3. Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya nchi ya Israeli, lakini, Alichagua kikundi cha watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.
Wakati huu, umuhimu, kusudi na awamu za kazi ya Yehova huko Israeli zilikuwa kuanzisha kazi Yake katika dunia nzima, ambayo, ikichukua Israeli kama kituo chake, ilienea polepole hadi kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hii ni kanuni ambayo kwayo Anafanya kazi katika ulimwengu mzima—kuunda mfano na kisha kuupanua hadi watu wote ulimwenguni watakuwa wamepokea injili Yake. Waisraeli wa kwanza walikuwa wa ukoo wa Nuhu. Watu hawa walikuwa wamejawa tu na pumzi ya Yehova, na walielewa kiasi cha kutosha ili kushughulikia mambo muhimu ya msingi ya maisha, lakini hawakujua Yehova alikuwa Mungu wa aina gani, au mapenzi Yake kwa mwanadamu, sembuse jinsi wanavyopaswa kumcha Bwana wa viumbe vyote. Kuhusu iwapo kulikuwa na sheria na kanuni za kutiiwa,[a] au iwapo kulikuwa na wajibu ambayo viumbe walioumbwa wanapaswa kumfanyia Muumba, wa ukoo wa Adamu hawakujua hata kidogo kuhusu mambo haya. Yote waliyojua ilikuwa kwamba mume anapaswa kutokwa jasho na kufanya kazi ili kukimu familia yake, na kwamba mke anapaswa kumtii mume wake na kuendeleza jamii ya binadamu ambao Yehova alikuwa ameumba. Kwa maneno mengine, watu wa aina hii, ambao walikuwa na pumzi ya Yehova na uzima Wake pekee, hawakujua kabisa kuhusu jinsi ya kufuata sheria za Mungu au jinsi ya kumridhisha Bwana wa viumbe vyote. Walielewa kidogo sana. Kwa hivyo ingawa hakukuwa na kitu kisicho kipotovu au cha udanganyifu mioyoni mwao na wivu na ugomvi viliibuka miongoni mwao mara chache, hata hivyo hawakuwa na maarifa au ufahamu wa Yehova, Bwana wa viumbe vyote. Mababu hawa wa mwanadamu walijua tu kula vitu vya Yehova, na kufurahia vitu vya Yehova, lakini hawakujua kumcha Yehova: hawakujua kwamba Yehova ndiye Yule wanayepaswa kumwabudu kwa kupiga magoti. Kwa hiyo wangeweza kuitwa viumbe Wake vipi? Kama hali ingekuwa hivi, je maneno, “Yehova ndiye Bwana wa viumbe vyote” na “Alimuumba mwanadamu ili mwanadamu aweze kumdhihirisha Yeye, kumtukuza Yeye, na kumwakilisha Yeye”—hayangekuwa yamesemwa bure? Watu ambao hawamchi Yehova wangewezaje kuwa ushuhuda kwa utukufu Wake? Wangewezaje kuwa dhihirisho la utukufu Wake? Je, maneno ya Yehova “Nilimuumba mwanadamu kwa mfano Wangu” si yangekuwa silaha mikononi mwa Shetani basi—yule mwovu? Maneno haya basi hayangekuwa alama ya fedheha kwa Yehova kumuumba mwanadamu? Ili kukamilisha hatua hiyo ya kazi, baada ya kuwaumba wanadamu, Yehova hakuwaagiza au kuwaongoza kutoka wakati wa Adamu hadi ule wa Nuhu. Badala yake, baada ya dunia kuharibiwa na gharika tu ndiyo wakati ambapo Alianza rasmi kuwaongoza Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa Adamu. Kazi na matamshi Yake huko Israeli yaliwapa watu wote wa Israeli mwongozo walipokuwa wakiishi maisha yao katika nchi yote ya Israeli, na kwa njia hii yakaonyesha binadamu kwamba Yehova hakuweza tu kupuliza pumzi ndani ya mwanadamu, ili aweze kuwa na uhai kutoka Kwake na kuinuka kutoka mavumbini kuwa mwanadamu aliyeumbwa, lakini kwamba pia Angeweza kuwachoma wanadamu, na kuwalaani wanadamu, na kutumia fimbo Yake kuwatawala wanadamu. Kwa hivyo, pia waliona kwamba Yehova angeweza kuyaongoza maisha ya mwanadamu duniani, na kuzungumza na kufanya kazi miongoni mwa binadamu kulingana na saa za mchana na za usiku. Alifanya kazi hiyo ili tu viumbe Wake waweze kujua kwamba mwanadamu alitoka kwa mavumbi yaliyochaguliwa na Yeye, na aidha kwamba mwanadamu alikuwa ameumbwa na Yeye. Siyo haya tu, lakini kazi Aliyoanza huko Israeli ilikusudiwa ili kwamba watu na mataifa (ambao kwa kweli hawakuwa wametengwa na Israeli, lakini badala yake walikuwa wameenea kutoka kwa Waisraeli, ilhali bado walikuwa wa ukoo wa Adamu na Hawa) waweze kupokea injili ya Yehova kutoka Israeli, ili viumbe wote walioumbwa ulimwenguni waweze kuwa na uwezo wa kumcha Yehova na kumchukulia kuwa mkuu. Yehova asingeanza kazi Yake huko Israeli, lakini badala yake, baada ya kuwaumba wanadamu, awaache waishi maisha machangamfu duniani, basi katika hali hiyo, kwa sababu ya asili ya maumbile ya mwanadamu (asili inamaanisha kwamba mwanadamu hawezi kamwe kujua vitu ambavyo hawezi kuviona, yaani kwamba hangejua kwamba ilikuwa ni Yehova ambaye aliwaumba wanadamu, sembuse sababu yake kufanya hivyo), hangejua kamwe kwamba ilikuwa Yehova aliyewaumba wanadamu au kwamba Yeye ni Bwana wa viumbe vyote. Kama Yehova angemuumba mwanadamu na kumweka duniani, na kutoshughulika na yeye na kuondoka tu, badala ya kubaki miongoni mwa wanadamu ili kuwaongoza kwa kipindi cha muda, basi katika hali hiyo wanadamu wote wangekuwa wamerudi kuwa bure: hata mbingu na dunia na vitu vyote vingi Alivyoviumba, na wanadamu wote, vingerudi kuwa bure na aidha vingekanyagwa na Shetani. Kwa njia hii matakwa ya Yehova kwamba “Duniani, yaani, miongoni mwa viumbe Vyake, Anapaswa kuwa na mahali pa kusimama, mahali patakatifu” yangevunjwa. Na hivyo, baada ya kuwaumba wanadamu, kwamba Aliweza kubaki miongoni mwao kuwaongoza katika maisha yao, na kuzungumza nao kutoka miongoni mwao, yote haya yalikuwa ili kufanikisha hamu Yake, na kutimiza mpango Wake. Kazi Aliyoifanya huko Israeli ilikusudiwa tu kutekeleza mpango Aliokuwa ameuweka kabla ya kuumba Kwake vitu vyote, na kwa hivyo Yeye kufanya kazi kwanza miongoni mwa Waisraeli na Yeye kuumba vitu vyote hakukutofautiana, lakini yote yalikuwa kwa ajili ya usimamizi Wake, kazi Yake, na utukufu Wake, na pia ili kuimarisha maana ya Yeye kuumba wanadamu. Aliyaongoza maisha ya wanadamu duniani kwa miaka elfu mbili baada ya Nuhu, wakati ambapo Aliwafunza wanadamu kuelewa jinsi ya kumcha Yehova Bwana wa viumbe vyote, jinsi ya kuendesha maisha yao na jinsi ya kuendelea kuishi, na zaidi ya yote, jinsi ya kutenda kama shahidi wa Yehova, kumtii, na kumcha, hata kumsifu kwa muziki kama Daudi na wakuhani wake walivyofanya.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria
Yehova aliwaumba wanadamu, ambayo ni kusema kwamba Yeye aliumba babu za wanadamu: Hawa na Adamu. Lakini hakuwapa akili zaidi au hekima. Ingawa walikuwa tayari wanaishi duniani, hawakuelewa takriban chochote. Na kwa hiyo, kazi ya Yehova ya kuwaumba wanadamu ilikuwa imefanyika nusu tu, haikuwa imekaribia kukamilika. Alikuwa ameumba tu mfano wa mwanadamu kutoka kwa udongo na kumpa pumzi Yake, lakini Hakuwa amempa mwanadamu radhi ya kutosha kumcha Yeye. Hapo mwanzo, mwanadamu hakuwa na akili ya kumcha Yeye, au kumwogopa Yeye. Mwanadamu alijua tu jinsi ya kuyasikiliza maneno Yake lakini hakujua ujuzi wa msingi wa maisha duniani na sheria za kawaida za maisha. Na kwa hiyo, ingawa Yehova aliumba mwanamume na mwanamke na kumaliza siku saba za shughuli, Hakukamilisha uumbaji wa mwanadamu hata kidogo, kwa maana mwanadamu alikuwa ganda tu, na hakuwa na uhalisi wa kuwa mwanadamu. Mwanadamu alijua tu kwamba ni Yehova aliyeumba wanadamu, lakini mwanadamu hakuwa na fununu ya jinsi ya kutii maneno na sheria za Yehova. Na kwa hiyo, baada ya kuumbwa kwa wanadamu, kazi ya Yehova ilikuwa mbali sana kumalizika. Pia alitakiwa kuwaongoza wanadamu kabisa mbele Yake ili wanadamu waweze kuishi pamoja duniani na kumcha Yeye, na ili wanadamu waweze kwa mwongozo Wake kuingia katika njia sahihi ya maisha ya kawaida ya binadamu duniani baada ya kuongozwa na Yeye. Kwa njia hii tu ndiyo kazi ambayo ilikuwa imeendeshwa kwa kiasi kikubwa kupitia jina la Yehova ilimalizika kabisa; yaani, kwa njia hii tu ndiyo kazi ya Yehova ya kuumba ulimwengu ilihitimishwa kabisa. Na kwa hiyo, kwa vile Alimuumba mwanadamu, Alipaswa kuongoza maisha ya wanadamu duniani kwa miaka elfu kadhaa, ili wanadamu waweze kutii amri na sheria Zake, na kushiriki katika shughuli zote za maisha ya kufaa ya binadamu duniani. Wakati huo tu ndio kazi ya Yehova ilikamilika kabisa. Alianza kazi hii baada ya kuumba wanadamu, na kazi Yake iliendelea mpaka wakati wa Yakobo, wakati wana kumi na wawili wa Yakobo walipokuwa makabila kumi na mbili ya Israeli. Tangu wakati huo na kuendelea, kila mtu katika Israeli akawa watu walioongozwa rasmi na Yeye duniani, na Israeli ikawa mahali maalumu duniani ambapo Alifanya kazi Yake. Yehova aliwafanya watu hawa kundi la kwanza kati ya watu ambalo kwalo Alifanya kazi Yake rasmi duniani, na kuifanya nchi nzima ya Israeli kuwa kiwango cha kuanzia kazi Yake. Aliwatumia kama mwanzo wa hata kazi kubwa zaidi, ili watu wote waliozaliwa kutoka Kwake duniani wangejua jinsi ya kumcha Yeye na kuishi duniani. Na kwa hiyo, matendo ya Waisraeli yakawa mfano wa kufuatwa na Mataifa, na kile kilichosemwa kati ya watu wa Israeli kikawa maneno ya kusikizwa na Mataifa. Kwa kuwa walikuwa wa kwanza kupokea sheria na amri za Yehova, na vivyo hivyo pia walikuwa wa kwanza kujua jinsi ya kuzicha njia za Yehova. Wao walikuwa mababu wa binadamu ambao walijua njia za Yehova, na walikuwa wawakilishi wa wanadamu waliochaguliwa na Yehova.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
Katika Enzi ya Sheria, Yehova aliweka amri nyingi za Musa kupitisha kwa Waisraeli waliomfuata kutoka Misri. Amri hizi walipewa Waisraeli na Yehova, na hazikuwa na uhusiano kwa Wamisri: zilinuiwa kuwazuia Waisraeli. Yeye alizitumia amri kuwatolea madai. Iwapo waliishika Sabato, iwapo waliwaheshimu wazazi wao, iwapo waliziabudu sanamu, na kadhalika: hizi zilikuwa kanuni ambazo kwazo walihukumiwa kuwa wenye dhambi au wenye haki. Miongoni mwao, kuna baadhi walioangamizwa kwa moto wa Yehova, baadhi waliopigwa mawe hadi kufa, na baadhi waliopokea baraka za Yehova, na haya yaliamuliwa kulingana na iwapo walizitii amri hizi au la. Wale ambao hawakuishika Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakuishika Sabato wangeangamizwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuwaheshimu wazazi wao pia wangepigwa mawe hadi kufa. Yote haya yalikubaliwa na Yehova. Yehova alianzisha amri na sheria Zake ili, Alipokuwa akiwaongoza katika maisha yao, watu wangesikiliza na kuti neno Lake na kutoasi dhidi Yake. Alitumia sheria hizi kuidhibiti jamii ya binadamu iliyokuwa imezaliwa karibuni, ili kuweka vizuri zaidi msingi wa kazi Yake ya baadaye. Na kwa hivyo, kwa msingi wa kazi ambayo Yehova alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya sheria. Ingawa Yehova alisema matamshi mengi na kufanya kazi nyingi, Aliwaongoza watu kwa njia njema tu, akiwafunza watu hawa wasiojua jinsi ya kuwa binadamu, jinsi ya kuishi, jinsi ya kuelewa njia ya Yehova. Kwa kiwango kikubwa sana, kazi Aliyoifanya ilikuwa ili kuwasababisha watu kutii njia Yake na kufuata sheria Zake. Kazi hii ilifanywa kwa watu waliokuwa wamepotoshwa kwa kiasi kidogo; haikuenea kiasi cha kubadili tabia yao au maendeleo katika maisha. Alijishughulisha tu na kutumia sheria kuwazuia na kuwadhibiti watu. Kwa Waisraeli wa wakati huo, Yehova alikuwa Mungu katika hekalu tu, Mungu huko mbinguni. Alikuwa nguzo ya wingu, nguzo ya moto. Yote ambayo Yehova aliwataka wafanye ilikuwa ni kutii kile ambacho watu wa leo wanakijua kama sheria na amri Zake—mtu anaweza pia kusema kanuni—kwa sababu kile ambacho Yehova alifanya hakikunuiwa kuwabadilisha, ila kuwapa vitu zaidi ambavyo mwanadamu anapaswa kuwa navyo, kuwaagiza kutoka kinywani Mwake mwenyewe, kwa sababu baada ya kuumbwa, mwanadamu hakuwa na chochote alichopaswa kumiliki. Na kwa hivyo, Yehova aliwapa watu vitu ambavyo walipaswa kumiliki kwa ajili ya maisha yao duniani, Akiwafanya watu Aliokuwa ameongoza kuwashinda mababu zao, Adamu na Hawa, kwa sababu kile Yehova alichowapa kilishinda kile Alichokuwa amewapa Adamu na Hawa mwanzoni. Bila kujali, kazi ambayo Yehova alifanya huko Israeli ilikuwa tu kuwaongoza binadamu na kuwafanya binadamu wamtambue Muumba wao. Hakuwashinda wala kuwabadilisha, ila Aliwaongoza tu. Hii ndiyo kazi yote ya Yehova katika Enzi ya Sheria. Ndio usuli, masimulizi ya kweli, kiini cha kazi Yake katika nchi nzima ya Israeli, na mwanzo wa kazi Yake ya miaka elfu sita—kuendeleza udhibiti wa wanadamu kwa mkono wa Yehova. Kutokana na hili kulizaliwa kazi zaidi katika mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi katika Enzi ya Sheria
Kazi ambayo Yesu alifanyika ililingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, ustahamilivu, huruma na wema. Aliwabariki wanadamu kwa wingi na kuwaletea neema nyingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu Wake na upendo, huruma Yake na wema. Katika siku hizo, chote alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, roho yake ilifarijika, na alikuwa anaruzukiwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi. Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa tayari na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji neema nyingi, ustahimili na uvumilivu usio na mwisho, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu walichoona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya kulipia dhambi za binadamu, yaani, Yesu. Yote waliyojua ni kwamba Mungu angeweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na yote waliyoona ni huruma ya Yesu na wema Wake. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu wao walizaliwa katika Enzi ya Neema. Na hivyo, kabla ya kuweza kukombolewa, walilazimika kufurahia neema za aina nyingi ambazo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na pia wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu pekee ndio walipata haki ya wa kupokea msamaha na kufurahia neema nyingi kutoka kwa Yesu—kama vile Yesu alivyosema: Sijakuja kuwakomboa wenye haki, ila wenye dhambi, kukubali dhambi zao zisamehewe. Kama Yesu angepata mwili wa tabia ya hukumu, laana, na kutovumilia makosa ya mwanadamu, basi mwanadamu kamwe hangeweza kupata nafasi ya kukombolewa, na daima yeye angebaki mwenye dhambi. Hali ingekuwa hivi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Sheria ingeendelea kwa miaka elfu sita. Dhambi za mwanadamu zingeongezeka zaidi na kuwa mbaya zaidi tu, na uumbaji wa binadamu ungekuwa wa bure. Wanadamu wangeweza tu kumtumikia Yehova chini ya sheria, bali dhambi zao zingezidi za wanadamu wa kwanza kuumbwa. Jinsi Yesu alivyowapenda wanadamu zaidi, Akisamehe dhambi zao na kuwapa huruma na wema wa kutosha, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, wa kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa gharama kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anavyotunza mtoto mchanga aliye kifuani pake. Yeye hakuwa na hasira nao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na ghadhabu miongoni mwao, lakini alistahimili dhambi zao na Akapuuza upumbavu wao na kutofahamu, hata kusema, “Uwasamehe wengine mara sabini mara saba.” Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine. Ilikuwa ni kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha wa dhambi kupitia uvumilivu Wake.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi
Ingawa Yesu katika mwili Wake hakuwa na hisia kabisa, Yeye daima Aliwafariji wanafunzi Wake, Aliwapa mahitaji yao, Akawasaidia, na Akawaruzuku. Bila kujali kiwango cha kazi Alichofanya au kiasi gani cha mateso Alivumilia, Yeye kamwe hakuwa na matarajio ya kupita kiasi kwa mwanadamu, lakini kila mara Alikuwa mwenye subira na kuvumilia dhambi zao, kiasi kwamba katika Enzi ya Neema kwa upendo watu walimwita “Mwokozi Yesu anayependeka.” Kwa watu wa wakati huo—kwa watu wote—kile Yesu Alikuwa nacho na kile Alichokuwa, kilikuwa huruma na wema. Yeye kamwe hakukumbuka dhambi za, na hakuwatendea kulingana na dhambi zao. Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, mara nyingi Alitoa chakula na vinywaji kwa watu ili waweze kula hadi washibe. Yeye Aliwatendea wafuasi Wake wote kwa ukarimu, akaponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kufufua wafu. Ili kwamba watu waweze kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanyika kwa bidii na kwa dhati, Yeye Alifika kiwango cha kufufua maiti iliyooza, kuwaonyesha kwamba mikononi Mwake hata wafu wanaweza kuwa hai tena. Kwa njia hii Alivumilia kwa kimya na kufanya kazi Yake ya ukombozi kati yao. Hata kabla Asulubiwe, Yesu Alikuwa tayari Amebeba dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu. Hata kabla Asulubiwe, Alikuwa tayari Amefungua njia ya msalaba ili kuwakomboa wanadamu. Mwishowe Aligongwa misumari msalabani, Alijitoa sadaka Yeye Mwenyewe kwa ajili ya msalaba, na Alitoa huruma Yake yote, wema Wake, na utakatifu kwa wanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi
Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, dunia yote ingekuwa mahali pa kulala pa Shetani, maskani yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji kuonyesha huruma na wema kwa wanadamu; kupitia kwa njia hiyo tu ndio wanadamu wangeweza kupokea msamaha na mwishowe kupata haki ya kukamilishwa na kumilikiwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Katika miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alitumia kufanya kazi Yake hapa duniani alikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha, kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa yule mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaendesha majaaliwa ya wanadamu. Baada ya Yeye kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo alipowakomboa wanadamu. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Akidhihakiwa, kukashifiwa, na kuachwa, kiasi cha Yeye kukosa mahali pa kulaza kichwa chake, mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, huku nafsi Yake yote—mwili mtakatifu na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani. Alivumilia kila namna ya mateso yaliyoko. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na maaskari hata wakamtemea mate usoni; ilhali Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa wanadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ambayo Yesu alifanya inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria wala si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo wanadamu wamepitia—Enzi ya Ukombozi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi
Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)
Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji
Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji
Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini hili halikumaanisha kuwa mwanadamu hakuwa na dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, “Neno kuonekana katika mwili”; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapumziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaufanyikia Misri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno "maneno" linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kufanya kazi Yake, na kufikia matokeo ya kazi Yake. Hatendi maajabu au kufanya miujiza, lakini hufanya kazi Yake kupitia katika maneno tu. Kwa sababu ya maneno haya, mwanadamu hulishwa na kuruzukiwa, na hupata maarifa na uzoefu wa kweli.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno
Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa enzi, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kutompitisha mwanadamu katika hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki: basi usimamizi wa Mungu ungetamatishwa lini? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kumtenganisha mwanadamu kulingana na aina yake na kumleta mwanadamu katika ufalme mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili hayana maneno “kutiiwa”.