2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu
Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kuelewa mapenzi Yangu, na wajue kwamba Mimi Ndimi ukweli.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi
Lazima ujue kuwa bila kujali kazi ambayo Yeye anatenda, lengo la kazi ya Mungu halibadiliki, kiini cha kazi Yake hakibadiliki, na mapenzi Yake kwa mwanadamu hayabadiliki. Bila kujali maneno Yake ni makali namna gani, haijalishi mazingira ni mabaya kiasi gani, kanuni za kazi Yake, na nia Yake ya kumwokoa mwanadamu hayatabadilika. Mradi tu si ufunuo wa mwisho wa mwanadamu au hatima ya mwanadamu, na si kazi ya awamu ya mwisho, au kazi ya kutamatisha mpango wote wa usimamizi wa Mungu, na mradi tu ni wakati Anapomfinyanga mwanadamu, basi kiini cha kazi Yake hakitabadilika: Daima kitakuwa wokovu wa mwanadamu. Hili linapaswa kuwa msingi wa imani yenu katika Mungu. Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Leo kwanza kabisa tutafanya muhtasari wa fikira, mawazo, na kila hatua ya Mungu tangu Alipomuumba binadamu, na kuangalia ni kazi gani Alitekeleza kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi mwanzo rasmi wa Enzi ya Neema. Tunaweza kisha kugundua ni fikira na mawazo yapi ya Mungu ambayo hayajulikani kwa binadamu, na kuanzia hapo tunaweza kuweka wazi mpangilio wa mpango wa usimamizi wa Mungu na kuelewa kwa kina muktadha ambao kwao Mungu alianzisha kazi Yake ya usimamizi, chanzo chake na mchakato wake wa maendeleo, na pia kuelewa kwa undani ni matokeo yapi Anayotaka kutoka katika kazi Yake ya usimamizi—yaani, kiini na kusudio la kazi Yake ya usimamizi. Kuelewa mambo haya tunahitaji kurudi hadi ule wakati wa kitambo, mtulivu na kimya ambapo hakukuwa na binadamu …
Wakati Mungu aliinuka kutoka kitandani Mwake, fikira ya kwanza Aliyokuwa nayo ilikuwa hii: kumuumba binadamu hai, halisi, binadamu anayeishi—mtu wa kuishi naye na kuwa mwenzake wa kila mara. Mtu huyu angemsikiliza, na Mungu angempa siri Zake na kuongea na yeye. Kisha, kwa mara ya kwanza, Mungu aliuchukua udongo kwenye mkono na kuutumia kumuumba mtu wa kwanza kabisa aliye hai ambaye Alikuwa amemfikiria, na kisha Akakipa kiumbe hiki hai jina—Adamu. Punde Mungu alipompata mtu huyu aliye hai na anayepumua, Alihisi vipi? Kwa mara ya kwanza, Alihisi furaha ya kuwa na mpendwa, na mwandani. Aliweza kuhisi pia kwa mara ya kwanza uwajibikaji wa kuwa baba pamoja na kujali kunakoandamana na hisia hizo. Mtu huyu aliye hai na anayepumua alimletea Mungu furaha na shangwe; Alihisi aliyefarijika kwa mara ya kwanza. Hili lilikuwa jambo la kwanza ambalo Mungu aliwahi kufanya ambalo halikukamilishwa kwa fikira Zake au hata matamshi Yake, lakini lilifanywa kwa mikono Yake miwili. Wakati kiumbe aina hii—mtu aliye hai na anayepumua—aliposimama mbele ya Mungu, aliyeumbwa kwa nyama na damu, aliye na mwili na umbo, na aliyeweza kuongea na Mungu, Alihisi aina ya shangwe ambayo Hakuwa amewahi kuhisi kabla. Kwa kweli alihisi kwamba uwajibikaji Wake na kiumbe huyu hai haukuwa na uhusiano tu katika moyo Wake, lakini kila jambo dogo alilofanya pia lilimgusa na likaupa moyo Wake furaha. Kwa hivyo wakati kiumbe huyu hai aliposimama mbele ya Mungu, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuwahi kufikiria kuwapata watu wengi zaidi kama hawa. Huu ndio uliokuwa msururu wa matukio ulioanza kwa fikira hii ya kwanza ambayo Mungu alikuwa nayo. Kwa Mungu, matukio haya yote yalikuwa yakifanyika kwa mara ya kwanza, lakini katika matukio haya ya kwanza, haijalishi vile Alivyohisi wakati huo—furaha, uwajibikaji, kujali—hakukuwa na yeyote yule wa kushiriki furaha hii na Yeye. Kuanzia wakati huo, Mungu alihisi kwa kweli upweke na huzuni ambayo Hakuwahi kuwa nao mbeleni. Alihisi kwamba binadamu wasingekubali au kuelewa mapenzi Yake na kujali Kwake, au nia Zake kwa mwanadamu, hivyo basi Alihisi huzuni na maumivu katika moyo Wake. Ingawa Alikuwa amefanya mambo haya kwa binadamu, binadamu hakuwa na habari na hakuelewa. Mbali na furaha, shangwe na hali njema ambayo binadamu alimletea pia viliandamana kwa haraka na hisia Zake za kwanza za huzuni na upweke. Hizi ndizo zilizokuwa fikira na hisia za Mungu wakati huo. Mungu alipokuwa akifanya mambo haya yote, moyoni Mwake Alitoka katika furaha Akaingia katika huzuni na kutoka katika huzuni Akaingia katika maumivu, vyote vikiwa vimechanganyika na wasiwasi. Kile Alichotaka kufanya tu kilikuwa kuharakisha kumruhusu mtu huyu, kizazi hiki cha binadamu kujua ni nini kilichokuwa moyoni Mwake na kuelewa nia Zake haraka iwezekanavyo. Kisha, wangekuwa wafuasi Wake na kupatana na Yeye. Wasingemsikiliza tena Mungu akiongea na kubakia kimya; wasingeendelea kutojua namna ya kujiunga na Mungu katika kazi Yake, na zaidi ya yote, wasingekuwa tena watu wasiojali na kuelewa mahitaji ya Mungu. Mambo haya ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ni yenye maana sana na yanashikilia thamani nyingi kwa minajili ya mpango Wake wa usimamizi na ule wa binadamu leo.
Baada ya kuviumba viumbe vyote na binadamu, Mungu hakupumzika. Asingesubiri kuutekeleza usimamizi Wake wala Asingeweza kusubiri kuwapata watu Aliowapenda mno miongoni mwa wanadamu.
…………
… Mungu anaona tukio hili la usimamizi wa binadamu, wa kuwaokoa wanadamu, kama muhimu sana kuliko chochote kingine. Huyafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia maneno Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa binadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi kazi ilivyo ngumu, haijalishi changamoto ni kubwa jinsi gani, haijalishi binadamu ni wanyonge jinsi gani, au binadamu amekuwa mwasi wa kweli, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake za bidii za kazi na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kusimamia na kumwokoa mwanadamu. Huku Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha binadamu bila kuficha bidii Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, hekima na uweza, na kila dhana ya tabia Yake. Anafichua bila kuacha chochote haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
Bila kujali kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kukifanya, bila kujali gharama, bila kujali lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, Shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemletea Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili; na inaonekana inatatanisha. Watu wanahisi kwamba ni kama hadithi ya visasili, na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, hata hawajui ni hadithi ngapi ambazo zimetokea katika huu ulimwengu. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu
Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote. Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Maangamizo ya mwisho ya wale wana wa uasi pia yatafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
Hatua tatu za kazi zitakapofikia tamati, patafanyika kundi la watu wanaomshuhudia Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuonyesha ukweli kwa matendo. Watakuwa na ubinadamu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo itatekelezwa mwishowe, na watu hawa ndio dhihirisho la kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ndio ushuhuda wenye nguvu zaidi kwa kushindwa kwa Shetani.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Baada ya kutekeleza kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua vitendo Vyake vingi, kimsingi kumshinda Shetani na kuwaokoa binadamu wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Yeye huchukua fursa ya kumshinda Shetani ili kufichua vitendo Vyake kwa binadamu na kuwaruhusu watu kuweza kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu duniani, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya wokovu Wake kwa binadamu. Viumbe wote wa Mungu humletea utukufu, humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio Lake si kumshinda Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia kushindwa kwa Shetani kuwaokoa binadamu; Anakutumia kushindwa kwa Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote. Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza kushuhudia utukufu Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio duniani na viumbe wote walio duniani watauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo. Viumbe vyake kule mbinguni na duniani vyote vitauona utukufu Wake, na Atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na kumruhusu binadamu amsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi vipengele hivi viwili. Mwishowe binadamu wote watashindwa na Yeye, na atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa wale wote wanaomilikiwa na Shetani.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo
Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawa Nimejazwa na hukumu na adabu kwa binadamu, kila ninachofanya bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, kwa ajili ya kueneza injili Yangu kwa njia bora zaidi na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. Kwa hiyo leo, katika wakati ambapo watu wengi tayari wametamauka pakubwa, Naendelea na kazi Yangu, Nikiendeleza kazi ambayo lazima Nifanye ili kuhukumu na kuadibu binadamu. Licha ya ukweli kwamba binadamu amechoshwa na kile Ninachosema na licha ya ukweli kwamba hana tamanio la kujali kuhusu kazi Yangu, Ningali natekeleza wajibu Wangu kwa sababu kusudio la kazi Yangu halijabadilika na mpango Wangu asilia hautabadilika. Kazi ya hukumu Yangu ni kumfanya binadamu anitii Mimi kwa njia bora zaidi, na kazi ya kuadibu Kwangu ni kuruhusu binadamu awe na mabadiliko bora zaidi. Ingawa kile Ninachofanya ni kwa minajili ya usimamizi Wangu, Sijawahi kufanya chochote ambacho hakikufaidi binadamu. Hiyo ndiyo maana Nataka kufanya mataifa yote nje ya Israeli kuwa matiifu tu kama Waisraeli na kuwabadilisha kuwa binadamu halisi, ili Niwe na mahali pa usalama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi Ninayotimiza katika nchi za Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajautilia maanani, badala yake wanafikiria tu kuhusu mustakabali na hatima zao. Haijalishi ni nini Ninachosema, watu hawajali kazi Yangu, badala yake wanalenga tu hatima zao za baadaye. Mambo yakiendelea kwa namna hii, kazi Yangu itapanuliwa vipi? Injili Yangu itaenezwa vipi kotekote ulimwenguni? Lazima mjue kwamba wakati kazi Yangu inapanuka, Nitawatawanya, Nitawaadhibu kama vile tu Yehova alivyoyaadhibu makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili injili Yangu iweze kuenea kotekote kwenye ulimwengu mzima, ili kazi Yangu iweze kuenezwa kwa Mataifa, ili kwamba jina Langu litukuzwe na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu litatukuzwa katika vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia