564 Kujitafakari kwa Njia Hii ni Muhimu

1 Umuhimu wa kujitafakari na kujijua ni huu: Kadiri unavyozidi kuhisi kuwa katika sehemu fulani umefanya vizuri au umefanya jambo linalofaa, na kadiri unavyofikiri kuwa unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu au kuweza kujivunia katika sehemu fulani, basi ndivyo inavyofaa zaidi kwako kujijua katika sehemu hizo na inavyofaa zaidi kwako kuzichunguza zaidi ili kuona ni uchafu gani uko ndani yako, pamoja na mambo gani ndani yako hayawezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hebu tumchukue Paulo kama mfano. Paulo alikuwa mwenye maarifa mno, na alivumilia mengi katika kazi yake ya kuhubiri. Alipendwa hasa sana na Wengu. Kama matokeo, baada ya kumaliza wingi wa kazi, alidhani kungekuwa na taji lililowekwa kando kwa ajili yake. Hili lilimfanya atembee zaidi na zaidi kwenye njia isiyo sahihi, hadi mwishowe akaadhibiwa na Mungu.

2 Paulo hakuwa amelenga kutafuta ukweli katika maneno ya Bwana Yesu; alikuwa tu ameamini mawazo na fikira zake mwenyewe. Alikuwa amedhani kwamba almradi afanye mambo machache mazuri na kuonyesha tabia nzuri, angesifiwa na kutuzwa kupewa tuzo na Mungu. Mwishowe, mawazo na fikira zake zilipofusha roho yake na kufunika hali yake ya kweli. Hadithi hii kumhusu Paulo inatumika kama onyo kwa kila mtu amwaminiye Mungu, ambalo ni kwamba wakati wowote tunapohisi kuwa tumefanya vizuri zaidi, au kuamini kwamba tuna vipawa zaidi katika mambo fulani, au kufikiria kwamba hatuhitaji kubadilika au kushughulikiwa katika jambo fulani, tunapaswa kujitahidi kutafakari na kujijua wenyewe zaidi katika suala hilo; jambo hili ni muhimu. Hii ni kwa sababu bila shaka hujafichua, kutilia maanani au kuchanganua vipengele kujihusu ambavyo unaamini kuwa mzuri, ili kuona kama kweli vina chochote kinachompinga Mungu au la.

3 Kila tendo lako, kila ufanyacho, mwelekeo unaotumia kukifanya, na yale ambayo malengo yako yaliyo, bila shaka, tayari yamedhamiriwa na mawazo na maoni yako. Watu wengine wamejificha vizuri sana, na si dhahiri kwamba wanampinga Mungu kwa njia yoyote. Wao hata hawasemi kuhusu upinzani wowote kwa Mungu. Hata hiyo, mambo ambayo yamekita mizizi akilini mwa mwanadamu yanachukiwa kabisa na Mungu. Hili ndilo Mungu anataka kulifichua na ambalo tunapaswa kulielewa. Ni kwa sababu hii ndiyo Mungu anasema kwamba kadiri unavyozidi kuhisi kwamba unafanya vizuri katika mawanda fulani, ndivyo inavyostahili zaidi wewe ujijue kuhusiana na suala hilo, na kwa hiyo, ndivyo unavyopaswa kuzidi kutafuta ukweli. Ni wakati huo pekee ndiyo unaweza kutakaswa na kukamilishwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kutambua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 563 Kanuni za Msingi za Kutatua Asili ya Mtu

Inayofuata: 565 Mtu Anaweza Kujichukia tu Anapojijua kwa Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp