurumo saba zinatotoka, na bakuli saba zinamwangwa—hivi vitadhihirika wazi kuanzia sasa kuendelea, na hakuwezi kuwa na shaka. Upendo wa Mungu hutujia kila siku. Ni Mwenyezi Mungu pekee Anayeweza kutuokoa; kama tunakabiliwa na bahati mbaya au tunapokea baraka yote yamo mikononi Mwake kabisa, na sisi binadamu hatuna njia ya kuamua hili. Wale wanaojitoa wenyewe kwa moyo wao wote hakika watapokea baraka tele tele, ilhali wale wanaotafuta kulinda maisha yao wanapoteza tu maisha yao; vitu vyote na mambo yote yamo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Usisitishe hatua zako tena. Mabadiliko ya kiwango kikubwa yanakuja mbinguni na duniani, ambayo mwanadamu hawezi kujificha kutoka kwayo. Hakutakuwa na chaguo lingine kwake ila kulia kwa uchungu mkubwa.

2 Fuata kazi ambayo Roho Mtakatifu anafanya leo. Unapaswa kuwa dhahiri ndani yako kuhusu hatua ambayo kwayo kazi Yake imeendelea, bila haja ya kukumbushwa na wengine. Rejea sasa katika uwepo wa Mwenyezi Mungu mara nyingi kadiri ya uwezo wako. Mwombe kila kitu. Hakika Atakupa nuru ndani na, katika nyakati muhimu kabisa, Atakulinda. Usiwe na hofu! Tayari Anamiliki nafsi yako yote. Kwa ulinzi Wake na huduma Yake, kuna nini cha wewe kuogopa? Leo mafanikio ya mapenzi ya Mungu umekaribia, na yeyote anayehofu anaelekea tu kupoteza. Kile Ninachokwambia ni ukweli. Fungua macho yako ya kiroho: Mbingu inaweza kubadilika ghafla, lakini kuna nini cha wewe kuhofu? Kwa ishara ndogo kabisa ya mkono Wake, mbingu na dunia vinaangamizwa mara moja. Kwa hivyo mwanadamu anaweza kufaidi nini kwa kuhofu? Je, si vitu vyote viko mikononi mwa Mungu?

3 Akiziamuru mbingu na dunia kubadilika, basi zitabadilika. Akisema tunapaswa kukamilishwa, basi tutakamilishwa. Mwanadamu hapaswi kuwa na haraka, bali anapaswa kuendelea kwa utulivu. Hata hivyo, unapaswa, kadiri ya uwezo wako, uwe msikivu sana na uwe macho. Mbingu inaweza kubadilika ghafla! Hata mwanadamu ayafungue macho yake wazi vipi, hataweza kuona kitu chochote. Kuwa mwangalifu sasa. Mapenzi ya Mungu yametimizwa, mradi Wake umekamilika, mpango Wake umefanikiwa, na wanawe wote wamefika kwenye kiti Chake cha enzi. Kwa pamoja wote wanakuja kukaa ili kuyahukumu mataifa yote na watu wote pamoja na Mwenyezi Mungu. Wale ambao wamekuwa wakilitesa kanisa na kuwadhuru wana wa Mungu watakutana na adhabu kali: Hilo ni bila shaka! Wale ambao hujitoa kwa dhati kwa Mungu, wanashikilia kila kitu, bila shaka Mungu atawapenda milele na milele, bila kubadilika kamwe!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 42” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 45 Mungu Yuko Mbinguni na Pia Duniani

Inayofuata: 47 Ni Mwenyezi Mungu Pekee Aliye Uzima Uliofufuka wa Milele

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp