V. Maneno Juu ya Uhusiano Kati ya Kila Hatua ya Kazi ya Mungu na Jina la Mungu
231. Kazi ya Mungu kokote katika usimamizi wake ni wazi kabisa: Enzi ya Neema ni Enzi ya Neema, na siku za mwisho ni siku za mwisho. Kuna tofauti baina ya kila enzi, kwa kuwa katika kila enzi Mungu Anafanya kazi ambayo inawakilisha enzi hiyo. Ili kazi ya siku za mwisho iweze kufanywa, lazima kuwe na kuungua, hukumu, kuadibu, ghadhabu, na uharibifu wa kuleta enzi kwenye kikomo. Siku za mwisho zinaashiria enzi ya mwisho. Wakati wa enzi ya mwisho, je, Mungu si Ataleta enzi kwenye kikomo? Na ni kwa njia tu ya kuadibu na hukumu ndio inaweza kuleta enzi kwenye kikomo. Ni kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kuitamatisha enzi hiyo. Madhumuni ya Yesu yalikuwa kwamba mwanadamu aweze kuendelea kuwepo, kuishi, na kuweza kuwepo kwa njia bora zaidi. Alimwokoa mwanadamu kutoka kwa dhambi ili mwanadamu akome upotovu wa kudumu na kamwe asiishi katika Kuzimu na jehanamu, na kwa kumwokoa mwanadamu kutoka kwa Kuzimu na jehanamu, Yesu alimwezesha mwanadamu kuendelea kuishi. Sasa, siku za mwisho zimewadia. Mungu atamwangamiza mwanadamu, Atamharibu mwanadamu kabisa, ambayo ina maana kuwa Atageuza uasi wa binadamu. Kwa hivyo, huruma ya Mungu na tabia yake ya hapo zamani ya kupenda haitakuwa na uwezo wa kuhitimisha enzi hiyo, na haitakuwa na uwezo wa kukamilisha usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita. Kila enzi inaonyesha uwakilishi maalum wa tabia ya Mungu, na kila enzi ina kazi ambayo inafaa kufanywa na Mungu. Kwa hivyo, kazi iliyofanywa na Mungu mwenyewe kwa kila enzi ina dhihirisho la tabia Yake ya ukweli, na jina Lake na kazi anaofanya hubadilika na enzi—zote ni mpya. Wakati wa Enzi ya Sheria, kazi ya kumwelekeza mwanadamu ilifanyika katika Jina la Yehova, na awamu ya kwanza ya kazi ilifanyika duniani. Kazi ya awamu hii ilikuwa ni kujenga hekalu na madhabahu, na kutumia sheria kuwaongoza watu wa Israeli na kufanya kazi miongoni mwao. Kwa kuongoza watu wa Israeli, Alizindua kituo cha kazi Yake hapa duniani. Kwa msingi huu, Yeye Alipanua kazi yake nje ya Israeli, ambayo ni kusema kwamba, kuanzia Israeli, Aliendeleza kazi yake nje, ili vizazi vya baadaye walikuja kujua polepole kwamba Yehova Alikuwa Mungu, na kuwa Yehova Alikuwa Ameumba mbingu na nchi na vitu vyote, Alitengeneza viumbe vyote. Yeye Alieneza kazi yake kupitia kwa watu wa Israeli. Nchi ya Israeli ilikuwa ya mahali takatifu pa kwanza pa kazi ya Yehova hapa duniani, na kazi ya Mungu ya hapo mwanzoni ilikuwa kote katika nchi ya Israeli. Hiyo ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria. Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu. Alichokuwa nacho na Aliyekuwa ni neema, upendo, huruma, uvumilivu, subira, unyenyekevu, huduma, na stahamala, na nyingi ya kazi ambayo Alifanya ilikuwa kwa ajili ya kumwokoa mwanadamu. Tabia Yake ilikuwa ya huruma na upendo, na kwa sababu Yeye Alikuwa na huruma na upendo, ilikuwa sharti asulubishwe msalabani kwa ajili ya mwanadamu, ili kuonyesha kwamba Mungu Alimpenda mwanadamu jinsi anavyojipenda, kwa kiasi kwamba Yeye mwenyewe Alijitoa kama kafara na kwa ukamilifu Wake. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu, ambalo lina maana kuwa Mungu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu, na ya kwamba Alikuwa Mungu wa rehema na wa upendo. Mungu Alikuwa na mwanadamu. Upendo wake, huruma yake, na wokovu wake uliandamana na kila mtu. Mwanadamu angeweza tu kupata amani na furaha, kupokea baraka zake, kupokea neema yake kubwa na nyingi, na kupokea wokovu wake iwapo mwanadamu angekubali jina lake na akubali uwepo wake. Kupitia kusulubiwa kwa Yesu, wale wote ambao walimfuata Yeye walipokea wokovu na walisamehewa dhambi zao. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu. Kwa maneno mengine, kazi ya Enzi ya Neema ilifanywa hasa katika Jina la Yesu. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu Aliitwa Yesu. Yeye Alifanya kazi mpya zaidi ya Agano la Kale, na kazi yake ilimalizika kwa kusulubiwa, na ya kwamba huo ulikuwa ukamilifu wa kazi yake. Kwa hivyo, wakati wa Enzi ya Sheria Yehova ndilo lilikuwa jina la Mungu, na katika Enzi ya Neema jina la Yesu lilimwakilisha Mungu. Katika siku za mwisho, jina lake ni Mwenyezi Mungu—mwenye uweza, na yeye hutumia nguvu zake kumwongoza mwanadamu, kumshinda mwanadamu, kumtwaa mwanadamu, na mwishowe, kuhitimisha enzi hiyo. Katika kila enzi, katika awamu yote ya kazi yake, tabia ya Mungu ni dhahiri.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
232. “Yehova” ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo, katika enzi ya sasa, Waisraeli wote, isipokuwa Wayahudi, wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”
233. Enzi ya Neema ilianza na Jina la Yesu. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu. Ushuhuda wa wale waliomwamini Yeye ulitolewa kwa ajili ya Yesu Kristo, na kazi waliyoifanya walifanya pia kwa ajili ya Yesu Kristo. Hitimisho Enzi ya Sheria ya Agano la Kale lilimaanisha kuwa kazi iliyofanywa hasa kutumia jina la Yehova ilikuwa imefikia kikomo. Baada ya hii, jina la Mungu halikuwa Yehova tena; badala yake Yeye Aliitwa Yesu, na kutoka hapa Roho Mtakatifu Alianza kazi hasa kwa kutumia jina la Yesu. Kwa hiyo leo, watu ambao leo bado hula na kunywa maneno ya Yehova, na bado hutumia kazi ya Enzi ya Sheria—je, hufuati masharti bila kufikiria? Je! Hujakwama katika siku za zamani? Leo, unajua kwamba siku za mwisho zimefika. Wakati Yesu atakapokuja, bado Ataitwa Yesu? Yehova aliwaambia watu wa Israeli kwamba Masihi angekuja, lakini alipofika, hakuitwa Masihi bali Yesu. Yesu alisema kwamba Angekuja tena, na kwamba Angekuja kama Alivyoondoka. Haya yalikuwa maneno ya Yesu, lakini je, ulishuhudia jinsi Yesu alivyoondoka? Yesu aliondoka akiwa juu ya wingu jeupe, lakini je, Yeye Mwenyewe angerudi kati ya binadamu juu ya wingu jeupe? Ingekuwa hivyo, je, si bado angeitwa Yesu? Wakati Yesu Atakuja tena, enzi itakuwa tayari imebadilika, je, hivyo bado Ataweza kuitwa Yesu? Je, Mungu Anajulikana tu kwa jina la Yesu? Je, hangeweza kuitwa kwa jina jipya katika enzi mpya? Je, sura ya mtu mmoja na hasa jina moja vinaweza kumwakilisha Mungu katika ukamilifu wake? Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima Atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha kipengele cha wakati cha tabia ya Mungu katika enzi fulani; yote linahitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima. Bila kujali iwapo ni enzi ya Yehova, au ni enzi ya Yesu, kila enzi inawakilishwa kwa jina.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
234. Wakati Yesu Alikuja kufanya kazi yake, ilikuwa ni kwa uongozi wa Roho Mtakatifu; Yeye Alitenda vile ambavyo Roho Mtakatifu Alitaka, na haikuwa kwa mujibu wa Enzi ya sheria ya Agano la Kale ama kwa mujibu wa kazi ya Yehova. Ingawa kazi ambayo Yesu Alikuja kufanya haikuambatana na sheria za Yehova ama amri za Yehova, chanzo chao kilikuwa sawa. Kazi ambayo Yesu Alifanya iliwakilisha jina la Yesu, na iliwakilisha Enzi ya Neema; kazi iliyofanywa na Yehova, iliwakilisha Yehova, na iliwakilisha Enzi ya Sheria. Kazi yao ilikuwa kazi ya Roho mmoja katika enzi tofauti. Kazi ambayo Yesu Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Neema, na kazi ambayo Yehova Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Yehova Aliwaongoza tu watu wa Israeli na Misri, na mataifa yote nje ya Israeli. Kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema ya Agano Jipya ilikuwa kazi ya Mungu katika jina la Yesu kwa kuwa Yesu ndiye Aliongoza enzi hii. … Kungekuwepo tu na enzi mpya wakati Yesu Alikuja kufanya kazi mpya, Alipozindua enzi mpya, na kupenya katika kazi iliyokuwa imefanyika hapo awali katika nchi ya Israeli, na hakufanya kazi yake kwa mujibu wa kazi iliyofanywa na Yehova huko Israeli, hakuzingatia sheria Yake ya zamani, na hakufuata kanuni zozote, na Alifanya kazi mpya ambayo Alitakiwa kufanya. Mungu Mwenyewe anakuja kuzindua enzi, na Mungu mwenyewe huja kuleta enzi kwenye kikomo. Mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi ya kuanzisha enzi hiyo na kuhitimisha enzi. Kama Yesu hakuleta kazi ya Yehova kwenye kikomo baada ya Yeye kuja, basi hio inadhihirisha ya kwamba Yeye Alikuwa tu mwanadamu, na hakuwakilisha Mungu. Kwa usahihi kwa sababu Yesu Alikuja na kuhitimisha kazi ya Yehova, Akaendeleza kazi ya Yehova na, aidha, Akatekeleza kazi Yake, kazi mpya, inathibitisha kuwa hii ilikuwa enzi mpya, na kwamba Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe. Walifanya kazi katika awamu mbili zinazotofautiana. Awamu moja ilifanyika katika hekalu, na hiyo nyingine ilifanyika nje ya hekalu. Awamu moja ilikuwa ya kuongoza maisha ya mwanadamu kwa mujibu wa sheria, na awamu nyingine ilikuwa ya kutoa kafara ya dhambi. Awamu hizi mbili za kazi bila shaka zilikuwa tofauti; huu ni mgawanyiko wa enzi ya zamani na enzi mpya, na hakuna kosa kusema kuwa hizo ni enzi mbili! Maeneo ya kazi yao yalikuwa tofauti, na kiini cha kazi yao kilikuwa tofauti, na lengo la kazi yao lilikuwa tofauti. Kwa hivyo, enzi hizi zinaweza kugawanywa kwa awamu mbili: Agano la Kale na Jipya, ambayo ni kusema, enzi mpya na ya zamani. Yesu alipokuja hakuenda katika hekalu, ambayo inathibitisha kwamba enzi ya Yehova ilikuwa imeisha. Hakuingia hekaluni kwa sababu kazi ya Yehova katika hekalu ilikuwa imekamilika, na haikuhitajika kufanywa tena, na kwa hiyo kuifanya tena kungekuwa kuirudia. Kwa kuondoka tu hekaluni, kuanza kazi mpya na kuzindua njia mpya nje ya hekalu, ndio Aliweza kuifikisha kazi ya Mungu kwa upeo wake. Kama Hangeenda nje ya hekalu kufanya kazi Yake, kazi ya Mungu haingeweza kamwe kuendelea mbele kupita hekalu, na hakungekuwa na mabadiliko yoyote mapya. Na kwa hiyo, Yesu Alipokuja, Hakuingia hekaluni, na Hakufanya kazi Yake hekaluni. Alifanya kazi Yake nje ya hekalu, na Akafanya kazi Yake kwa uhuru Akiandamana na wanafunzi. Kuondoka kwa Mungu katika hekalu kufanya kazi Yake kulikuwa na maana kwamba Mungu alikuwa na mpango mpya. Kazi Yake ilikuwa ifanyike nje ya hekalu, na ilikuwa iwe kazi mpya ambayo haingezuiliwa kwa njia ya utekelezaji wake. Kuwasili kwa Yesu kulimaliza kazi ya Yehova ya wakati wa Agano la Kale. Ingawa ziliitwa kwa majina mawili tofauti, awamu zote mbili za kazi zilifanywa na Roho mmoja, na kazi ya pili ilikuwa mwendelezo wa kazi ya kwanza. Kwa kuwa jina lilikuwa tofauti, na kiini cha kazi kilikuwa tofauti, basi enzi ilikuwa tofauti. Wakati Yehova Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yehova, na wakati Yesu Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yesu. Na kwa hivyo, kila wakati Mungu Anapokuja, anaitwa kwa jina moja, Yeye anawakilisha enzi moja, na Yeye anazindua njia mpya; na kwa kila njia mpya, Yeye huchukua jina jipya, ambalo inaonyesha kuwa Mungu daima ni mpya na wala si wa zamani, na ya kwamba kazi yake daima inasonga mbele. Historia inasonga mbele daima, na kazi ya Mungu inasonga mbele daima. Ili mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita ufike upeo wake, lazima uendelee kusonga mbele. Kila siku ni sharti Yeye afanye kazi mpya, kila mwaka lazima Yeye afanye kazi mpya, ni sharti Yeye azindue njia mpya, azindue enzi mpya, aanzishe kazi mpya na kubwa zaidi, na ni sharti alete majina mapya na kazi mpya.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
235. Kama kazi ya Mungu katika kila enzi ni sawa daima, naye daima anaitwa kwa jina sawa, ni jinsi gani basi mwanadamu atamjua Yeye? Mungu lazima aitwe Yehova, na mbali na Mungu kuitwa Yehova, yeyote ambaye ataitwa jina jingine si Mungu. Ama kwa njia nyingine Mungu Anaweza tu kuitwa Yesu, na Mungu hawezi kuitwa jina lingine isipokuwa Yesu; na mbali na Yesu, Yehova si Mungu, na wala Mwenyezi Mungu si Mungu. Mwanadamu anaamini kuwa ni ukweli Mungu ni mwenye uweza, lakini Mungu ni Mungu pamoja na mwanadamu; Sharti aitwe Yesu, kwa kuwa Mungu yu pamoja na mwanadamu. Kufanya hili ni kufuata mafundisho, na kumshurutisha Mungu kwenye eneo fulani. Kwa hivyo, kazi ambayo Mungu hufanya katika kila enzi, jina ambalo Yeye huitwa, na mfano ambao Yeye hutwaa—kazi ambayo Yeye hufanya katika kila hatua mpaka leo—hivi havifuati kanuni hata moja, na hayakabiliwi na kikwazo chochote. Yeye ni Yehova lakini pia ni Yesu, na vile vile ni Masihi, na Mwenyezi Mungu. Kazi yake inaweza kubadilika polepole, na kuna mabadiliko sambamba katika jina lake. Hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Yeye kikamilifu, lakini majina yote ambayo Yeye huitwa yanaweza kumwakilisha Yeye, na kazi ambayo Amefanya katika kila enzi inawakilisha tabia yake.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
236. Wengine wanasema kwamba jina la Mungu halibadiliki, hivyo, mbona basi jina la Yehova likawa Yesu? Ilitabiriwa kuja kwa Masihi, hivyo mbona basi mwanadamu kwa jina Yesu alikuja? Mbona jina la Mungu lilibadilika? Kazi kama hiyo haikufanyika muda mrefu uliopita? Hawezi Mungu leo kufanya kazi mpya? Kazi ya jana inaweza kubadilishwa, na kazi ya Yesu inaweza kufuata baada ya hiyo ya Yehova. Haiwezi kazi ya Yesu kurithiwa na kazi nyingine? Ikiwa jina la Yehova linaweza kubadilishwa kuwa Yesu, basi jina la Yesu haliwezi kubadilishwa pia? Hakuna jambo lolote hapa lisilo la kawaida; ni kwamba tu watu ni punguani sana. Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele. Ikiwa unaamini kwamba Mungu anaweza tu kuitwa na jina Yesu, basi unajua machache sana. Unathubutu kudai kwamba Yesu milele ni jina la Mungu, kwamba Mungu milele na daima atajulikana kwa jina Yesu, na kwamba haya hayatabadilika? Unathubutu kudai kwa uhakika ni jina la Yesu lililohitimisha Enzi ya Sheria na pia kuhitimisha enzi ya mwisho? Nani anaweza kusema kwamba neema ya Yesu inaweza kuhitimisha enzi?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?
237. Je, Jina la Yesu—“Mungu pamoja nasi,”—linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu. Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na yanazidi uwezo wa mwanadamu kumjua Yeye. Lugha ya mwanadamu haina uwezo wa kumfafanua Mungu kwa ukamilifu. Mwanadamu ana msamiati finyu tu ambao anaweza kufafanua yote anayojua kuhusu tabia ya Mungu: kubwa, yenye heshima, ya ajabu, isiyoeleweka, kuu, takatifu, yenye haki, yenye hekima, na kadhalika. Maneno mengi sana! Msamiati kama huo finyu hauwezi kuelezea kile kidogo mtu ameshuhudia juu ya tabia ya Mungu. Baadaye, watu wengi waliongeza maneno zaidi ili kueleza vizuri zaidi ari ndani ya mioyo yao: Mungu ni mkuu sana! Mungu ni mtakatifu sana! Mungu ni wa kupendeza sana! Leo, maneno kama haya yamefikia kilele chake, lakini bado mwanadamu hawezi kujieleza wazi wazi. Na kwa hiyo, kwa mwanadamu, Mungu ana majina mengi, lakini Hana jina moja, na hilo ni kwa sababu nafsi ya Mungu ni ya ukarimu sana, na lugha ya mwanadamu haitoshi sana. Neno au jina moja maalum halina uwezo wa kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake. Kwa hivyo, je, Mungu Anaweza kuchukua jina moja lisilobadilika? Mungu ni mkuu sana na mtakatifu sana, kwa hivyo mbona wewe huwezi kumruhusu Yeye abadili jina Lake katika kila enzi mpya? Kwa hivyo, katika kila enzi ambayo Mungu binafsi hufanya kazi yake mwenyewe, Yeye hutumia jina ambalo linafaa enzi hiyo ili kujumlisha kazi ambayo anaifanya. Yeye hutumia hili jina haswa, ambalo linamiliki umuhimu wa wakati, kuwakilisha tabia yake katika enzi hiyo. Mungu hutumia lugha ya mwanadamu kuelezea tabia yake mwenyewe. Hata hivyo, watu wengi ambao wamepata uzoefu wa kiroho na wamemuona Mungu binafsi bado wanahisi kuwa jina moja maalumu haliwezi kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake—ole wetu, hili linasikitisha, hivyo mwanadamu hamwiti Mungu kwa jina lolote, lakini humwita tu “Mungu.” Moyo wa mwanadamu unaonekana kujawa na upendo, lakini pia unaonekana kuzongwa na ukinzani, kwa maana mwanadamu hajui jinsi ya kumueleza Mungu. Kile Mungu alicho ni cha ukarimu sana kiasi kwamba hakuna kabisa njia ya kukieleza. Hakuna jina moja ambalo linaweza kutoa muhtasari wa tabia Ya Mungu, na hakuna jina moja ambalo linaweza kuelezea yote ambayo Mungu anacho na Alicho. Kama mtu ataniuliza, “Ni jina gani hasa unalotumia?” Nitamwambia, “Mungu ni Mungu!” Je, hilo silo jina bora zaidi la Mungu? Je, huko sio kufafanua bora zaidi kuhusu tabia ya Mungu? Hali ikiwa hivi, kwa nini mnatumia juhudi nyingi sana kutafuta jina la Mungu? Kwa nini ufikirie sana, kukaa bila kula na kulala, kwa ajili ya jina? Siku itawadia ambapo Mungu hataitwa Yehova, Yesu, au Masihi—Yeye Ataitwa tu Muumba. Wakati huo, majina yote ambayo Alichukua hapa duniani yatafikia kikomo, kwa kuwa kazi yake hapa duniani itakuwa imefika mwisho, na baada ya hapo Mungu hatakuwa na jina. Wakati mambo yote yatakuja kuwa chini ya utawala wa Muumba, kwa nini umwite kwa jina sahihi ila bado halijakamilika? Je, bado unatafuta jina la Mungu sasa? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaitwa tu Yehova? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaweza tu kuitwa Yesu? Je, unaweza kubeba dhambi ya kumkufuru Mungu? Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu. Jina lolote ambalo anaitwa Yeye, je, si lile analolichagua kwa hiari yake? Je, Yeye atakuhitaji wewe, mmoja wa viumbe wake Wake, kuliamua? Jina ambalo Mungu Anaitwa ni kwa mujibu wa kile ambacho mwanadamu anaweza kufahamu na lugha ya mwanadamu, lakini hili jina haliwezi kujumlishwa na mwanadamu. Wewe unaweza kusema tu kuwa mbinguni kuna Mungu, ya kwamba Yeye anaitwa Mungu, na kwamba Yeye mwenyewe ni Mungu mwenye nguvu nyingi, busara tele, wakuinuliwa sana, wa ajabu kuu, mwenye siri kuu, mwenye uweza mkuu sana, na huwezi kusema mengi zaidi; hayo ndiyo yote unayoyajua. Kwa njia hii, je, jina la Yesu tu linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe? Wakati siku za mwisho zitawadia, ingawa ni Mungu ndiye anafanya kazi yake, ni sharti jina lake libadilike, kwa kuwa ni enzi tofauti.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
238. Kila wakati ambao Mungu Atawasili hapa duniani, Yeye Atabadilisha jina lake, jinsia yake, mfano wake, na kazi yake; Yeye harudii kazi yake, na Yeye daima yu mpya na kamwe si wa zamani. Wakati Alikuja hapo awali, Aliitwa Yesu; Je, anaweza bado kuitwa Yesu anapokuja tena wakati huu? Alipokuja hapo awali, Alikuwa wa kiume, Ataweza kuwa wa kiume tena wakati huu? Kazi Yake Alipokuja wakati wa Enzi ya Neema ilikuwa ya kusulubishwa msalabani; Atakapokuja tena, je, bado Atawakomboa wanadamu kutoka kwenye dhambi? Je, bado Atasulubishwa msalabani? Je, huko hakutakuwa kurudia kazi Yake? Je, hukujua kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani? Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria kutobadilika kwa tabia ya Mungu na kiini Chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? Kazi yake daima inaendelea mbele, na hivyo pia ndivyo tabia yake inafichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, na kile ambacho kinafichuliwa ni tabia yake ya asilia. Hapo mwanzo, tabia ya Mungu ilikuwa siri kwa mwanadamu, na kamwe Yeye hadharani hakumfichulia mwanadamu tabia yake, na mwanadamu hakuwa na ufahamu kuhusu Yeye, na hivyo hatua kwa hatua Alitumia kazi Yake kumfichulia mwanadamu tabia Yake, lakini hii haina maana kuwa tabia Yake inabadilika katika kila enzi. Sio kweli kuwa tabia ya Mungu kila wakati inabadilika kwa ajili mapenzi Yake daima hubadilika. Bali, kwa kuwa enzi za kazi Yake ni tofauti, asili ya tabia Yake kwa ujumla hufichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, ili mwanadamu aweze kumjua Yeye. Lakini hii si kwa njia yoyote ushahidi kuwa Mungu hapo awali hakuwa na tabia fulani na tabia Yake imebadilika hatua kwa hatua kwenye enzi zinazopita—ufahamu kama huo ni wenye kosa. Mungu humfichulia mwanadamu tabia yake fulani ya asili, kile Alicho, kwa mujibu wa enzi zinazopita. Kazi ya enzi moja haiwezi kueleza tabia nzima ya Mungu. Na kwa hivyo, maneno haya “Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani” yanarejelea kazi yake, na maneno haya “Mungu habadiliki” kinarejelea kile ambacho Mungu anacho na alicho kiasili. Bila kujali, huwezi kubaini kazi ya miaka elfu sita kwa mtazamo mmoja, ama kwa kuielezea tu kwa maneno ambayo hayabadiliki. Huo ni ujinga wa mwanadamu. Mungu si wazi kama mwanadamu anavyofikiria, na kazi yake haitasimama katika enzi moja. Yehova, kwa mfano, haliwezi daima kusimamia jina la Mungu; Mungu pia hufanya kazi yake kwa kutumia Jina la Yesu, ambayo ni ishara ya vile ambavyo kazi ya Mungu daima husonga kwenda mbele.
Mungu siku zote huwa Mungu, na kamwe Yeye hatakuwa Shetani; Shetani daima ni Shetani, na yeye hawezi kuwa Mungu. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, haki ya Mungu, na adhama ya Mungu kamwe hayatabadilika. Kiini chake na anachomiliki na kile Anacho na alicho kamwe hakitabadilika. Kazi yake, hata hivyo, daima inaendelea mbele, daima inaenda ndani zaidi, kwa kuwa Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani. Katika kila enzi Mungu huchukua jina jipya, katika kila enzi anafanya kazi mpya, na katika kila enzi Yeye huwaruhusu viumbe Wake kuona mapenzi Yake mapya na tabia Yake mpya. Ikiwa watu hawaoni dhihirisho la tabia mpya ya Mungu katika enzi mpya, wao si watamsulubisha msalabani milele? Na kwa kufanya hivyo, si watakuwa wamebaini Mungu?
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)
239. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote. Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.
Mwokozi atakapofika katika siku za mwisho, kama bado angeitwa Yesu, na kuzaliwa mara nyingine katika Uyahudi, na kufanya kazi Yake katika Uyahudi, basi hii ingethibitisha kuwa Niliumba Wayahudi peke yao na kuwakomboa Wayahudi peke yao, na kuwa Sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hii haitakuwa kinyume cha maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote”? Nilitoka Uyahudi nami Nafanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, ila Mungu wa viumbe vyote. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi si Yehova, Mungu wa Wayahudi tu, lakini, zaidi ya hayo, kwa sababu Mimi ni Muumba wa wateule Wangu wote kati ya Mataifa. Sikuumba Uyahudi, Misri, na Lebanoni pekee, bali pia Niliumba Mataifa yote mbali na Israeli. Na kwa sababu hiyo, Mimi ni Bwana wa viumbe vyote. Nilitumia Uyahudi tu kama hatua ya kwanza ya kazi Yangu, Nikayatumia Uyahudi na Galilaya kama ngome za kazi Yangu ya ukombozi, nami Natumia Mataifa kama msingi ambao Nitatumia kuikamilisha enzi nzima. Nilifanya hatua mbili za kazi katika Uyahudi (hatua mbili za kazi ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), nami Nimekuwa Nikitekeleza hatua mbili zaidi za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine zote zaidi ya Uyahudi. Nitafanya kazi ya kushinda kati ya Mataifa, na hivyo kuikamilisha enzi. Mwanadamu akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa Nimeianza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa shauku kuwasili kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao wale wasioniamini. Wao ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni ya bandia. Je, watu kama hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja si kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, lakini badala yake wanatamani kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, ndipo watakapokombolewa; wanamtazamia Yesu kuwakomboa wanadamu wote mara nyingine kutoka nchi hii iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu kama hao watawezaje kuwa wale wanaoikamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Matamanio ya mwanadamu hayawezi kufikia mapenzi Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani au kuthamini tu kazi ambayo Nimeifanya hapo awali, naye hajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya siku zote na si mzee kamwe. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, naye hana fununu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule ambaye Atawaangamiza wanadamu. Mwanadamu anachotamani na kujua tu ni kuhusu dhana yake mwenyewe, nayo ni yale tu ambayo anaweza kuyaona kwa macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayoifanya, bali hayatangamani nayo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”