846 Watu Waliokamilishwa na Maneno ya Mungu

1 Ikiwa mtu anaweza kumridhisha Mungu huku akitimiza wajibu wake, ni mwenye maadili katika maneno ya matendo yake, na anaweza kuingia katika uhalisi a vipengele vya ukweli, basi huyu ni mtu ambaye anakamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yamekuwa ya kufaa kabisa kwa watu kama hao, kwamba maneno ya Mungu yamekuwa maisha yao, wamepata ukweli, na wanaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili, asili ya mwili wao—yaani, msingi maalum wa uwepo wao wa kwanza—itatikisika na kuanguka. Baada ya watu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yao, watakuwa watu wapya.

2 Maneno ya Mungu yakiwa maisha yao, maono ya kazi ya Mungu, matakwa Yake kwa wanadamu, ufunuo Wake kwa wanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anawahitaji watimize vikiwa maisha yao, wakiishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, basi wanakamilishwa na Mungu. Watu kama hawa wanazaliwa tena, na wamekuwa watu wapya kupitia maneno ya Mungu. Hii ni njia ambayo Petro aliitumia kuufuatilia ukweli; Ilikuwa njia ya kukamilishwa, kukamilishwa na maneno ya Mungu, na kupata uzima kutoka kwa maneno ya Mungu. Ukweli ulioonyeshwa na Mungu ulikuwa maisha yake, na wakati huo tu ndipo alikuwa mtu aliyepata ukweli.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 845 Ni Wale tu Wanaokamilishwa na Mungu Wanaweza Kumpenda kwa Kweli

Inayofuata: 847 Kutafuta Ukweli Ndiyo Fursa ya Pekee ya Kukamilishwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp